CCM tawi la mitandaoni! Kulikoni?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
284,401
738,620
Tumebebwa na mang'azi yatokanayo Dodoma mpaka kuna ombwe umeshindwa kuliona na hili ni tangu ishu ya Bashite (special one)
Kuna kundi la propaganda mitandaoni maarufu kama lumumba buku 7! Hili kundi ni noma wanajua fitina majungu na vijembe kwa kiwango cha juu mno
Kundi hili lilianza kudhoofika taratibu baada ya uchaguzi awamu ya tano...likaanza kupotea taratibu likionekana occasionally kwa kulenga lakini bila mvuto
Halafu akajitokeza mdau mmoja aliyekuwa na cheo cha kujipa? Cha MWENYEKITI wa CCM mitandaoni.... Lakini huyu jamaa kwa kiasi fulani alikuwa positive sana hata kwa ishu za wapinzani...naona wakaona hafai.... Amepotea simsikii tena
Kwenye mkutano huu mada zimekosa msisimko kwakuwa LUMUMBA BUKU 7 wameingia mitini mazima
Je ni coincidence au kuna kitu kinaendelea? Hii si kawaida yao kabisa

Sent from my INFINIX-X551 using JamiiForums mobile app
 
Wanazisoma # kimya kimya mkuu
Kufikia 2020 hatutakua na department ya propaganda toka Lumumba tena
Tutabaki kina sie waganga na masangoma tu
 
Hawa jamaa huwa hawajielewi hata wanatetea nini..

Hizo 7000 wanazohongwa zinawalevya kiasi kwamba wanasahau wazazi wao waliowaacha huko mikoani ndo wanateseka na sera za hovyo wanazozitetea..

CCM ya sasa haitaki shobo ndo maana wameanza kupoteana..

Sent from my INFINIX-X551 using JamiiForums mobile app
 
Hali ya yao kifedha mbaya Mkuu. Makusanyo kwa maelezo ya Kikwete yalistahili kuwa bilioni 12 kwa mwaka kutoka kwenye Ada za wanachama milioni 8 lakini wanakusanya milioni 500 tu! Hayapendwi MACCM! Sasa labda hata buku 7 kwa siku zimekula mkasi ili kunusuru ukwasi wa chama.

Tumebebwa na mang'azi yatokanayo Dodoma mpaka kuna ombwe umeshindwa kuliona na hili ni tangu ishu ya Bashite (special one)
Kuna kundi la propaganda mitandaoni maarufu kama lumumba buku 7! Hili kundi ni noma wanajua fitina majungu na vijembe kwa kiwango cha juu mno
Kundi hili lilianza kudhoofika taratibu baada ya uchaguzi awamu ya tano...likaanza kupotea taratibu likionekana occasionally kwa kulenga lakini bila mvuto
Halafu akajitokeza mdau mmoja aliyekuwa na cheo cha kujipa? Cha MWENYEKITI wa CCM mitandaoni.... Lakini huyu jamaa kwa kiasi fulani alikuwa positive sana hata kwa ishu za wapinzani...naona wakaona hafai.... Amepotea simsikii tena
Kwenye mkutano huu mada zimekosa msisimko kwakuwa LUMUMBA BUKU 7 wameingia mitini mazima
Je ni coincidence au kuna kitu kinaendelea? Hii si kawaida yao kabisa

Sent from my INFINIX-X551 using JamiiForums mobile app
 
Ukweli ni kuwa Pesa waliokuwa wanaipata kutoka kwa vigogo mbalimbali wa CCM sasahivi imekata(haipo na kama ipo basi inatolewa kidogo sana)

Na tukumbuke UVccm ndio wanaoongoza maisha ya kujikomba komba. (rejea historia ya Bashite)

Hivyo wameona Biashara wanayofanya kwa sasa hailipi.

Kuna member wa lumumba kila akitoa thread anaweka na namba za simu, lakini sasa haonekani.
 
Maisha Kwasasa Hata Nao Wanayao Yalivyo
Huku Jukwaani Huwa Hatuwezi Kukitetea Chama Chochote Cha Upinzani Ikiwa Konakosea Tena Dhahiri.

Ila Mleta Mada Hao Vijana/Wazee Wa Lumumba 7000 Ni Kama Hawaikubali Ccm Ila Wanajitoa Akili Kuitetea Hata Baada Ya Kuona Wako Kimya Sana Maana Yake Chama
Hakibebeki Hata Kinavyofanya Ni Kinyume

Ila Nchi Hii Hasa Ndani Ya Ccm Kuna Ganzi Sana Watu Wanataka Kusema Ila Mkulu Amekuwa Mtata Yaani Leo Dodoma Wamepiga Kula Ya Ndiyo Kienyeji Kabisa

Wangewapa Wajumbe Karatasi Halafu Kura Zikahesabiwa Hadharani
Tungeona Vioja Kweli Kweli

Kwakifupi Chama Hakiuziki/Hakibebeki Ila Basi Tu Ndiyo Maana Hilo Kundi Limekosa Nguvu Siyo Mitandaoni Hata Watu Wa Ccm Kila Kona Nchini Hawana Amani Pia Hawajivunii Ccm Tena
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom