Mwingereza
JF-Expert Member
- Jan 21, 2014
- 1,111
- 2,741
Kwa miaka mitano uwanja ulikuwa ni wetu. Tumewafunga minyororo ya miguuni, mikononi na hata shingoni huku midomo yao tumeyafunga kwa vitambaa. Uwanja ulikuwa ni wetu, tumewakejeli, tumewasimanga tumewaita kila haina ya majina huku wasiojulikana wakiwafanyia kweli bila kujulikana.
Tumewasweka lupango, tumewanunua kana kwamba ni mitumba. Tumetumia vyombo vya habari peke yetu. Tuliwazibia kila kona, ilikuwa ni CCM. Tumetembea vifua mbele huku tukijinasibu kama wana maendeleo. Polisi wamewatesa sana wana CHADEMA. Hawa jamaa wamekiona cha moto lakini bado wanapumua !
Tumeimba singeli za Stigllers Gorge, tumenunua midege, SGR, Flyovers, elimu bure, na kila haina ya maendeleo. Hatukuwa na kosa, tulikuwa weupe kama theluji bila kujua kwamba tulikuwa wachafu mithili ya nguruwe alijetumbukiza kwenye matope.
Ghafla bin vuu, maendeleo yote tuliyokuwa tunajivunia imegeuka kuwa kamba ya kutunyongea. Mwenyekiti wangu kakamatwa suruali chini Kibiti, "Anatoa Rushwa".
Maendeleo ya kujenga Uwanja wa ndege Kijijini Chato imegeuka kuwa kashfa ya karne.
Laiti tungalijua, tungewahacha hawa watu waongee, maana watu wangechoka mapema na hii mashambulizi yao isingekuwa kivutio kama ilivyo leo. Kwa hali iliyopo, ukigeuka kulia, watu wanataka kusikia nondo za Lisu. Kuhsoto wataka kumsikiliza Lissu. Kwenye daladala lissu, sehemu za starehe ni Lissu. Makanisani Lissu. Vijijini Lissu kila kona Lissu na Chadema.
Ingawa tumeziba vyombo vya habari kutangaza habari za Chadema, Instagram na mitandaoni ni hoja nzito za Lissu. Mbaya zaidi, muda wa kujitetea haitoshi nikiangalia miaka mitano na siku 60 za kampeni. hesabn haiku bali. Hatuwezi kutoboa
Mikutano yetu iliyokuwa Mubashara toka Ikulu, leo imegeuka kuwa Maigizo ya wana usalama kuchoma mahindi na bastola kiunoni. Maendeleo yetu ya Flyovers imekuwa Wapinzania kutaka kuuza Scrapper. Hoja mfu!
Bandugu kwa miaka mitano tumelikoroga. Sasa inabidi tulinywe. Mwaka huu kuiba kura ni kaa la moto na atakayethubutu anakwenda na maji.
Ama kweli majuto ni mjukuu!