CCM WAKE UP!! We Are At War! So All Weapons Are Fair Game!!

Status
Not open for further replies.
Hajui itikadi ya CCM wala maana ya itikadi, wala sera za CCM hazijui, wala Katiba wala Kanuni, wala hajui anachotaka kukifia huko CCM, wala hajui kuwa Nyerere mwenyewe aliekianzisha alisema "CCM sio baba wala mama yangu!" akimaanisha anaweza akakiacha tu, wala hajui kwanini viongozi wake wakuu wanakiri kuwa kimekosa mvuto kwa Watanzania, hajui lolote kuhusu CCM bali anaburuzika tu kutafuta misifa ambayo kamwe hataipata!
 
- ITIKADI ZIPO LAKINI NYINGI ZIMEPITWA NA WAKATI NDIO MAANA TUPO KWENYE KUZI-REDEFINE NA SOON UTAONA ZIKIMWAGWA HAPA JF, MAANA SASA CCM NI KAZI TUPU, CCM NI UMOJA!, NA CCM NI USHINDI TU!! - KIDUMU CCM!!
Es!
Maswali machache kwako;

  • Kwa nini umetumia herufi kubwa?
  • Kama itikadi zenu zimepitwa na wakati, je mmeachana nazo?
  • Kama mmeachana nazo, hizo unazozitetea hivi sasa ni zipi?
  • Kama hazipo na bado mnazi-redefine, haraka hii ya nini?
Baada ya maswali hayo naomba nikupe ushauri kidogo mtoto wa Malecela...chukua likizo kidogo, unachefua watu humu kwa kuzusha mijadala ya hovyo. Unataka kujua kwa nini watu wanachangia? Ngoja nikudokeze...ni sababu zile zile zinazowafanya watu wengi kukimbilia kulikotokea ajali? Ni kuona maiti!

Kwa ukumbusho tu kijana, Katiba ya CCM toleo la 2010, toleo ambalo limezingatia na kuweka pamoja marekebisho yaliyofanywa katika Katiba ya Chama Cha Mapinduzi ya 1977 matoleo ya 1980, 1982, 1984, 1987, 1990, Machi 1992,
Septemba1992, 1994, 1995, 1997, 2005 na 2007, Chama Cha Mapinduzi kinaamini kwamba:

  1. Binadamu wote ni sawa.
  2. Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake.
  3. Ujamaa na Kujitegemea ndiyo njia pekee ya kujenga jamii ya watu walio sawa na huru.
Kati ya imani hizi william, ni ipi imepitwa na wakati na ipi ina-redefiniwa?
 
Last edited by a moderator:
Maswali machache kwako;

  • Kwa nini umetumia herufi kubwa?
  • Kama itikadi zenu zimepitwa na wakati, je mmeachana nazo?
  • Kama mmeachana nazo, hizo unazozitetea hivi sasa ni zipi?
  • Kama hazipo na bado mnazi-redefine, haraka hii ya nini?
Baada ya maswali hayo naomba nikupe ushauri kidogo mtoto wa Malecela...chukua likizo kidogo, unachefua watu humu kwa kuzusha mijadala ya hovyo. Unataka kujua kwa nini watu wanachangia? Ngoja nikudokeze...ni sababu zile zile zinazowafanya watu wengi hukimbilia kulikotokea ajali? Ni kuona maiti!

- Unajua my goal ni kuhakikisha kwamba Chadema kwenye next uchaguzi inasambaratika kabisa na that can happen wakikosa Urais, and believe me anything I can do on that line will do with all heart and soul as I am doing it now! so fasten your belt!!

Es!
 
- Naomba kuwaaamsha usingizini wale wote ambao bado wamelala usingizini, people tupo vitani yaani kwenye vita vya Itikadi za vyama vyetu vya siasa, wenzetu huko Chadema walianza siku nyingi sisi CCM tulikuwa bado hatujaelewa hilo, lakini Inshallah sasa somo limeanza kueleweka, matusi hapana, viroja hapana, hoja tu jamani lakini ni lazima tusimamie na kutetea itikadi zetu, kama huwezi kusimama kutetea itikadi ya chama chako cha siasa sio sawa hata kuwa mwanachama wa CCM!!

- Simama juu uhesabiwe! People msidanganywe hakuna chama cha upinzani kinachotutakia mema CCM wote wanegependa kuona wanatushinda na CCM inakufa, sasa msijidanganye na siasa za kujifanya kukubalika kila upande ninawaona wanasiasa wengi wakijaribu kuwa kila upande poleni sana, CCM lazima tusimame imara na hakuna kuogopa!! Tusimamie itikadi yetu hata kama it means kufa na tufe lakini hatuwezi kukubali kushindwa kusimamia itikadi, kumbukeni kwamba:- "IN LIFE IF YOU DON'T STAND FOR SOMETHING, YOU WILL FALL FOR ANYTHING"

- KIDUMU CCM! KIDUMU CHAMA TAWALA!!

FMES - SAUTI YA UMEME!!
Itikadi ya CCM haifuatwi na uongozi uliopo wa CCM.
Hujui hilo?
 
Itikadi ya CCM ni WIZI na UFISADI...so Mko tayari kufa kuliko kuacha kuendelea kufanya UFISADI kwa Rasilimali ambazo mungu amewapa Watanzania!!! ooh grrrr ???!!! Loudly n clear!!! umesomeka bila chenga! kiama kitawafika 2015...
 
- iTIKADI ZIPO NDIO MAANA TUMEKUWA TUKICHAGULIWA KWA MIAKA 51 SASA KUTAWALA NCHI, LAKINI NYINGI ZIMEPITWA NA WAKATI NDIO MAANA TUPO KWENYE KUZI-REDEFINE NA SOON UTAONA ZIKIMWAGWA HAPA JF, MAANA SASA CCM NI KAZI TUPU, CCM NI UMOJA!, NA CCM NI USHINDI TU!!

- KIDUMU CCM!!

Es!

Ni kwa muda gani CCM imekua ikitawala kwa kutumia itikadi "nyingi" zilizopitwa na wakati?
 
- iTIKADI ZIPO NDIO MAANA TUMEKUWA TUKICHAGULIWA KWA MIAKA 51 SASA KUTAWALA NCHI, LAKINI NYINGI ZIMEPITWA NA WAKATI NDIO MAANA TUPO KWENYE KUZI-REDEFINE NA SOON UTAONA ZIKIMWAGWA HAPA JF, MAANA SASA CCM NI KAZI TUPU, CCM NI UMOJA!, NA CCM NI USHINDI TU!!

- KIDUMU CCM!!

Es!

CHADEMA ni chama cha itikadi ya mremgo wa kati (center party with orientation on market economy).

CUF inafuata itikadi ya uliberali ambayo inalenga kuwazindua wananchi waweze kuitumia neema waliyopewa na Mungu kwa manufaa yao binafsi na taifa kwa ujumla.

Kwa kweli sijui itikadi ya CCM. Lakini hapo kwenye red umesema in fact zipo itikadi. Kwa hiyo, CCM ina itikadi zaidi ya moja. Kama CCM ina itikadi zaidi mmoja, unaweza kututajia angalao itikadi tatu tuu?

Hapa sina maana ya sera aka policy, bali itikadi aka ideology. Ukiweza kunipa itikadi tatu za CCM naenda kula peaceful.
 
Absolutely hilarious, you know what, when you think you know, you do not know and when you know you do not know the other people think about you. What the heck! Pesa mbaya jamani tufanye kazi na kukubali kipato tunachokipata bila kuwadhulumu walipa kodi wa nchi hii. Malipo ni hapa hapa duniani … .. wewe kama kiongozi unalipwa na pesa za masikini kabisa timiza wajibu wako, mali ya dhuluma hailipi.
 
Jibu lako lipo hapa alishajibu siku nyingi tu wewe wala usisumbuke kubishana n mtu aliyechanganyikiwa na maisha uzeeni.


Lakini kwenye hiyo post alikuwa anaongelea sera. Ninachotaka mimi ni itikadi na siyo sera.

Ndiyo maana niliweka angalizo mapemaaaa.
 
Mimi naamini huyu mtoto wa malecela ana mission au Mkono uliofichama wa kuisambaratisha ccm chini ya JK!...Ukiunganisha dots kwa kupitia threads zote zilizoibuliwa na Matola utapata jawabu. Hii kasi yake ya kupost threads irrelevant na zinazoonyesha kuwa ccm ni kundi la hamnazo ni alarming kwa sasa.

Kabila la Igbo huko Nigeria wana Saying inayosema...' If the child discovers the person who killed his father, and the Killer knows that he has been discovered, he may kill the child too!
Sasa Field Mrshall ES ameamua kuwa kabla hajauawa na muuaji wa baba yake, acha naye aue japo kidogo, ndiyo mission anayoifanya huyu baharia. Ndiyo maana amethubutu kugombea nafasi zozote zinazotokea ndani ya ccm bila kujali ziko low kiasi gani...hata angetangaziwa nafasi ya mwenyekiti wa ccm wa kijiji lazima angegombea tu, kichwani anajua lengo lake!
Kumchinja kobe ni timing, acheni mwenzetu aifanye!
 

Kwa maana nyingine, anayepiga vita ufisadi anaipiga vita CCM na wanaodai wanaipiga vita ufisadi wakiwa ndani ya CCM wanajipiga vita wenyewe, kitu kisichowezekana! Sasa mkuu Mchambuzi, kwa kuwa wewe hata siku moja hujauficha ukweli kuwa ni mwana CCM, tuchukulie kuwa sisi tunaopiga vita ufisadi tunakupiga vita wewe? Kama jibu ni ndio, kwa nini sisi wengine tusiamini kuwa ukosoaji wako wa CCM ni sawa na machozi ya samaki? Kama jibu ni hapana, unaeleza vipi kwa nini bado ni mwana CCM hadi leo Ijumaa tarehe 7, Desemba 2012?
 
Kwa maana nyingine, anayepiga vita ufisadi anaipiga vita CCM na wanaodai wanaipiga vita ufisadi wakiwa ndani ya CCM wanajipiga vita wenyewe, kitu kisichowezekana! Sasa mkuu Mchambuzi, kwa kuwa wewe hata siku moja hujauficha ukweli kuwa ni mwana CCM, tuchukulie kuwa sisi tunaopiga vita ufisadi tunakupiga vita wewe? Kama jibu ni ndio, kwa nini sisi wengine tusiamini kuwa ukosoaji wako wa CCM ni sawa na machozi ya samaki? Kama jibu ni hapana, unaeleza vipi kwa nini bado ni mwana CCM hadi leo Ijumaa tarehe 7, Desemba 2012?

Ningekuwa kwenye uongozi wa CCM, ningepingana na ufisadi kwa nguvu zangu zote bila kujali kutishiwa maisha, kutishiwa kuvuliwa madaraka, au kunyimwa mshahara/posho; Na ingetokea naambiwa maneno kama aliyoyasema mwandishi husika - kwamba wapambanaji wa ufisadi sasa wametulia baada ya kuambiwa wapeleke harakati zao nje ya Chama, ningejiuzulu mara moja na aidha kubakia kuwa Mwanachama na kusubiri fursa nyingine ya mapambano from within, au kuhama kabisa Chama na kwenda upinzani, bila ya kujali sana naenda chama gani kwani nachojali ni kupata fursa ya kuchangia taifa langu kupitia a political process, in or outside a political office;

Kwa sasa, zaidi ya kuwa mwanachama hai, sina nafasi yoyote ya uongozi ndani ya CCM, hata ngazi ya mfereji, na sina nia ya kutafuta uongozi wa ngazi yoyote katika awamu ya sasa; Kwa majaliwa ya mwenyezi Mungu, Nitakuwa tayari kushiriki katika uongozi wa kisiasa katika ngazi yoyote nitakayoombwa au kusukumwa na moyo wangu, lakini hii ni pale tu nitakaporidhika kwamba sasa CCM inadhamiria kuja na mabadiliko ya kweli, hasa iwapo CCM itachukua uamuzi mgumu ya kugeuza adui kutokea Upinzani na kuelekeza kwenye Ufisadi;

Vinginevyo, binafsi sioni tatizo kuendelea kuwa mwanachama wa CCM licha ya mapungufu yake kwa sasa, Chama ambacho bado naamini katika misingi yake, na hii ndio huwa nguzo kuu ya hoja zangu mbalimbali kila ninapokuwa Critical on CCM; Na ndio maana more often than not, huwa naunga mkono hoja nyingi sana za Chadema kuhusu Ufisadi kwani zinaendana na Mwongozo wa Chama Changu (1982) ambao bado upo hai; UFISADI ni adui wa watanzania wote, Chadema na pia wana CCM wenye kutambua kwamba mafanikio yao ya maisha yanatokana na unyonywaji wa maskini, wana CCM wenye uzalendo na pia mapenzi na nchi yao; Kwa maana hii, hata ingekuwa ni kwenye senate, kwenye suala la Ufisadi, I would cross the aisle to Join Chadema kwani kuna mambo ambayo kwa mantiki tu yanatakiwa kuwa bi-partisan, not partisan;

Kuhusu machozi ya Samaki: Tatizo la Rushwa hata Mwalimu lilimshinda mpaka umauti ulipomkuta licha ya kuwa na msimamo mkali sana dhidi yake, je na yeye alikuwa na machozi ya Samaki? Mimi naamini kwamba kupingana na Ufisadi kwa dhati kkama mwanachama wa CCM haina tofauti na kupingana na ufisadi kwa dhati kama mwanachama wa Chadema; Tofauti inakuja pale mtu unapokuwa kwenye nafasi ya kufanya maamuzi yanayoweza kuleta mabadiliko katika suala husika; Sote, yani mimi na wewe hatupo katika nafasi hiyo, licha ya kuwa wanachama wa vyama viwili tofauti;
 
Kwa maana nyingine, anayepiga vita ufisadi anaipiga vita CCM na wanaodai wanaipiga vita ufisadi wakiwa ndani ya CCM wanajipiga vita wenyewe, kitu kisichowezekana! Sasa mkuu Mchambuzi, kwa kuwa wewe hata siku moja hujauficha ukweli kuwa ni mwana CCM, tuchukulie kuwa sisi tunaopiga vita ufisadi tunakupiga vita wewe? Kama jibu ni ndio, kwa nini sisi wengine tusiamini kuwa ukosoaji wako wa CCM ni sawa na machozi ya samaki? Kama jibu ni hapana, unaeleza vipi kwa nini bado ni mwana CCM hadi leo Ijumaa tarehe 7, Desemba 2012?

Mkuu, may be labda demokrasia yetu haijakomaa lakini sidhani the fact kuwa mtu bado yuko CCM automatically anaunga mkono ufisadi.

Kama uko Chadema halafu kikatokea kuwa chama cha kifisadi utahama? If so, vipi chama utakachohamia nacho kikiwa pia cha kifisadi utahamia chama kingine? How long will you be doing this?

Do you run or fight for what you believe in? Kuna watu kibao tuu waliikimbia CCM na kujiunga na vyama vingine, lakini baadae wakaamua kurudi tena CCM.

This country doesn't need timid persons that run away from problems simply because that's what the others do. This country need persons who say "No way, it's my good damn right and I will stand up for it".

We don't need politicians wanaobadilisha vyama kama soksi vile. We need strong politicians who believe in what they stand for hata kama wengine kwenye chama wanampinga or practice the other way round.

Tuachane na fasheni ya kuhamahama vyama. It is not worth it.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom