CCM, TRA inawahujumu na itawaangusha

Mimi nilisha achia zaidi ya magari 4 miaka 2 iliyopita nikachanganyikiwa hadi nikasahau na kuzoea na kuanza A. Unanunua gari $2600 lipo Dar, ushuru $4,600!!!
duu Mungu tunusuru
 
Hakuna msukumo wa kisiasa hiyo ni fact. Wakuu wa Idara zote wamewekewa malengo ya kukusanya kodi ambayo ni ya juu sana inabidii na wao wapige kodi za juu. Ukichunguza mzunguko wa kifedha (buying and selling) upo chini sana sasa unategemea hiyo kodi itatoka wapi. Wafanyabiashara kutoka DRC na Zambia walikuwa wanakuja kununua bidhaa kariakoo kwasasa hawaji jiulize why. Mheshimiwa Rais Magufuli achukue hatua za haraka la sivyo uchumi utazidi kudorora. Bandari ya Dar sehemu kubwa ya kazi yao ni mizigo ya Transit tu.
 
Kma imefkia hapo basi hawana nia njema na wafanya biashara.
 
Weka ushahidi tu manake maneno mengi hayasaidii
 
Hahaa...siku nyingine umzabue kofi
 
Hakuna cha Chadema wala CCM bali mfumo mbovu wa Uchumi.
 
Nyie msi walaumu TIARAEI.
Tatizo ni target wanazo pewa na hofu ya kutumbuliwa.
Mm kama mfanyabiashara ni kweli tuba hali ngumu sana sana.
Jamaa wakija kwako ni shiida sio suala la rushwa ila wanataka waonekane wanafanya kazi.
 
Huyu aliyeandika hapa kulingana na maelezo yake bila shaka ni mfanyakazi wa TRA.Alishihudia huo ubambikaji.Why in the first place msiweke matozo halali mpaka tuanze kuAppeal na kupelekana kwa maboss?
 
Nyie msi walaumu TIARAEI.
Tatizo ni target wanazo pewa na hofu ya kutumbuliwa.
Mm kama mfanyabiashara ni kweli tuba hali ngumu sana sana.
Jamaa wakija kwako ni shiida sio suala la rushwa ila wanataka waonekane wanafanya kazi.
Kuonekana kufanya kazi ni pamoja na kusimamia kwenye haki.Kwanini wafanye uonevu?
 
U


Umasikini unakusumbua
Lipa kodi kwa maendeleo ya nchi,hizo porojo zenu na ujanjaujanja wa kijinga umepitwa na wakati.

Poleni kwa kushikwa pabaya.

Tunajenga nchi,Tanzania kwanza.
 
Ushahidi usikae kwenye vijiwe vya kahawa zunguka ufanye mahojiano na research na wafanyabiashara na wafanyakazi wa TRA utapata jibu.
Wewe ndiye uliyeleta hoja km sikosei,vivyohivyo jukumu la kuithibotisha ni lako si la mtu mwingine.Please weka ushahidi manake who aserts must proof
 
Mlizoea mteremko lipeni kodi kwa maendeleo ya Taifa.

Mzigo wa $4600 kodi milioni 16, halafu unawaambia watu walipe kodi..
Mkuu hujawahi kufanya biashara, na kama ungekuwa mfanya biashara ungejua kwa nini watu hukwepa kodi..
Kodi Tanzania sio rafiki kuanzia kwa mfanya biashara mpaka mfanyakazi, tukiwa na mawazo huru tutajenga hii nchi..
 
Toa maelezo ya kutosha na yaliyosheheni ndo ueleweke
 
Muda mwingine naona kama TRA inalaumiwa bureeeeee... ili kuondosha mzigo inatakiwa taasisi nyingine kama TBS au TFDA na zingine...
 
Alianza sumri kauza mabasi kaenda kulima, sasa hivi katagi zinauzwa nae kaenda kulima, muro kabakiza zakuleta hela ya mboga, happy nation nae kauza, green star kauza, hajjs kayakatakata screpa, bado mnawadanganya watu kuwa mnakusanya kodi? Muda sio mrefu mtarudisha kodi ya kichwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…