Muungano wetu uliundwa kwa njia ya legal manipulations and political expediency. Ndio maana muungano mpaka leo umejengwa chini ya shaky legal and political framework. Lakini kama nilivyojadili
#1 , kwa vile uhalali wa serikali chini ya Mwalimu Nyerere haukutokana na katiba per se bali masuala mengine makuu matatu niliyojadili, kwa ilikuwa ni rahisi kufunika chemchem ya moto mkali uliokuwa unafukuta chini ya framework hizi hafifu za kisheria na kisiasa.
Tukumbuke kwamba kwa mwalimu nyerere, serikali mbili haikuwa ni final destination bali mpito kuelekea serikali moja aidha under his watch au kwa wale watakaomfuatia baadae. Lakini cha ajabu ni kwamba, waliomfuatia wana-treat mfumo wa serikali mbili kama ni the alpha and omega. Chama gani duniani kina sera static? Sera inatakiwa kuwa dynamic kuendana na nyakati, lakini hasa, kuendana na matakwa ya umma. Kwa ccm kung'ang'ania sera husika wakati umma haukubaliani na sera hiyo ni kitu cha ajabu sana kwa chama kikongwe kama ccm.
Viongozi wa ccm wanasahau kwamba mwalimu aliwahi kutamka kwamba iwapo umma utapinga muungano, hatowapiga mabomu bali kukubaliana na matakwa yao. Mwalimu alitetea mfumo wa sasa kwa hoja na uzalendo uliotukuka na bila ya partisan bias ya aina yoyote ndio maana pamoja na mapungufu ya mfumo husika, mambo yalijadilika na people lived with hopes. Leo wanasiasa wa ccm hawana hata chembe ya uzalendo kutetea mfumo uliopo; hawaonyeshi hata mapenzi kwa taifa lao la tanganyika, na mbaya zaidi, hawana hoja zaidi ya kejeli, mipasho, matusi na vitisho kwa wale wanaopinga serikali mbili kwa hoja; Leo umma umekataa mfumo uliopo, watawala hawapo mbali kupiga mabomu wananchi iwapo wataandamana kama matakwa yao ya mfumo wa muungano yatakataliwa na bunge la katiba.
Viongozi wa ccm wanasahau kwamba muungano ulikuwa ni wa kisiasa zaidi kuliko kiuchumi, na katika hiki wazanzibari got away with a lot kama
Nguruvi3 anavyojadili kwa muda mrefu sana. Sasa watanganyika wamechoka na siasa za muungano ambazo haziwasaidii lolote na sasa wanataka uchumi uwe kipaumbele. Katika hili, baadhi ya viongozi wababaishaji ccm wanawatishia wananchi kwamba kiuchumi wataumia chini ya serikali tatu.
Wanasiasa wa aina hii hawawaelezi wananchi ukweli kwamba serikali mbili ndio mzigo zaidi kwa mwananchi, hasa mtanganyika kwani ni kwa mfumo wanaoutaka ccm, kwa kiasi kikubwa, mwananchi wa tanganyika ndiye anagharamia maisha ya mzanzibari na ya kwake kwa wakati mmoja; wanasiasa hawa wanaficha ukweli kwamba muundo wa serikali mbili umesababisha kuwepo kwa: *Wizara na taasisi zinazofanya kazi za muungano peke yake;
*zinazoshughulikia mambo ya Tanzania bara; na
*zinazoshughulikia mambo mchanganyiko yani ya muungano na yasiyo ya muungano.
Katika haya, hasa la tatu hapo juu, ni vigumu kutofautisha gharama za muungano na zisizo za muungano kwenye taasisi na idara husika.
Kwanini wanasiasa hawa wa ccm hawaelezi wananchi ukweli kwamba muungano ulikaa chini ya katiba ya muda kwa miaka karibia kumi na tatu kutokana na ugumu wa kuunda serikali moja? Kwanini hawaelezei umma kwamba miaka 12 baadae (1965-77) ndio TANU ikabuni muungano wa serikali mbili kwa imani kwamba muungano wa aina hiyo utawezekana tu chini ya one party state and one party constitution? Hii ndio maana nzima behind ndoa ya TANU na ASP;
Kama alivyoeleza
Nguruvi3, wa kumlaumu sio jaji warioba bali ccm wenyewe kwa kutosoma alama za nyakati. Vinginevyo waseme kwamba warioba alikuwa nyuma ya sakata la kina Mzee Jumbe 1984; mzee mmoja mkongwe wa chama ananukuliwa akisema kwamba Jaji Warioba alikuwa kwenye G55 kwa kujificha kwa kumuogopa mwalimu. Kwa watu wenye akili na mapenzi kwa taifa lao, hizi ni breaking news na ni habari njema sana kwani wengi tulidhania warioba ameanza kukubaliana na hoja ya tanganyika baada ya kustaafu. Actually this makes him more credible for job, na hakika, unlike wakongwe wengine wa chama, he will be on the correct side of our history. Pamoja na hayo, je cha ajabu nini kwa mwanasheria (warioba)kuwa upande wa G55, ikizingatiwa kwamba muungano uliundwa chini ya legal manipulations? Ina maana mkongwe huyu wa ccm anayemshambulia warioba anataka kutuambia kwamba mwalimu alikuwa sahihi na mfumo uliopo? Kwa kweli angekuwa na hoja angalau ya kisiasa iwapo angesema kwamba warioba awali alikuwa pro two governments.
Historia tayari inaweka wazi kwamba miongoni mwa makosa na mapungufu makubwa ya Nyerere, moja wapo ilikuwa ni imano yake kwamba muungano wa serikali mbili unawezekana. Pengine aliamini hivyo kutokana na serikali yake kupata uhalali kutawala nje ya uhalali wa kikatiba kama nilivyojadili, suala ambalo kwa hilo siwezi mlaumu mwalimu. Lakini nitamlaumu kiongozi yoyote ambae bado anaamini katika formula ya serikali mbili ambayo ilijengwa kwa kutegemea uwepo wa one party state and one party constitution, serikali ambayo haikuhitaji katiba ya nchi kupata uhalali wa kutawala. Lakini miaka 50 baadae, kiongozi ambae anatetea muungano unaotawaliwa na legal manipulations and political expediency, huyo hatufai kwani anatupeleka kubaya kama taifa.
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums