Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 25,838
- 50,542
Kuna jambo limekuwa kama kitendawili kwangu, na sielewi tafsiri yake ni nini!
Kwenye maisha ya kawaida ya watanzania na huku kwenye mitandao ya kijamii, watu hupata wasiwasi na hatima ya mtu anayeikosoa CCM kuliko anayeikosoa CHADEMA.
Imekuwa ni kawaida mtu kuonywa ama watu kuandika maneno yenye kuashiria kuna jambo la hatari linaweza kumtokea mtu anayeikosoa CCM.
Lakini sijawahi kuona watu wakitia shaka kuhusu usalama wa uhai au maisha ya mtu anayeikosoa CHADEMA au viongozi wake.
Kuna wakati wanachama wa CCM au wafuasi wao husema maneno ya vitisho yenye kuonesha wanachadema na viongozi wao wanatakiwa kudhuriwa lakini hakuna mtu yeyote anayeonesha hao wana CCM uhai ama maisha yao yako hatarini.
Hebu wana CCM nisaidieni kutegua hiki kitendawil. Ni kwa nini nyie mkikosolewa watu waone hao wanaowakosoa wamo hatarini lakini chadema wakikosolewa hakuna mtu anayeonesha hao wakosoaji wa CHADEMA wamo hatarini?