CCM wakiri kusahau waasisi wa TANU

SubiriJibu

JF-Expert Member
Jun 26, 2009
1,803
1,863
Kuna wale ambao siku zote inaposemwa kwambahistoria ya nchi imepindishwa wanakuja juu kuitetea CCM kwamba haikuipindisha popote. Humu JF wamejaa wengi wa aina hiyo

Aina hii ndio wale ambao CCM sasa inapokiri kwamba ni kweli waliipindisha, hawa washabiki wanabaki na aibu kuzidi mtu aliyefumaniwa.

Gazeti la MAJIRA toleo la Julai 07, 2011 linaelezea jinsi Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Bw. John Chiligati alivyokiri kwamba CCM imewasahau waasisi wa TANU.

Pata full story kwenye attachment hii.
 

Attachments

  • CCM Kusahau.jpg
    CCM Kusahau.jpg
    194.9 KB · Views: 59
TANU ILIZIKWA RASMI 1977 FEB 5. Lilipoanzishwa dudu liitwalo CCM, hii ilimaanisha kwamba TANU na WAASISI wake ilikuwa KUSHNEHI! Ila mali za TANU zilirithiwa na CCM si na WATANZANIA!!! ndio maana hata VIWANJA na TAASISI zingine vilivyojengwa kwa NGUVU ZA WANANCHI vikaitwa VYA CCM!!!

Kama ilikuwa nia ni njema kwanini WAKFU za TANU hazikuwekwa kuwa URITHI WA TAIFA? na kama nia bado ni njema kwanini leo visirudishwe kwa WANANCHI?

Hakuna Mtanzania aliyehoji wala anaehoji kwa nguvu juu ya hilo leo! sote tunalisemea chinichini!

LA WAZEE WAASISI KUSAHAULIKA NI JAMBO LA MAKUSUDI KUWATOA KUNDINI NA KELELE ZAO ZISIWEPO....
WAASISI WA TANU WALIFUNIKWA KITAMBO NA ILIDHANIWA WENGI WATAKUWA WAMESHAKUFA KUFIKIA WAKATI HUU!! ILA WAPO WANADUNDA BADO NA WANAONA KINACHOTOKEA NI KINYUME NA WALICHOTARAJIA WALIPOPIGANIA UHURU...
KICHEFUCHEFU KITUPU... TOKEA MIAKA MITANO BAADA YA UHURU MPAKA LEO...
 
Back
Top Bottom