Nadhani wana haki ya kufanya hivyo, ninazipongeza juhudi zinazoonyeshwa na CCM kwa ujumla, ingawa ninathubutu kusema gharama ya juhudu hizi ni kubwa mno kupita wanavyofikiri sasa. Pia itachukua muda kuweza kuweka mambo sawa na kurudisha imani, si kwamba haiwezekani, ila kwa tabia za hao wasio na maadili ambao bado ndio wafadhili wakuu, na ukizingatia CCM haina vyanzo vya kutosha vya mapato zaidi ya tabia mbaya iliyojengwa ya kuombaomba kutokana na ufisadi uliofanywa kwa mali za CCM (kipindi hicho).
Kijana Nape bila kujali itikadi anaonyesha kuwa mwenye uwezo katika kujenga na kutoa hoja (tuache ushabiki) ila yuko isolated, maana akitoka yeye kwenye jukwaa anaefuata anaongea pumba so anadilute points na hoja zote alizokuwa anaziwekea mkazo Nape... kazi ipo sidhani kama moto huu utawafikisha popote
Mpanda sishangai maana ndio nyumbani kwa WM.
CHADEMA ongezeni nguvu, imarisheni vita vyenu kwa hoja kama mnavyofanya, ila wale wana CHADEMA ndani ya JF punguzeni siasa za matusi ili kuonyesha busara na upevu mlio nao maana hata kama una hoja ukitukana unaonekana uwezo wako wa kuwakilisha au kukazzia hoja ni mdogo unategemea zaidi jazba na ushabiki. Igeni mfano wa baadhi ya viongozi wenu