CCM tuna hali mbaya sana, inasikitisha kweli!

Kwanza nianze kwa kusema, nimesikitishwa na kukosekana kwa watu makini wa kujaza nafasi sita zilizobaki kwenye wizara muhimu katika baraza hili la mawaziri.

Nina amini kabisa hata wengine wanaweza kukubaliana na mimi kwamba Raisi Magufuli ni mtu makini kwenye kazi yake na kutopitishwa kwa watu kama Membe, Nyalandu, Asha Migiro, Tibaijuka, Chenge, Kagasheki ni kuonyesha kwamba kwa kiasi kikubwa ufanisi na 'makandokando' hayana nafasi kwenye serikali ya JPM.

Ila pia kurudi kwa watu kama Makamba na Muhongo ni kudhihirisha sio kila anayelaumiwa na kusemwa, "hafai", na ukweli daima usimama baadaye.

MSHITUKO mkubwa niliopata ni hasa kuhusiana na kukosekana kwa watu KAMILI 34 kwenye baraza la mawaziri hasa kwenye wizara muhimu sana ILHALI ccm tuna wabunge 277+... Mimi nimesikitika sana kwamba wana ccm hasa wateuliwa hawana uzoefu au weledi wa kujumlishwa kwenye kuongoza taifa to the extend that Raisi ilibidi atoke nje ya wabunge wa ccm wateule kwenda kutafuta walioko nje ili waje kujazia.

Kwa kipindi kirefu niliamini kwamba walioweka CCM dosari ni watu wachache wasiozidi 20 (hasa wale waliokuwa kwenye uongozi hivi karibuni), sikujua tatizo ni kubwa sana kiasi hiki kama alivyotuonyesha Raisi Magufuli.

Watu wote 277+ hata wale wasiofahamika hawafai? Hali ni mbaya ndani ya CCM.

SIKUJUA KAMA HALI NI MBAYA KIASI HIKI.

Kwa sisi Great thinker tunaona kuwa, sio kweli kwamba watu wamekosekana; Ni hivi.....

1. Kwanza walio teuliwa kuwa naibu waziri wa hizo waizara Ndio mawaziri ila kwa sababu nafasi ni sensitive, wamepewa muda waprove kama wanaweza (hii itamsaidia muheshimiwa kuepuka kufukuza waziri kwa muda mfupi)...Nafikiri unajua kuwa hakuna kuhamishwa kwa ambaye hata perfom

2. Uchaguzi wa znz hauja kamilika hivyo ni habari njema kwa Muheshimiwa kuwa anapata muda kidogo wa kutadhmini utendaji kazi wa mawaziri wake kabla ya kujaza hizo nafasi

Maji marefu darasa la nne, Deo Sanga la pili, Musukuma la saba, Jumanne Kishimba la saba, Njalu Silanga la nne sasa unategemea rais apate wapi mawaziri kama nyie CCM mlikataa wazo la Warioba kuwa mbunge walau aanze na digrii moja

Ongezea wabunge wenye degree ambao walifeli mitihani ya form four na form six
 
Nape Nnauye ndio KASOMA SANA CCM...haaaa...!! 🙆🙆 lol..!!

January Makamba unayemsifia ndio FORM 4 kafutiwa mtihani kwa kuiba... Mbaya zaidi Form 6, January Makamba ali score Div." 0 " ndio unamsifia... Prof. Muhongo alirudia std. 7 mara 3, sbb ya kufeli....!!! I think u have seen his personal behaviours, the worst of the worst...!!!
Hamis Kigwangala kaiba jina la mtoto wa mwingine... na sbb alifeli std 7, so alichukua jina la mtoto mwingine na kuendelea sekondari... hili ni kosa kuu...!!! Wengine wengiiii huko ni std 7 tupu.. sasa ulizia VITU MAALUM... ni vikuku tupu...!! 🚶🚶🚶

Sasa to you hao ndio unaona wana IQ nzuri, 👉🐗 even ur IQ is of the Lowest and poorest..!! Jichunguze...

👉 Ole Sendeka, alipata PCB div 0, ... A- level

CCM ulijua kuna mtu ANA AKILI...? Labda ya uwizi like Chenge...!!!
 
Ulikuwa unasikiliza hotuba za Kinana katika ziara yake ambayo Chadema waliita ya maigizo?
Ni ile ziara iliyoibua 'mawaziri mizigo".
Kinana alisema kweli kabisa.
Je ulisikia ahadi za JPM na safisha safisha ya ccm?
Hali mbaya na uozo uliokuwepo ccm ulokuwa sio siri labda tu kama uliamua kutoziamini taarifa za wana ccm wenyewe.

Nilimsikia Kinana, na nilimwelewa lakini wengi wa waliolengwa ni Mawaziri mizigo waliokuwa awamu ya nne, na inafahamika wengi walikuwa marafiki wa Raisi JMK. Kwahiyo to some extend ilikuwa inatarajiwa wengi wao walipewa kwasababu ya ukaribu na sio kwasababu ni 'competitive' kwenye kazi.

Ila mimi nilidhani ukitoa marafiki wa Raisi JMK, kuna wengi walikuwa wana uwezo mkubwa lakini hawakupata nafasi ya kuongoza serikali kwasababu tu hawakuwa karibu na Raisi Kikwete. Na ndio hawa nilikuwa natarajia kung'ara na Raisi JP Magufuli.
 
Kwa sisi Great thinker tunaona kuwa, sio kweli kwamba watu wamekosekana; Ni hivi.....

1. Kwanza walio teuliwa kuwa naibu waziri wa hizo waizara Ndio mawaziri ila kwa sababu nafasi ni sensitive, wamepewa muda waprove kama wanaweza (hii itamsaidia muheshimiwa kuepuka kufukuza waziri kwa muda mfupi)...Nafikiri unajua kuwa hakuna kuhamishwa kwa ambaye hata perfom

2. Uchaguzi wa znz hauja kamilika hivyo ni habari njema kwa Muheshimiwa kuwa anapata muda kidogo wa kutadhmini utendaji kazi wa mawaziri wake kabla ya kujaza hizo nafasi

Kwahiyo unamaanisha:-

1. Manaibu ndio mawaziri, wamepewa internship - hilo lina support mawazo yangu kwamba HATUNA WATU 'ready made' WALIO TAYARI kuendesha serikali -

2. Wawakilishi ZNZ kupitia CCM ni kidogo sana kulinganisha na utitiri wa wabunge wa JMT (250+) - hilo pia lina prove my point kwamba hatuna watu kamili kutoka CCM wanaoweza kuendesha serikali.
 
Hahahaaaaa wewe ni Kiroba na nyumbu katika yale malofa yanayotajwa nawe ni Mmoja. Hata mimi ni Chadema lakini nasikitika sana katika miaka 20 ya kujenga chama na tambo zote tumekosa wagombea hadi kukodi fisadi na muuza mishikaki kugombea urais?
 
sio kwamba watu hawapo wakujaza hizo nafasi ila amekosa kuwatambua umakin wao kazn. Hataki kukurupuka anamchunguza mtu na kujua utendaji wake kiundan.

Hayo mnayotaka ya kujaza nafasi tu pasipo kujua ni mtu gani amewekwa ilimradi nafasi imejazwa ndio hayo yaliyompoza vasco da gama wa msoga

Nini kilimfanya awahi kutangaza wakati bado alikuwa anawachunguza,halafuhawa si ndio alikuwa anawanadi na kuwaita majembe.
 
Ni rahisi zaidi kwa Ngamia kupenya kwenye tundu la sindano kuliko kumpata KIONGOZI mweledi, msafi na makini kutoka CCM!!

Kwanza nianze kwa kusema, nimesikitishwa na kukosekana kwa watu makini wa kujaza nafasi sita zilizobaki kwenye wizara muhimu katika baraza hili la mawaziri.

Nina amini kabisa hata wengine wanaweza kukubaliana na mimi kwamba Raisi Magufuli ni mtu makini kwenye kazi yake na kutopitishwa kwa watu kama Membe, Nyalandu, Asha Migiro, Tibaijuka, Chenge, Kagasheki ni kuonyesha kwamba kwa kiasi kikubwa ufanisi na 'makandokando' hayana nafasi kwenye serikali ya JPM.

Ila pia kurudi kwa watu kama Makamba na Muhongo ni kudhihirisha sio kila anayelaumiwa na kusemwa, "hafai", na ukweli daima usimama baadaye.

MSHITUKO mkubwa niliopata ni hasa kuhusiana na kukosekana kwa watu KAMILI 34 kwenye baraza la mawaziri hasa kwenye wizara muhimu sana ILHALI ccm tuna wabunge 277+... Mimi nimesikitika sana kwamba wana ccm hasa wateuliwa hawana uzoefu au weledi wa kujumlishwa kwenye kuongoza taifa to the extend that Raisi ilibidi atoke nje ya wabunge wa ccm wateule kwenda kutafuta walioko nje ili waje kujazia.

Kwa kipindi kirefu niliamini kwamba walioweka CCM dosari ni watu wachache wasiozidi 20 (hasa wale waliokuwa kwenye uongozi hivi karibuni), sikujua tatizo ni kubwa sana kiasi hiki kama alivyotuonyesha Raisi Magufuli.

Watu wote 277+ hata wale wasiofahamika hawafai? Hali ni mbaya ndani ya CCM.

SIKUJUA KAMA HALI NI MBAYA KIASI HIKI.
 
Maji marefu darasa la nne, Deo Sanga la pili, Musukuma la saba, Jumanne Kishimba la saba, Njalu Silanga la nne sasa unategemea rais apate wapi mawaziri kama nyie CCM mlikataa wazo la Warioba kuwa mbunge walau aanze na digrii moja

Umemsahau La Kairo Yule Wa Rorya,nasikia Alikomea Chekechea Enzi Hizo Ikiitwa Vidudu,akalala Mbele!!
 
Ccm wengi na wabunge wao hawajasoma ukienda lindi huko mtwara ruvuma ndo usiseme mamburura tupu
 
Narudia Tena,watz Wasipojifunza Kupitia Huu Uteuzi Wa JPM Kuwa Wabunge Wa Ccm Ni Mizigo Kwa Taifa,basi Mungu Awalaani Tu.Kipindi Cha Uchaguzi Watu Walichagua Kishabiki Wakidhani Wanakomoa Upinzani Kumbe Hata Rais Wao Mpendwa Nae Yamemuathiri.
 
Hapa tumepata funzo, kumbe kesho nzuri ni lazima iandaliwe leo; wengi walichagua wabunge kwa kutegemea kesho nzuri itaandaliwa kesho. sasa haya ndo matokeo. Kuna haja kubwa ya sisi wapiga kura kujitathimini vigezo tunavyotumia kumchagua mtu kuwa mbunge. pamoja na sifa nyinginezo lakini elimu, maadili mema ya uongozi ni miongoni mwa sifa muhimu sana tunazozipuuza. So tuamke!!!!!!
 
Nape Nnauye ndio KASOMA SANA CCM...haaaa...!! 🙆🙆 lol..!!

January Makamba unayemsifia ndio FORM 4 kafutiwa mtihani kwa kuiba... Mbaya zaidi Form 6, January Makamba ali score Div." 0 " ndio unamsifia... Prof. Muhongo alirudia std. 7 mara 3, sbb ya kufeli....!!! I think u have seen his personal behaviours, the worst of the worst...!!!
Hamis Kigwangala kaiba jina la mtoto wa mwingine... na sbb alifeli std 7, so alichukua jina la mtoto mwingine na kuendelea sekondari... hili ni kosa kuu...!!! Wengine wengiiii huko ni std 7 tupu.. sasa ulizia VITU MAALUM... ni vikuku tupu...!! 🚶🚶🚶

Sasa to you hao ndio unaona wana IQ nzuri, 👉🐗 even ur IQ is of the Lowest and poorest..!! Jichunguze...

👉 Ole Sendeka, alipata PCB div 0, ... A- level

CCM ulijua kuna mtu ANA AKILI...? Labda ya uwizi like Chenge...!!!

Mdau hii analysis yako kali sana👏👏👏👏👏👏👏👏
 
Hapa tumepata funzo, kumbe kesho nzuri ni lazima iandaliwe leo; wengi walichagua wabunge kwa kutegemea kesho nzuri itaandaliwa kesho. sasa haya ndo matokeo. Kuna haja kubwa ya sisi wapiga kura kujitathimini vigezo tunavyotumia kumchagua mtu kuwa mbunge. pamoja na sifa nyinginezo lakini elimu, maadili mema ya uongozi ni miongoni mwa sifa muhimu sana tunazozipuuza. So tuamke!!!!!!

Hilo lianzie kwenye kura za maoni ndani ya Vyama
 
Ccm wengi na wabunge wao hawajasoma ukienda lindi huko mtwara ruvuma ndo usiseme mamburura tupu

maeneo ya kusini hasa mashariki na visiwani, mwamko wa elimu huko chini, na hayo ndio ngome ya CCM. tubadilike, dunia inabadilika, CCM tubadilike.
 
Narudia Tena,watz Wasipojifunza Kupitia Huu Uteuzi Wa JPM Kuwa Wabunge Wa Ccm Ni Mizigo Kwa Taifa,basi Mungu Awalaani Tu.Kipindi Cha Uchaguzi Watu Walichagua Kishabiki Wakidhani Wanakomoa Upinzani Kumbe Hata Rais Wao Mpendwa Nae Yamemuathiri.

wakati mwingine, nahisi kama Raisi JP amefungwa mikono hana nyenzo ndani ya wabunge wa CCM, amepewa boksi la zawadi, ndani hakuna kitu cha maana.

Hapa tumepata funzo, kumbe kesho nzuri ni lazima iandaliwe leo; wengi walichagua wabunge kwa kutegemea kesho nzuri itaandaliwa kesho. sasa haya ndo matokeo. Kuna haja kubwa ya sisi wapiga kura kujitathimini vigezo tunavyotumia kumchagua mtu kuwa mbunge. pamoja na sifa nyinginezo lakini elimu, maadili mema ya uongozi ni miongoni mwa sifa muhimu sana tunazozipuuza. So tuamke!!!!!!

kabisa, na hii hali haitabadilika, maana mpaka tuanze kupeleka watu shule, sio chini ya miaka 5-10 ndio tuwe na cream ya watu waliowekeza kwenye vichwa vyao. huko UVCCM ndio sehemu nzuri ya kuanza, maana juu ya UVCCM sidhani kuna samaki wabichi bado, na hauwezi kumfundisha mbwa mzee sarakasi mpya.
 
hizo wizara zote ndio ufisadi umejaa,atakuwa anataka kupasafisha sema ameona kutumia hajapata mtu itakuwa nafuu kidogo.
 
Back
Top Bottom