Elections 2010 CCM Primaries: Somebody got to say it... "It borders stupidity!"

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Well the way CCM primaries are supposed to work toward getting candidates for different political offices in the General Elections. Watch this:

TAREHE
TUKIO
21/7/2010
Mara baada ya muda wa kurudisha fomu kumalizika saa 10 jioni, Kamati za Siasa za Wilaya zitafanya mikutano ya pamoja na wagombea wao wa nafasi za Udiwani, Ubunge au Uwakilishi, waliorudisha fomu; kwa madhumuni ya kujadili na kuafikiana juu ya ratiba na vituo vya mikutano hiyo; michango ya usafiri wa pamoja wakati wa mikutano ya kampeni; na kukumbushana juu ya umuhimu wa kila mgombea kuzingatia maadili ya Chama Cha Mapinduzi na miiko ya uchaguzi wa ndani ya Chama chetu.

22 - 31/7/2010
Kipindi cha Mikutano ya kampeni ya wagombea
Ubunge/Uwakilishi na Udiwani.

1/8/2010
Siku ya Upigaji Kura za maoni kwa wagombea wote katika Matawi.

2-3/8/2010
Kuandaa matokeo (siyo kutangaza MM) kwa ajili ya vikao.

5-6/8/2010
Kamati za Siasa za Wilaya kuwajadili wagombea (siyo kutangaza matokeo MM)Ubunge/Uwakilishi na Udiwani.

Kabla ya kuanza agenda ya kuwajadili wagombea, Kamati za Siasa za Wilaya zitafanya mikutano ya pamoja na wagombea wao waliopigiwa kura za maoni, kwa madhumuni ya kukubaliana juu ya suala la kuvunja makundi ya wagombea hao ili kuimarisha umoja na mshikamano ndani ya Chama chetu. (siyo kutangaza matokeo MM)

7/8/2010
Kamati za Siasa za Mikoa kujadili na kutoa mapendekezo (siyo kutangaza wagombea M.M) kwa Kamati Kuu kuhusu wagombea wote.

Ngazi ya Taifa

TAREHE
TUKIO
9/8/2010
Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa Zanzibar, kuwajadili wagombea Ubunge/Uwakilishi (siyo kutangaza wagombea MM) wa Majimbo na Viti Maalum Wanawake.

10-11/8/2010
Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa.

12-13/8/2010
Kamati Kuu kupendekeza wagombea (siyo kutangaza wagombea MM) Ubunge/Uwakilishi.

14/8/2010
Halmashauri Kuu ya Taifa kufanya uteuzi wa mwisho wa wagombea Ubunge/Uwakilishi wa Majimbo (siyo kutangaza wagombea MM) na wa viti maalum.

Well.. what the heli is wrong with this people.. if they don't trust their own voters why vote? Why don't they just announce who who on Sunday or Monday so we get over with it.. but for 15 days they are still discussing the same thing.

What suprise me, some people who are considered to be educated are willing to participate in this illusion of democracy! Am I wrong to call this arrangement bordering stupidity?
 
Mzee mwanakijiji
Unategemea chama cha kifisadi kiwe na taratibu za nuruni?
 
Well the way CCM primaries are supposed to work toward getting candidates for different political offices in the General Elections. Watch this:

Well.. what the heli is wrong with this people.. if they don't trust their own voters why vote? Why don't they just announce who who on Sunday or Monday so we get over with it.. but for 15 days they are still discussing the same thing.

What suprise me, some people who are considered to be educated are willing to participate in this illusion of democracy! Am I wrong to call this arrangement bordering stupidity?
.

Mzee MKJJ, huo ndio utaratibu waliona unafaa kwa chama chao. Wamejifunza kwa makosa yaliyofanyika Zanzibar mwaka 2000 pale Kamati Maalum (CCM), Zanzibar ilipompa alama juu kabisa Dr. Bilal na za chini kabisa Karume, majina yalipoletwa NEC panga likamshukia Bilal na Karume akabebwa na NEC Bara, na aliposhinda tuu, akaiweka kando timu nzima ya Komandoo, isipokuwa yule Mzee wa TISS, (Mwakanjuki). Kilichofuatia sote tunakielewa.

Huu utaratibu ni kura za maoni tuu, mwenye uamuzi wa kutangaza ni vikao vya juu vya kufanya uteuzi ili kuzuia vilio vya kutotendewa haki na kudhibiti makundi, mathalani mgombea fulani ndio kipenzi cha wengi, nyinyi mpigieni tuu kura na hapo ndio mwisho wa kazi yenu na kusubiri maamuzi ya vikao vya uteuzi.

Matokeo yakitangazwa baada ya kura, watu wataanza kusherehekea ushindi kabla, halafu panga la NEC likiwashukia, nani huku chini atawaelewa. Hiyo process wanayoitumia ni kwa lengo la " Consolidation of Party Unity" na sio lack of transparence.

Wale ambao hamkuujua mlolongo huu, uko wazi kwenye website ya CCM, wale wapenzi tembeleeni kama wenzenu, ila hata wale wengine kama kina sisi, tunapita pita kote tuu for information seach, tuwe tunapenda au laa, kama alivyofanya Mzee Mwanakijiji na hapa ametufungua macho.
 
I agree with you its something of stupidity and a big lie to citizen. I thought on the next day we will know the contestants. ina maana kuwa siku hiyo ya kura za maoni watachagua zaidi ya mgombea mmoja. hebu nihabarishe.. kweli mi ignorant to that much.......!
 
Basi kwa maelezo ya Paco haina haja ya kura za maoni ni usanii mkubwa na danganya toto wa vigogo kwa wananchi.
 
Sasa wakati hayo yote yanaendelea, wale wote waliokuwa na nyadhifa serikalini na ndani ya chama wataendelea na nafasi zao. Hakuna namna ya kuwazuia kushininiza watangazwe kuwa washindi kwa heshima ya nafasi walio nayo dhidi ya voters.
 
Wameweka mlolongo huo makusudi ili watakaokuwa wameshinda kwenye kura za maoni na kupigwa panga kwenye vikao vya uteuzi wasipate muda wa kutimkia kwenye vyama vya upinzani.
 
Ila UDIWANI VITI MAALUMU matokea on the spot!!!!! wako toafutiii hawa jamaaa...
 
.

Mzee MKJJ, huo ndio utaratibu waliona unafaa kwa chama chao. Wamejifunza kwa makosa yaliyofanyika Zanzibar mwaka 2000 pale Kamati Maalum (CCM), Zanzibar ilipompa alama juu kabisa Dr. Bilal na za chini kabisa Karume, majina yalipoletwa NEC panga likamshukia Bilal na Karume akabebwa na NEC Bara, na aliposhinda tuu, akaiweka kando timu nzima ya Komandoo, isipokuwa yule Mzee wa TISS, (Mwakanjuki). Kilichofuatia sote tunakielewa.

Huu utaratibu ni kura za maoni tuu, mwenye uamuzi wa kutangaza ni vikao vya juu vya kufanya uteuzi ili kuzuia vilio vya kutotendewa haki na kudhibiti makundi, mathalani mgombea fulani ndio kipenzi cha wengi, nyinyi mpigieni tuu kura na hapo ndio mwisho wa kazi yenu na kusubiri maamuzi ya vikao vya uteuzi.

Matokeo yakitangazwa baada ya kura, watu wataanza kusherehekea ushindi kabla, halafu panga la NEC likiwashukia, nani huku chini atawaelewa. Hiyo process wanayoitumia ni kwa lengo la " Consolidation of Party Unity" na sio lack of transparence.

Wale ambao hamkuujua mlolongo huu, uko wazi kwenye website ya CCM, wale wapenzi tembeleeni kama wenzenu, ila hata wale wengine kama kina sisi, tunapita pita kote tuu for information seach, tuwe tunapenda au laa, kama alivyofanya Mzee Mwanakijiji na hapa ametufungua macho.

Wamejifunza nini hasa? Mbona wanachokifanya ni kile kile. Inanikumbusha maneno ya mwanafalsafa mmoja aliyesema 'mtu anayefanya jambo lile lile kwa namna ile ile akitegemea motokeo tofauti basi ujue huyo ni mwendawazimu!'.
 
Wameweka mlolongo huo makusudi ili watakaokuwa wameshinda kwenye kura za maoni na kupigwa panga kwenye vikao vya uteuzi wasipate muda wa kutimkia kwenye vyama vya upinzani.

Kyachakiche, nami naanza kuona mantinki ya mtazamo wako, nakumbuka mwaka ule Njelu Kasaka alipotemwa na CCM na kuanza mchakato wa timka timka alijikuta yuko time barred na miongozo ya tume ya uchaguzi. Mwenyezi Mungu abariki demokrasia katika nchi changa ili maslahi binafsi yasitawale!!!
 
Mama Mdogo na Kyachakiche sidhani kama ni muafaka kutaka watu waliotemwa na CCM kuja kugombea kwa vyama vingine waacheni wang'ang'anie huko huko wakitemwa mwishoni sisi tutakuwa tumepata watu wenye nia ya dhati ya mageuzi sio wanaotaka uongozi bila kujali wako chama gani.
 
Mani, nakubaliana na wewe kwa kiasi fulani. Lakini kumbuka kuwa, hawa wanaokuwa wameshinda kura za maoni (kihalali) ndio chaguo la wakaazi wa eneo husika. Kama itakujakutokea huko mbele wakaondolewa kwa mizengwe ya vikao vya juu(mafisadi) na kumpitasha mwingine ambaye alikataliwa na hao hao wapiga kura, na endapo eneo husika halijamsimamisha mgombea makini wa chama cha upinzani, basi huyu aki-cross huwa anashinda kirahisi sana. Mfano mzuri ni huyu huyu Dr. Slaa alipokataliwa na ccm. Kwa kubana muda hadi dk za mwisho, watu wa jinsi hii huwa wanakuwa wamepotea moja kwa moja kwenye ulingo wa siasa.
 
Kweli umenena. Ila wazee walishasema kuwa sikio la kufa halisikii dawa. CCM is surely going down unless wafanye kama walivyofanya ZNZ 1995 na 2000. Kama kweli hawataki kuleta uhasama basi wahakikishe wagombea hawajui matokeo ya kura za maoni (which is impossible). Mimi nafikiri wanachokifanya ni kuhakikisha kuwa wagombea watakaopigwa chini hawapati nafasi ya kuhamia upande wa pili. Hivi ni lini mwisho wa kuchukua form za ubunge???
 
Duh! democrasia ndani ya chama indeed!!!
These people are going down this time....even if we wont take them all the way, they will be walking on one leg for five years, the boom!!!
 
Now I understand when Mahatma Gandhi said to many "Democracy is a good idea.."
 
kama kura za maoni zinahitaji vikao vingine (karibu vinne) ili kujua matokeo why waste time?
 
MM nataka kujua kwenye hizo kura za maruhani ni akina nani wanapiga kura, wanachama wote wa CCM au kuna wateule.
 
Back
Top Bottom