CCM Yakwama kuzindua Kampeni Kalenga leo

CCM Yakwama kuzindua Kampeni Kalenga leo

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
Katika hali ya kushangaza chama cha CCM kimeshindwa kuzindua kampeni zake katika jimbo la Kalenga leo kama walivyotangaza awali.

Badala yake wamesema uzinduzi utafanyika siku nyingine itakayotangazwa.

Inadaiwa mbali na sababu nyingine mojawapo ni kutokana na mgombea wake kutokukubalika jimboni humo.Mgombea huyo wa CCM Godfrey Mgimwa alikuwa akiishi Uingereza na ameoa mke wake Mzungu raia wa huko huko.Pia wananchi wa Kalenga wanadai walimfahamu siku ya mazishi ya baba yake.

Inawezekana pia Ahirisho hilo linatokana na Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa kuzindua kwa kishindo kikubwa kampeni za chama chake hapo jana Jumamosi huku akisindikizwa na Chief wa Kabila la Wahehe Abdu Sapi Mkwawa.
 
Last edited by a moderator:
Wanatafuta mtu mwenye Jina la Mkwawa eti naye apande kwenye jukwaa Lao ili kupinga kauli ya Chifu halali wa jana Sappi ......mwaka huu tunaona mengi......
 
Godfrey analaana ya baba yake!!
Baba yake kafa kifo cha kutatanisha

Laana haitomuacha, baba yake kaitwa mzigo, watu hao hao Kijana God anaungana nao. (Kajitakia laana mwenyewe)
 
molemo,mbona taarifa haina chanzo wala haijakamilika kuweza kukaa kwenye hili jukwaa letu pendwa au zile pesa ulizokula za m4c bado zinakutia uchizi kula fedha za walala hoi maskin wa nchi hii hutakaa salama.
 
Godfrey analaana ya baba yake!!
Baba yake kafa kifo cha kutatanisha

Laana haitomuacha, baba yake kaitwa mzigo, watu hao hao Kijana God anaungana nao. (Kajitakia laana mwenyewe)

kuitwa mzigo na laana wapi na wapi?
 
molemo,mbona taarifa haina chanzo wala haijakamilika kuweza kukaa kwenye hili jukwaa letu pendwa au zile pesa ulizokula za m4c bado zinakutia uchizi kula fedha za walala hoi maskin wa nchi hii hutakaa salama.
Mkuu ulitaka na picha, mbona taarifa inajitosheleza, ni kwamba nyinyiem mnaogopa kuanza kampeni kwa kuwa dogo hakubaliki, labda mtafanya kampeni za kitanda kwa kitanda, na hizi anazipenda sana Mwigulu Nchemba
 
Eeh tuliwaambia lakini kwamba Kalenga na watu wake ni wale wale aina ya wataka mabadiliko, wasiotaka unyonyaji na unyanyasaji ndio
maana jana sapoti kubwa ilionekana kwenye uzinduzi wa kampeni za CHADEMA. Wanaamini CHADEMA ndiye chama chenye majibu ya matatizo yao

kiukweli Mgimwa Jr ana wakati mgumu sana mbele ya wanakalenga, hauziki, hakubaliki.

Grace Tendega mwanakalenga wa kweli songa mbele, mkombozi wa kweli wa wanakalenga
 
kuipigania ccm ni lazima uwe na moyo wa CHUMA ! Maana haikubaliki bali inalindwa na madaraka tu !
 
molemo,mbona taarifa haina chanzo wala haijakamilika kuweza kukaa kwenye hili jukwaa letu pendwa au zile pesa ulizokula za m4c bado zinakutia uchizi kula fedha za walala hoi maskin wa nchi hii hutakaa salama.

unataka picha?
 
Mkuu ulitaka na picha, mbona taarifa inajitosheleza, ni kwamba nyinyiem mnaogopa kuanza kampeni kwa kuwa dogo hakubaliki, labda mtafanya kampeni za kitanda kwa kitanda, na hizi anazipenda sana Mwigulu Nchemba

mapema
 
Hii ya CCM kuhairisha msifanye kubeza na kujitadutia sababu za kujipa moyo. Nachojua CCM huwa hawashindwi kirahisi hivyo. Nashauri muendeleze kampeni zenu kwa umakini na kuto kubweteka.
 
Back
Top Bottom