SOBY
JF-Expert Member
- Sep 19, 2011
- 1,268
- 458
Sera/itikadi ndiyo zinazo affect the rule of law.Kila ninapokutana na maneno kama haya hubaki nikijiuliza hivi Watanzania tuna laana gani. Hii hoja ukiitafakari kwa ndani unabaki tu unajiuliza mwandishi alitaka kufikisha ujumbe gani na kwa wasomaji wa aina gani. Je mwandishi huo ujumbe ameuelekeza kwa Watanzania kwa ujumla wao bila kujali itikadi zao au wana CCM peke yao. Kwa vyovyote vile na bila kujali ujumbe uliwalenga watu wa aina gani kuna mapungufu makubwa kwenye ujumbe huu ambayo ni vigumu kuyanyamazia.
Picha ninayopata kwa haraka haraka ni kuwa yawezekana mwandishi, kama walivyo wananchi wengi, anaamini kutoka moyoni mwake kuwa Tanzania bila CCM haiwezekani. Kabla sijaendelea kuchangia kwenye hii mada namwomba mwandishi atoe ufafanuzi kidogo kuhusu mchango wa watu kama sisi ambao tunaamini kwa dhati kabisa kuwa tatizo kubwa linalotukabili Watanzania sio sera wala itikadi bali utawala madhubuti unaoheshimu sheria, ambao CCM imeshindwa kuusimamia kwa miaka 27.
Since 1992, tumeona ufisadi na uroho wa fedha unavyoweza kuifanya sheria yeyote nchini ionekane kama ni wimbo wa kihindi, ambao haueleweki.
Ingawa mimi si mwandishi, ningependa kuchangia kwamba itikadi huzaa sera ambazo zinaelekeza utawala jinsi ya kutunga sheria ambazo hazina budi kuheshimiwa, kwa sabababu consequences zake zitakuwa deadly.