Yericko Nyerere: Lowassa na Jakaya Kikwete ndio Maadui wakuu wa CCM sio CHADEMA [Majibu]

LUCAS KISIMIR

Member
Joined
Sep 11, 2012
Messages
29
Points
0

LUCAS KISIMIR

Member
Joined Sep 11, 2012
29 0
UFAFANUZI: Maelezo yaliyo katika maandishi ya rangi nyekundu ni yaYeriko Nyerere na maandishi ya rangi nyeusi ni mawazo yangu.

1.Lowassa na Jakaya Kikwete ndio Maadui wakuuwa ushindi wa CCM 2015 sio CHADEMA-YERIKO NYERERE. Pengine wanaCCM wanajua ama hawajui adui yao mkuu katikakilele cha kushika dola ya nchi hii tajiri huku wakaazi wake ni MAFUKARAtotoro.
Napenda kuchangia mawazo yangu kwenye hojaya Yeriko Nyerere kwa kujikita katika kichwa cha hoja yake kama kinavyojinadi. Naanzakwa kukanusha hoja isemayo; maadui wakuuwa CCM kwenye ushindi wa CCM 2015 ni Lowassa na Jakaya Kikwete. Sio kwelikwamba viongozi na makada hawa maarufu walioshiriki kwa hali na mali katikakujenga historia njema ya chama chetu wanaweza kuwa chanzo cha maanguko ya CCM.Hoja yenye kufikirika dhidi ya ushindi huo wa CCM 2015 ni kwamba tutaendelea kugawanakura na wapinzani kama kawaida, lakini uhakika wa CCM kushinda ni mkubwa nadhahiri.

Tunajiimarisha kwa kupalilia imani na mapenzi ya umma kwa CCM kwakuitekeleza Ilani ya Uchaguzi na kushughulikia kero zinazowasibu wananchi kwawakati na ufanisi.
IkiwaRais anapimwa kwa kigezo cha utekelezaji wa ilani na ahadi, katika awamu hii yanne, masuala mengi yamefanyika kwa ufanisi mkubwa tena ndani ya wakati. Raisangeshukuriwa na kupewa heshima stahiki na WaTanzania wenzake kama ile apewayona wazungu. Ufanisi wa JK, Mbowe alikiri kwa kauli yake bila kushawishiwa. Tatizola aina ya upinzani tulionao dhidi ya CCM ni chuki na wivu inayoimarishwa natamaa ya uongozi. Chuki imepandikizwa hadi kwenye rangi ya bendera na mavaziyetu.

Mahusiano yoyote ya wapinzani na rangi yoyote ya kijani yamedorora hataiwe kwenye mboga za majani! Taarifa zinazowasilishwa maadamu gamba la taarifani kijani na mtekelezaji na mwasilishaji ni mwanaCCM na au Serikali yake, hataiwe inajulisha idadi ya watu waliopewa maziwa, siagi na asali, haitasikilizwana hawataki kukubaliana, kutambua na wala kuuona ukweli huo. Wamekula yamini yaupofu. Rangi ya ganda (Cover) la taarifa ikiwa kijani, tayari wamekerwa (mfanomzuri-Tundu Lisu) na taarifa hiyo haisomwi labda iwe kama kwamba wanatafutahoja ya kizushi. Wamehitimu upofu katika kuona ukweli wa ufanisi wa CCM nakuziba fikra zao zisikubaliane na uhalisia na hawaishii hapo bali huwapotoshawananchi wenzao (Vipofu dhidi ya Ukweli-VDU). Miongoni mwao wapo vipofuwasiokubaliana na ukweli wowote na wapo wenye matongotongo ambao mara zinginehuzinduka na kukubaliana na ukweli.Wazalendowa kweli hutambua kiwango halisi cha ufanisi kupitia mchango wa Serikali yao katikamaendeleo ya nchi na kusema ukweli wao ikiwa yapo marekebisho ya upungufu. Nanikawafundisha wapinzani kuidharau nchi yao? Wakidharau mambo ya kwao watasifu yanani? Hawa wanatumika tu kirahisi-rahisi kupunguza fahari na kudhoofishautawala wa mwafrika.

Ndiyo maana wakienda ughaibuni wanaitangaza nchi yao kwakuidhalilisha ili wapewe vijisenti wakijifanya wakandarasi wenye uwezo wakufanya marekebisho ya kudhoofisha mifumo ya utawala. Kwatabia ya VDU, sio kwamba Kikwete hakuleta ufanisi katika nchi hii, bali nikipindi tu cha wenye tamaa ya kuongoza kwa kulaghai ndicho sasa. Nakirikabisa kwamba wapo maadui wengi wadogo wadogo dhidi ya CCM, lakini kama yupoadui mkubwa, ndiye anayefaa kutugharimu rasilimali na kipaumbele kumshughulikia.Katika hali ya kawaida, ikiwa unapambana na maadui wawili, mmoja ndani namwingine nje, shughulika na yule wa ndani kwanza kwani ni wa hatari zaidi.Ikumbukwe kwamba kati ya maadui wa ndani tunaowafahamu sisi, hao unaowatuhumu siosehemu na hawatadhuru ushindi wa CCM 2015 bali watachangia kwenye ushindi huo.

Maaduiwabaya wa ndani ni hawa ambao wamelewa ghilba za ughaibuni na wanataka kuingizaubia wa wazungu katika utawala wa nchi yetu. Hawa ni wa hatari zaidi na sijuiwanamwakilisha na kumsemea nani wanapoiaibisha na kuidhalilisha nchi yetuughaibuni!? Kimsingi,adui mkubwa wa CCM unatakiwa umjifunze nami nitajitolea kukufundisha ili umjuekweli. Huyu ni tofauti kabisa na ulichotaja kwa msingi wa mtazamo wako na sivema sana ukashambuliwa na wala kuhukumiwa kwa fikra yako tu, bali, kila mwenyemtazamo na fikra sahihi zaidi anao wajibu wa kukuongoza kuijua kweli halisi. Unafaakupambanishwa na NGUVU YA HOJA.CCMni umoja wa watu wenye nia moja na lengo moja kuu ambalo ni kuunda dola itakayongoza,kulinda na kusimamia mustakabali na utawala wa nchi pamoja na kuwaendeleza kiuendelevuwatu wake.

Uchambuzi wa kisayansi kwa mnasaba na zama za sasa, ni kuwa, aduimkubwa wa kwanza wa CCM ni historia yake kongwe iliyotukuka nasi wanaCCMtunajua hivyo na kujivunia. CCMni uzao uliotokana na kuunganishwa kwa TANU na ASP. Huko nyuma kabla yakuviunganisha vyama hivyo, kila kimoja kilikuwa CHAMA DOLA katika eneo lake lakijiografia. Lakini hata baada ya kuviunganisha vyama hivyo kwa jina moja,maeneo ya kijiografia ya utawala wa awali wa vyama vilivyounganishwa, nayoyaliendelea kuwepo chini ya utawala wa Chama kilichokuja kuzaliwa ambacho nachokilipokea na kuendeleza historia ya kimapokeo ya kuwa CHAMA-DOLA katikajiografia ile ile iliyokuwa chini ya vyama viasisi. Napenda ieleweke vemakwamba kilichounganishwa hapo ni historia iliyojigeuzwa kuwa urithi wetu. Kamanilivyosimulia hapo juu, utakumbuka kwamba Chama ni umoja wa watu na kwa hiyochama ni watu wenye kuamini katika ITIKADI moja.

Itikadi imo ndani ya fikra.Kwa hiyo mahusiano ya Chama na wanachama ni mnyororo wa fikra uliounganishwa navipingili vya imani ya wahusika. Huwezi kukitengenisha chama na watuwake-wafuasi wake au wanachama wake na vigumu pia kukitenganisha na wapenzi namashabiki wake kwa kuwa watakuwa wanayaelewa barabara madhumuni ya muunganikowao. Fikra hutawala imani. Watu hawa waliojiunga chini ya imani, malengo namadhumuni mamoja, hawakutoa mwanya wa fikra mbadala yenye kumomonyoa umoja wao,heshima na matumaini yao chini ya chama chao ambacho kiliongoza umma kikiwaCHAMA-DOLA.

Ulikuwa umoja wa watu waliohusika moja kwa moja na umaarufu uliopatikanakupitia imani ya umma iliyojengeka katika msingi wa ufanisi wa itikadi ya chamachao. Utulivu wa kisaikolojia wa watu hawa ulirutubishwa na hali ya Chama kushikahatamu bila kuwepo mbadala wenye uhalali wa kutofautiana kiitikadi. Kipinditulichomo hivi sasa, kinatulazimisha kuona mfumuko wa itikadi zenye haki ya kutofautianabila kuthibitiana-yaani, vyama vingi vya kisiasa kuzingatia mtawanyiko wakukubalika kwao nchini. Tupo katika kipindi ambacho utofauti unaokubalika katiya vyama ni ule wa kuwa CHAMA TAWALA na sio CHAMA-DOLA, ni Kipindi chaKUKUBALIKA. Hili ndilo tunaloshindania miongoni mwa vyama vilivyosajiliwa. Jukumukubwa ni kujenga mtaji wa ushindi kwa kuwashawishi wasio na chama kujiunganasi, kuwavua waliojiunga na vyama vingine na kuendesha maadili yetu kwahadhari inayotambua mahitaji ya kizazi cha sasa katika kipindi tulichomo.

Wakatitulipobadili mwendo (change gear) kutoka CHAMA-DOLA kuja vyama vingi,utakumbuka kwamba tumebadilika hivyo kwa utashi wa asilimia 20 tu ya watu wetu hukuasilimia 80 iliyosalia ya WaTanzania ikikataa kubadili mwendo kwa hoja zilizokuwaimara wakati huo. Kumbuka kwamba, wakati ule mtu asiyekuwa na Kadi ya Chama alihesabiwatu kuwa mwanachama kwa mantiki ya kutokuwepo mbadala halali wa kiitikadi na kinyumechake ni usaliti wa kutupwa unaompambanua na kumtenga mhusika na jamii yake.Kilichokuwepo wakati ule ni kutihibitiana kwa hatua za marekebisho ya kimaadilidhidi ya wakiukaji na wakati huo hakukuwa na hofu ya mbadala wa kiitikadi kamailivyo sasa. Upya huu ndiyo asili ya tabia ya wapenda madaraka kuhamahama-yaaniatoke chama kimoja hadi kingine hadi hamu na matamanio yake yafaulu na amaachokwe. WanaCCMwengi hadi sasa tunajikuta bado tupo katika athari ya mfumo ule tuliouzoeakwamba Chama chetu kinastahili heshima ile ile ya kipindi cha CHAMA-DOLA nahivyo tupo katika ganzi. Wengi wetu tupo kwenye mtazamo kwamba CCM, Tunacho;na aliyenacho, daima hakumbuki kupoteza, bali asiyenacho hapotezi ilahujibidisha daima kupata". Nasema; aduiyetu mkubwa ni historia na kamwe hatutahukumiana kwayo bali tutambue kwambasheria ya historia inayoishi haina mbadala. Nje ya historia, kuna nyongeza tuya masula madogo madogo ya ndani ambayo yapo kila pahala.

Tangu rais wangu kipenzi Jakaya wa Musoga ashike hatamuza uongozi mwaka mwaka 2005, chama kilianza kupoteza umaarufu ndani na nje yanchi, niukweli uaiopingika kuwa JK alikikuta chama kikiwa katika mwangaza mkuuwa kisiasa, chama kikijinadi chenyewe, chama kikisikika hata kwa walioendavidatu, chama kikisikika hata kwa walio peponi.

Fikiria sana mwanaccm, nini sababu za ccm kutoweka moyoni mwa Watanzania?Jiulize sana, je Jakaya ni sababu? Tafakari zaidi mwana ccm, harakati za raisiJK za kuelekea magogoni na kampeni za urais wake wa mwaka 2005 ziliratibiwa nakufanikishwa kwa fedha kharamu, nasema kharamu kwa ukweli ulio wazi,
Sioukweli mkamilifu kwamba CCM kimechokwa na WaTanzania na kwamba kimewatokamoyoni. Ingekuwa hivyo kisingeshinda. Kimeshinda kwa sababu kipo katika mioyoya waTanzania. Kuhusu fedha haramu, mimi sitii neno bali ingelikuwa jambo labusara kama utaisaidia TAKUKURU ili iwawajibishe kwa kuwapeleka wahusikapanapostahili. Ufafanuzini huu ufuatao;-

MOJA:CCM kimechokwa na wale wanaotafuta uongozi huku wakiwa hawakubaliki ndani yaCCM kwa kuvunja maadili. Hawa hufukuzwa na kuwa makapi ambayo wapinzanihuyaokota na kuyakaanga kwa kuyawekea bizari ndipo wayapeleke kwa walaji. Kwakuokoteza hawa tunaowafukuza, wanakuwa wamefaulu kubadili shati tu lakini siodhamira ya mhusika kwani hata huko walipopokelewa huendeleza maisha yao machafuna mifano hai tunaiona. Mwizi wa nyumbani kwangu abadan hawezi kubadilika nakuwa Askofu na wala Sheikh wa nyumbani kwako.

PILI:Ukweli mwingine ni kwamba uborekaji wa sasa wa elimu umetuletea waborekajiwengi katika kizazi kisichokubaliana na suala la kuchuma kupitia jasho na mavumbi.Kumejengeka msongamano/shindikizo (pressure) katika soko la ajira zifanyikazochini ya viyoyozi kunakoenda sanjari na elimu yao, dhidi ya uchache wa nafasi zakutolandana na wingi wa idadi ya wabobezi wanaozalishwa kila mwaka.

TATU:Lakini wapo pia wabobezi ambao hawapendi kuwa chini ya uangalizi mkali nauthibiti wa karibu katika kazi za taaluma zao. Hawa, shinikizo la matamanio yaolitaakisiwa kama athari katika shughuli zingine zenye kipato kikubwakisichovujisha jasho ambapo bosi huwa yeye mwenyewe, asiyekuwa na mdhibiti wakuonekana. Katika CCM, nafasi hizo zinawaniwa na wengi na kwa hiyo ni lazimamlango mwingine utafutwe-upinzani.

NNE:katika kutibu kiu ya kutaka uongozi, mlango halali ni vyama vingi ambavyovitampa mhusika fursa ya kujaribu bahati yake. Hawa wanajikuta katika mazingiraambamo, hutoa hoja za kutunga zisizokuwa na ukweli wowote wa dhati na kuuteteakwa hali na mali ili kukiangamiza CCM. Hii ndiyo maana hoja zao nyingihazikidhi matakwa ya kisheria na wakitakiwa kuwataja watuhumiwa waliohusika na ubadhirifuna kuwasilisha ushahidi, hukwama na kujitetea kwa maneno mengi. Kingine nimisamiati tunayoitunga sisi wenyewe katika kushambuliana ambayo baadayetunashindwa kuithibiti.

TANO:Siasa ni ajira ya mkataba wa uhakika na kazi ya heshima isiyovujisha jasho nandiyo maana wasiopenda kupigiwa kelele kwa kuchelewa kufika kazini wanafia nakukubali kuzitosa taaluma zao ili waingie.

SITA:Jingine ni wastaafu ambao hawakujiandaa katika maisha-nje ya fursazinazoambatana na ajira. Hawa wamegeuza siasa kama bustani ya wastaafu na kwahiyo ukiwaweka pamoja WAHITAJI WOTE wote hawa, msongamano katika nafasi zakisiasa unakuwa mkubwa mno na hivyo kuwa sababu ya kufungua milango mingine mbadalanje ya CCM kwani tayari tumejazana! Kimsingi wote hao hawana nyongo ya dhati naCCM bali wanakabiliwa na changamoto ya hitaji la kazi na salama ya maisha yao.Mkitaka kuithibitisha kauli hii, tangazeni kwamba nafasi za majimbo zimeongezwakuwa tatu! Mara moja utaona wote wanarudi CCM kwa kuwa kinaaminika na kupendwa.Matope yote yaliyopakwa CCM yatafanana na yalipakaliwa katika chupa!

SABA:Elimu tuipatayo haituandai kikamilifu katika kuwa wabunifu na wenye ari ya kuitumiaelimu hiyo kujiajiri wenyewe katika mazingira ya uchache wa kazi za ajirahususan Serikalini. Wasomi na wataalamu wengi, kutokana na hili wamegeuza siasakuwa mtaji na msingi wa utatuzi wa matatizo yao ya kiuchumi badala ya kuitumia sayansikatika kuongoza ubunifu wa kujikomboa kiuchumi. Kuitelekeza taaluma na kujiungana siasa ni kuisaliti nafsi hususan katika nchi ambayo taaluma hizozinahitajika katika kumkomboa mwananchi kutoka katika lindi la umaskini. Siasahuandaa mazingira ya wataalamu kuiendeleza nchi yao kupitia taaluma zao. Sasaikiwa taaluma zote zitalundikana Mjengoni kubishania siasa, nchi yetu itaendelezwana nani kiteknolojia?

NANE:Baadhi ya watendaji Serikalini wanasaliti nafasi zao za kazi kwa kutokuwajibikakikamilifu. Miongoni mwao, wapo wanaodanganywa kwamba Serikali ya CCM ikiondokamadarakani, wao wataendelea kuwa watendaji katika Serikali ya upinzani. Huu niupofu wa aina yake kwa kuwa, wapinzani wakifanikiwa kuwalaghai nao wakaasi nahivyo kufanikisha kuundwa kwa Serikali nyingine, kamwe watumishi wa ainahiyo hawataingia katika Serikali mpya kwaniwalikosa utii na uaminifu kwenye Serikali ya awali na walikuwa rahisikughilibiwa. Hakuna mtu atakayejenga imani na matumaini kwa mtu anayeshawishikakirahisi kumuua mzazi wake kwa matumaini tu. Mtu huyu ni wa kutumika mara mojatu na akishakufanikisha lengo lililokusudiwa hutengwa kwa kutokuaminika kwani akitokeamshawishi mwingine atatekwa kwa ajili ya maslahi na kusaliti tena, sawa naAskari wa kukodiwa!

TISA:Baadhi ya watu wetu wamepungukiwa na umahiri katika kufanya uchambuzi wa mambo.Wanakuwa rahisi kupotoshwa na hivyo kujikuta wamefanya maamuzi kwa hisia tuzisizohimiliwa na upembuzi wa kisayansi. Hawa ndio wale wanodanganyika kirahisikwa maneno matupu ya upotoshaji huku wangali wanayaona mambo mbele ya machoyao. Hawa wanazidi kuongezeka siku hadi siku na kuwa kimbilio la wapinzani.
Labda nirejea kidogo mapito ya KAGODA=CCM, MEREMETA=CCM,DEEP GREEN=CCM nk. Hayo yote makampuni yalizaliwa kwa lengo la kufanikishaushindi wa ccm,
Chamamakini na endelevu kinapaswa kujenga uchumi wakukiwezesha kujitegemea ili kiweze kukamilisha kwa ufanisi na uhakika jukumulake la msingi la kuunda dola. Chama chetu kinajizatiti hivi sasa katikakujiimarisha kiuchumi kama taasisi ya kijamii yenye jukumu la kudumu lakutekeleza. Kwa ujumla mimi sielewi chochote kuhusu makampuni uliyoyataja kuwana uhusiano na CCM. Hapa unachotakiwa kukifanya ni kuchunguza vyama ambavyo vinapatafedha kutoka nje ya nchi kwamba wanapewa hizo fedha ili wazirejeshe kwa kuuzanini? Wanaowapa fedha hizo ndio wanaojitangaza na kujigamba kuwa wabobezi wakidemokrasia huku wakishawishi vyama vya ulimwengu wa tatu kununua utawala. MAKUWADIwanawasujudu ili wapewe fedha za kuiharibu nchi yao na kuifanya isitawalike!Washindwe kwa jina la CCM......!!!

Hivyo rais wa Tanzania ni moja ya maadui wa ccm kushinda 2015 kwakuwa ametokanana zao la ufisadi, kamwe hawezi kunyoshea kidole mafisadi waliomuwekamadarakani, zaidi atawasamehe na kuwaambia warudishe pesa hizo huku wananchiwakishindwa kuthibitisha kama kweli zimerudi au laa, Watanzania sio wajinga,wanaelewa na wataijibu ccm 2015, na jibu litakuwa na kishindo kikuu. Baada yakuingia madarakani Jk alimteua SWAHIBA wake Edward Lowassa kuwa Waziri Mkuu waNchi, Malengo ya wawili hawa na mazingira yao ilikuwa waje wapokezane kijiti,na walikula nadhiri kabisa hata kujipambanua mbele za umma kuwa urafiki wao HAWAKUKUTANA barabarani ni (urafiki maalumu)
Mwaka 2007 tofauti za wawili waliokula nadhiri maalumu ilianza kuonekana hasabaada ya kuanza kuingizana mjini, wanaiba wote mwisho wasiku mmoja anajifanyahahusiki, Lowasa alichukia sana akawa mweusi tiiiiii, yaani kwa tuliobahatikakumtizama kupitia runinga ya TBCccm pale Dodoma siku ile nae anaamua kumwagamboga (kujiuzuru) tulifaidi kuona hasira ya waliokula nadhiri.

Tangu siku hiyo Lowassa aliamua kuingia msituni kukivuruga chama cha mapinduzi,kuivuruga serikali na kuifanya nchi isitawalike. Katika hili amefanikiwa kwanitangu mwaka 2007 alipoachia madaraka, ndipo umaarufu wa ccm ulipoanzakuporomoka kwa kasi, makundi masilahi yakaibuka, serikali ikanza sasa kuishikwa maruhani ya akina Mwaisapile, kila kukicha linaibuka hili mara lile, raisakaugua ghafla ugonjwa wa kusafiri hataki kabisa kuishi ikulu, Hayo yakitendeka kwa kasi Lowasa kila siku yupo misikitini na makanisanikuwania Baraka za Muumba huku ccm na serikali yake wakiweweseka na CHADEMA, etindicho kinafanya nchi isitawalike? Kinaongoza migomo? Kinaiyumbisha ccm?Kinaleta makundi ndani ya ccm?
Viongozi hawa unaowataja kwa majina, wanao ubavu wa kutoa kauli zao nami si msemaji waokama wewe ulivyotumwa na MAKUWADI kuwavunjia heshima ukiwa kijana mdogo tu. Nidhamu,maadili na Demokrasia katika CCM ni vya hali ya juu, na chama kinaheshimumawazo. Hii ndiyo sababu Mwenyekiti JK hutoa JIRUSHE kwenye vikao na hachokikufanya hivyo kila wakati tunapokutana ili kupisha demokrasia ya kutoa maoniitekelezeke kwa ukamilifu. Hakuna mjumbe aliyewahi kuwasilisha hoja yake namashtaka yake kwa Mwenyekiti naye akapuuzia. Uthibiti ni mchakato wa kikanunina kikatiba. Chama chetu kina mifumo hai na imara ya uthibiti na nidhamu. Kwavyovyote vile chama kwa mifumo yake kisingesita kuchukuwa hadhari na hatua.
USHAURI WANGU KWA JK NA CCM YAKE.Kama kweli JK unataka kutawala kwa amani kwa mdauliosalia na kuinusuru nchi hii na machafuko ifikapo 2015, nakushauri kwa moyomkunjufu, KAMATA Lowasa weka ndani pale Ukonga au Segerea kwa kosa la UHAINI,Likikushinda hilo mkabidhi chama kwa amani, hakuna njia ya mkato Lowasa amejiandaa kwa vita ya kisiasa, yupo tayari nchiiingie kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe ilimradi NADHIRI mliyokula pamojainatimia.

Nawahakikishieni wanaccm, adui yenu sio CHADEMA, bali ni JAKAYA KIKWETE naEDWARD LOWASA

Mkifaulu kuwaunganisha hawa wakawa na malengo sawa hata kama hawataongea, chamakitashinda 2015, Kumbuke kuwa Lowasa ana nusu ya wajumbe wa mkutano mkuu wa ccmambao wanaishi wa PESA yake.


Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika
Hakunamtu atakayezingatia na wala kufikiria ushauri duni kama huo. CHADEMA endeleenikujidanganya.
 

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2011
Messages
15,383
Points
2,000

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined Feb 8, 2011
15,383 2,000
Hivi umejibu hoja au umeongeza hoja?

Bado hoja ipo peupe na inaitafuna ccm,

Wenye uchungu na chama chukueni yaliyomazuri niliyowashauri na mabaya yaacheni hapa hapa!
Kitu kinachofurahisha CCM wamekuja na staili ya kujibu hoja humu badala ya ze comedy ya akina ritz na wenzake.Hii itapanua mijadala na wajiandae kujibu hoja za msingi za wananchi.
 

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Messages
15,005
Points
2,000

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2010
15,005 2,000
[h=2]Yericko nyerere: Lowassa na Jakaya Kikwete ndio Maadui wakuuwa sio CDM [Majibu][/h]
Waambie mode wa rekebishe heading yako hasa hilo neno la rangi nyekundu.
 

Henry Kilewo

Verified Member
Joined
Feb 9, 2010
Messages
898
Points
250

Henry Kilewo

Verified Member
Joined Feb 9, 2010
898 250
Kitu kinachofurahisha CCM wamekuja na staili ya kujibu hoja humu badala ya ze comedy ya akina ritz na wenzake.Hii itapanua mijadala na wajiandae kujibu hoja za msingi za wananchi.
Mkuu hakuna mtu hata mmoja hapo aliyejibu hoja ya Komredi Yeriko nyerere , huwezi kujibu hoja ukasema madai ya ufisadi huna la kusema watasema wenyewe( utakuwa umeacha mashaka kwenye swali gumu linalohitaji jibu la utekelezaji) Magamba hapo watapiga danadana hutowaona wakijibu @ Nepi.... wewe siulisema unapambana na mafisadi? Umewza kumshughulikia Luwassa? badala yake ulishika karatasi na kumtaja kama mjumbe wa Nec!

Kwasasa kilichopo ndani ya ccm ni kiini macho tu, ila hakuna mwenye dhamira ya kweli ya kushughulikia maovu yaliyomo ndani ya chama hicho kwani wote ni wachafu.... anayebisha abisha tuanike uchafu wa mmoja mmoja hapa.
 
Last edited by a moderator:

Yericko Nyerere

Verified Member
Joined
Dec 22, 2010
Messages
16,755
Points
2,000

Yericko Nyerere

Verified Member
Joined Dec 22, 2010
16,755 2,000
Mkuu hakuna mtu hata mmoja hapo aliyejibu hoja ya Komredi Yeriko nyerere , huwezi kujibu hoja ukasema madai ya ufisadi huna la kusema watasema wenyewe( utakuwa umeacha mashaka kwenye swali gumu linalohitaji jibu la utekelezaji) Magamba hapo watapiga danadana hutowaona wakijibu @ Nepi.... wewe siulisema unapambana na mafisadi? Umewza kumshughulikia Luwassa? badala yake ulishika karatasi na kumtaja kama mjumbe wa Nec!

Kwasasa kilichopo ndani ya ccm ni kiini macho tu, ila hakuna mwenye dhamira ya kweli ya kushughulikia maovu yaliyomo ndani ya chama hicho kwani wote ni wachafu.... anayebisha abisha tuanike uchafu wa mmoja mmoja hapa.
Yeye moyoni anahisi amejibu hoja kwa ustadi mkubwa,

Kinyume chake amekuja kujivua nguo zaidi,

Maneno mareeeeeeeeefu jibu la hoja ni sifuri
 
Last edited by a moderator:

Yericko Nyerere

Verified Member
Joined
Dec 22, 2010
Messages
16,755
Points
2,000

Yericko Nyerere

Verified Member
Joined Dec 22, 2010
16,755 2,000
LUCAS KISIMIR

Tuna hasara na member kama wewe humu kitengoni!
Jirekebishe mapema iwezekanavyo! Humu tumo na tunajaji ya uwazi na ukweli!
Hahaahaaa wametumia zaidi ya wiki mbili kukaa nakujibu hoja tena kwakushirikisha NEC lakini wamejibu kinyume na hoja ilivyo!
 
Last edited by a moderator:

Alfred Daud Pigangoma

Verified Member
Joined
Mar 30, 2009
Messages
1,792
Points
1,250

Alfred Daud Pigangoma

Verified Member
Joined Mar 30, 2009
1,792 1,250
Hahaahaaa wametumia zaidi ya wiki mbili kukaa nakujibu hoja tena kwakushirikisha NEC lakini wamejibu kinyume na hoja ilivyo!

Mkuu Yericko; Kinachofuata sasa utasikia "Tunaomba utusamehe hatukujua kama hatujui kujibu hoja"....... Najua wote tunafahamu kilichotokea kwa Hawa Ng'humbi kuomba asamehewe kulipa gharama za kuendeshea kesi baada ya Makamba Senior kumdanganya kukatarufaa na yeye akaingia king... Matokeo yake anadhani mahakama ni mahali pa kucheza upatu...
 

Kisindika

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2012
Messages
515
Points
0

Kisindika

JF-Expert Member
Joined Oct 19, 2012
515 0
Kama kweli Lowasa ni tatizo kiasi hicho basi mfupa uliomshinda Fisi (Nyerere) nani atauweza? Mwaka 1995 wakati Lowasa akiwa kwenye kinyan'ganyiro cha kwenda Ikulu, alikuwa na nafasi kubwa sana ya kushinda. Nyerere alikuwa na mtu wake (Mkapa) hivyo akahakikisha anamdhibiti Lowasa kwa mabavu ili jina lake lisipitishwe ndani ya CCM. Sababu kuu aliyombania ni kwamba mtoto mdogo huyu mali yote kapata wapi? Kwa hiyo alichokuwa anatuambia ni kwamba Lowasa ni mwizi hivyo hafai kwenda Ikulu.

Sasa swali linakuja kama Lowasa ni mwizi kwa nini Nyerere alimuacha aibe tu mali ya umma mpaka anamsubiri wakati anataka kugombea urais ndo aseme? Kwa hiyo Nyerere aliruhusu wana CCM waibe mali ya umma watakavyo ili mradi wasimwekee kiwingu katika kumteua mteule wake kwenda Ikulu? Kwa nini Nyerere hakuagiza vyombo vya dola vimkamate ili vimuhoji kuhusu mali isiyo na maelezo kama kweli yeye alikuwa anachukia wizi wa mali ya umma? Inawezekanaje uwe na mamlaka ya kumdhibiti mwizi wa mali ya umma na usifanye hivyo kama wewe mwenyewe sio mwizi?

Haya, mtu wake (Mkapa) akapita na baadaye akamteua Lowasa kama waziri wake wakati Nyerere bado yuko hai. Kwa nini Nyerere alimruhusu Mkapa kumuweka mwizi wa mali ya umma kwenye baraza lake la mawaziri?

Sasa nasema haya ili watanzania tufahamu kwamba tatizo si Kikwete, tatizo si Lowasa. Tatizo ni mfumo mzima wa CCM tangu awamu ya kwanza mpaka sasa hivi. Kuwanyooshea vidole Kikwete na Lowasa na kuwaacha watawala waalifu wengine waliowatangulia kabla yao hakutasaidia kuiondoa CCM madarakani. Kutachochea tu chuki ndani ya Jamii kwani watu watasema mbona mambo haya ya kula pamoja na wezi yalianza toka enzi za Nyerere? Kwa nini ashushumaliwe Kikwete peke yake? Katika kutafuta majibu ya maswali haya watu hawataishia hapo. Watasema Kikwete anabanwa kwa sababu ya dini yake au kabila lake, n.k. Hivyo ushabiki wa kisiasa utageuka ushabiki wa kidini, kikabila, n.k. Hali hii itaifanya CCM iendelee kutawala milele.

Ukweli ni kwamba CCM hakijawahi kuwa chama sahihi kwa maendeleo ya taifa letu tangu awamu ya kwanza mpaka sasa hivi. Hivyo kudai kwamba Kikwete and Lowasa ndio wanaokibomoa chama si sahihi kwa sababu hiki chama hakijawahi kuwa chama makini tangu kinazaliwa hadi leo. Ni ubabaishaji, wizi na sera za utopia (Ujamaa) mpaka hii leo!!!
 

Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2007
Messages
17,677
Points
2,000

Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2007
17,677 2,000
Amekuja na Majibu Mepesi sana. Yeriko japo NEC hawajajibu hoja, tafadhali jibu tu hizi hoja mpya na nyepesi alizoleta ambazo kila nikisoma naona anaamini Adui wa CCM ni MFUMO WA UPINZANI,
Kila point aliyo ongelea anaonekana kuumwa sana kwanini kuna UPINZANI.
 

kupelwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2011
Messages
1,060
Points
1,500

kupelwa

JF-Expert Member
Joined Aug 24, 2011
1,060 1,500
bila kumumunya majibu ya hoja si ya mwanasiasa ni mshabiki wa siasa anayetokea saigon anayetumika kuweka propanganda bila ufahamu wa majibu ya kweli kwa umma.kimsingi adui wa ccm ni chama kukosa itikadi, kukosa uongozi thabiti , kukosa mfumo mzuri wenye dhamira kiungozi na hivyo chama kuwa club ya umbeya na unafiki huku mamabo yakiharibika.CCM ya miaka ile si hii tunayoiona, iliyokuwa na mfumo wenye dira na itikadi sitahiki, safu ya uongozi madhubuti, na dhamira ya kweli ya kuutumikia umma upate maendeleo na si maendeleo ya vitu bali wananchi hasa wanyonge na masikini.
 

Yericko Nyerere

Verified Member
Joined
Dec 22, 2010
Messages
16,755
Points
2,000

Yericko Nyerere

Verified Member
Joined Dec 22, 2010
16,755 2,000
Amekuja na Majibu Mepesi sana. Yeriko japo NEC hawajajibu hoja, tafadhali jibu tu hizi hoja mpya na nyepesi alizoleta ambazo kila nikisoma naona anaamini Adui wa CCM ni MFUMO WA UPINZANI,
Kila point aliyo ongelea anaonekana kuumwa sana kwanini kuna UPINZANI.
Nimeangalia majibu ya hoja yangu, sijaona kama kunahaja ya kumjibu tena ilihali hajajibu hoja kuu,

Amekuja kulia tu, hakuna hoja yakujibu labda kuongeza wingi wa wachangiaji tu!
 

sokoinei

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2012
Messages
1,835
Points
0

sokoinei

JF-Expert Member
Joined Feb 27, 2012
1,835 0
Cdm tujipange kuna hoja mfu zinakuja sijui hawa watu walikuaga wapi! Na wanahoja nyepes sanaa tukaen mko wa kuwajibu hawa wajinga watu wanaandika huku wanatoa mapovu!!kunamtu anawasukuma nyuma hawa.cdm tupo majembe yakukwel hatuongeki mpaka kieleweke
 

lengijave

Senior Member
Joined
Apr 4, 2012
Messages
116
Points
0

lengijave

Senior Member
Joined Apr 4, 2012
116 0
Mr.Yericko Nyerere,
Kwanza kabisa nakushukuru sana kwa jinsi ulivyotupa updates ya kesi ya Lema,na kwa muda wa masaa machache tu zile update zako ziliangaliwa na watu zaidi ya 25,000 baada ya wewe kurusha ile update kwa umakini sana,hawa jamaa wanataka uache ku concentrate katika kujenga nguvu ya kuaondoa madarakani.
Nyerere your very strong,lakini sorry sitaweza kukoment kuhusu mada ya leo sababu siwezi kusoma ujinga wao.
 

Yericko Nyerere

Verified Member
Joined
Dec 22, 2010
Messages
16,755
Points
2,000

Yericko Nyerere

Verified Member
Joined Dec 22, 2010
16,755 2,000
Mr.Yericko Nyerere,
Kwanza kabisa nakushukuru sana kwa jinsi ulivyotupa updates ya kesi ya Lema,na kwa muda wa masaa machache tu zile update zako ziliangaliwa na watu zaidi ya 25,000 baada ya wewe kurusha ile update kwa umakini sana,hawa jamaa wanataka uache ku concentrate katika kujenga nguvu ya kuaondoa madarakani.
Nyerere your very strong,lakini sorry sitaweza kukoment kuhusu mada ya leo sababu siwezi kusoma ujinga wao.
Asante sana mkuu, pamoja sana,

Hawataweza kwaaina hii ya kujibu hoja ngumu!
 

Forum statistics

Threads 1,392,380
Members 528,604
Posts 34,107,347
Top