Ccm wanakotupeleka siko | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ccm wanakotupeleka siko

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tikerra, Sep 29, 2008.

 1. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #1
  Sep 29, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Katika uchaguzi mdogo unao endelea hivi sasa Tarime kuna mengi ya kujifunza.La msingi hata hivyo ni hili la CCM kutumia nguvu nyingi kupita kiasi.Tumeshuhudia bwana Steven Wasira akitumia hata gari la serikali kufanyia kampeini na hatimaye kuonywa.Tumeshuhudia pia viongozi mbalimbali wa ngazi za juu kabisa wa CCM wakiongeza nguvu katika suala zima la kampeini.Na katika hali isiyo ya kawaida kabisa, hata Mtikila amekuwa 'drafted' kuongeza nguvu na hati za kupigia kura za CCM zinauzwa hovyo mitaani,ushahidi wa kijana yule aliyekamatwa mtaani ni dhahiri.Kwangu mimi hii ni ishara tosha kwamba CCM hawakubaliki tena na wako tayari kutumia mbinu zozote, hata chafu, kufanikisha adhma yao ya kupata kiti cha Tarime.Kama wangekuwa wanakubakika nguvu hizi zisingekuwa za lazima.Lakini ninalojiuliza mimi ni kwamba wanataka kumuongoza nani hasa,na wanachong'ang'nia ni nini?CCM wameshapoteza 'credibility'
  kwa wananchi na hawaaminiki tena kabisa.Ni vema wakalitambua hilo na wakapisha wengine ambao wana nia ya kweli ya kuwasaidia wananchi wa Tanzania.CCM wanakotupeleka siko,tunawaomba kwa nia njema kabisa waondoke.
   
 2. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #2
  Sep 29, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Si siri sisiemu ni chama mabavu sasa na kinatumia pesa yetu sisi wenyewe kujirudisha madarakani. Kumbe mmeshaona?
  Wanazidi ku inject umaskini ili mwisho wa siku wawanunue wapiga kura maskini.
  Hawakubariki hata kwa mtoto mdogo. Hata hivyo kila kitu kina mwisho.
  Iko siku mwsho utakuja. Nao watajuta.
  Mi nikisikia majina ya wakina wasira na wakina ngawaiya nasikia harufu mbaya maana hao walikuwa vibaraka wa sisisemu ndni ya upinzani na ndio waliofikisha upinzani hapo ulipo na sasa wanajifanya kuubeza. Na walaaniwe kwa ulafi wao.
   
Loading...