CCM tuna hali mbaya sana, inasikitisha kweli!

CCM tuna hali mbaya sana, inasikitisha kweli!

Kuna umuhimu wa mbunge awe na elimu kuanzia kidato cha nne au sita kwenda mbele maana chama fulani kimejaza wasema "ndiooooo" na wagonga meza tu
 
JE ANGEKUWA NA BARAZA KAMA LA JK WIZARA KIBAO!!
=> HAYA NDO MADHARA YA KURA ZA WIZI
=> WABUNGE 270+ UNAKOSA JE ANGEPEWA 90 TU, INGEKUWAJE?

NOTE: ccm ni ile ile
 
Pole sana.Wewe ni mkweli.Ila nasikitika sana kwamba watanzania tulio wengi ufahamu wetu ni mdogo sana,ndio maana viongozi wetu inakuwa rahisi sana kutudanganya.Tupende kusoma na kutafuta taarifa ili tusidanganyike kirahisi.

Lakini niseme kwamba hata hao mawaziri kutoka CCM Rais aliowaweka kwenye serikali yake sio kwamba wanafaa,lahasha.Sina shaka yeyote kwamba watu kama akina Muhongo,Mwakyembe,Nape na Mwigulu Rais amewaweka kwa shinikizo la CCM.Si watu wenye sifa nzuri kwa kuwa wengine wana tuhuma za ufisadi na wengine tabia zisizokubalika kimaadili katika jamii yetu.Naamini kabisa kwamba kama Magufuli asingekuwa na shinikizo kutoka CCM, kusingekuwa na waziri hata mmoja kutoka CCM.Hivi inaingia akilini kwamba Nape ni waziri kweli,hata kama wizara aliyopewa haina umuhimu kihivyo.Kuna mambo mazito nyuma ya pazia.

Nape, huyu sidhani kama ni chaguo la mkuu wa kaya. Ni shinikizo la ccm. But time will tell. Mchana kweupe wataumbuka. Ajiandae kulivunja na kuapisha kila mwaka.
 
Siamini kuwa ameshindwa kuwapata, ninachoona anataka muendelee kusubiria kama makinda ya ndege kana kwamba hao mawaziri watakuwa na jipya lolote.
Kwa upande wa magufuli, hiyo itamfanya aendelee kuwa kwenye midomo yenu na kwenye vyombo vya habari (vya mijini) angalau hadi bunge litakapoanza.

Nahisi humu umeangukia bahati mbaya hili si jukwaa lako!
 
Nape, huyu sidhani kama ni chaguo la mkuu wa kaya. Ni shinikizo la ccm. But time will tell. Mchana kweupe wataumbuka. Ajiandae kulivunja na kuapisha kila mwaka.

Kuna wawili watatu naona kama wamelipwa fadhila hata 'chemistry' wakati wa kuapishwa haikuwepo, ila tutaona.

Muda ni mtoa siri mzuri.
 
upo sawasawa mkuu hili ni tatizo kwa ccm

CCM tuna matawi vyuoni, na hata ughaibuni. Kwanini tusiwape nafasi wasomi na watu waaminifu.. Hawa darasa la nne na saba tunawapa ubunge alafu huko mbeleni tunashindwa kuwaangalia machoni kuwapa uwaziri kwasababu hatutaki kubadilisha badilisha baraza.

Hiyo ni strategy ya kukata tawi tulilokalia.
 
Kingunge Alivyosema hivyo walimponda, ila January Makamba akaja akasema Magufulia amerudisha uhai ndani ya ccm. Baada ya kusema hivyo nikaamini Kingunge alikuwa sahihi. Na Rais ameonyesha kweli hakuna mtu anayefaa ccm. Ndio maana anarudisha walewale. Na sitarajii rais akachagua wabunge wakuteuliwa kama kweli analengo la kubana matumizi.
 
hii inatokana FIGISUFIGISU ZA UPATIKANAJI WAO MAJIMBONI INAKUWA NGUMU KWA MKUU WA NCHI KUWATEUWA WATU AMBAO UWAKILISHI NI KIFIGISUFIGISU HIVI. MM NAMUUNGA MKONO ATEUE TU PENGINE NA MIMI ATANITEUA KTK NAFASI ZILIZOBAKI
 
Lusinde alishawahi kuwa mesi wa CCM pale aliposema nchi inahitaji mtu mmoja tu ili ipone.
Magufuli ashauriwe ampe nafasi Tena alikuwa chachu ya ushindi wake kitengo cha matusi.
 
Kingunge Alivyosema hivyo walimponda, ila January Makamba akaja akasema Magufulia amerudisha uhai ndani ya ccm. Baada ya kusema hivyo nikaamini Kingunge alikuwa sahihi. Na Rais ameonyesha kweli hakuna mtu anayefaa ccm. Ndio maana anarudisha walewale. Na sitarajii rais akachagua wabunge wakuteuliwa kama kweli analengo la kubana matumizi.

ni wakati tubadilike, tuache kuwa chama cha wacheza bao (sio kwamba nataka kuwatukana watu wa Pemba). Ila mtu aende shule ndio apewe uongozi.. Kwenye taasisi nyingine haupiti pita vyeti kwanini CCM tusifanye hivyo pia?

Tukiendelea kuwapa madaraka watu kutokana na maneno mengi badala ya kichwani wamewekeza nini.. Kuna mambo mawili yatatokea.. 1. Either tutafeli kama awamu iliyopita au 2. Tutakwama kama kwenye awamu hii.
 
Hivi Kagasheki si alishindwa ubunge? Migiro na Membe nao waligombea wapi vile au ulitaka wateuliwe? kwahiyo hao walioteuliwa hawafai? Nadhani Dr Magufuli kaziweka kando teuzi katika wizara hizi mpaka ahakikishe madudu yoote yaliyopo kwenye wizara hizo kaya compile in a single file na kutumbua majipu yote! wizara nyeti kama maliasili na fedha huko kuna mafisadi papa na ndo chimbuko la mdororo wa uchumi wetu.
Tumpe muda Mh Rais ila nakubaliana nawe kwamba CCM hakuna watu wa kucover hizo wizara inabidi tu awatoe nje ya BUNGE.
 
Ashumpta mshana huyu mama ni kichwaa sana sijui kwann ameachwa kuna lusinde huyu jamaa naye ni mtaalam sana kuna prof maji marefu huyu jamaa angefaa sana wizara ya afya kuna murad sadiq na aziz abood hawa wangefaa sana wizara ya uchukuzi kuna dahh list ni ndefu sanaaa

sasa huyo jamaa ukimpa uchukuzi si ataua njia za reli, waha na wasukuma waende kwao na mabasi yake?
 
kwa wabunge wengi wa ccm wana hali mbaya sana. wanachojua ni mipasho tu....
 
Inategemea na vigezo vya rais.kuwa mbunge hakukuhakikishii uwaziri
 
Kwanza nianze kwa kusema, nimesikitishwa na kukosekana kwa watu makini wa kujaza nafasi sita zilizobaki kwenye wizara muhimu katika baraza hili la mawaziri.

Nina amini kabisa hata wengine wanaweza kukubaliana na mimi kwamba Raisi Magufuli ni mtu makini kwenye kazi yake na kutopitishwa kwa watu kama Membe, Nyalandu, Asha Migiro, Tibaijuka, Chenge, Kagasheki ni kuonyesha kwamba kwa kiasi kikubwa ufanisi na 'makandokando' hayana nafasi kwenye serikali ya JPM.

Ila pia kurudi kwa watu kama Makamba na Muhongo ni kudhihirisha sio kila anayelaumiwa na kusemwa, "hafai", na ukweli daima usimama baadaye.

MSHITUKO mkubwa niliopata ni hasa kuhusiana na kukosekana kwa watu KAMILI 34 kwenye baraza la mawaziri hasa kwenye wizara muhimu sana ILHALI ccm tuna wabunge 277+... Mimi nimesikitika sana kwamba wana ccm hasa wateuliwa hawana uzoefu au weledi wa kujumlishwa kwenye kuongoza taifa to the extend that Raisi ilibidi atoke nje ya wabunge wa ccm wateule kwenda kutafuta walioko nje ili waje kujazia.

Kwa kipindi kirefu niliamini kwamba walioweka CCM dosari ni watu wachache wasiozidi 20 (hasa wale waliokuwa kwenye uongozi hivi karibuni), sikujua tatizo ni kubwa sana kiasi hiki kama alivyotuonyesha Raisi Magufuli.

Watu wote 277+ hata wale wasiofahamika hawafai? Hali ni mbaya ndani ya CCM.

SIKUJUA KAMA HALI NI MBAYA KIASI HIKI.

Ulikuwa unasikiliza hotuba za Kinana katika ziara yake ambayo Chadema waliita ya maigizo?
Ni ile ziara iliyoibua 'mawaziri mizigo".
Kinana alisema kweli kabisa.
Je ulisikia ahadi za JPM na safisha safisha ya ccm?
Hali mbaya na uozo uliokuwepo ccm ulokuwa sio siri labda tu kama uliamua kutoziamini taarifa za wana ccm wenyewe.
 
Hivi Kagasheki si alishindwa ubunge? Migiro na Membe nao waligombea wapi vile au ulitaka wateuliwe? kwahiyo hao walioteuliwa hawafai? Nadhani Dr Magufuli kaziweka kando teuzi katika wizara hizi mpaka ahakikishe madudu yoote yaliyopo kwenye wizara hizo kaya compile in a single file na kutumbua majipu yote! wizara nyeti kama maliasili na fedha huko kuna mafisadi papa na ndo chimbuko la mdororo wa uchumi wetu.
Tumpe muda Mh Rais ila nakubaliana nawe kwamba CCM hakuna watu wa kucover hizo wizara inabidi tu awatoe nje ya BUNGE.

Waswahili kwa.sasa tunaskia 'TUMPE MUDA' Baadae yatakuja 'AMEANGUSHWA NA WASAIDIZI WAKE' hakuna cha muda tangu akiwa anawania urais alipaswa kuwa na tim yake kichwani,visingizio kibaaao,kuna wizara isiyo na madudu?kila wizara ina madudu,kuna mdau alisema hizo wizara ni muhimu ndo maana kaziweka viporo,nami najiuliza hizi alizoziteua sio muhim?
 
Back
Top Bottom