CCM yafunika Mpanda

Naona ccm mnajipa moyo na nyie




katibu wa nec, itikadi na uenezi, nape nnauye na katibu wa uchumi na fedha mwigulu nchemba wameongoza maandamano leo kutoka ofisi ya ccm wilaya ya mpanda kwenda kwenye uwanja wa shaulili ambapo wamefanya mkutano mkubwa wa hadhara uliohudhuriwa na maelfu ya watu. Hakika wana mpanda wameikubali sana ccm.

ccm-mpanda.jpg

mabango-mpanda.jpg

umati-mpanda.jpg
 
KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Katibu wa uchumi na fedha Mwigulu Nchemba wameongoza maandamano leo kutoka ofisi ya CCM wilaya ya Mpanda kwenda kwenye Uwanja wa Shaulili ambapo wamefanya mkutano mkubwa wa hadhara uliohudhuriwa na maelfu ya watu. Hakika wana Mpanda wameikubali sana CCM.

CCM yafunika Mpanda!


Bwana Achebe tufanye hivi,
Kweli ccm imefunika, na walioudhuria ni watu mamilion zaidi sio hao elfu tu!

Je, kwa hilo ndio kuwaambia nini watz?

Ambao ndio walewale wamekuwa wakikiamini hiki chama kwa miaka 50 sasa?

Cameon Achebe, tusitoke kwenye hoja za msingi!

Hoja za msingi sio ccm kujaza watu kwenye mikutano kuliko chama kingine,

Hoja za msingi sio umaarufu wa ccm upoje kwa wananchi.

Hoja kuu ya msingi taifa lipo wapi baada ya miaka 50 ya "uhuru"... vipi mkuhusu muelekeo wa taifa upo? ni wapi?

Haya maswali yanajibiwa kwenye hiyo mikutano ya Nape na wenzake?

Kuna manufaa ya kufunika kama maswali bado ni mabichi mno mbele ya umma uliochoka hivyo?
 
Chama tawala na maandamano ya nini huu ni wakati wa kushughulikia matatizo ya wananchi na kutekeleza ahadi badala ya kuandamana.

Khaa, unanshangaza, kwani kuwa chama tawala ndio usihamasishe? ikiwa serikalini hata wapinzani wapo, au wale kule bungeni, na wale madiwani wa upinzani sio serikali? ingawa wachache saana lakini wapo.
 
Waandamanaji wote ndani ya nguo za bure.
Cha ajabu mabango yao hayaeleweki yanataka nini hasa.
 
Duh! Siasa za bongo huwa zinanichekesha sana, si ni hwa walikuwa wanabeza maandamano juzi juzi tu?
 
Watu wa CCM wote wanahongwa t-shirt mazafanta, ujinga mtupu.....hamna jipya sasa hivi na wasiosoma na kujua madudu yenu ndio wanakuwa hivyo.
 
Asante sana kwa picha, JF tuna ukweli siku zote ndiyo maana huwa tuna dai source of information, Je, hawa watu walikuja hiyari ? hizi sare wamezinnunua kwa mapenzi ya dhati au wamepewa Hilo NAPE kawadanya Ufisadi ni idiology ya chama kama huamini fikiri nini chama kinamfanyia mwanachama Fisadi Hao wazee munao wasumhua kushika mabango hali maisha yao yanazidi kuwatesa MUNGU ATAWAHUKUMU
 
Hao watu hawazidi 150 pamoja na kuhamasishwa na t-shet na kofia. Maana si mbali sana naona gari nyuma yao kama mita 20 tu. Haibu hiyo. Ccm wamebaki viongozi tu! Hakuna wanachama huo ndo ukwel! Hata mkikata mara 100000.
 
...kuna huyu mmama mwenye bango la ufisadi, kavaa tshirt yenye picha ya Pinda..ukimuangalia kwa makini utagundua kabisa alikua 'matingas'...pozi la uso wake linaelezea kabisa aina ya kilevi, kama sio aliamka na komoni, basi ni supu ya mawe kabisaaa...

USHAURI KWA NAPE....
..Next time jaribuni hata kuchakachua picha (mambo ya photoshop) at least muonekane mpo serious!!! Kwa idadi ya kuhesabu kama hii,chama kitasitisha hizo ziara uchwara, mtakosa posho!!
 
jamani mnyonge mnyongeni haki yake mpeni!!Acheni ushabiki usiokuwa na maana kuna picha za cdm zina idadi ndogo za waandamanaji vilevile,hii ni sawa na msemo wa KUNYA ANYE KUKU,AKINYA BATA ANAHARISHA !!LOL Tubishane kwa hoja jamani sio picha au nani alianza kufanya nini???
 
Sasa hapo anaeneza nini kama watu wanaomsikiliza ni wana CCM wenyewe? Au mpaka sasa hao wana CCM hawaijui CCM ni nini?
 
Chama tawala na maandamano ya nini huu ni wakati wa kushughulikia matatizo ya wananchi na kutekeleza ahadi badala ya kuandamana.

CCM vituko kweli, hawa si walisema maandamano ya CDM yanahatarisha amani? Wanachokikataza ndicho wanachokifanya. Hawa wanafanya maandalizi ya kuwa wapinzani.
 
Maandamano hayana tija na yanachochea vurugu, yanahatarisha amani na utulivu wa nchi. "John Chiligati"

Kinacho ni sononesha ni hawa ndugu zetu Chadema, wanafanya maandamano kuwahamasisha wananchi ili kuitoa serikali halali madarakani, naomba muwapuuze maana mchezo wao ni mauti yetu sote, wana uchu wa madaraka. "Jakaya Kikwete"

Natangaza kufuta maandamano ya chadema kutokana na taarifa za kiintelijensia ambazo zimeonyesha kutakuwa na uvunjifu wa amani na vurugu "Saidi Mwema"

Tumejivua gamba tunajenga upya mfumo wa chama chetu na kukirudisha kwa wakulima na wafanyakazi, Chadema wao wamekalia maandamano ya uchochezi na kuhatarisha amani, tunawapuuza na sasa ni muda CdM kucheza ngoma yetu na si sisi kucheza ngoma yao "Nape Mnauye"

Ukitafakari kwa makini hizi kauli utapata jibu moja tu. CDM ni tishio kwa CcM na bado wanaendelea kucheza Ngoma ya CdM.
 
Haijafunika na haitafunika hivi karibuni, Nape angemaliza ziara ndani ya miezi 3 kama wanafunika, lakini kwa ugumu aliouona/waliouona inabidi wafanye miaka 3 labda watabadili mioyo ya wadanganyika
 
'ccm yafunika mpanda'.Kichwa cha habari ni tofauti kabisa na picha inavyoonesha,Ila Kama watu hao wachache na jezi zao kwa ccm ni kufunika basi ccm inazidi kwenda na maji.Ni kwa nini wavae sare wote?Lazima wametembezewa chochote hawa watanzania ili wahudhurie na jezi wakapewa.Ktk mikutano ya ccm wengi wanaenda kwa sababu ya kupewa (kudanganywa)kanga,kofia,tishirt nk.
 
Hakika CDM ni dira ya taifa hili, CCM nao wameamua kufuata nyayo,ila aliyetangulia katangulia, CDM wakitanagaza maanadamano watu wanakuja wenyewe kwa maelfu, Magamba wao wanaokoteza wanachama wao waliojichokea na maisha na kuwapa T-shirt na kanga wanaambulia watu 200, aibu iliyoje hii kwa Magamba.
 
Back
Top Bottom