Alwatan
JF-Expert Member
- May 19, 2009
- 409
- 129
Siku mbili zilizopita nilimuuliza Alwatan swali moja, ingawa swali lilikuwa wazi kwa kila mtu kwamba Je, ikiwa tunakubaliana kimsingi kwamba CCM imekuwa haina dira kwa miaka 20 sasa; na pia haina itikadi ya kweli (Kinadharia na majukwaani ni Ujamaa na Kujitegemea, Kivitendo na kisera ni Azimio la Zanzibar likitekeleza sera za soko huria bila kulichuja), na kama tunakubaliana pia kwamba itikadi ndio dereva/ubongo wa chama chochote, na kama haieleweki basi survival ya chama hicho ni kwa nguvu uncontrollable na actors ndani ya chama; kama tunakubaliana na haya, ni dhahiri kwamba ili CCM iweze kubakia katika siasa za ushindani, ni lazima chama kimeguke kiitikadi:
Upande mmoja uwe na yale yanayotekelezwa sasahizi ya soko huru bila mchujo, sera ambazo hata mshindani wa karibu wa CCM – CHADEMA wanazitekeleza; vyama vingine vingi vya upinzani;
Upande mwingine kiwe kipande cha CCM kinachosimamia mazuri ya azimio la arusha ambayo tumeshayataja huko nyuma;
Iwapo tunakubaliana hadi hapa, nadhani basi kinachosubiriwa ni uthubutu na siasa za mitego za 'anza wewe';
Swali ambalo nilimuuliza Alwatan, pamoja na wengine ni kwamba:
Je best way for Chama kumeguka ni kwa viongozi waliopo sasa (walio waadilifu, wazalendo na wanaokunwa na kauli ya Mwalimu kwamba upinzani wa kweli lazima utokee CCM na kwamba CCM sio mama mzazi wa mtanzania yoyote), hawa wameguke na in the process kuchota wanachama meaning a top - down approach, au the best way ni wanachama wenyewe kwa wingi kumeguka i.e. bottom – up, wanachama wenyewe waamke na kutaka chama chao chenye elements nzuri za azimio la Arusha (badala ya kwenda upinzani moja kwa moja baada ya kupata uelewa na elimu kwamba kote ni yale yale)?
Kwani ukweli uliowazi ni kwamba wakulima ambao ni maskini na wengi sana vijijini, wafanyabishara ndogo ndogo (machinga), wafanyakazi wa kipato cha chini, wanafunzi waliokufa matumani ambao muundo wan chi unawa lebal kama ‘failures' (darsa la saba na kidato cha nne), wote hawa hawana mtetezi wa kweli ndani ya CCM na CHADEMA ya sasa; na ni dhahiri kwamba kwa hali ya maisha yao, hawapo tayari kushiriki kikamilifu katika soko huria kwani hawakuandalia bali walishtukizwa; wanahitaji maandalizi ya hali ya juu nay a muda mrefu yatakayoongozwa na itikadi iliyo radical na inayohimiza ‘ownership of our development agenda'; Watanzania waliojiandaa kikamilifu kushiriki katika soko hruia la kushtukizwa kama kufumaniwa ilikuwa ni wanasiasa wachache, bureaucrats wachache na wafanyabiashara wa aina mbalimbali ambao katika kipindi chote cha Ujamaa walikwua wanashirikiana na mabepari wan je to undermine Mwalimu; Wanasiasa na bureaucrats wengi mabadiliko yalikuwakuta wakiwa katika nafasi nzuri za kutekeleza sera za azimio la Zanzibar kwa vitendo na hivyo kujinufaisha;
Kwa maelezo haya, nadhani si vigumu kuona kwamba pakiibuka CCM ya kutetea wanyonge, tayari the prospective political party kina support base kubwa sana tayari inayosubiri kuelimishwa zaidi na kuhamasishwa; kilichobakia ni kitu cha ku - ignite tu the process;
Wana JF, kwa mawazo yenu/mtazamo wenu, njia ipi ni bora katika hili, top - down approach au bottom - up approach? Ni suala lilo wazi kwamba kuna wana CCM ambao wanaona hizi hoja ni za kiwendawazimu; lakini hii sio ajabu kwani tuna wana CCM wengi katika uongozi ambao wamejaa fikra mgando, ubinafsi, na unafiki; kwa wengi wao sio rahisi kuona hili kwani wao CCM ni ajira yako,sio utumishi kwa umma; hali zao za kimaisha na zile za wanaowaongoza hazifanani, nah ii ipo reinforced katika itikadi ninayoizungumzia; Viongozi wa namna hii hawajui kwamba siku moja wanachama wa CCM, hususan vijana ambao kutwa wanaimbishwa kwamba ‘imani yetu ni kulinda na kutetea siasa ya ujamaa na kujitegemea', huku viongozi meza kuu wamekaa na wakitabasamu kibepari, na kuangalia saa zao ili kubaini kama muda wa kwenda kwenye biashara umefika au lah, - siku vijana hawa wanachama wa CCM watakapoamka na kutambua kwamba kumbe imani yao sio imani sahihi, itakuwa too late kwa viongozi wa CCM to determine the fate of such an event; sote tunajua umuhimu wa kutocheza na imani ya mtu, imani ambayo mtu unalelewa na kuiamini ndani ya maisha yako ya kila siku;
Kinachoisaida CCM kutokumbana na demands from the bottom kwa sasa ni sababu nyingi lakini moja ya zile muhimu ni bahati – inawezekana ilikuwa ni mkakati lakini nitaita bahati ya Chama kujiingiza katika mchakato wa kutafuta maoni ya wananchi juu ya mfumo wa vyama vingi miaka ya mwanzo ya 1990 kabla wananchi hawajajua nini kinaendelea katika dunia ya sasa ya mageuzi ya kidemokrasia; Wananchi walichagua kubakia na chama kimoja (80% ya wananchi walitaka hivyo), hii kwa maana nyingine ni kwamba waliona waendelee na siasa za Ujamaa na Kujitegemea, kwani hata kama kulikuwa na mabadiliko kidogo katika maisha yao tofauti na miaka ya nyuma, hawakupewa elimu yoyote juu ya mazuri na mabaya ya Ujamaa, badala yake walishtukizwa tu na kuingizwa katika mageuzi ya kiuchumi bila maandalizi, ingawa haikuwa muda mrefu wakaanza kuona tofauti kubwa katika maisha yao kwenye maeneo ya huduma za jamii n.k; Vinginevyo pamoja na ukweli kwamba uongozi wa CCM ndio ulio administer mchakato wote kuingia vyama vingi na sio through popular demand, b dhahiri kwamba hapakuwepo na njia mbadala bali kuruhusu vyama vingi; kilichoipa bahati CCM ni umiliki wa mchakato mzima, ndio maana hadi sasa wanachama wengi hawana utamaduni wa to demand from the bottom – up; kwani democratic transition Tanzania in Tanzania was top - down – wanachama wengi wa CCM perceived/still perceive kwamba ni uongozi wa CCM ulioamua kuruhusu upinzani na kwamba ilikuwa kwa hiyari, sio ulazima; bado wananchi wengi wanaona kwamba kwa kufanya hivyo ilikuwa moyo wa huruma kuwaruhusu wapinzani kushiriki katika siasa za ushindani; vinginevyo kama CCM ingechelewa kidogo tu na kupelekea demands for such changes ziwe bottom - up driven, CCM ya sasa ingekuwa tofauti sana, na pengine isingekuwepo madarakani leo hii;
Ndio maana ya swali langu kwamba, kwa wale wanaokubaliana na hoja kwamba CCM kumeguka is not only inevitable but desirable, kwa mazingira ya leo, njii sahihi ni sahihi, top - down (kusubiri viongozi kadhaa wajiengue ) au bottom up (kuwaamsha, elimisha and mobilize wanachama, vijana husasan) halafu watafute viongozi wao au kukaribisha watakaojiengua na kujiunga na wanachama hao?
Mkuu Mchambuzi, kwanza nashukuru kwa kuendeleza mjadala wenye afya kwa Taifa.
Binafsi ningependelea the Bottom up approach, ila kwa hali halisi ya ukondoo wa watanzania(ya kusubiria nani aanze kujitoa muhanga), nadhani the Top bottom approach ndiyo itakua na the loudest bang.
Ni second nature katika mila nyingi za kiafrika kuwa wasikivu kwa viongozi, au wale tunaowa"perceive" kuwa ni viongozi wetu. Hivyo basi ufa mkubwa ukianzia juu, na kukawa na wasemaji wazuri(articulate speakers) wa kufafanua ni nini hasa tatizo na kwanini wameamua waliyoamua, ninaamini bado watanzania wengi >30yrs wanakumbukia the good old days ambako kila mtanzania alikua ni ndugu yako, uzalendo ulikua ni kitu cha kujivunia, na kujitegemea ilikua ndiyo shabaha yetu.
So yeah, I would go for the Top Bottom Approach PROVIDED baada ya uchaguzi wa 2012 mambo yatakua ni yaleyale. Hatutaki kwenye uchaguzi mkuu wa 2015 tulazimishwe kuchagua between Red Apples and Green Apples. They are all apples...
Otherwise walete katiba mpya itakayoruhusu Independent Candidates...