CCM tuna hali mbaya sana, inasikitisha kweli!

CCM tuna hali mbaya sana, inasikitisha kweli!

Kuna diwani wa ccm njombe kiapo chake kinasambazwa sana whatsapp . ukisikia anavoapa ndio utajua ccm tuna adui wa nne wa taifa baada ya wale3 tulioachiwa na mwalimu.
Rais hana jinsi msimlaumu kwa kusema ukweli kuwa hao200+ ni wabunge mizigo. Hata vichwa ivo 34 na naibu spika bado kawachomoa nje ya bunge na kuwapa vyote. Kama tungekuwa na katiba ya warioba nionavyo rais na cabinet wake wooote wasingetoka bungeni. Wasomi wote waliangukia pua kura za maoni. Msomi na mtoto wa balozi wema sepetu alishindwa pia ivo kuhitimisha watu wasomi wengi hawako bungeni. Kusingizia Zanzibar sio saw a mbona HUSSEIN Mwinyi katolewa uko? Rais hakuwa na jinsi bora kumrudisha muhongo kuliko umpe maji marefu na irene wizara!!
 
Mi nafikiri anataka aziweke sawa yeye mwenyewe zilizobak kabla hajamkabizi mtu,anahofia itaonekana anawaingilia.

Mkuu kauli yako sio nzuri. Iki kiswahili sio cha kuandika bila kukamilisha mkuu. Ukitumia ayo maneno hakikisha unaongezea kielezi , nomino au kivumishi aisee!
 
Wasomi wote waliangukia pua kura za maoni. !!

Hapo nadhani ndio kuna tatizo kubwa sana. Ni kama wengi ndani ya CCM hawathamini elimu na wenye elimu inabidi Raisi awatoe kutoka nje ya Bunge maana ndani walishanyimwa kuwa viongozi.
 
Maji marefu darasa la nne, Deo Sanga la pili, Musukuma la saba, Jumanne Kishimba la saba, Njalu Silanga la nne sasa unategemea rais apate wapi mawaziri kama nyie CCM mlikataa wazo la Warioba kuwa mbunge walau aanze na digrii moja

CHADEMA :Onesmo Nangole darasa la 7,Sugu la 7,Lema form 2,Mbowe kapata div '0' form 6,Kubenea ni kanjanja,Kalanga ni la 7,Jafari Michael hivyo hivyo
 
Wee mpuuzi acha upuuzi, una uhakika na hiyo ngazi ya elimu unayoitaja?. Wewe ni mvivu wa kufikiri....
 
Hapa tumepata funzo, kumbe kesho nzuri ni lazima iandaliwe leo; wengi walichagua wabunge kwa kutegemea kesho nzuri itaandaliwa kesho. sasa haya ndo matokeo. Kuna haja kubwa ya sisi wapiga kura kujitathimini vigezo tunavyotumia kumchagua mtu kuwa mbunge. pamoja na sifa nyinginezo lakini elimu, maadili mema ya uongozi ni miongoni mwa sifa muhimu sana tunazozipuuza. So tuamke!!!!!!

Ni mpaka pale kukiwa na TUME huru ya UCHAGUZI yenye meno na pia kukiwa na TAKUKURU isiyohitaji kuTAKAKAKURIWA.

Rushwa ya uongozi ndiyo inayozaa RUSHWA NA UFISADI.Tukiweza kusema hapana kwenye rushwa na Tume ya uchaguzi ikawa na meno ya kuwaondoa watoarushwa wote ili watakaoingia kwenye kinyang'anyiro wawe kweli wamechaguliwa kwa haki.
 
Hapo nadhani ndio kuna tatizo kubwa sana. Ni kama wengi ndani ya CCM hawathamini elimu na wenye elimu inabidi Raisi awatoe kutoka nje ya Bunge maana ndani walishanyimwa kuwa viongozi.

TUliambiwa wabunge atleat wawe wamemaliza form four tukaona HAKI za binadamu ni tatizo.Ngoja tuendelee hivi hivi tu
 
Wee mpuuzi acha upuuzi, una uhakika na hiyo ngazi ya elimu unayoitaja?. Wewe ni mvivu wa kufikiri....

acha matuc c unaweka facts tu
sema mf mbowe form vi shulle flani mwaka flani div ....
hizo ndio facts.
unapotukana halafu huna facts jf inakosa umaana
matuc pelekeni kule mtaani maeneo km haya ya watu wanaopingana kwa hoja ni facts tu ndo zinabeba hoja
 
Kwanza nianze kwa kusema, nimesikitishwa na kukosekana kwa watu makini wa kujaza nafasi sita zilizobaki kwenye wizara muhimu katika baraza hili la mawaziri.

Nina amini kabisa hata wengine wanaweza kukubaliana na mimi kwamba Rais Magufuli ni mtu makini kwenye kazi yake na kutopitishwa kwa watu kama Membe, Nyalandu, Asha Migiro, Tibaijuka, Chenge, Kagasheki ni kuonyesha kwamba kwa kiasi kikubwa ufanisi na 'makandokando' hayana nafasi kwenye serikali ya JPM.

Ila pia kurudi kwa watu kama Makamba na Muhongo ni kudhihirisha sio kila anayelaumiwa na kusemwa, "hafai", na ukweli daima husimama baadaye.

MSHITUKO mkubwa niliopata ni hasa kuhusiana na kukosekana kwa watu KAMILI 34 kwenye baraza la mawaziri hasa kwenye wizara muhimu sana ILHALI CCM tuna wabunge 277+... Mimi nimesikitika sana kwamba wana CCM hasa wateuliwa hawana uzoefu au weledi wa kujumlishwa kwenye kuongoza taifa to the extend that Rais ilibidi atoke nje ya wabunge wa CCM wateule kwenda kutafuta walioko nje ili waje kujazia.

Kwa kipindi kirefu niliamini kwamba walioweka CCM dosari ni watu wachache wasiozidi 20 (hasa wale waliokuwa kwenye uongozi hivi karibuni), sikujua tatizo ni kubwa sana kiasi hiki kama alivyotuonyesha Rais Magufuli.

Watu wote 277+ hata wale wasiofahamika hawafai? Hali ni mbaya ndani ya CCM.

SIKUJUA KAMA HALI NI MBAYA KIASI HIKI.

Afanye by partsan, ayende mpaka kambi ya wapinzani
 
Inasikitisha kundi lote hili tulilonalo bungeni watu karibia mia 3 hakuna anayefaa kujaza hizi nafasi..

Nia ya CCM iikuwa ni kupata watu wengi bungeni kwa akili ya kujibu Ndiyooooo! Habari ya uongoza watanzania haipo. Unategemea kwenye kundi hilo atoke waziri! Thubutu.Ujinga ndiyo silaha ya ccm.
 
Maji marefu darasa la nne, Deo Sanga la pili, Musukuma la saba, Jumanne Kishimba la saba, Njalu Silanga la nne sasa unategemea rais apate wapi mawaziri kama nyie CCM mlikataa wazo la Warioba kuwa mbunge walau aanze na digrii moja
kishmba hakusoma hata darasa moja believe me,mwingine ni stdVII leaver ni Lameck Airo
 
Siamini kuwa ameshindwa kuwapata, ninachoona anataka muendelee kusubiria kama makinda ya ndege kana kwamba hao mawaziri watakuwa na jipya lolote.
Kwa upande wa magufuli, hiyo itamfanya aendelee kuwa kwenye midomo yenu na kwenye vyombo vya habari (vya mijini) angalau hadi bunge litakapoanza.

Na litakapo kaa sasa, sjui! maana nahisi patakua hapatoshi kwa wenye style zile za kulalaaa wakikurupuka wao ni mkaofi tu , ipiteeeee bila kuja wanachokipitisha kinakuja kua na madhara gani kwa raia na taifa kwa ujumla. Mungu tusaidie tu waja wako baba
 
Wengi wao ni wanafiki.....wahujumu uchumi na wasio na mapenzi mema na Nchi zaidi ya matumbo yao....nahisi anajua kwa kasi yake wengi watamrudisha nyuma ndo maana kawapiga chini kaamua kuteua sura mpya

Japo kachemka kwa kiasi chake kama bianadam
 
Nia ya CCM iikuwa ni kupata watu wengi bungeni kwa akili ya kujibu Ndiyooooo! Habari ya uongoza watanzania haipo. Unategemea kwenye kundi hilo atoke waziri! Thubutu.Ujinga ndiyo silaha ya ccm.

Tena kuna mwingine alijaribi kuseama au kulaumu kiaina kwa nini JPM asinge chagua mawaziri kutoka kila mkoa akidhani kila mkoa una mtu anayefaa kushika huo uongozi. Yan kuna watu hawafikirii sana ila nikama wameagizwa kusema tu kulingana na maagizo.
 
kishmba hakusoma hata darasa moja believe me,mwingine ni stdVII leaver ni Lameck Airo

Vipi mmoja apewe uwaziri na mwingine unaibu???????????????? ccm choka mbaya ila washukuru Mungu Jembe anawabeba kimtindo.
 
Afanye by partsan, ayende mpaka kambi ya wapinzani

Thubutu yaaake, Hapo itakua ndo sawa yake ila atakua amewagusa watu flani pabaya, yan hapo ndo utajua kama ccm (chama) na JPM Mwana chama asiye na cheo chochote ndani ya chama)nani yuko juu.
 
acha matuc c unaweka facts tu
sema mf mbowe form vi shulle flani mwaka flani div ....
hizo ndio facts.
unapotukana halafu huna facts jf inakosa umaana
matuc pelekeni kule mtaani maeneo km haya ya watu wanaopingana kwa hoja ni facts tu ndo zinabeba hoja

Big up sana maana kuna watu wana midomo michafu humu!!!!!!!!!!!!! bora hata wasiopiga miswaki wana afadhali wakila mikongoraa kuliko huyo wa matusi yasiyo na tija.
 
Ni mpaka pale kukiwa na TUME huru ya UCHAGUZI yenye meno na pia kukiwa na TAKUKURU isiyohitaji kuTAKAKAKURIWA.

Rushwa ya uongozi ndiyo inayozaa RUSHWA NA UFISADI.Tukiweza kusema hapana kwenye rushwa na Tume ya uchaguzi ikawa na meno ya kuwaondoa watoarushwa wote ili watakaoingia kwenye kinyang'anyiro wawe kweli wamechaguliwa kwa haki.

Inabidi tuanze na KATIBA mpya ya warioba nda tume itapata mwanya wa kuwa huru na vyombo vingine kama takukukuru
 
Back
Top Bottom