1. "From Each According to His Ability. To Each According to His Needs" Embu kuwa mkweli Mkuu wangu, huo ndio Ujamaa, ni wapi unakopata jeuri ya kuthubutu kusema Ujamaa ni Unyonyaji? Demokrasi iliyopo imesukwa kulinda ubepari, na ubepari ni "Private Ownership" wapi kwenye mianya mikubwa zaidi kati ya hiyo mifumo miwili?
Mbona hii quote "From Each According to His Ability. To Each According to His Needs" si ya kijamaa.Ujamaa unabeba wavivu.Na huyo mvivu si lazima awe amewekeza akili au mtaji ambao unaweza comperate nguvu alizopaswa ziweka.
Private onwership ni uhuru, ni umiliki na si umilikiwa.Unawajibika bila wajibishwa.
Mkuu aje uogope kufungwa na sheria za kikundi? Nilisema kuwa Ujamaa unatambua wazi kuwa hakuna mtu bila watu, hivyo hakuna ustawi wa mtu mmoja mmoja kama hakuna ustawi wa wote, hiyo ndio collectiveness. Na sheria ziltungwa kusimamia hilo, na kutekeleza hilo ndio KUWAJIBIKA. "HAKUNA WAJIBU WA MTU UNAOJENGWA KWA TAMAA/HULKA ZA MTU MMOJA. Huo ni Ubatili, Unafiki na Uongo mkubwa. WAJIBU HUJENGWA NA WATU kwa kujali UMOJA wao" Lakini ubepari unaamini kuwa mtu mmoja mmoja anaweza kujikwamua pasi na kujali hali za wengine! Sasa tujiulize, ni nani anaweza kuishi peke yake pasi na kufungamana na mtu yeyote? Kama hayupo, unadhani MAFUNGAMANO yao yanapaswa kufungwa na nini? Je, ni kanuni za watu au mtu? Ujamaa una miiko thabiti na yenye tija kabisa kuleta usawa katika jamii, uvivu, uzembe, kutegea, n.k hakuvumiliki katika Ujamaa. Nahisi unazungumzia kitu ambacho hukukitafakari critically, wengi wanaoubeza ujamaa hudai ni mfumo dhahania lakini si madai ya unyonyaji, hayajawahi kusimama hata!
Ni ngumu kuwa na sheria za kundi zikawa sahihi kwa kila mtu, lazima wengine wakubali compromise kwa manufaa ya wengine na si hata manufaa ya kundi.Kwa manufaa ya waliokaa ktk mirija.
Mbona unajiambia sana mambo hambayo si sahihi hata kwa viwango vyako na kutaka yafanya fact.Nani kaongelea kuwa kuwajibika kunajengwa na tamaa?Ndio maana hatuendi kwani kwa kiasi kikubwa ni hisia tuu za ushindani zianwaendesha ila ukweli ni kwamba umejiingira na kuwa central kwa kitu usichokijua.
Nani kakuambia binadamu tupo sawa kama equal?Tupo sawa ktk asect za utu ila si ktk capabalities,and mind power na flexibilities, na mengine yanayompatia kila mtu edge ktk mambo fulani.
Ujamaa utakuweje ni misingi thabiti ya utu wakati si natural wala hautambui values za bindamu zinamhusisha na mUngu wake?Ujamaa wa Nyerere ni version yake iliyoongezewa Mungu ,ila ujamaa halisi ulipingana na Mungu.Nchi za kijamaa zinaabudu sana viongozi wake.Kwetu Nyerere alipotezea kwa vile dini ilimsuta,ila sasa hivi Kikwete anafaidi kuabudiwa kwa sana.
Viongozi wa Urusi, North Korea, Cuba,China, etc wanaabudiwa kabisa.Hayo mengine ni coating tuu..."huo usawa" uliouweka unakuumbua kabisa.Kwani ndipo ujamaa unakuwa adhabu kwa hard working,na reward kwa lazy,na viongozi.Yule mvivu anakuwa subsidized na ziada ya mwenye bidii au aliyetumikishwa kwa sheria kwa kiasi cha ziada.Ndio maana leo CCM wanang`ang`ana maliza wengine ziende kwingine Zote, na si kile kiwango kinachokubaliwa kwenda Hazina ya serikali Kuu.Hata ktk Nyumba za ibada yale mafungu yanayohifadhiwa hutumika kuwasaidia masikini na mayatima wanaokosa msaada.
Binadamu ni social creature ,ila naturally ni "Selfish", ndio maana ana mkewe, ana nyumba yake etc.Na Mungu alimpa Adamu,Ibrahimu, Wana wa Israel, ..na wengine kw akuwaambia ni chako, na ukimiliki.Minadamu ni mmiliki na si mmlikiwa.Ujamaa unamiss a apoint hapo.Ndio maana mashirika yanayoitw aya umma ni shamba la bibi kwa vile hayana mwenyewe.Umma si real entity....waulize mafisadi wa nchi zote za kijamaa.Na hat amabepari wanasema kabisa serikali ni spender si producer, na ikibaki na hela inaongeza matumizi kwa kuongeza ajira hata apsipo hitajika.
Leo Tanzania matnzania ni masikini kwa vile hana ardhi,hawezi endeleza kwa kiwango pale anapoambiwa serikali inapahitaji.Ndio maana hatukopesheki.
Katika misingi ya UTU wa mtu mweusi, wajibu wake mtu wa kwanza na mkuu kabisa, ni KUMFIKIRIA MWENZAKE. "Nipo vile Tulivyo"
Leo under Ubepari kutofanya kazi ni sehemu ya uhuru wako, hufanyi kazi huhojiwi-unakula huhojiwi, eti kila mtu yuko huru. Ni UBATILI.
Misingi ya mtu mweusi kaweka nani?wavuta bangi kama Bob marleyna magaidi km akina malcolm X?Au vichaa wengine wenye maono yanayopoteza vijana na generations.Huu ujinga wa sijui mtu mweusi na kinachoitwa asili yake ndicho huwa kinawashika sana watu shallow.Hata waislamw engi hudanganywa kuwa ni asili ya tu mweusi, marasta nao hivyo hivyo.
Nani kakwambia mabepari hawawafikirii wengine?Mabepari wapo responsible ktk mazingira yao sana,kuanzia kuinua kipato cha watu,kuwapatiwa watu elimu ,afya na mengine yatakayopanua domain ya yeye kupata hela zaidi.Yani kuwafanya watu waweze kwenda afuta hela kwingine na kuongeza hela endelevu ktk domain yake.Wanajua kabisa kuwa maisha ni mutuallly dependent.Wanajua kuwa ukiwa mbahili na kuwapa watu vitu duni,itaikia mahali watakuwa hawana pa kupata hela za kureplace ulizochukua,na hivyo kuwauzia vitu hadi kuwafilisi na wewe kufa.Ndio maana wa sehemu ya philanthropic au social responsibility.Na wapo serious kunagalia hawamalizi hadi mtaji wa soko lake.
Mkuu katika kuishi kama wamoja, bado unataka kufanya kazi kuwe ni swala la hiyari? Yaani msimu ni wa kupanda wewe unataka ulale eti utapanda utakapojisikia. Taifa lina uhaba wa chakula eti wewe unataka uachwe uwajibike katika kuzalisha mkonge, wapi na wapi? Ndio uhuru unaosema huo? Ndio huo unaotaka usiwe na mipaka? ITAWEZEKANAJE? Gharama halisi za kauli ya "Uhuru ni Uwajibikaji" sizo unazodai. Udaicho na Uaminicho ni dhana mbili tofauti kabisa!
mbona unajipa hisia zisizo halisi na kuzipa ground y akujenga hoja zako?Kazi ni hiari kam umeweza fanya kazi extra n akuweza fidia kipindi hufanyi kazi.Ila ni kutowajibika na kunaweza kupelekea filisika au kuanza ingilia majukumu ya mtu baada ya kuanza kumbushwa na njaa.
Kwa taarifa yako,mwajibikaji mzuri ktk utumwa wa kijamaa akipewa uhuru wake akawajibika ktk haki yake,huwa nafanikiwa sana kwa vile anafanya kazi sana, na hana mvivu pembeni wa kugawana naye sawa.belive me kuna watu ambao hunyang`anywa mali zote na kuanza moja na musa si mrefu wanawapita waliochukua mali za mwanzo.
2. "the more you, earn the more you gain" kauli hizi ndizo zanazowapoteza kabisi. Unadhani mlemavu wa miguu na mikono na miguu anaweza kujikusanyia nini? Je, ni toshelevu kwake? Je, ni vibaya kuunda sheria ya wewe kamili kutoa ziada yako kwake? Ndio muitacho Unyonyaji hicho?Wangapi wamezaliwa sehemu hazina shule wala zahanati, je utawafanishaje nawe uliyezaliwa Obay? Kugawa ziada yako kwao kutokana na afya yako bora na elimu bora uliyopata, ndio unaouita Unyonyaji? Unathubutuje? Hujui kwamba wao walikosa facilities za kuwawezesha? Hujui kuwa kipindi wewe upo shule, wenzako walikuwa mtaani kutafuta chochote kutia kinywani? Kaitika hilo atakayesema WAJIBU wako ni kugawa surplus yako kwao kuwainua, na yule atakayesema wajibu wako ni kuitumia surplus yako vile upendavyo, yupi kwako ni bora?
hapa umechanganya hisia, woga wa kuface ukweli na mengine...kumlazimisha mtu kulipa ziada kwa ajili ya walemavu ni unyang`anyi ndugu yangu.Huwezi iba hela halafu ukatoe sadaka si sadaka.
Kuzaliwa sehemu ambazo hazina shule, na sijui nini...Hayo ni matokeo ya mambo mengine,ambayo lazima yashughulikiwe.Pengine hawataki shule, hawataki jitolea kwa lolote, hubomboa shule,pengine serikali iliyopo ni mbovu na baguzi.
Kutoa si lazima iwe ziada, kutoa kwa mabepari ni ni sehemu ya business, wanaiwekea budget,malengo na kuitafuta hiyo hela na si kusubiri ibaki.Huo ndio uovu wa ujamaa,kutoa mabaki.Hata kwa sadaka haikubaliki.Punguza hisia ndugu yangu, bado wewe unatoa ziada?Wenzio wanafanya tafiti kiasi kinachohitajika,wana set goals na wanapanga pa kuzipata hizo hela na watu wanazifanyia kazi.Na mara nyingi kuna taasisi kabisa.
Wapo waliotumia Ujamaa vibaya, hatukatai. Uzuri kanuni bora zilikuwepo Kuepusha na Kuwashughulikia hao. Lakini Ubepari wenyewe ni UBATILI, WIZI na UNYONYAJI.
Hujui gharama halisi ya madai yako Mkuu wangu! Rudi katika tafiti yako upya.
Yu tayari kutushindia. Anaita sasa!
Wapo waliotumia ubepari vibaya pia kwa kuwa wanyang`anyi.So whats a point.Ubepari si negative behaviour ni wajamaa tuu na matamshi yao kwa kiswahili ndio una amplify negative view.Ni km mtu anaweza tamka kabila au jina lako so negatively linaweza project hiyo image vibaya kama tusi vile..Kama sasa hivi "waliitwa mabeberu" ila beberu ni dume.Na mwanamume kapewa sifa sana ktk mila zetu.Nikupe mfano.Characters wa gazeti la sani, wengi wamepewa majina mazuri sana ya makabila fulani ila matendo waliyopewa ,ukisikia mtu leo anaitwa hayo majina utadhani ni tusi. Mfano. Kobelo ,kwa waluguru ni jina maarufu,ila kamwambie msoma sani wa Arusha kuwa jina lako ni kobelo atakuuliza tena umpe jina kamili.Pia Pimbi,kipepe na wengine..
So usifikiri kiswahili n kijamaa unapolisikia neno Ubepari.Capitalism ni Jina la heshima na mapepai wanajitambulisha hivyo.
Mjamaa atapata wapi kanuni za haki za kuwaadhibu wengine wakati naye ni uzao wa huo uovu?Mara nyingi wana side mbilimbili,na wanazuia kuhoji.Kila ukihoji wenzio wanakuambia unaonekana kuanza usaliti.Unafungwa mdomo kama si kushughulikiwa.Ndio kinachoendelea China,TZ, na kwingineko.Wanaweza pia kuzimisha just because wanakuambia unachokisema kitaabisha taifa,kinahitaji semwa ktk vikao vya siri.