CCM Wameishika CHADEMA PABAYA... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Wameishika CHADEMA PABAYA...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, May 16, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 16, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Monday, 16 May 2011

  * Akomba wanachama wake 239
  * Chiligati: Mamluki CCM kudhibitiwa


  Na Ghati Msamba, Bunda
  Gazeti la Uhuru


  KIMBUNGA cha Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama, kimeitikisa CHADEMA, ambapo ngome yake imepata nyufa. Ngome ya CHADEMA imepata nyufa baada ya wanachama 239 kuihama na kujiunga na CCM, huku wakiponda kauli za kejeli na kuvuruga amani zinazotolewa na viongozi wa chama hicho.


  Wanachama hao wapya wa CCM wamesema wameridhishwa na kasi ya maendeleo na utekelezaji wa Ilani ya CCM katika kuondoa kero za wananchi. Mukama akiwa katika siku ya kwanza ya ziara wilayani Bunda, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Kata ya Kibara, wananchi hao walitangaza kujiengua CHADEMA na kujiunga na CCM. Katika mkutano huo, Mukama alisema CCM ndicho Chama pekee kinachoweza kusimamia rasilimali na kubadilisha maisha ya wananchi. Aliwaasa Watanzania kutokubali kurubuniwa na kuwasikiliza watu wanaopotosha ukweli kuhusu dhana ya CCM kujivua gamba kwa kuwatosa watuhumiwa wa ufisadi.

  Katibu Mkuu alisema CCM ni taasisi kubwa, hivyo haiwezi kufa kirahisi kama wanavyoota wapinzani, hususan CHADEMA kwa kuwa ina viongozi wenye maadili ya uongozi. "Miaka 34 ya CCM ni mingi, hivyo ni lazima viongozi wabadilike na ndiyo dhana ya kujivua gamba ili kuleta mageuzi, kwani kwa kufanya hivyo ni kuonyesha ukomavu na umakini," alisema.

  Alitumia fursa hiyo kuwataka wakuu wa wilaya mkoani Mara kusimamia kikamilifu fedha za miradi ya maendeleo ya wananchi zinazotengwa na serikali kwa halmashauri.

  Katika mkutano huo, wazee wa Bunda wakiwakilishwa na Raphael Gurinja, walimuomba Mukama kurudi wilayani humo ili kusafisha siasa chafu na sumu iliyoenezwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa. Alisema Dk. Slaa amekuwa akieneza siasa chafu zenye mwelekeo wa kuvuruga amani nchini, hivyo kumuomba Mukama amfundishe siasa.

  "Dk. Slaa anaeneza chuki wakati wenzake wanamwaga sera, sasa inabidi afundishwe jinsi ya kuhubiri sera na si siasa chafu," alisema Gurinja. Akikabidhi kadi kwa wanachama wapya, Mukama alisema wamechukua uamuzi sahihi kurejea CCM, kwani vyama vya upinzani havina sera. "Nawapongeza kwa uamuzi wa kujiunga na CCM. Kitendo hiki kimewaziba midomo wale wanaodai eti Chama hiki kinakufa, karibuni nyumbani," alisema.


  Mukama pia alikabidhi kadi kwa wanachama wapya 175 wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) na kuwataka kuimarisha jumuia hiyo kikamilifu.

  Katibu Mkuu Mukama yuko katika ziara ya siku nane mkoani Mara, ambapo pamoja na mambo mengine atahimiza uhai wa Chama. Mamluki CCM kudhibitiwa CCM imesema itahifadhi majina na kumbukumbu za wanachama wake nchini kwa kutumia mfumo wa kompyuta.

  Hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa mageuzi ndani ya Chama, ambapo imewaagiza makatibu kukusanya kumbukumbu kutoka kwenye matawi na kuzipeleka makao makuu ya CCM, mjini Dodoma, ambako zitahifadhiwa. Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), John Chiligati, alisema hayo wakati akihitimisha ziara ya wajumbe wa sekretarieti mpya ya CCM.

  Alisema utaratibu huo unatakiwa kukamilika kabla ya uchaguzi mkuu wa CCM na jumuia zake utakaofanyika mwakani. Chiligati ametoa miezi mitatu kwa makatibu kuwa wamewasilisha kumbukumbu na majina ya wanachama makao makuu kwenye Kitengo cha Oganaizesheni kinachosimamia uratibu wa masuala ya uchaguzi, uhai wa Chama na jumuia zake.

  Alisema makatibu watapeleka wanachama hai kwa kulipa ada na wale ambao hawajalipa watatakiwa kutuma makao makuu kila yanapotokea mabadiliko, yakiwemo ya wanachama wapya, wanaoacha uanachama au kufariki dunia. Chiligati alisema utaratibu huo unalenga kukomesha uwepo wa wanachama mamluki na wa msimu wa uchaguzi, ambao hawana faida kwa uhai wa Chama.


  Ziara ya wajumbe wa sekretarieti ya CCM iliyofanyika kwa siku sita katika maeneo mbalimbali mkoani Singida, iliwahusisha Chiligati, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha, Mwingulu Nchemba na Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Asha Juma Abdallah.
   
 2. n

  ngaluma Member

  #2
  May 16, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hao waliopo ata mia awafiki...
   
 3. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #3
  May 16, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  * IT Seems that CCM own Tanzania People Man is by nature a political animal


  Monday, 16 May 2011
  NA PETER KATULANDA, LAMADI
  Gazeti la Uhuru


  MBUNGE wa Busega Dk. Titus Kamani, amewapasha wana CCM kuwa ni lazima wawe makini na jasiri ili kukitetea na kukiwezesha kuendelea kushika dola.

  Pia, amesema iwapo wana-CCM watashindwa kuungana na kukabiliana na watu wasio na nia njema na taifa, nchi inaweza kuangukia mikononi mwa wanasiasa wasio na sera makini. Dk. Kamani aliyasema hayo mjini hapa juzi, alipokuwa akizungumzia na wanachama na viongozi wa CCM waliompokea na kumsindikiza Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama, kutoka Mwanza hadi Lamadi kabla ya kuanza ziara yake mkoani Mara.

  "Tunapaswa kuwa makini na kujitokeza kwa ujasiri kuinadi CCM na serikali yake. Tukikaa pembeni tunaweza kuacha nchi ikitawaliwa na watu wasiokuwa na sera. Vijana tujitokeza kutetea Chama," alisisitiza Dk. Kamani. Alisema vijana wa CCM wanapaswa kuwa mstari wa mbele kuelimisha jamii juu ya sera za Chama na utekelezaji wa Ilani yake kwa ujasiri bila woga.

  Awali, Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza, Alhaji Rajabu Kundya akimkaribisha Dk. Kamani kutoa shukrani kwa niaba ya wabunge wa CCM mkoani humo, alisema kwa muda mfupi waliokuwa na Katibu Mkuu wamenufaika na kupata uhai mpya. Kundya alisema kila mwana- CCM na kiongozi wake atumie fursa aliyonayo kukijenga Chama, kushirikiana kikamilifu na wanachama wengine, pia wananchi kwa ujumla ili kurejesha imani iliyoanza kutoweka miongoni mwa Watanzania.
   
 4. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #4
  May 16, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwi kwi kwi!! Yale yale ya ma ka mba.sasa naamini ccm wameshindwa kuvua gamba.
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  May 16, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mukama anaona kavuna saaana kupata 239? mwenziwe Dr Slaa anavuna 23,000 na leo ilikuwa zamu ya Njombe.
   
 6. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #6
  May 16, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Eti "wameridhishwa na kasi ya maendeleo na utekele utekelezaji wa ilani ya CCM".
  Hivi hospitali ya MIREMBE imefungwa?
   
 7. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #7
  May 16, 2011
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Mie nilikuwepo bunda wote waliochukuwa kadi za ccm ni wana ccm tayari nawajuwa. Huyo mzee si alikuwa mwenyekiti wa kitongoji kupitia ccm kipindi fulani hivi, na kama kweli mwandishi ulikuwepo weka picha acha unafiki na story za kutunga.

  Ndiyo mie niko bunda hapa ukanda wa benki kule kwenye mkutano walikuwepo wazee tu, na hata kama waliorudisha kadi ni idadi unayotaja wewe, kwenye mkutano watu wengi saizi hiyo hawakuwepo labda mkutano mzima walikuwa wanrudisha kadi acha uongo.

  Pia mie ni mwana ccm acha kutuharibia chama hivi kama chama hakina mvuto kwa sasa why mseme uongo na kesho story kama hii utaikuta gazeti la mzalendo, uhuru na habari leo huo ni ujinga na upuuzi ndiyo maana hamuuzi, mwambie Nape , huyo mukama wako na chiligati waende chuo chochote tanzania ambapo kuna vijana wasomi hata mwalimu nyerere university kigamboni uone kama hawajazomewa achani ujinga na unafiki chama kwa sasa hakikubaliki lazima tubadilike, hao wazee wanaotudanganya kuwa chama kipo they will be dying soon.

  "Nape mtetezi wa CCM na mwanzilishi wa CCJ"
   
 8. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #8
  May 16, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Kuna mwana JF aliwahi kusema hapa kuwa ccm waache kushindana na kulumbana na CDM, watekeleze sera za kuongoza nchi.
   
 9. J

  Jenifa JF-Expert Member

  #9
  May 16, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  nape amefurahi kweli kuwashika pabaya chadema
   
 10. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #10
  May 16, 2011
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Kudanganya ndiyo kushika pabaya wewe
   
 11. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #11
  May 16, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  CCM kila wakienda kwenye Mikutano yao Wamekamilika Wana Waandishi wa habari, Wana Wapiga Picha wanapiga only kiongozi hawapigi picha umati wa wananchi, wanaweka vitu, vivuli ni Mkutano wa Chama au ni Sherehe kila wakati hizo pesa zinapatikana wapi?

  What I'm trying to say is Political fake advertising ought to be stopped. It's the only really dishonest kind of advertising that's left. It's totally dishonest.
   
 12. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #12
  May 16, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,250
  Likes Received: 3,863
  Trophy Points: 280
  Acha uongo wewe dunia ikusute na roho yako itetereke! Wale vikongwe wanaomwimbia nyimbo za kisukuma hawafiki hata mia! Kama mimi sikuona vizuri hebu weka picha ionyeshe huo umati na hao waliojiunga leo hii!!!
   
 13. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #13
  May 16, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Nikitaka kwenda kuitetea CCM niwaambie nini watu.
  1.Kwamba hakuna ufisadi nchini,hizo zote ni kelele za Slah.
  2.Kwamba gharama za maisha zipo chini sana ila wapinzani hawaoni.
  3.Kwamba tumevua gamba sisi si nyoka tena bali tumekuwa jongoo.
  4.Kwamba wapinzani si wazuri kwa sababu wanaleta upinzani.
  5.Kwamba tuache kuilaumu serikali umskini ni mipango ya Mungu.
   
 14. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #14
  May 16, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  UHURU na MZALENDO wanakupongeza kwa kuwauzia habari zao maana umeonekana humu JF huwa unajifanya huoni habari za magazeti mengine.
   
 15. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #15
  May 16, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Sio kuwauzia habari naona ni bora kuangalia what your enemies wanafanya nini, siishi Tanzania ninasoma online na nikiona habari ni nzuri kujadiliwa naipost sababu kuwa bora ni kuangalia wapinzani wako wanafanya nini kizuri au kibaya, na kama unaona ni vibaya wewe sio Mwanasiasa Mzuri hapa US wanafuatilia kila jambo kuona wapinzani wao wanafanya nini always sio kuangalia Mazuri tu;

  INA MAANA DEMOCRASIA YETU NI FUNYU NI KUSIKILIZA MAZURI TUU?
   
 16. N

  Nyakarungu JF-Expert Member

  #16
  May 16, 2011
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  Mwambieni aende serengeti,aseme maneno yake hayo, mawe ya kule ni mepesi mkononi, ila mazito usoni.
   
 17. k

  kiloni JF-Expert Member

  #17
  May 16, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 575
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  MIAKA 5 HIYOOOOOO!!!!!!!!!! INAYOYOMA! VILAZA WAMEBAKI KUPIGA PARAPATA NA UDANGANYIFU KIBAO. TUTAWAULIZA UTEKELEZAJI WA MOJA YA KILA AHADI ZENU HEWA, TUTAWAULIZA MATUMIZI YA KODI ZETU, TUTATOBOA MATUMBO YENU TUTOE FEDHA MLIZOIBA EPA, RICHMOND,RADAR, DOWANS ETC. Mnaolumbana nao hawajakabidhiwa nchi wala Kodi. OOHHHHHHH lazima tuonane wabaya kabla ya 2015. Nyie endeleeni kupotezea tuuu!!!!!!!
   
 18. z

  zamlock JF-Expert Member

  #18
  May 16, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  yani kwa bunda wasitudanganye hata kidogo ule mji naujua hata juzi nilikuwa pale wote ni chadema na wale waliokuwa kwenye mkutano wa mkama ni wakina mama ambao amecheza nao wakiwa wadogo na wazee wenzake na amewapa kadi kwa sababu kadi zao zilikuwa zimezeeka tunajua sana ujanja wa ccm wao wakubali chama chao akina mvuto
   
 19. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #19
  May 16, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,012
  Trophy Points: 280
  Hawa sisiem ni walagh'ai wakubwa, na watanzania mbona tushashtukia propaganda zao!! Yaani angalia pecha zao wanazoweka hapa ni za kijukwaa alichosimama mhubiri propaganda. Kwa nini hawaweki picha ya umati uliohudhuria mkutano? Au wanaogopa aibu kwa sababu watu watajaribu kufananishia na ile nyombi inayoonakana kwenye mikutano ya chadema na kufanya uamuzi wa za mbayuwayu, changanya na zako? AKILI NI NYWELE KILA MTU ANA ZAKE.
   
 20. menyidyo

  menyidyo JF-Expert Member

  #20
  May 16, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 1,339
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  wekeni picha tuone umati wa watu. eti ccm imeishika pabaya ....,. kwenda.
   
Loading...