Elections 2010 Mzimu wa Chadema waitesa CCM

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Mzimu wa Chadema waitesa CCM
Tuesday, 01 February 2011 21:29

makamba%202.jpg
Katibu Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba

Fidelis Butahe na Neema Myovela

MZIMU wa Chadema umeonekana kuendelea kukitesa CCM kufuatia viongozi wakuu wa chama hicho kutumia muda mwingi kuzungumzia hofu dhidi ya chama hicho cha upinzani kuelekea katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, katika uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 34 ya chama hicho tawala.

Viongozi hao walionyesha wasiwasi wao dhidi ya Chadema wakati wakizungumza katika mkutano wa ufunguzi wa maadhimisho ya miaka 34 ya kuzaliwa kwa CCM, yaliyofanyika jana katika viwanja vya Biafra, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Viongozi hao ni pamoja na Rais Mstaafu wa Zanzibar ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CCM visiwani humo, Aman Abeid Karume, Katibu Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita pamoja na katibu wake, Kilumbe Ng’enda.

Hatua hiyo ya CCM kutumia muda mwingi kuzungumzia Chadema badala ya mafanikio ya uwepo wake nchini kwa miaka 34, unachukuliwa na wachunguzi wa masuala ya kisiasa kama dalili ya kuumizwa na wapinzani hao ambao walizoa majimbo 23 ya ubunge hasa katika miji mikubwa nchini.

Miongoni mwa majibo hayo ni Kawe na Ubungo jijini Dar es Salaam, Ilemela na Nyamagana jijini Mwanza, Arusha Mjini, Iringa Mjini, Moshi Mjini, Musoma Mjini na Mbeya Mjini.

Akizungumza katika mkutano huo, Karume alisema majimbo mawili yaliyochukuliwa na Chadema mkoani Dar es Salaam kuwa ni kama wamewakopeshwa.

“Wapizani walikamia sana uchaguzi hasa hapa Dar es Salaam, lakini matokeo ndio hayo kati ya majimbo nane tumechukua sita, hayo mawili tumewakopesha tu,”alisema Karume.

Katika mkutano huo, Karume alitumia dakika 16 kuzungumza na wananachi huku wanaCCM waliohuduria mkutano huo wakionekana wanyonge ambapo alisema kuwa viongozi wa CCM wanatakiwa kutembea kifua mbele kwa kuwa hata huo ushindi walioupata ni mkubwa na kwamba zipo njia nyingi za kukiondoa Chadema.

“Njia ni nyingi za kuwaondoa, kama hawataki kutoka basi tunawafuata huko huko, uwezo, sababu na nia ya kurejesha majimbo yetu tunao, wakae chonjo 2015 tunachukua wenyewe au sio Guninita,”alisema Karume akimuuliza Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam.

Alisema CCM ndio iliyoruhusu upinzani nchini mwaka 1992 ili wawasikilize wapinzani na kwamba kwa kuwa chama hicho kina uzoefu kinatakiwa kutumia uzoefu huo kuwasomesha wapinzani.

“Wana CCM wote wasisahau dhamana hiyo, tukiwachoka watatupeleka sehemu isiyo sahihi, mtambue kuwa kuna tofauti kubwa sana kati ya mwalimu na mwanafunzi,”alisema Karume na kuongeza:

“Msikubali kudanganywa na propaganda za wapinzani katika magazeti, CCM ina itikadi na sera zake, tujiandae na uchaguzi wa chama mwaka 2012 ili tuchague viongozi bora kwa ajili ya kushinda mwaka 2015”.

Awali kabla ya Karume kuzungumza, Katibu Mkuu wa CCM, Makamba alisema ushindi iliopata chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka 2010 sio mdogo.

Alisema kuwa ushindi wa Rais Jakaya Kikwete wa kura milioni 5 huku mpinzani wake, Dk Willibrod Slaa akiambulia kura milioni 2 sio wa kubeza na kwamba kwa matokeo hayo, Dk Slaa ni mpangaji ndani ya nyumba ya rais Kikwete.

“Dk Slaa atambue kuwa kashindwa, ndio kashindwa…., hivi mpangaji unaweza kumfungia mlango mwenye nyumba,”alihoji Makamba na kuwafanya wanachama wa chama hicho kuangua kicheko.

“Kikwete ndio baba mwenye nyumba bwana, hao wapinzani ni wapangaji tu, Guninita usisikitike sana, hata hao wabunge wa upinzani huko katika majimbo yao chumvi, binzari wanapata kutoka kwa CCM, hizo ni kelele za wapangaji tu, tujipange kwa uchaguzi mwingine,”alisema Makamba.

Alisema wanachotakiwa kufanya CCM ni kuzika tofauti zilizopo, kama kupanda kwa gharama za bei ya umeme na kuongeza kuwa upandaji wa gharama hizo ni jambo la kawaida.

“Hapa sio peponi, Mungu anasema kwa jasho lako utakula, ni wakati wa kuwapa nafasi mawaziri wetu wafanye kazi, tusifanye maandamano kama wao wasitutoe katika ajenda zetu, sisi tuna kazi za kufanya,”alisema Makamba.

Kwa msimamo huo, Makamba anapingana na Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), ambao wametishia kuitisha maandamano nchi nzima iwapo Serikali haitachukua hatua za haraka kutatua matatizo ambayo yanawakabili wananfunzi katika vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu nchini.

UVCCM katika siku za karibini wamekuwa wakitoa matamshi makali dhidi ya viongozi wa chama chao na Serikali, hali ambayo inaashiria kuwepo kwa mgawanyiko ndani ya chama hicho.

Kwa uapnde wake akitoa salamu za CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Katibu wa chama hicho mkoani humo, Kilumbe Ng’enda alisema kuwa dharau ndio zimekiponza chama hicho na kwamba zimesababisha baadhi ya majimbo washinde wabunge wa upinzani ambao hawana sifa.

“Majimbo tuliyoyapoteza tutayarudisha, tulidharau siasa zao za chuki, ushabiki, upandikizi na uchochezi, lakini ndio zilizotuponza, tumevumilia mengi, lakini tukajikuta tumepoteza majimbo kwa propaganda na uchochezi wa wapinzani, "alisema Ng’enda.

Alisema kuwa wanachama wa CCM itafikia wakati watachoka na siasa zinazofanywa na wapinzani na kwamba wanaweza kufikia wakati wakachukua hatua.

“Ukicheka na nyani utavuna mabua, umefikia wakati wa kuchukua hatua, yaliyotokea mkoani Arusha ni uchochezi na ushabiki tu, ni mambo ambayo yanaweza kuleta vurugu na amani kuwa mashakani,” alisema Ng’enda.

Alifafanua kwamba tabia ya baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani kuwachochea vijana kufanya vurugu kutalipeleka taifa katika hatua mbaya.

Akizungumza kwa ukali alisema, “Wana CCM wa Dar es Salaam tunasema hivi, ‘tumechoka’, uvumilivu unatosha, Serikali isimame kama Serikali kwa sababu hivi sasa uchaguzi umekwisha”.

Kuhusu katiba mpya, Ng’enda alisema mapendekezo yaliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete yanatakiwa kufuatwa na wananchi.

“Asiye na hoja ya katiba akae pembeni, wapo wanaozungumzia suala la katiba ili wapate umaarufu tu, tufuate yale yaliyozungumzwa na Rais ili tuweze kufikia muafaka ulio bora,”alisema.

Kauli ya Ng’enda iliungwa mkono na Guninita ambaye alisema kuwa yaliyozungumzwa na Katibu wake ndio kauli ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam.

“Kazi yangu kubwa ilikuwa kumkaribisha Katibu wa CCM, lakini acha niseme machache, Dar es Salaam waliojiandikisha kupiga kura ni watu 2.4 milioni, lakini waliopiga kura ni watu 700,000 tu, hili si tatizo la CCM bali ni jukumu letu sote,”alisema Guninita.

Huku akizungumza kwa upole, Guninita alifafanua kwamba wanachama wa CCM hawatakiwi kuwa na huzuni yoyote kwa kuwa kati ya majimbo nane ya jijini humo ni mawili tu ndio yaliyokwenda kwa wapinzani .

“Ubunge tumepoteza majimbo mawili kati ya nane, Kata tumepoteza 16 tu kati ya 90, lakini mkumbuke kuwa katika uchaguzi wa mwaka 1995 Dar es Salaam tulipoteza majimbo matatu na tukafanikiwa kuyarejesha tena kwetu,” alisema Guninita. Hata hivyo, wakati huo Guninita alikuwa kiongozi wa Chadema.

Huku akizungumza kwa jazba, Guninita alisema kuwa hata Uchaguzi Mkuu ukirudiwa kesho (leo) CCM ina uhakika wa kuyachukua majimbo iliyoyapoteza kwa kuwa imeshajua kosa lake.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites


Last Updated on Tuesday, 01 February 2011 22:20 Comments

1234



+1 #47 emanuel mikomangwa 2011-02-02 17:44 sasa mbona Amani karume anashindwa kuona aibu ya uongo anaoueneza hapa!Zaanzibar imebidi yeye mwenyewe awakubali wapinzani na kuwakaribisha Sisiemi yake hiyo ili wawalambishe asali Kama kweli wapinzani hawawezi kuongoza Zanzibar kwa nini wameunda Serikali.Kaa Zanzibar hukoo usituharibie Tanganyika yetu haikuhusu.Wewe ndo umekuwa bingwa wa kuvuruga katiba ya CCmafisadi na kujenga Serikali ya Zanzibar ambayo haipo katika Katiba halafu unasema u[NENO BAYA] gani tena hapa!Wakati wa Siasa za vijiweni umepita Watanzania wa leo wana akili na ufahamu zaidi ya mnavyojidangany a.Yale ya Misri si mbali yanakuja tutawalazimisha kwa nguvu ya UMMA mtuondokee wezi wakubwa!
Quote









+1 #46 Grace 2011-02-02 17:22 Mwananchi si gazeti la wapinzani ni gazeti linaloruhusu uhuru wa mawazo ni ndiyo kiini cha maendeleo ya nchi yoyote. Mbona gazeti letu la serikali (Daily News) walipoona kura za maoni zinaangukia upinzani walifuta sehemu ya kura za maoni? Juu ya udini kama chama chochote ni cha kidini hakisajiliwi Tanzania, kama kimesajiliwa na serikali ya CCM inayoruhusu vyama kusajiliwa hii ni sababu tosha kuwatosha madarakani maana hawatendi kwa umakini!! Digree ya uchumi wa JK tunaiona inavyofanya kazi ajira zimeongezeka, bei za vitu zimeshuka, wafanyakazi hawagomi, wanafunzi mashuleni na hasa vyuo vikuu wanapata posho zao kwa wakati, na wewe unayeandika umejaza mapesa mfukoni kwa sera ya UDP.... Kama unaona hivyo kwa Tanzania na wewe hustahili kujadili masuala ya uchumi maana we ni mshabiki tu.
Juu ya Teolojia, kama ni degree ya Teolojia kwa taarifa yako degree ya namna hiyo si UKATOLIKI bali hata mwislamu anaruhusiwa kuipata. Hali kadhalika Mwanglikana, Mluteri, Myahudi na asiye na dini. Kasome ukitaka utapata. Ukijipachika au wakikupachika degree hiyo kwa heshima siku ukiwaudhi wanakunyang'anya (kamuulize Mugabe) ndo utajua tofauti ya degree za kweli na za heshima.
Tatizo la CCM ni ufisadi na kutojali wananchi wenzetu na hii msiporekebisha pigeni propaganda lazima mtakiona tu!!! Ushauri wa bure nduguzanguni... CCM HOYEE!

Quote









+1 #45 mateso 2011-02-02 17:17 Ninadhani ukiisoma hii habari utajua ya kuwa CCM imekwisha habari yake (imefilisika) ni majungu tu, hakuna ambaye anamawazo ya kuweza kushawishi mtu aendelee kukiamini hiki chama cha sisiem. Na wala hawana kitu kipya cha kuweza kueleza wananchi.

Wote walioongea wanajipa matumaini na ndoto ambazo zilishatoweka siku nyingi na hasa kwa wanasisiem wenyewe. Yaani badala ya kuongea mambo ya kutokomeza mararadhi, u[NENO BAYA] na kuleta uongozi bora katika jamii wanatuletea habari za tathimini za uchaguzi. Hawakuweza kujiuliza kwa nini walinuna na kusikiliza kwa masikitiko. Wajiuliza je wanayowatendea ni sahihi katika maisha haya yalivyokuwa magumu?


Watoa comment kama mlivyosema kilichopo ni kuingia vijijini hili ninawaunga mkono iamshwe sangara ipite kijiji kwa kijiji. Lengo ni kujua matatizo yao na kuongea nao moja kwa moja ili kujua kama haya mafungu yanayotengwa kama yanatumika inavyotakiwa. Kama hayatumika inavyotakiwa msisite kuhoji na ndio maana ya upinzani. Hii sangara ikiamka tunajua wengi watatimuliwa huko kwenye Manispaa na Halmashauri kama hawatalindana.

Tuwaache hao wanaong'ang'ania PhD za Dr Slaa. Dr Slaa wewe endelea kuwatimulia vumbi tu.

Quote









+1 #44 Amka Tanzania 2011-02-02 16:31 Wewe Kasuku hebu tuambie chama chenye sifa ya kushika Dola kinakuwaje maana hata hiyo CCM ilanzishwa na watu na inaongozwa na watu.Haikuteremshwa kutoka mbinguni wala hakiongozwi na malaika.

Wewe Amina Juma, Kikwete ana shahada moja.Hiyo ya Udaktari ni shahada ya kupewa. Ni shahada ya heshima. Inakupasa kuwa muangalifu unapochangia hoja usiropoke.

Quote









+1 #43 mwanamaendeleo 2011-02-02 15:59 ni kweli tunapaswa kuwaelimisha wa vijijini,nimeku mbuka tulikuwa tunaenda kutoa elimu ya utunzaji wa vyanzo vyamaji Mbulu wanafunzi walikuwa kwenye maafali ya darasa la saba wakatukaribisha walikuwa wanaimba zile nyimbo za aaaa,ccm yajenga nchi,lakini aliyewafundisha ni mwalimu ambaye mshahara wake kuupata ni taabu naishia kuwa na nidhamu ya woga kuwa ni ccm bado inajenga nchi au inabomoa so ni wajibu wetu sote kuwaelimisha watu wanaowaamini ndo wanaosababisha mpka leo hawana huduma ya maji,umeme,afya ,elimu duni,miundo mbinu kama barabara,wakish ajua hilo watajua jinsi ya kumuwajibisha kiongozi kule Mtendaji kata ni mnyanyasaji kwani ndo anajifanya mungu mtu,kisa kutekeleza ilani zisizo na tija bali ni mzigo kwa mwananchi huku wachache wakineemeka na watoto wao kuajiriwa kwenye kampuni ambazo hisa nyingi ni za mafisadi.
mwenye akili na afahamu

Quote









0 #42 Amina Juma 2011-02-02 15:41 Quoting mpenda maendeleo:
huwa naangalia kwa haraka haraka tu wengi hawaungi mkono ccm kama hapa kati ya sms 16 tatu ndo wanaiunga ccm ujue hiyo ni proportion ya wananchi hata uraiani, wamebaki vijiji ndio hawajafunguka maana hawajui ulimwengu unaendaje ccm fanyeni utafiti wa haraka haraka tu mtajua kura mnazopata has za rais ni watu mbumbumbu. wenye uelewa hasa mijini hawawataki ng'o basi waboresheeni maisha hao wa vijiji maana ndo wanawachagua chama ya nyerere,bila nyerere nyie mngekwisha mapema mno.



Nimeipenda sana coment yako nahis ccm kama wanazisoma hizi coment watajiona kuwa wanamatatizo ila kuhusu vijijini umeniumiza kuwaita mambumbumbu, usiwaite hivyo inatupasa tuwa elimishe coz wao ndo wanao ichagua ccm afu ndo wanaoathirika nayo zaidi mfano shule zakata zilianzishwa kisiasa zaidi wakajaza majengo bilakuwa nanyezo na walimu wakutosha unakuta shule ina walimu 2, (sikuwa walimu hawapo ila maslah madogo wanaenda shule za prive) afu wanaosoma hizo shule wengi wao ni wakutoka vijijini ambao hawana uwezo wa kwenda shule nzuri, nahao hao wakienda kupiga kura utasikia ccm tu jamani ccm msiwatumie wenzenu coz uelewa wao mdogo fanyeni maendeleo huko vijijini basi mlipe hata fadhila kwao mana hao ndo wapenzi wenu ,inamana malipo yao ndo haya kweli!!!!!!!!!! !????????? TAFAKARI CHUKUA HATUA

Quote









+2 #41 mwanamaendeleo 2011-02-02 15:40 ni kweli Amina hujakosea hiki ni chama cha majungu mipasho na ujambazi,hawana na tija ni aibu kujisifu halafu kufananisha phd ya kupewa na kutafuta mwenyewe,yaliku wa ya zamani mvi kuitwa hekima yaani wamefilisika vibaya hadi kwenye hotuba
Quote









0 #40 Amina Juma 2011-02-02 15:25 Quoting mwanamaendeleo:
Quoting Kasuku:
mimi nataka niwaambie CHADEMA kwamba hawana sifa ya kushika dola na kamwe hilo halitotokea kwani Mwl. Nyerere alishatuachia usia kuwa vyama vya kidini tuvikae.

kweli wewe ndo hamnazo unashindwa kutofautisha chama cha siasa na taasisi ya dini,kwani walioanzisha propaganda za udini ni nani kama si ccm au hujui kuwa gazeti larostam azizi lilianza kwa kejeli kuwa Slaa anatafuta kura kwa wakatoliki na akanyamaziwa sababu ni mwenzenu na ndiyo maana mkanyamaza mkijua watz wooote ni wakuburuzwa haya sasa inawatafuna nyie wenyewe kwani chadema ni cha dini au dhehemu gani na ibada zao hufanyika wapii acha ushamba,na kwa taarifa yako manatafutwa mtumike kwa rushwa za t.shirt huku wenzenu wakijimilikisha rasilimali za nchi huku wewe ukipauka na rangi ya njano na kijani,na mahakama ya kadhi nani aliiweka katika ilani ya uchaguzikama mnajua Tz ni nchi isiyo na dini manapeleka mambo ya dini na udhehebu kwenye chombo cha kutungia sheria kama si ninyi kuwalaghai watu ili muwaibie kura zao,usiwe shabiki maandazi elewa unachosema na ukifanyie utafiti,mlianza oooh mageuzi ni vita,haya mmekuja udini,mmeona haifanyi kazi mnakuja kusema mmewakopesha majimbo yaani huko ni kuwadhalilisha waliopiga kura kwani walipiga kihalali hawamilikiwi na chama na m[NENO BAYA]ma mataadabishwa 2015 mkifikiri mtakaa hapo milele muulizeni Mubarak ana hali gani ili mjifunze yakiwafika

Quoting Kasuku:
Msagala usiwe mvivu wa kufikiri , huyo unaye mwita Doctor (SLAA), PhD yake ni ya mambo ya Theology (ukatoliki mtupu hapo), sasa watanzania kama taifa itawanufaisha nini, tunahitaji watu wenye elimu zinazohusiana na matatizo yetu kama Dk. Kikwete mwenye shahada ya UCHUMI.

Quoting Kasuku:
Msagala usiwe mvivu wa kufikiri , huyo unaye mwita Doctor (SLAA), PhD yake ni ya mambo ya Theology (ukatoliki mtupu hapo), sasa watanzania kama taifa itawanufaisha nini, tunahitaji watu wenye elimu zinazohusiana na matatizo yetu kama Dk. Kikwete mwenye shahada ya UCHUMI.

[quote name="Kasuku"]Msagala usiwe mvivu wa kufikiri , huyo unaye mwita Doctor (SLAA), PhD yake ni ya mambo ya Theology (ukatoliki mtupu hapo), sasa watanzania kama taifa itawanufaisha nini, tunahitaji watu wenye elimu zinazohusiana na matatizo yetu kama Dk. Kikwete mwenye shahada ya UCHUMI.[/quot

kweli wewe ni kasuku hivi unatua sifa za kasuku??????????? nikupayuka hivyo sishangai coment zako jamani tuangalie kurasa zingine zenye mambo yenyetija coz naona hawa viongozi wao waliamua kugeuza mkutano kama kuwa kikundi cha taarabu wanapasha wenzio amabao wanaendelea kujitengenezea kura kwakufanya mambo yenyemaendoleo kwa mwananchi maskin afu nawafuasi wao wanaendeleza mipasho kwenye coment zao hi nidalili ya kufilisika kama kweli watarudisha majimbo yao siwanyamaze tuone 2015, afuwamesema kuna njia nyingi za kurudisha kama nikuchakachua tutalinda kura zetu zote nchinzima, washamba wakubwa badili ya kufikiri nijinsikani mta rudisha heshima ya chama mnaleta mipasho

Quote









+1 #39 Amina Juma 2011-02-02 15:05 Quoting Athumani:
Quoting mwanamaendeleo:
Quoting Kasuku:
Msagala usiwe mvivu wa kufikiri , huyo unaye mwita Doctor (SLAA), PhD yake ni ya mambo ya Theology (ukatoliki mtupu hapo), sasa watanzania kama taifa itawanufaisha nini, tunahitaji watu wenye elimu zinazohusiana na matatizo yetu kama Dk. Kikwete mwenye shahada ya UCHUMI.

kasuku acha kuropoka kama huna vitu vya kusema,tembelea Karatu huduma ya maji ya hadi vijini na zote ni sababu ya Slaa,waliletaga propaganda kipindi cha nyuma huko sasa wamefyata midomo yao maana hakuna walichowasaidia hadi sasa Kaviwasu iliyoanzishwa na Mheshimiwa Slaa kupitia mradi wa maji Mbulu,sasa wewe unaanza kuhoji eti Taaluma yake ya Theolojia ni ukatoliki u[NENO BAYA] kabisa kama huyo mwenye shahada ya uchumi mbona anashindwa kudhibiti mfumuko wa bei maisha magumu kwa watu anaowaongoza acha uzembe kwenye kufanya analysis


we kasuku huyo kikwete wako hiyo Phd yake kasomea wapi? huna akili unaropoka tu hiyo phd ni yakupewa tu yule kichwa maji hana akili. alafu kumbuka huwezi ata siku moja kumfananisha slaa na kikwete kikwete ni mshamba flani tu!


Acha ushabiki waki[NENO BAYA] ambaounakusabab ishia maisha magumu shida zimekusonga unang'ang'ania ccm utazani uliachiwa radhi na babu yako ukihama utalaaniwa hiv huoni aibu kusema dr kikwete? kwanza nikilaza ana degree 1 tu nayenyewe alipita kwa kiwango ambacho hawezi kuendelea degree ya pili labda mpaka angesoma degree nyingine yoyote afauli, usitu[NENO BAYA]ze tunajua mengi hivyo huwezi linganisha uwezo wake na slaa hata siku moja hanalolote amebahatisha tu zali akatunukiwa huo udoctor, hvyo vituvingine tusimlaumu sana siyo ajabu hafanyimakusudi ila ndouwezo wake ulivyomtuma mie siko chama chochote nawapenda viongozi wote waadilifu kutoka vyama vyote hata ccm sitta, mwakyembe, magufuli nawakubali sana hivyo sinachuki na ccm ila Dr slaa angepewa hii nchi ndo angeiweza hi nhi isha haribika inatakiwa mtu mbunifu, muadilifu mzalendo na aliye serious siyo wakuchekacheka na watendaji wake japo watu wengi husems slaa anajasba! ila anajazba kwaviongozi wazembe na mafifadi hana jazba kwa wananchi kwanza anaongea nasi vizuri sana na kutupa maneno yenye matumaini, rais anatakiwa awe mkali kwa watendaji wake watamuheshimu,n a watimize wajibu wao kikowapi kikwete wenu asiye na jazba! nchi imeoza watendaji wake wote wamemwangusha mpaka anaonekana ovyo kabsaa hata watoto wanamzarau lait slaa angekuwa anajazba kwa wananchi tusingempenda hiv!!!!!!!!!!!

Quote









0 #38 Mugharuka 2011-02-02 14:55 Waliosema elimu ni ufunguo wa maisha hawajakosea,you can see the difference kati ya viongozi wa ccem na chadema,hao wazee wa ccem wamekosa upembuzi yakinifu,hawana constructive ideas,kwa kifupi wamefilisika,wa nabaki kupiga majungu tu angalia viongozi wenyewe akina makamba,tambwe hiza,guninita,h awa vilaza watupu unatarajia wawe na mawazo na mipango madhubuti ya kumuondoa mtanzania katika dimbwi la umasikini thubutu,tunatak a watu wenye uwezo wa kukaa chini kutafakari,kufa nya critical analysis kwa nini watanzania tuko hapa saizi,tunatakiw a kwenda wapi,what are the challenges and finally waje na problem solving strategies and the way forward sio mnabaki kujadili chadema,hayo sio matatizo halisi ya watanzania,jifu nzeni kwa wenzenu!!!!!
Quote









0 #37 Side 2011-02-02 14:04 Huyo anaejiita makamba simpendi K U M A M A M A Ke yani angejua ata iyo picha yake apo juu wangeitoa
Quote









0 #36 Athumani 2011-02-02 13:54 Quoting mwanamaendeleo:
Quoting Kasuku:
Msagala usiwe mvivu wa kufikiri , huyo unaye mwita Doctor (SLAA), PhD yake ni ya mambo ya Theology (ukatoliki mtupu hapo), sasa watanzania kama taifa itawanufaisha nini, tunahitaji watu wenye elimu zinazohusiana na matatizo yetu kama Dk. Kikwete mwenye shahada ya UCHUMI.

kasuku acha kuropoka kama huna vitu vya kusema,tembelea Karatu huduma ya maji ya hadi vijini na zote ni sababu ya Slaa,waliletaga propaganda kipindi cha nyuma huko sasa wamefyata midomo yao maana hakuna walichowasaidia hadi sasa Kaviwasu iliyoanzishwa na Mheshimiwa Slaa kupitia mradi wa maji Mbulu,sasa wewe unaanza kuhoji eti Taaluma yake ya Theolojia ni ukatoliki u[NENO BAYA] kabisa kama huyo mwenye shahada ya uchumi mbona anashindwa kudhibiti mfumuko wa bei maisha magumu kwa watu anaowaongoza acha uzembe kwenye kufanya analysis


we kasuku huyo kikwete wako hiyo Phd yake kasomea wapi? huna akili unaropoka tu hiyo phd ni yakupewa tu yule kichwa maji hana akili. alafu kumbuka huwezi ata siku moja kumfananisha slaa na kikwete kikwete ni mshamba flani tu!

Quote









0 #35 mwanamaendeleo 2011-02-02 13:40 Quoting Kasuku:
Msagala usiwe mvivu wa kufikiri , huyo unaye mwita Doctor (SLAA), PhD yake ni ya mambo ya Theology (ukatoliki mtupu hapo), sasa watanzania kama taifa itawanufaisha nini, tunahitaji watu wenye elimu zinazohusiana na matatizo yetu kama Dk. Kikwete mwenye shahada ya UCHUMI.

kasuku acha kuropoka kama huna vitu vya kusema,tembelea Karatu huduma ya maji ya hadi vijini na zote ni sababu ya Slaa,waliletaga propaganda kipindi cha nyuma huko sasa wamefyata midomo yao maana hakuna walichowasaidia hadi sasa Kaviwasu iliyoanzishwa na Mheshimiwa Slaa kupitia mradi wa maji Mbulu,sasa wewe unaanza kuhoji eti Taaluma yake ya Theolojia ni ukatoliki u[NENO BAYA] kabisa kama huyo mwenye shahada ya uchumi mbona anashindwa kudhibiti mfumuko wa bei maisha magumu kwa watu anaowaongoza acha uzembe kwenye kufanya analysis

Quote









0 #34 Mchungu wa Bongo 2011-02-02 13:34 Sasa mwaka 2010 mmefanya kila ufisadi lakini bado tumenyakua 23, sasa 2015 nyie ccm muende kuzimu tu, lazima anguko litakuwa kubwa si mnacheza na maisha ya Watanzania, Makamba always talks nosense, zero zero hata shule iliyotajwa jina lake zero zipo 314, sasa huyu naye ni mtu wa ku-argue naye...asomaye na afahamu
Quote









+1 #33 Mohamed Kingalu 2011-02-02 13:02 CCM Tunajiangusha wenyewe,kwa majungu na mizengwe isiyo na tija,chuki,mape nzi ya machoni si moyoni,eee jama tusipoangalia 2015 tutatwanga maji katika Kinu(TUJILEKEBI SHE JAMANI)
Quote







1234
Refresh comments list
 
Kinachoimaliza CCM siyo Chadema bali ni ufisadi ambayo ndiyo dhuluma kuu kwa wapigakura...........................
 
:clap2:CHADEMA OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! CCM KABURI LENU LI-WAZI, SUBIRINI KUZIKWA RASMI 2015:clap2:
 
Ni ajabu. Badala ya kufikiria namna ya kutekeleza ahadi na sera, tunaanza kuwaza namna ya kushinda 2015! Hii kali. Eti kuweka mikakati ya kushinda 2015! Eti tumewakopesha majimbo mawili! Kwa mwendo huu, usijeshangaa ukakosha tena 4 kuwa sita kwa DSM tu.
 
Mnaposema habari za kulikomboa Taifa kutoka huku tulikopelekwa kuwekwa Rehani na hawa SI SI EMUwenu mm siwaoni watu hawa kama ni raia wenzetu wa kitanzania naona some People kama ni wazamiaji ambao wameahidiwa hifadhi na hii serikali ya kishikaji,KIKUBWA WAKUU SI SUALA LA UDINI TUTOE MIJADALA SAHIHI NINI KIFANYIKE MAANA HATA WATOTO WA CHEKECHEA WANAJUA NCHI IMEWEKWA BONDI kwanza suala la udini lipo CCM coz CDM sijawahi kusikia wanaongelea udini zaidi ya kusema hali halisi ya maisha magumu tulonayo watanzania.Makamba ndo mwenye udini mkubwa sijui 2015 mtasema nn maana hamna option inabidi mrudi kanisani ili mpate Candidate mzuri mwenye kuleta changamoto katika hiyo duru.
 
Back
Top Bottom