a4afrika
JF-Expert Member
- Apr 13, 2012
- 1,781
- 1,814
Mkuu Nicholas, nadhani umeleta jambo zuri ila jazba na mapenzi ya kisiasa yanaweza kuvuruga hoja yako. Binafsi ninakubaliana nawe kabisa kuwa "UHURU NI UWAJIBIKAJI" Kuwa huru ni katika kutekeleza wajibu wako, hujatekeleza wajibu wako wewe ni mtumwa tena mfu". Yeyote anayekwepa kutekeleza wajibu wake, atakuwa AMEJIFUNGA MWENYEWE, ndicho kinachowakuta wanasiasa wetu wa leo! UHURU ni uhalali na nafasi kamili ya kupata haki yako, na haki yake mtu kuu na ya msingi kabisa ni kutekeleza WAJIBU wake" Hivyo ni kweli kabisa kuwa Uhuru ni Kuwajibika. Swali, je tunaposema Uhuru ni KUWAJIBIKA ni kwa kutumia misingi gani? Je, ya kiafrika(Ubuntu)? Ama Kidemokrasia? Au ipi?
Ni wazi kuwa Mkuu wangu kwa kuuchukia ujamaa na sera zake, nashawishika kuamini kuwa unaposema Uhuru ni Uwajibikaji, unasema hayo kwa misingi ya kidemokrasia, na hapo ndipo ninapotofautiana nawe! Katika misingi ya Demokrasia, Uhuru si Uwajibikaji hata siku moja! Lakini ninaamini kabisa katika misingi ya Ujamaa-Uhuru ni Uwajibikaji. Uhuru ni uhalali na nafasi kamili katika kupata haki yake mtu, na HAKI ni kutekeleza wajibu! Katika ujamaa, kila mtu ana mafungamano muhimu na mwenzake, hivyo kulinda HAKI za wote ni wajibu wa wote! Kuhakikisha wewe unawajibika ni wajibu wangu, kwa namna yoyote ile ni lazima nihakikishe UNAWAJIBIKA, na huo ndio Uhuru tunaousema hapa!
Nakataa kuwa Uhuru si Uwajibikaji katika Demokrasia kwa sababu, moja Demokrasia inamrubuni mtu kuwa anaweza kuishi binafsi pasi na kufungamana na wengine, hivyo KUWAJIBIKA kwake ni HIYARI. Je, Uhuru ni Hiyari? Ni wazi SIVYO.
Ndio maana leo hii tuko mstari wa mbele kudai Kudai fulani apewe uhuru tukidhani kwamba ni kitu kutoka kwa wengine, mbaya zaidi hatutaki kuhoji KUWAJIBIKA kwao, ila tu tunalalama hawako huru. Ni UNAFIKI na USALITI wa nafsi zetu wenyewe! Kinyume cha Kuwajibika ni KUTOWAJIBIKA, hivyo tunapohoji hili ni lazima tujiulize kama kila mtu alicheza nafasi yake, ni Ujamaa tu ulioweza hoji hivyo!
Katika kuhakikisha kila mtu anawajibika, binadamu ALIFUNGWA. Mahusiano ya mwanadamu kwa mwanadamu, na mazingira yake, imani zake, fikra, n.k yalifungwa na MIIKO thabiti yenye uuwiano sahihi wa Mazingira na Nyakati zake mtu, Demokrasia ikavunja vifungo hivyo, kamwe haiwezi kuwa tena "UHURU ni UWAJIBIKAJI" kilichobaki ni KIINI MACHO/UBATILI, hakipaswi kupiganiwa!
"Utii bila Uhuru ni Utumwa! Na Uhuru bila nidhamu ni Wendawazimu" JKN.
Mkuu Nicholas, kama kauli yako ya Uhuru ni Uwajibikaji ni ya dhati kabisa, uliyoipata ukiwa na Fikra huru pasi na kufungwa na chochote kitu, basi adui yako si CCM tu bali ni pamoja na CDM, CUF, n.k maana ni wahubiri wazuri wa Demokrasia, sumu ya imani ya kuwa "UHURU ni UWAJIBIKAJI"
Ni vyema tukatambua, gharama halisi ya Maendeleo yetu!
Mungu wetu anaita sasa!

Last edited by a moderator: