Hii quote "From Each According to His Ability. To Each According to His Needs".hata mkii paint vipi haiwezi kuwa ya kijamaa.personal ability si mara zote ina direct maping to personal needs.Watu wanaweza kuwa na ability ya kuzalsha zaidi ya wanavyohitaji, na hivyo wakawa na surplus.Mabepari wachache sana wanalisha nchi,ila wajamaa wengi sana hawawezi jilisha wenyewe.Hapa needs ni kubwa ability ni ndogo kwa wastage of resources. Africanism haiusiano na huo ujinga kutoka ktk skewed thoughts za kina Bob Marley, wanoasoma biblia na kupata tafsiri zao za kiwendawazimu.
Nilishatoa angalizo kwamba, kama unadai mimi si mwizi, wathibitishie watu kwa hoja kuwa huyu si mwizi, kung'ang'ania tu kujiapiza eti "Haki ya Mungu tena huyu si Mwizi, ukarudiarudia kadri uwezavyo, HAUTAELEWEKA zaidi ya Kujidharirisha"
Nakuuliza tena, Ni kwa namna gani Ujamaa unapingana na kauli hii "From Each According to His Ability. To Each According to His Needs". Ndio maana nimeuliza, ipi ni tafsiri ya Ujamaa kwako? Husianisha nukuu hiyo juu na msingi Mkuu wa Ujamaa "Collectiveness", ukiweza kuonesha zinakopingana, kuanzia leo mimi ni mfuasi wako. "Great thinker, discusses no small matters but how we ought to live" ushabiki wa kisiasa, dini, n.k hauna nafasi hapa!
Alafu kumbe unatambua fika kabisa kuwa si mara zote personal ability zitakuwa na direct maping to personal needs, kipi kinachokufanya ujitoe ufahamu? (a) Wapo wenye hitaji kubwa kuliko uwezo wao wa kuzailisha, wanaishi hand to hand na wale wenye uwezo mkubwa wa kuzalisha na hitaji lao dogo" Ipi thamani halisi ya mafungamano yao katika kuhakisha sustainability ya proper human qualities kwa wote wawili?" Nilishakuambia Hakuna binadamu asiyefungamana na wengine, pima mwenyewe kama Individuality/Ubinafsi una nafasi katika maisha haya.
"Ubepari to Surplus, ni kweli, kakini ni kwa ku-oppress nafasi za wengi ili ku-exploit resources zao. Ujamaa to Njaa-wastage of resources-U can't be serious Mkuu"
Ujina ni kufikiria thamani halisi ya maendeleo ni VITU, ni ULIMBUKENI. Huo ndio muitao ujanja mliopandikiziwa na nguruwe weupe leo mnapata kiburi cha kutukana Uafrika wenu-mental slavery. Maendeleo hayapimwi kwa VITU tu(uchumi tu) MMEPOTEA. Maendeleo hupimwa kwa mahusiano sahihi uliopo kati ya Uchumi, Siasa na Utamaduni, uhusiano utakao-guarantee sustainability of proper human qualities. Uhusiano wa uchumi, siasa na tamaduni za mtu mweusi. Mtu mweusi anaita UTU. Nipo vile tulivyo-KUFIKIRIANA. Sema ni wapi Ujamaa unapimgana na hilo. (najua ni ngumu kumeza kwako, lakini jitahidi kwa faida ya watototo wako)
"Ujamaa ulilishwa kwa wajinga wa Afrika" Hapa sina neno zaidi ya kusema asante. So, ubepari mlilishwa nyie wajanja wa Afrika. Hongereni maana leo mmeufakamia vizuri kusahau mlikotoka. Cha kushangaza leo mnamchukia Lowasa, Abood na wenzao vile wasivyobuguziwa na chochote si serikali wala jajamii.
Unapokosea zaidi ni kunidhania kwamba naipigia debe CCM hii-hii inukayo uvundo, over my dead body-never happen, na iko hivyo na kwa CDM, CUF, NCCR, kwa kifupi Demokrasia iliyopo na elements zake zote! Ndio maana uliposema "Uhuru ni Uwajibikaji" nilikubaliana nawe, lakini kumbe tafsiri yako katika hilo si ile niliyonayo! Siwezi kuichukia CCM wala CDM, kabla sijachukia kile kilichowaunda! CCM na CDM ni mapacha wa kufanana, mama mmoja!
Tunaweza kujadili zaidi kama utatolea majibu ya hicho nilichokuuliza hapo juu!
Mungu wetu anaita sasa. a4afrika.