Nilisha sema humu kila siku kuwa wakina
Nape Nnauye na ccm ni waasisi wa vurugu za kidini na wao ndio wapanda chuki kwa wananchi!
Ccm wanafikiri wanapo tumia dini, ukanda na makabila kuitusi chadema wanafikiri madhara yake ni kwa chadema tuu kumbe ni taifa zima na matokeo yake tunayaona kila hiitwapo leo!
Nilishangazwa na kauli za jk za kukemea wanasiasa kutumia dini kuwagawa watanzania wakati anajua fika chama chake ndio kinara wa hizi propaganda na naona leo wameona madhara hayajatosha sasa wakiongozwa na
Nape Nnauye wameendelea kuhubiri udini!
Nape Nnauye hii dhambi haitamuacha mtu na haitakuwa na mshindi kabisa, utatoa meno jukwaani kwa kufikiri umeimaliza chadema kumbe unaimaliza jamii na kuhimiza utengano kabisa!
Mtatumia rasilmali nyingi kutatua matatizo ya kidini lakini dhambii hii ya kuwagawa watanzania haita waacha kamwe!
Naona hamjatosheka kuona damu za watanzania zikimwagika huku nyie mkichekelea!
Mli hubiri sana Cuf chama cha kidini mkaona madhara yake na bado mme hamia kwa chadema na bado hamjachoka kuona taifa linakuwa vipande vipande!
Pengine ccm ndio mnaongoza kumdharau rais jk kuliko wengine kwani sikutegemea mgeendeleza hizi propaganda zinazo sababisha watu wapoteze maisha!
Kwenye hili hakuna mshindi!
Chadema ni chama cha ukanda na kidini.. Iliundwa tume.. Katika wakuregenzi wanane.. Wanne wametoka kilimanjaro.. Minutes zimo humu (ameshika kijitabu)..