CCM yafunika Mpanda

CCM yafunika Mpanda

huyo mama aloshika bango la kaki inaonekana kabisa amelazimishwa kuja, tena inaonyesha hajala kabisa, na kama sijakosea bango alilobeba liliandaliwa na NAPE, ule muandiko wa NAPE kabisaaaaa.... huyo mama hata kusoma hajui.
 
jamani tuweni wawazi, hilo bango kaandika huyo mama kweli????
 
Hii ni style yao katika majimbo ya CHADEMA....! Hata kipindi cha uchaguzi JK alifunika kule Karatu (kwa mujibu wa picha na taarifa zao), lakini manufaa yako wapi? .... ! Ewe Great Thinker, fikiria hili, lakini changanya na zako....!
 
jamani mnyonge mnyongeni haki yake mpeni!!Acheni ushabiki usiokuwa na maana kuna picha za cdm zina idadi ndogo za waandamanaji vilevile,hii ni sawa na msemo wa KUNYA ANYE KUKU,AKINYA BATA ANAHARISHA !!LOL Tubishane kwa hoja jamani sio picha au nani alianza kufanya nini???

CCM yafunika Mpanda!


Bwana Achebe tufanye hivi,
Kweli ccm imefunika, na walioudhuria ni watu mamilion zaidi sio hao elfu tu!

Je, kwa hilo ndio kuwaambia nini watz?

Ambao ndio walewale wamekuwa wakikiamini hiki chama kwa miaka 50 sasa?

Cameon Achebe, tusitoke kwenye hoja za msingi!

Hoja za msingi sio ccm kujaza watu kwenye mikutano kuliko chama kingine,

Hoja za msingi sio umaarufu wa ccm upoje kwa wananchi.

Hoja kuu ya msingi taifa lipo wapi baada ya miaka 50 ya "uhuru"... vipi mkuhusu muelekeo wa taifa upo? ni wapi?

Haya maswali yanajibiwa kwenye hiyo mikutano ya Nape na wenzake?

Kuna manufaa ya kufunika kama maswali bado ni mabichi mno mbele ya umma uliochoka hivyo?



Sagwa kwani tunabishana hapa?
Hoja za ccm na Nape kwenye majibu hayo ni zipi?
 
Wao hawa hatarishi amani ya nchni?!

Nimependa sana hili bango la Nape, huu ni Ujumbe tosha kuwa CCM imekubali kuwa wanao mafisadi na hawata wafukuza kama walivyotaka kutudanganya!yaani mafisadi wanao na sehemu yao milele maana wao wanaamini wanaweza kuwepo chama chochote!

Kazi kweni watanzania habari mmeipata
attachment.php

Hawa watu walioandamana kwa kupewa kofia, t-shirt na mshiko kidogo ni wakuhurumia. Tungepata picha za huyu mama aliyeshika bango akiwa kwake tungemuhurumia zaidi. Sifahamu unahitaji uwe mjinga kiasi gani kuamini kwamba umaskini hauwezi kuondolewa na uongozi uliopo umeshashindwa kwenye hilo
 
Hao ndio maelfu jamani watu hata 100 kufika ni bahati kwan kama wajumbe wa CCM ni zaidi ya 200 ina maanisha kuwa hao ni wajumbe tu wa CCM na hakuna mwananchi hata mmoja humo na kama wamo basi hawafiki 50,,, pole sana NNAPE maana huu ndio mwisho wako kujiua kisiasa,,,
 
Hao ndio maelfu jamani watu hata 100 kufika ni bahati kwan kama wajumbe wa CCM ni zaidi ya 200 ina maanisha kuwa hao ni wajumbe tu wa CCM na hakuna mwananchi hata mmoja humo na kama wamo basi hawafiki 50,,, pole sana NNAPE maana huu ndio mwisho wako kujiua kisiasa,,,
Kuna mtu kasema wao 133 tu. Na wote ni ten cell leaders wa ccm.
 
Jamani, mbona ni KIJANI tu? Mbona hawana shangwe? Mbona wananchi wa pembeni kwao hawana time nao hata kuonesha alama ya Dolegumba?

Mungu wangu, CCM kwa mtindo huu hawafiki 2015.
 
'ccm yafunika mpanda'.Kichwa cha habari ni tofauti kabisa na picha inavyoonesha,Ila Kama watu hao wachache na jezi zao kwa ccm ni kufunika basi ccm inazidi kwenda na maji.Ni kwa nini wavae sare wote?Lazima wametembezewa chochote hawa watanzania ili wahudhurie na jezi wakapewa.Ktk mikutano ya ccm wengi wanaenda kwa sababu ya kupewa (kudanganywa)kanga,kofia,tishirt nk.

Walisahau fomular hii, labda Nape pesa zote anakula mwenyewe agawi kwa wazee wa mipango.

CCm2010.jpg
 
HAO NI KAMA WATU 190 HIVI UKITOA VIONGOZI WA CCM WILAYA NA UKITOA WAKINA NAPE NA MADREVA WAO MAKE HAPO HATA DREVA WA NAPE YUKO KWENYE HAYO MANADAMANO NA WALIO SALIA NI MABALOZI WA NYUMBA KUMIKUMI.
SUMRY ALITOA MALORO KUWA BEBA ILI KUFUNIKA AJARI YA BASI LAKE KULE MBEYA.
Na hizo tsheti sio mpya ni za kampeni za mwaka jana nyie hamjui ndo nguo za kutokea?
 
Hao wakina mama wataandikaje mabango wakati hata shule hawajaenda? Huo ni mwandiko wa katibu wa ccm wilaya ya mpanda.
 
umeshika madaraka halafu unatafuta kufunuka kwenye mikutano?
ndicho wananchi wanachotarajia?kila siku upokwenye kampeni ni lini utaanza kutekeleza ahadi?
 
KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Katibu wa uchumi na fedha Mwigulu Nchemba wameongoza maandamano leo kutoka ofisi ya CCM wilaya ya Mpanda kwenda kwenye Uwanja wa Shaulili ambapo wamefanya mkutano mkubwa wa hadhara uliohudhuriwa na maelfu ya watu. Hakika wana Mpanda wameikubali sana CCM.

CCM-Mpanda.jpg

mabango-mpanda.jpg

umati-mpanda.jpg

Huyu mama aliyebeba bango la Ufisadi, Hakya Mungu anaitukana CCM kwa staili ya rejareja
CCM kazi mnayo
 
Haya magamba yanawatesa sana mama zetu. Sijui tutumie nini ili watuelewe maana wao na kanga tu basi wanayafuata magamba. Nadhani kuna haja ya viongozi wanawake wa CDM kulifanyia kazi jambo hili. Inabidi waende vijijini wakawaelimishe mama zetu maana bado hawajajua kuwa watu walishaachana na ccm muda mrefu lakini wao hawajui kama CCM ilishakufa.


Jamani Wanawake wa CDM mnamkakati gani na hawa mama zetu huko vijijini? Hatunashida na vijana wanafanya vizuri na ndo tunawaona wakiwa mstari wa mbele kwenye maandamano kila mahali yanapofanyika.

Kuna haja ya CDM kukaa chini na kulifikiria hili maana tukumbuke hawa tusipofanya hivyo tunaweza kujikuta 2015 na hawa wa mama bado wako magambani na wananawake ni wapiga kura wazuri sana na hata magamba yanajua na ndiyo mtaji wao mkubwa.

Ngonini umeongea jambo la maana sana, inabidi hawa kina mama ambao bado wamelala wapigwe semina elekezi ili wajitambue, maana wanachofanya sasa ni kufuata mkumbo tu, ukiwapa kanga ukawapigia taarab za TOT basi umewamaliza kabisa. Halima Mdee, Regia Mtema na wanawake wote wapenda maendeleo ndani ya cdm hebu anzeni mara moja kampeni ya kuelimisha wanawake wenzenu wa Tanzania hasa vijijini, ili by 2015 ccm wawe wamebaki peke yao.
 
Chrolophobia is the fear of green color, that's is exactly what I am suffering from in the mean time, so nimeacha kula mboga za majani (za kijani) pilipili nakula nyekundu tu, nyumbani kwangu nimeng'oa majani yote kwenye garden hivi sasa naweka paving blocks, michongoma nimeng'oa najenga ukuta. So please, kindly keep all green colors out of my sight.
 
Mafisadi mnao huko lakini kilasiku mnapiga kelele utafikiri hamuwajui! sasa hayo mabango mnamuonyesha nana mbona hamjawaandika majina hawa watu?

Wao hawa hatarishi amani ya nchni?!

Nimependa sana hili bango la Nape, huu ni Ujumbe tosha kuwa CCM imekubali kuwa wanao mafisadi na hawata wafukuza kama walivyotaka kutudanganya!yaani mafisadi wanao na sehemu yao milele maana wao wanaamini wanaweza kuwepo chama chochote!

Kazi kweni watanzania habari mmeipata
attachment.php
 
Back
Top Bottom