Uzinduzi wa kampeni za CCM jimbo la Kalenga,Mwigulu Nchemba atikisa Kalenga

Mohamed Mwaupete

JF-Expert Member
Oct 7, 2013
375
133
Ni live Kutoka Kalenga Alhamis ya 27/02/2014 CCM wanafanya Ufunguzi/uzinduzi wa Kampeni.Watu wanazidi Kumininika hapa Viwanja Vya Kalenga waliovalia Nguo za CCM na wale Wananchi waliopigilia Mavazi yao ya kawaida kabisa.

Komrade Mwigulu lameck Nchemba ndiye anayeongoza Ufunguzi wa Kampeni hizi hapa Kalenga,Hakika Godfrey Mgimwa Ushindi Upo mikononi Mwake.

1922197_673148576080550_1317729300_n.jpg
998154_673148509413890_866782362_n.jpg

Mgombea Ubunge wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Godfrey William Mgimwa akibebwa Juu na Wanachama/wapenzi wa CCM mara baada ya Kuwasili Viwanja Vya Stendi-kata ya Ifunda.

1920092_673149482747126_1709045094_n.jpg
1922456_673150029413738_1705757025_n.jpg
1902910_673150139413727_1773692866_n.jpg
1800203_673150216080386_1798829731_n.jpg

Mapokezi Mazito yakiendelea ya Naibu Katibu Mkuu CCM-Bara na Kijana Mgombea Ubunge Jimbo la Kalenga Ndugu Godfrey William Mgimwa kwenye uwanja wa Stedi-Kata ya Ifakara hii leo wakati wa Mkutano wa Ufunguzi wa Kampeni za Ubunge Jimbo la Kalenga.

1921966_673148426080565_261341706_n.jpg

Mh:Naibu Katibu Mkuu CCM-Bara akisaini Kitabu akiwa na Mgombea Ubunge Jimbo la Kalenga Ndugu Godfrey William Mgimwa mara baada ya kuwasili Viwanja Vya Stendi Kata ya Ifunda.
1888549_673147896080618_348924720_n.jpg
1888549_673147976080610_661538409_n.jpg
1959988_673148062747268_1024847000_n.jpg

Chief Wa Wahehe,Chief Mkwawa ambaye pia ni Kada Mtiifu wa Chama Cha Mapinduzi akishikana Mikono ya Baraka na Mgombea Ubunge Jimbo la Kalenga Godfrey William Mgimwa,Pia akisalimana na Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Mh:Mwigulu Nchemba hii leo kwenye Mkutano wa Ufunguzi wa Kampeni kata ya Ifunda-Kalenga.Kubwa zaidi CHIEF MKWAWA ambaye ni Mtoto wa Marehemu Mkwawa alikuwa anakanusha taarifa kuhusu Yeye Kuunga Mkono Chadema,Amesema hawezi kuunga Mkono chama ambacho hakieleweki kuanzia muundo wake na hata maamuzi yake ndani ya Chama.Yeye ni MwanaCCM damu damu,na ameapa atafia CCM.

1797426_673145792747495_18005571_n.jpg

Msanii Dokii ambaye ni kada wa Chama Cha Mapinduzi akitumbuiza kwenye ufunguzi wa kampeni wa Jimbo la Kalenga kwa Chama Cha Mapinduzi.Dokii ametunga wimbo rasmi kwaajili ya Kalenga na Umuhimu wa Kijana Godfrey William Mgimwa kuwa Mbunge wa Jimbo hilo,

1782048_673148132747261_723439966_n.jpg
1902727_673148216080586_1805694855_n.jpg

Katibu Msaidizi wa CCM Wilaya ya Iringa Vijijini Ndugu Mtatulu akionesha baadhi ya Mitego inayodaiwa kuwekwa na Vijana wa CHADEMA kwenye njia ili Magari ya CCM yanayozunguka kwenye Kampeni yapata matatizo.Pia Ndugu Mtatulu alitaja majina ya Wahusika na ameshayapeleka Polisi kwa hatua zaidi za kisheria.

1939913_673147369414004_1013933446_n.jpg

Naibu katibu Mkuu CCM Bara Mh:Mwigulu Nchemba akiteta Jambo na Kijana Godfrey William Mgimwa ambaye ni Mgombe Ubunge Jimbo la Kalenga.
1796508_673147039414037_1820245886_n.jpg

Wabunge wa Iringa(Wilaya+majimbo) wakitoa neno la kuomba Kura kwa Wananchi Wa Ifunda ili wamchague Mgombe wa CCM Kijana Godfrey William Mgimwa.

1604966_673147126080695_2047039991_n.jpg
1690017_673146509414090_417516203_n.jpg
1800268_673146769414064_902539448_n.jpg
1009973_673145979414143_612310108_n.jpg
1932458_673146076080800_1084116287_n.jpg
1798027_673146112747463_961830305_n.jpg
1966845_673146386080769_1801564682_n.jpg

Ni Naibu Katibu Mkuu CCM_Bara Mh:Mwigulu Nchemba akizungumza na mamia ya Wananchi waliofurika Viwanja Vya Stendi Kata ya Ifunda hii leo kuhudhuria Mkutano wa hadhara wa ufunguzi wa Kampeni za Ubunge Jimbo la Kalenga(CCM).Mh:Mwigulu Nchemba amewaomba Wananchi wa Kalenga kumchagua Kijana Godfrey William Mgimwa kwa sababu anakila sifa za kuwatumikia Wananchi wa Kelenga,Lakini pia ni Kijana aliyependekezwa na Chama kuanzia ngazi ya Chini hadi Taifa kwa mtindo wa Kura za maoni na amewashinda wenzake 9.
Mh:Mwigulu Nchemba amesisitiza kuwa Kwa namna Marehemu Mgimwa alivyolitumikia Jimbo lake na kuiletea Heshima Nchi yetu na Jimbo la Kalenga,kuna kila sababu ya Kuipa nafasi CCM iendelee kutekeleza Ilani yake ndani ya Jimbo hilo.Mh:Mgimwa tangu kufariki kwake Vyama vya siasa vimekuwa mstari wa mbele kumsifia kutokana na Utendaji wake Kuanzia Wizara ya Fedha hadi Jimboni kwake hasa upande wa Miundombinu,Maendeleo yote yaliyofanyika ndani ya Jimbo la Kalenga ni Matunda ya sera nzuri za CCM na Ilani ya CCM ndani ya Jimbo hilo.Pia Mwigulu amezungumzia kuhusu Amani na Mshikamano ulipo kwa Wananchi wa Kalenga ni lazima uendelee kudumishwa,Kitendo cha kukaribisha wapinzani kwenye jimbo hili ni sawa na kukaribisha Vurugu kwasababu Wapinzani hasa Chadema katika Taifa hili hawana rekodi nzuri ya kudumisha amani kwenye maneo wanayoongoza. Kubwa zaidi Mh:Mwigulu Nchemba ameendelea kuwaomba Wanakalenga kufanya Kampeni za Ustaarabu,Kampeni za Amani na Utulivu.Kwa MwanaCCM kufanya Vurugu sio Jambo jema,bali tutumie Amani tuliyonayo kuwaelimisha hata wenzetu wa Upinzani kufanya siasa za kistaarabu,Waache michezo ya Kusababisha Vifo kwa Wananchi wasio na hatia yoyote ile.Siasa safi ni zile za Kupambanisha Sera na Uwezo wa Kujenga hoja majukwaani.
Hivyo tar.16/03/2014 Wanakalenga Wote wanajitokeze Kupiga Kura na Kumchagua Mgombea wa CCM Kijana Godfrey William Mgimwa kwa maendeleo ya Wote Wanakalenga.
1970810_673145652747509_662874180_n.jpg

Kijana huyu ameamua kurudisha Kadi ya Chadema baada ya Somo zuri Kutoka kwa Mh:Mwigulu Nchemba kwenye Mkutano wa Ufunguzi wa Kampeni Jimbo la Kalenga.
1975053_673145836080824_1402178756_n.jpg
1920468_673145896080818_1234731803_n.jpg

Naibu Katibu Mkuu CCM_Bara Mh:Mwigulu Nchemba akimnadi Mgombea wa Ubunge Jimbo la Kalenga Ndugu Godfrey Mgimwa hii leo kwenye Ufunguzi wa Kampeni Jimbo la kalenga.Uchaguzi unategemewa Kufanyika tar.16/03/2014.

Picha zote na Habari kwanza Blog
 
Haya asiye na Mwana ..... Mafuba nje nje leo -- boda boda mpo??? Meli hiyo!! pakueni msepe!!
 
Ni live Kutoka Kalenga Alhamis ya 27/02/2014 CCM wanafanya Ufunguzi/uzinduzi wa Kampeni.Watu wanazidi Kumininika hapa Viwanja Vya Kalenga waliovalia Nguo za CCM na wale Wananchi waliopigilia Mavazi yao ya kawaida kabisa.
Komrade Mwigulu lameck Nchemba ndiye anayeongoza Ufunguzi wa Kampeni hizi hapa Kalenga,Hakika Godfrey Mgimwa Ushindi Upo mikononi Mwake.
Picha zinawajia hivi Punde za nmana Uzinduzi unavyoendelea hapa Kalenga,CCM wamefunika haijawahi kutokea.
Hiyo live iko wapi?? Unajua maana ya live au unarafuta bk7 Za Lumumba??
 
Ni live Kutoka Kalenga Alhamis ya 27/02/2014 CCM wanafanya Ufunguzi/uzinduzi wa Kampeni.Watu wanazidi Kumininika hapa Viwanja Vya Kalenga waliovalia Nguo za CCM na wale Wananchi waliopigilia Mavazi yao ya kawaida kabisa.
Komrade Mwigulu lameck Nchemba ndiye anayeongoza Ufunguzi wa Kampeni hizi hapa Kalenga,Hakika Godfrey Mgimwa Ushindi Upo mikononi Mwake.
Picha zinawajia hivi Punde za nmana Uzinduzi unavyoendelea hapa Kalenga,CCM wamefunika haijawahi kutokea.
mwongo wewe Mwigulu mwenyewe bado kajikunja na m.kiti mkoa,weka picha
 
Mkimaliza kuhutubia hao mliowasomba kwa maroli mwende vijijini mkahutubie watoto wa shule maana Kalenga wameshamkataa Mzungu mweusi na Mwana Mfalme!
 
...katika ufisadi kama richmond,epa,ujangili,uharamia,uwizi wa pesa za umma,upendeleo kwa watoto , familia zao,jamaa zao,ukwepaji kodi....mfano katika wilaya nitokako ya rorya ccm ndo wameshika wanaiba mpaka wanasahau fedha walizonazo.....fedha za vijana,hakina mama,miradi yote ndani...kalenga kama rorya iko hivyo hivyo hawana cha maana zaidi ya gonjera ya kila mwaka maji,umeme sijui na nini..............tubadilike huyo mwigulu ananufaika ndio maana amepelekwa hazina kupitisha pesa za uwizi........hana kitu na siku moja tutawauliza yote hayo...tuko tayari...serikali 3 must,tume uhuru ya uchaguzi must,huru wa mahakama must.uwazi na uwajibikaji must...hata kwa nguvu tutadai...muda wa kubebeleza umekwisha kupita.....wenye maskio na wasikie.
 
Narudia tena cdm kamwe hawatashinda chaguzi ndogo yoyote mkoa wa iringa mpaka msigwa anaondoka 2015, hata wabunge wao wote wawe mawakala haitatokea.
 
Back
Top Bottom