CCM yaendelea kukataliwa na wananchi IGUNGA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yaendelea kukataliwa na wananchi IGUNGA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by The Hyper, Feb 26, 2012.

 1. The Hyper

  The Hyper JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 890
  Likes Received: 263
  Trophy Points: 80
  Hakika CCM bado kinazidi kupoteza mvuto&kukataliwa na wananchi,mijini na hata vijijini.Leo trh 26.Feb.2012,kulikuwa na mkutano&sherehe ya CCM,mjini Igunga kwa madhumuni ya:-

  1.Kumpongeza D.P.Kafumu(mbunge wa Igunga kupitia tiketi ya CCM)kwa ushindi alioupata(ambao ni wa kuchakachua)
  na
  2.Kuwashukuru wananchi kwa kuichagua CCM na Kafumu katika uchaguzi mdogo uliofanyika 2011 Igunga.
  Mkutano&sherehe ilifanyikia katika uwanja wa,Sokoine jirani&jengo la ofisi za CCM.Muda ulikuwa ni kuanzia saa4 asubuhi hadi saa10 jioni.

  Mahudhurio;Watoto 80%(wengi wao nadhani walifika kwa dhamira ya kutaka kushiriki kuumega mkate ulioandaliwa na CCM),Wazee15%&Vijana 5%(Hawa ni wanachama,watu walio kodiwa&kusombwa na malori kutoka vijijini). Idadi kubwa ya wazee walikuwa hawajiwezi hata kutembea vyema(umri mkubwa&uchovu).

  Kwa ujumla hali ya Magamba ni mbaya sana Igunga,huku mbunge{Kafumu} akizidi kupata upinzani mkali kutoka kwa wananchi walio wengi.

  NAWASILISHA
   
 2. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  picha????????????????????????????
   
 3. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #3
  Feb 26, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Utakuwa chizi wewe picha ya nini sasa wakati maelezo yamejitosheleza?
   
 4. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #4
  Feb 26, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180

  [​IMG]
   
 5. The Hyper

  The Hyper JF-Expert Member

  #5
  Feb 26, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 890
  Likes Received: 263
  Trophy Points: 80
  Palalisote nisingeweza kuchukua picha,kwa kuhofia usalama wangu.Kumbuka Magamba wana hasira sana na vijana hapa Igunga,pia wanatutambua vyema kwa sura na itikadi zetu.Kwa upande wa pili kufika kwangu eneo lile ningeitwa msaliti,kwani vijana waliweka msimamo mapema wa kutokanyaga eneo hilo!
   
 6. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #6
  Feb 26, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  thibitisha kuwa hayo maelezo ni ya ukweli
   
 7. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #7
  Feb 26, 2012
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Usiku mwema Feedback.
   
 8. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #8
  Feb 26, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Kweli umeamua kumkomeshea kabisa jamaa
   
 9. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #9
  Feb 26, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  umesomeka
   
 10. M

  Molemo JF-Expert Member

  #10
  Feb 26, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Hongereni wana Igunga kwa msimamo wenu madhubuti
   
 11. Godlisten Masawe

  Godlisten Masawe Verified User

  #11
  Feb 26, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 739
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tumekukubali kamanda, pia asante kwa taharifa.
   
 12. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #12
  Feb 26, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Unajua watu wengine wanaudhi siku hizi umekuwa kama wimbo picha picha, wakiambiwa Mwigulu alifumaniwa wanadai eti picha hadi inakera.
   
 13. Somji Juma

  Somji Juma Verified User

  #13
  Feb 26, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,514
  Likes Received: 2,059
  Trophy Points: 280
  hahaha..sahv igunga tunawaongeza kwenye CWW(Chama Cha Wananchi Wasiotawalika)..ambamo tupo wananchi wa MBEYA,MWANZA,ARUSHA,SONGEA(tumewaongeza juz),IGUNGA..
   
 14. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #14
  Feb 26, 2012
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Tanzania ya kesho hii.

  [​IMG]
   
 15. Pendael laizer

  Pendael laizer JF-Expert Member

  #15
  Feb 26, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 961
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kweli ma.gamba watatoka magamba yao tu bila shaka.
   
 16. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #16
  Feb 26, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  well kama watu wanaendelea kuwa na mwamko kiasi hiko its good. real good. Mwl kashindye kwa maoni yangu asilale,,aendele na mikutano ya kuhamasisha watu watambue mabadiliko,that way yeye ama yeyote atakayesimama for cdm 2015 atashinda
   
 17. m

  mubi JF-Expert Member

  #17
  Feb 27, 2012
  Joined: Feb 3, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  kwa mtazamo wangu naona ni vizuri au itakuwa ni busara sana kushirikiana na Mbunge huyu aliyekwisha apishwa tayari. Sioni ubaya wowote kwa Dr. Kafumu kuwa mbunge wa Igunga.

  Dr Kafumu kwa taaluma yake ni vizuri kumback up kwa kumpatia maoni mbalimbali yanayohusu maendeleo ya jimbo la Igunga na taifa kwa ujumla. Tabora ni mkoa wenye madini mengi sana. je tukimwomba awakilishe bungeni hoja ambayo itakuwa na tija kwa wachimbaji wadogo wadogo wa madini kwa kufanya demonstrated examples hapo mkoani Tabora.

  Au kwa kumshwishi engalau basi hapo Igunga pawe na hata kiwanda kikubwa cha serikali cha kuprocess concerntrates za copper, gold,lead, iron, zinc, manganese, madini hayo yote yapatikana Tabora. au kumwomba awakilishe serikalini hoja ya kutengeneza maabara ya serikali ya kupima madini iwe hapo Igunga...

  Naandika haya nikijua kabisa Dr. Kafumu amesomea haya mambo. Naomba ndugu zangu tushirikiane naye ili tuweze kupata kazi za kufanya , watu wengi wako idle, hawajui wakiamka waende wapi, wafanye nini. Lakini kukiwa na vitu kama hivyo nilivyotaja , maabara za madini, kiwanda cha kutengeneza concentrates, ajira zitaongezeka.

  Au hata kumtuma awakilishe taifani ya kwamba wawekezaji wa adini wafanye kuprocess tu, wachimbaji wawe wazawa na godown ziwe za serikali.......n.k... fikiria faida itakayopatikana Igunga kwa njia ninayojaribu kuwaeleza tushirikiane na Mbunge wetu, ukilinganisha na kumsusia mikutano yake.
   
 18. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #18
  Feb 27, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  hapa angekuwa Narubongo ameleta habari kama hii kuhusu cdm sasa hivi kungekuwa kumejaa kila aina ya matusi na kabehi lkn kwa kuwa ameleta kada wa cdm basi ni habari ya ukweli
   
 19. B

  BABU IDDI New Member

  #19
  Feb 27, 2012
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sio tu igunga hata huku kwetu temeke mambo yameshaanza, maana kila mtaa wananchi wa lika zote wanajadili mambo ya siasa huku wakikituhumu chama cha mapinduzi kushindwa kuongoza nchi
   
 20. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #20
  Feb 27, 2012
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Dr. Dalali Peter Kafumu ni mtu makini na wanaomfahamu watathibitisha hili. Sina shaka na utendaji kazi wake. Na kwa wasifu huo ndiyo maana watu wa Igunga walimchagua kwenye uchaguzi ule mdogo mbali na jitihada za baadhi ya vyama kutumia pesa nyingi sana kununua kura.

  Unaposema watu walikuwa katika proportions ulizozisema hivi unakuwa umepimaje?
   
Loading...