Tetesi: CCM wanaoutamani urais 2025 Wakinyimwa kugombea kutimkia upinzani na kujaza fomu za kugombea Urais

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,823
21,427
Kuna wimbi limeanza kujinadi kuchukua fomu ya kugombea Urais kupitia CCM na kundi hilo linakubalika.

Iwapo fomu ya kugombea Urais kupitia CCM itatolewa fomu moja ni wazi kuwa wagombea hao wataamua kuchukua fomu za kugombea urais kupitia upande wa pili.

Wananchi walio wengi wamekumbwa na taharuki ya kupanda kwa maisha kupita kiasi ambapo wanatarajia kufanya mabadiliko ya kiuongozi 2025.

Pia kuna kila dalili wabunge wengi wa ccm kukutana ha upinzani mkubwa ndani na nje ya CCM kwani wameshindwa kutafsiri au kuelezea hali ngumu ya maisha iliyopo majimboni mwao.

Baadhi ya wananchi mfano Jimbo la monduli wananchi wanapata mlo mmoja kwa siku na hakuna msemaji wa ccm amefika kujionea au kuwafariji wananchi hao
 
2025 fomu ni Moja tu
Naunga mkono hoja;

Enyi wana CCM wenzangu kamuulize Mzee Membe kama alivyohamia ACT alihutubia hata mkutano mmoja kama mgombea Urais.

Ewe mwana CCM nakushauri usijisumbue kuutafuta Urais, fuata utaratibu na utamaduni wetu ndani ya chama - mwenyekiti wetu lazima ale 10 ya kwake kuanzia 2025 maana hii ya sasa ni ya kikatiba tu, baada ya hapo ndipo tutaangalia nani anatufaa.

Msiwe na wasiwasi Tanzania ipo nchi ya himaya yetu, cha msingi ni utii na uvumilivu unaweza kukufikisha pazuri.
 
Muhimu mgombea wa upinzani atokee kanda ya Ziwa na mgombea wa ccm atokee Unguja.
Serikali 3 ndo itamaliza Mgogoro huo.

Angalizo; Mgombea urais Kutoka Visiwani hatochagulika bara.

Tupambanie KATIBA mpya itokanayo na Rasimu alosimamia Judge WARIOBA.
 
Kupeleka kura unguja ili hali unaishi kibondo hiyo ni habari mpya
Nafasi ya umakamo wa Rais inawatosha, Wana Rais Zanzibar, so haiwezekani tuwe na 2 presidents Kutoka Visiwani.

Sijawahi bet, bt ni Rahisi sana kubashiri kuwa aliyepo ni WA mpito.

HATOGOMBEA.
 
Kuna wimbi limeanza kujinadi kuchukua fomu ya kugombea Urais kupitia CCM na kundi hilo linakubalika...
Acha unaa. Unajipromote wewe mwenyewe wakati sis tuko na mama mpaka afie madarakani. Ametuajiri wote na hakuna aliyehitimu chuo kikuu mwenye akili ambaye Yuko mtaani bila kazi kwa sasa tofauti na jpm aliyetufanya manamba ndani ya nchi yetu kwa kutaka wote tuwe machinga
 
Kuna wimbi limeanza kujinadi kuchukua fomu ya kugombea Urais kupitia CCM na kundi hilo linakubalika.

Iwapo fomu ya kugombea Urais kupitia ccm itatolewa fomu moja ni wazi kuwa wagombea hao wataamua kuchukua fomu za kugombea urais kupitia upande wa pili.

Wananchi walio wengi wamekumbwa na taharuki ya kupanda kwa maisha kupita kiasi ambapo wanatarajia kufanya mabadiliko ya kiuongozi 2025.

Pia kuna kila dalili wabunge wengi wa ccm kukutana ha upinzani mkubwa ndani na nje ya ccm kwani wameshindwa kutafsiri au kuelezea hali ngumu ya maisha iliyopo majimboni mwao.

Baadhi ya wananchi mfano Jimbo la monduli wananchi wanapata mlo mmoja kwa siku na hakuna msemaji wa ccm amefika kujionea au kuwafariji wananchi hao
LABDA WAENDE CCM B ya ZITTO
 
Back
Top Bottom