CCM na Hatima Ya Bunge La Katiba

CCM na Hatima Ya Bunge La Katiba

Huyo Mchambuzi wako analeta thread/mnakasha ambao ndani yake pana elements/pattern ya kuhalalisha na ku-justify ule uharamia woote wa Nyerere na jinsi alivyotuadhibu Watanzania chini ya ile One Party Communist almost Juche System...khalafu wewe unangia hapa na kumwambia aondoke!? Aende wapi sasa!?

Hivi nyinyi Chadema mna maarifa japo kiduchu ya kuazima!?

Kwa mfano Mkuu Mchambuzi anajaribu kutuaminisha yakuwa ati wakti wa Mwalimu aka "Baba wa Taifa"...ya kwamba baadhi ya sababu kadhaa zilohalalisha ile Katiba ya kinyama ya wakti ule na kumfanza Nyerere bado awe "Halali"...ametaja ati ni Azimio la Arusha na uwepo wa ati wale alowaita ndo popular and Charismatic Leaders kama vile Nyerere!? Looh!

Sasa embu tupeni majina ya hao Viongozi walokua/waliowahi ati ndo kupendwa na Wananchi wakti,au ndo mna maana ya yule Nyerere!? Duh!

Kama kwa sifa za aina hiyo...hata Hitler,Kim Il Sung na Family yake,Saddam Hussein na Hafidh Al Assad mbona hawa woote nao walikua ni popular and charismatic Leaders!?

Hao Viongozi madhalimu woote,nao kama Nyerere tu yaani hawakuwa na tafauti kubwa mno! Na kwenye chaguzi takriban zoote ndani ya nchi zao,nao pia kama vile yule Nyerere...walikua wakipata taakriban 80-90% ya Kura!? Duh!

Badala ya Mkuu Mchambuzi kujaribu kuudanganya umma wa Watanzania na ulimwengu ati yakuwa wakti wa utawala wa kidhalimu wa yule Nyerere,Watanzania walikua Loyal!? Looh!

Kwanini hamtaki kusema kweli yakuwa wakti huo Wananchi/Watanzania woote walikua hawana option yoyote maskini dhidi ya utawala wa kimabavu wa yule Nyerere!?

Nafikiri yeye Nyerere ndo Kiongozi pekee katika nchi yetu alofanziwa majaribio ya kutaka kumpindua zaidi ya mara tatu,kama sikosei!? Sasa hiyo Loyalty asemayo huyo ajiitae ndo Mchambuzi iwapi hapo!?

Nafahamu kwa yakini yakuwa Mkuu Mchambuzi na takriban hao wenzie nyoote alowa-tag kwenye hii thread/mnakasha ni wenye mwelekeo,lengo,madhumuni na mtazamo mmoja naye! Si kitu kibaya mno,ndo maana hapa jamvini hazitakuwapo hoja zenye maana...sababu upinzani khalis hautakuwapo asilan,abadan!!

Nimechungulia baadhi ya michango ya Wanajamvi wenye kujimudu kimaarifa japo kiduchu hapa jamvini...si weye pimbi ujiitae Parameter lakini!

Kwa kifupi nimehuzunika kiduchu!

Ukiangalia kiundani,wachangiaji woote mnamsifia yule Dictator Nyerere na utawala wake dhalim na kujaribu kumchafua mtu kama Rais wenu wa sasa Dr Kikwete...ambae katika kipindi kifupi mno cha utawala wake...pamoja na tafran na changamoto zoote zinazomkabili lakini amejitahidi mno kuimarisha mojawapao ya mambo makubwa vitu kama Democratic Institutions,freedom of speech and freedom of expression!

Nani alithubutu hata kuviota vitu kama hivyo wakti wa yule Nyerere!?

Mnaweza vipi nyinyi maharamia wa hoja,kuthubutu kuchangia tena ati kwa kuhalalisha makosa na nakma zoote yule Nyerere alizowafanzia Watanzania...lakini kwa unafiki ulotamalaki ndani ya nyoyo zenu,ati mnajaribu kuichafua CCM na Rais Dr Kikwete!? Looh!

Embu jaribuni kuwa objective na impartial japo kiduchu...kama kweli mwahitaji wangine wachangie kitaaluma na kuleta mazungumzo yenye uzalendo na tija kwa Taifa letu hili changa!

Yawaje leo hiyo CCM na Kikwete ati ndo wawe wabaya na history na Katiba yoote mwajaribu kuionyesha mapungufu makubwa!...kitu ambacho ni kweli,yaani kwa hili nakubaliana nanyi!?

Sasa yawezekana vipi hapa huyo Nyerere awe exonorated na asihusishwe/asizungumzwe kimapungufu kwayo au na huo muonao nyinyi yakuwa ndo uchafu/mapungufu ya hiyo CCM na hata chimbuko la haya yoote Taifa letu lipitiamo leo hii!? Kwani yeye Nyerere si ndo alokua mwasisi na mwandishi wa hiyo CCM na Pia Katiba iliyopo!?

Au kama si hivyo yakhusu nini basi nyinyi mum-glorify and/or glamourise kula kukacha mpaka kufikia kumwita ati Baba wa Taifa"!?

Nyinyi nyoote mkitajiwa tu yule Nyerere,hata kwa hoja zenye ukweli yakinifu...kwanini mwaruka Kimanga mpaka Salalah! Teeh! Teeh! Teeh!

Nimemsoma huyo Mchambuzi...ati anajaribu kutuhadaa hapa jamvini yakuwa mojawapo ya sifa kubwa za yule Nyerere ati alikua ni Pan-Afrikanist!? Looh!

Nyerere si ndo yule yule alionyesha ile Non Pan-Afrikanist views at International arenas/hadharani kwenye ule mgogoro wa Biafra...na mpaka kufikia kuingiza nchi yetu changa kwenye ule mgogoro mkali wa Nigeria...na kututia dosari la kuonekana Wazandiki na Wanafiki!?

Nguruvi3...anafahamu kiundani kabisa jinsi gani yule hasidi Nyerere alivyochangia kiundani kwa njia moja amma nyangine kuudhoofisha na mwishowe kuutokomeza ule Muungano wa awali hapo East Afrika-EAC!?

Sina haja asilan ya kujichosha mno kwa kutaja udhaifu na madhila kadhaa ili tujikumbushe tulipotoka na tusiwe wivi wa shukran.

Sasa kabla sijataja mangi kiundani...kwa hayo mawili kiduchu tu,kwanini mnajaribu kutuaminisha yakuwa huyo Nyerere ati alikua na sifa za Pan-Afrikanist!?

Nyerere alikua haamini asilan katika democratic institutions,democracy itself,freedom of speech/experssion...hii ni open secret kwenye World corridors of Politics...yaani kila mwenye akili na maarifa yake timamu anafahamu hili jambo!

Nyerere si ndo huyu huyu alokwenda kumsaidia yule haramia Albert Rene pale Seychelles(someone who was already implicated on systematic tortures and other Human Right abuses!) ili aendelee kuketi madarakani pale Seychelles...na Tanzania ikapeleka mpaka majeshi-JWZT kwa amri ya yule Nyerere!! Duh!

Kwa kifupi...Nyerere hakuwa intellectual capable wala hakuwa na integrity ya kupambana na nyakati/dunia mpya...yaani kwa kumsifia japo kiduchu,alishatambua yakuwa Watanzania tayari wameshaamka na wana fikara/mwamko mpya tena usio na woga asilan!

Kwa hiyo nyoote acheni au punguzeni kutuaminisha yakuwa ati Nyerere...aliamua tu kuachia kiti/nchi kwa mapenzi yake ya nchi/Taifa na Watanzania wenzie,au ati alikua akipenda/kuabudu mno Demokrasia!? Duh! Teeh! Teeh! Teeh!

Kwa kifupi...endeleeni tu na huo mchakato wenu wa Katiba hapa jamvini,lakini kila mtakapokua mwasema urongo,basi sisi tutakua twajawarekebisha kiduchu na kwenda zetu!

La si hivyo...yaani ikiwa twakaa tu kimya itakua hatuwatendei haki Watanzania wenzetu wangine,na pia itakua hata nyinyi pia hatukupendeni!? Maana akupendae ni yule akwambiae kweli!

Ahsantani sana!
Mkuu gombesugu

Hii bayana yako ni ulimbo tosha, ninaamini kabisa watu wamefyonza Ilm.
 
Last edited by a moderator:
Wakuu,

kuna umuhimu kwetu sote kurudi kwenye mada iliyo mbele yetu badala ya kulumbana kwa hoja zisizo na maslahi kwa suala lililo mbele yetu. Iwapo tofauti yetu no mawazo na mitazamo, basi tufanye hivyo kwa hoja. Watu wengi sana wanatusoma humu kwa vile wanaipa JF heshima kubwa. Tujaribu kuilinda heshima hiyo kwa manufaa yetu sote.

Nikirudi kwenye mada, nianze na hoja ya mzee kisumo. Inaniwia vigumu sana kuelewa msingi wa hoja yake ni nini, hasa anapomshambulia jaji warioba na pia kusema kwamba - kama mfumo uliopo wa serikali mbili una matatizo, yanaweza rekebishwa. Naungana na mdau mmoja humu aliyehoji kwamba hivi kweli Kisumo na uzoefu wake wote haoni mfumo wa sasa una matatizo? Hata mwalimu aliwahi kukubali mara nyingi tu kuna matatizo lakini tofauti ya mwalimu na wazee wa sasa, mwalimu aliujadili muungano kwa hoja, uzalendo and in a non partisan fashion, hivyo kupelekea kero zilizopo kujadilika na pia watu kuishi kwa matumaini kwani no doubt, nyerere was a visionary, and "visionaries inspire".

Ni vigumu kuelewa kwanini peter kisumo na wengine wenye mtazamo wake ndani ya ccm wanamlaumu jaji warioba 2014 wakati:

1. Kwa mara ya kwanza suala la muundo wa muungano lilikitokeza kwa hisia kali mwaka 1984 katika kipindi kilichoitwa "kuchafuka kwa hali ya hewa".

2. Mwaka 1991, tume ya nyalali ikaja na kupendekeza serikali tatu.

3. Mwaka 1993, kikundi cha wabunge "G55" kikaja na hoja ya serikali tatu, na hii ilikuwa karibia miaka kumi baada ya sakata la mzee aboud jumbe. Lakini pamoja na hayo, peter kisumo anaruka matukio mawili ya awali na kujadili suala la G55 as if wao ndio walikuwa innovators wa hoja husika. Tukumbuke kwamba bunge liliridhia mfumo wa serikali tatu kufuatia hoja ya G55.

4. Mwaka 1999 ikaja kamati ya jaji kisanga, nayo ikapendekeza serikali tatu.

5. Vile vile ziliundwa tume nyingi kujaribu kutatua kero za muungano kama vile kamati ya amina salum ali, shelukindo na nyingine nyingi. Zote hazikuweza kutatua kera za muungano.

Tume ya warioba ni lazima ilijiridhisha na matukio yote haya kabla ya kukaa na kutengeneza hadidu rejea. Na kimsingi, hoja zilizotolewa mwaka 1984 (sakata la jumbe) hadi tume ya jaji kisanga, hoja hizi zinafanana, lakini muhimu zaidi, wakati wa maoni ya kitaasisi na mtu mmoja mmoja kwa tume ya warioba 2013, msingi wa hoja ukawa ni ule ule ulioanza miaka 20 iliyopita. Kwanini CCM hailioni hilo na badala yake baadhi ya makada wake wanamshambulia warioba na tume yake?

Binafsi nadhani katika viongozi wachache wenye busara waliobaki ccm, pamoja na mapungufu yao ya hapa na pale ni rais kikwete na samual sitta. Kikwete alisoma alama za nyakazi na kukubali sio tu kuanzisha mchakato wa katiba mpya, bali pia kuwaeleza wana ccm juu ya umuhimu wa kujiandaa kisaikolojia na kurudi kwa Tanganyika. Samuel sitta nae anastahili pongezi kwa kukiokoa ccm kule zanzibar ambako aliiwakilisha serikali katika halfa ya uzinduzi wa muswada wa mabadiliko ya katiba. Umma wa wazanzibari waliuchoma mswaada ule kwa sababu uliwazuia kujadili muungano. Iwapo serikali ingekuwa imetuma viongozi wengine kama kina nanihii badala ya sitta, leo tungekuwa tunaongea mengine.

Pia ni muhimu tutambue kwamba ni wazanzibari ndio waliosaidia kuweka shinikizo suala la muungano liwe sehemu ya muswada husika, hivyo kutoa fursa kwa Tanganyika kujadiliwa. Hakuna ushahidi sehemu yoyote kwamba wananchi wa Tanzania bara walikuwa wamejiandaa to revolt. Kwa maana nyingine, tukubali ukweli kwamba madai ya Tanganyika kwa wabara walio wengi yana uhusiano wa moja kwa moja na harakati za wazanzibari kudai autonomy yao, na ni harakati hizo ndio zimewazindua watanganyika wengi kutoka kwenye usingizi mzito. Kwa hilo, binafsi nawashukuru sana wazanzibari.

Nikijikita kwenye hoja yangu ya msingi katika bandiko hili, tutazame, je malalamiko makubwa ya wazanzibari juu ya muungano ni yepi?

1. Tanganyika inafaidika zaidi kuliko Zanzibar kwani chini ya mfumo uliopo, Tanganyika ndio Tanzania. Hoja hii imejadiliwa na tume ya warioba kwa hoja kwamba "Tanganyika imevaa koti la serikali ya muungano".

Je kuna ukweli katika hili? Binafsi nasema NDIO, ukweli upo tena mkubwa sana lakini utaugundua iwapo utafanikiwa kutambua kiini macho kilichopo. Kwa mfano:

Kwa mujibu wa katiba ya JMT (1977), chombo chenye mamlaka ya kusimamia masuala ya muungano ni serikali ya muungano. Lakini pia chombo chenye mamlaka ya kusimamia masuala yasiyo ya muungano (the so called "Tanzania Bara"), pia ni serikali ya muungano. Kama hadi hapa tupo sawa, tuendelee:

Kwa mantiki hiyo, ni serikali ya muungano ndio inayoshughulikia sana masuala kama vile ujenzi, uchukuzi, afya, kilimo, maji, maliasili na utalii,elimu, nishati na madini, na mengine mengi tu ambayo kimsingi ni ya Tanzania bara na sio ya muungano. Iwapo tupo sawa hadi hapa, tuendelee:

Wakati wa vikao vya bajeti ya bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania (chombo ambacho kipo kuwakilisha maslahi ya wa zanzibari na watanganyika equally), je:

*bunge hutenga siku ngapi kujadili masuala ya Tanzania Bara (Tanganyika)? Siku mbili hadi Nne. Je:
*bunge hutenga siku ngapi kujadili mambo ya muungano? Nusu siku hadi siku moja!

Suala lingine muhimu ni kwamba - maswali ya wabunge kuhusu mambo yanayowagusa sana wananchi (development and poverty issues) yanahusu zaidi Tanzania bara na mambo haya bungeni yanasimamiwa na waziri mkuu ambae hana mamlaka wala madaraka ya aina yoyote kwa zanzibar. Je haki za kimaendeleo za wazanzibari katika bunge la JMT chini ya mfumo wa sasa zinasimamiwa na nani?

Lalamiko lingine kubwa la wazanzibari dhidi ya mfumo wa serikali mbili ni kwamba - mambo ya muungano yamekuwa yakiongezeka na hivyo kuathiri "identity" na "autonomy" ya zanzibar na kupelekea znz kuwa katika hatari ya kumezwa. Lalamiko hili pia kwa mtazamo wangu lina mashiko, na tumeshajadili sana huko nyuma jinsi gani mkataba wa muungano (1964) ulichakachuliwa na kufikisha taifa katika sakata la jumbe la 1984.

Lalamiko lingine kubwa la wazanzibar ni kwamba Rais wao ameondolewa katika umakamo wa rais wa JMT. Mkataba wa muungano ulimtaja rais wa znz kuwa makamo wa rais katika kipindi cha mpito kuelekea katiba mpya, lakini kama tunavyoelewa, mchakato wa katiba hiyo haukutokea, ikaja katiba ya muda ya JMT (1965) ambayo ikiangiza chama cha TANU kwenye muungano kinyume na mkataba wa muungano (1964). Pamoja na mapungufu yote haya, rais wa znz akaendelea kuwa makamo wa rais mpaka pale weakness za legal and political framework za union zilipokuja kuwa dhahiri kufuatia mfumo wa vyama vingi. Muungano ambao Nyerere alieleza umma kwamba umeiga muungano wa uingereza ambayo inafuata a unitary form of government, miaka ya mwanzo ya tisini jaji bomani akapewa jukumu la kutatua kitendawili cha muungano ndani ya mfumo wa vyama vingi, akaja na solution ya mgombea mwenza kwa kuiga mfumo wa federation wa marekani ili kuepusha ccm na aibu ya kupata rais wa ccm upande wa bara na rais wa Upinzani upande wa zanzibar. Hapa tukabaki kujiuliza, ni muungano gani huu unaoazima elements za federation wakati tuliambiwa msingi wake ni unitary?Ni katika mazingira haya, rais wa znz akaondolewa kwenye umakamu wa rais wa JMT. Sasa cha ajabu nini hapa kwa znz kuanza kufukiria mchakato wa katiba yake ambayo lengo ni kulipa taifa lao madaraka kamili?

Upande wa bara nao una malalamiko mengi lakini muhimu ni pamoja na:

1. Zanzibar imebadili katiba yake na kuchukua madaraka ya jamhuri ya muungano kwa mfano kuelekeza sheria za muungano zilizopitishwa na bunge la JMT kupelekwa kwenye BLW. Kwa mantiki hii, katiba ya zanzibar sasa ipo juu ya katiba ya JMT, na tukumbuke hapa kwamba katiba ya JMT ndio katiba ya Tanzania bara au ukipenda Tanganyika. Kwahiyo maamuzi juu ya hali za maisha ya watanzania bara au ukitaka watanganyika milioni 43 kuanzia 2010 yapo mikononi mwa BLW linalowakilisha wananchi sio zaidi ya milioni moja na nusu.

Lalamiko la pili kubwa kwa upande wetu Bara ni kwamba - wananchi wetu hawana haki ya kumiliki ardhi znz wakati wenzetu wa znz wanayo haki hiyo tanzania bara au ukipenda Tanganyika.

Eneo lingine na malalamiko upande wa bara ni kwamba - zanzibar sasa imekuwa ni nchi huru, ina bendera yake wimbo wa taifa serikali yake na imeshabadili katiba yake ili ijitambue kama nchi wakati kwa mantiki hii Tanzania bara imeshapoteza utambulisho wake kwani katiba ya JMT inasema Tanzania ni nchi moja wakati katiba ya znz inasema Tanzania ni nchi mbili. Katika hili, kuna makosa gani kwa rasimu ya katiba kusema Tanzania ni nchi inayotokana na Tanganyika na zanzibar? Kwani ni dhahiri katika suala la utambulisho wao kama taifa, zanzibar haitarudi nyuma tena.

Nadhani haya ni baadhi ya mambo ambayo wawakilishi wetu kwenye bunge lijalo la katiba wakayakumbuka.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Mkuu Mchambuzi,

Nini kilichokufanya upige about turn na sasa unakuja na hii historia ambayo sasa imekuwa wimbo wa taifa kwa wananchi wa Zanzibar.

Mbali ya nia yako njema ya kuleta huu mnakasha bado nakuona huutendei haki huu mnakasha wala hutendei haki wananchi wa pande zote mbili za Muungano kwa kumpa credit Mwalimu aka Baba Yenu wa Taifa.

Mwalimu hakuwa na niq hata ya saa limoja kuwapa wananchi nafasi ya kuubadili katiba kwa mawazo yao wenyewe wala kuujaadili Muungano. Hilo kwake ilikuwa ni Uhaini na kama alikuwa na vision basi asingali mlazimisha Mzee A.Jumbe kujiuzulu, wala asingali wapinga G55, wala asingalipuuzia mabali mapendekezo yoyote aliyopewa na taasisi yoyote.
Nakutanabahisha pia sio kweli kama hili suala la kero za Muungano zilianza kuibuka na sakata la Jumbe. Tumemsikia Mzee H.N.Moyo mara zaidi ya mbili kuwa katika 1970 walienda kwa Mwalimu kutaka baadhi ya mambo yale kumi na moja ya Muungano yapunguzwe na Mwalimu alikataa na.mwisho aliyachukuwa hata yale makbrasha.waliyokwenda nayo ili kuzima huo mwamko wa Serikali ya Zanzibar.

Umeleta mada nzuri lakini nakupa pole, watu kama kina Pasco na Parameter ambao wameishi ki kasuku kasuku wanauharibu huu mnakasha sababu wameshazoea itabidi uvumilie

Ahsante
 
I bet, this should be one of the best political analysis ever in Jf!

Am fed up, congratulation to analyst!

Wajumbe WA katiba wangeupitia huu Uzi, daaah!
 
Mr. Mchambuzi hongera kwa kunitisha. Yaani gwanda ulilovaaa na ulichoandika ni vitu vitatu tofauti yaani WEWE ni tofauti na CCM na ni tofauti na MAVAZI

ILA ukweli utabaki kuwa CCM wakiamua kwa scenario yoyote kati ya hizo lakini pia wakiwa wanafiki kwa kuwa 90% ni wao wenyewe kwa kuteuana kinamna, watapata wakati mgumu sana. Ni heri wapitishe tu halafu wamalizane na raia kwenye uchaguzi wa 2015 la sivyo wataisoma ramani.

WASIPOIPITSHA ccm hawatakuwa na namna ya kuwalaghai watanzania kuwa wana dhamira ya dhati ya muungano na utatuzi wa changamoto zilizopo.

WAKIPITISHA wamerahisisha kuondoka maana masuala ya wizi na kuogopeka kuwa baada ya uchaguzi nitakosa kibarua kwa wale waamuzi muhimu wa matokeo ya uchaguzi hautakuwepo na hivyo kushinda kihalali ni "issue".
 
Mkuu Mchambuzi,

Nini kilichokufanya upige about turn na sasa unakuja na hii historia ambayo sasa imekuwa wimbo wa taifa kwa wananchi wa Zanzibar.

Mbali ya nia yako njema ya kuleta huu mnakasha bado nakuona huutendei haki huu mnakasha wala hutendei haki wananchi wa pande zote mbili za Muungano kwa kumpa credit Mwalimu aka Baba Yenu wa Taifa.

Mwalimu hakuwa na niq hata ya saa limoja kuwapa wananchi nafasi ya kuubadili katiba kwa mawazo yao wenyewe wala kuujaadili Muungano. Hilo kwake ilikuwa ni Uhaini na kama alikuwa na vision basi asingali mlazimisha Mzee A.Jumbe kujiuzulu, wala asingali wapinga G55, wala asingalipuuzia mabali mapendekezo yoyote aliyopewa na taasisi yoyote.
Nakutanabahisha pia sio kweli kama hili suala la kero za Muungano zilianza kuibuka na sakata la Jumbe. Tumemsikia Mzee H.N.Moyo mara zaidi ya mbili kuwa katika 1970 walienda kwa Mwalimu kutaka baadhi ya mambo yale kumi na moja ya Muungano yapunguzwe na Mwalimu alikataa na.mwisho aliyachukuwa hata yale makbrasha.waliyokwenda nayo ili kuzima huo mwamko wa Serikali ya Zanzibar.

Umeleta mada nzuri lakini nakupa pole, watu kama kina Pasco na Parameter ambao wameishi ki kasuku kasuku wanauharibu huu mnakasha sababu wameshazoea itabidi uvumilie

Ahsante

Mkuu Khawarizm.

Nimesoma bayana zako zimenigusa sana ni vema kujikita zaidi kwenye mada kuliko huku tunakoelekea ,na haya yote kaleta Pasco na mwenzake.

Tukirudi kwenye mada mimi napenda kumuita Abdu Jumbe "The man who saw tomorrow" huyu mzee wetu aliona mbali sana kuhusu suala la serikali tatu,lakini sujui tuite udikteta/udhalimu wa Nyerere akaamua chambelecho watoto wa mjini akamchinjia baharini.

Kinacho nishangaza watu wengi wanaona/wanaitazama Zanzibar kama ni mzigo mkubwa kwa Tanganyika,mimi binafsi mpaka sasa hivi sijajua ni vigezo gani haswa walivyo vitumia au uelewa wangu mdogo ningeomba Nguruvi anithibitishie hili.
 
Wakuu,
afkuna umuhimu kwetu sote kurudi kwenye mada iliyo mbele yetu badala ya kulumbana kwa hoja zisizo na maslahi kwa suala lililo mbele yetu. Iwapo tofauti yetu no mawazo na mitazamo, basi tufanye hivyo kwa hoja. Watu wengi sana wanatusoma humu kwa vile wanaipa JF heshima kubwa. Tujaribu kuilinda heshima hiyo kwa manufaa yetu sote.
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Mkuu Mchambuzi, heshima mbele.
Asante kwa angalizo hili, nasisitiza kulizingatia.
Pasco.
 
Mkuu Mchambuzi,.
Umeleta mada nzuri lakini nakupa pole, watu kama kina Pasco ambao wameishi ki kasuku kasuku wanauharibu huu mnakasha sababu wameshazoea itabidi uvumilie

Ahsante

Wakuu,
afkuna umuhimu kwetu sote kurudi kwenye mada iliyo mbele yetu badala ya kulumbana kwa hoja zisizo na maslahi kwa suala lililo mbele yetu. Iwapo tofauti yetu no mawazo na mitazamo, basi tufanye hivyo kwa hoja. Watu wengi sana wanatusoma humu kwa vile wanaipa JF heshima kubwa. Tujaribu kuilinda heshima hiyo kwa manufaa yetu sote.
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
.
Zingatia!
Pasco.
 
Mkuu Khawarizm.

Nimesoma bayana zako zimenigusa sana ni vema kujikita zaidi kwenye mada kuliko huku tunakoelekea ,na haya yote kaleta Pasco na mwenzake.

Tukirudi kwenye mada mimi napenda kumuita Abdu Jumbe "The man who saw tomorrow" huyu mzee wetu aliona mbali sana kuhusu suala la serikali tatu,lakini sujui tuite udikteta/udhalimu wa Nyerere akaamua chambelecho watoto wa mjini akamchinjia baharini.

Kinacho nishangaza watu wengi wanaona/wanaitazama Zanzibar kama ni mzigo mkubwa kwa Tanganyika,mimi binafsi mpaka sasa hivi sijajua ni vigezo gani haswa walivyo vitumia au uelewa wangu mdogo ningeomba Nguruvi anithibitishie hili.

Ulamaa Boko,

Unajuwa hapo Tanganyika kuna vijana wengi wamepata fursa kusoma mpaka kuhitimu vyuo vizuri tu hasa vya Kanisa na kutoka kidedea lakini kuna kitu walicholishwa ambacho hawakijui nacho ni dhana ya dini ya kristo dhidi ya uislam. Na hii imepelekea kusomeshwa historia ya iliyichakachuliwa ya Tanganyika na Zanzibar.

Mimi nadhani kuna watu wengi humu JF labuda wana dhana kuwa Zanzibar ilikuwa ni break away state or province within Tanganyika na Muungano wa 1964 umeirejesha Zanzibar katika mamalaka ya Tanganyika.

Pia system au nguvu zinazotumika kutoa kauli mgando kama alotamka Pasco "Tuulinde Muungano kwa hali yoyote" zitaizipeleka nchi hizi pabaya.

Kwa kweli tukiwachunguza hawa wanaoimba nyimbo hizi ni wale viongozi wanaoishi kwa kutegemea vyeo vyao na nafasi zao za kazi kujinufaisha binafsi na kutegemea maisha yao katika hizo nafasi zao za kazi na utwaona viongozi hao kuwa hawana muono wa mustakbal wao wala hawana mipango yoyote ya baadae watakopoacha hizo kazi zao ama kwa kuondolewa au kustaafu. Sababu ni kuwa wao hata hilo neno kustaafu halimo katika akili zao. Fikira zao wavikalie viti mpaka wanaingiza makaburini.
 
Mkuu Khawarizm.

Nimesoma bayana zako zimenigusa sana ni vema kujikita zaidi kwenye mada kuliko huku tunakoelekea ,na haya yote kaleta Pasco
Wakuu,
afkuna umuhimu kwetu sote kurudi kwenye mada iliyo mbele yetu badala ya kulumbana kwa hoja zisizo na maslahi kwa suala lililo mbele yetu. Iwapo tofauti yetu no mawazo na mitazamo, basi tufanye hivyo kwa hoja. Watu wengi sana wanatusoma humu kwa vile wanaipa JF heshima kubwa. Tujaribu kuilinda heshima hiyo kwa manufaa yetu sote.
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Nimezingatia, naomba uzingatie, tuzingatie!
Pasco.
 
Ulamaa Boko,
Pia system au nguvu zinazotumika kutoa kauli mgando kama alotamka Pasco "Tuulinde Muungano kwa hali yoyote" zitaizipeleka nchi hizi pabaya.
Wakuu,
afkuna umuhimu kwetu sote kurudi kwenye mada iliyo mbele yetu badala ya kulumbana kwa hoja zisizo na maslahi kwa suala lililo mbele yetu. Iwapo tofauti yetu no mawazo na mitazamo, basi tufanye hivyo kwa hoja. Watu wengi sana wanatusoma humu kwa vile wanaipa JF heshima kubwa. Tujaribu kuilinda heshima hiyo kwa manufaa yetu sote.
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Nasisitiza tuzingatie angalizo hili.
Pasco.
 
Wazanzibari Hawahitaji mtu kama wewe na Pasco kuwatetea kinafiki, na wakati huo huo Mnapenyeza maneno ya kuwadhalilisha na kuwaona hawanba maana sana!

na istoshe kwa mtu mwenye Upeo wa kawaida tu wa kufikiri akisoma mabango yako na yule mwenzako Pasco, Atagundua 100% kuwa NYINYI SIO WAPENDA HAKI HATTA KIDOGO! Bali ni watu wa kujaribu kupotosha ukweli halisi na kupenyeza propoganda za NYERERE {Mnajifanya kuuma huku mnapuliza.} huo unaitwa UNAFIKI. na ni mbaya kuliko UCHAWI.

WAZANZIBARI HAWAKUHITAJI WEWE WALA MTANGANYIKA YOYOTE KUWASAIDIA KUPIGANIA HAKI ZAKO,TENA HASSA WALE WALIO NDANI YA HUO MFUMO KRISTO!
NA mwisho!Labda lugha inakupa tabu kidogo MI SINA HAJA YA KUKUTISHA WEWE! bali nimekutahadharisha kuwa NAKUTAZAMA UNAVYOMWAGA PUMBA HAPA JUKWAANI UKIZIITA, "MAWAZO YANGU BINAFSI"!

ILANI.
Shika heshima yako kuingiza jina la mzee Mohamed said ktk maongezi yangu mi na wewe, au sasa hivi utachukia huu uzi
!
Wakuu,
afkuna umuhimu kwetu sote kurudi kwenye mada iliyo mbele yetu badala ya kulumbana kwa hoja zisizo na maslahi kwa suala lililo mbele yetu. Iwapo tofauti yetu no mawazo na mitazamo, basi tufanye hivyo kwa hoja. Watu wengi sana wanatusoma humu kwa vile wanaipa JF heshima kubwa. Tujaribu kuilinda heshima hiyo kwa manufaa yetu sote.
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Hili ni angalizo muhimu kulingatia.
Pasco.
 
Mkuu Ritz, please zingatia
Wakuu,
afkuna umuhimu kwetu sote kurudi kwenye mada iliyo mbele yetu badala ya kulumbana kwa hoja zisizo na maslahi kwa suala lililo mbele yetu. Iwapo tofauti yetu no mawazo na mitazamo, basi tufanye hivyo kwa hoja. Watu wengi sana wanatusoma humu kwa vile wanaipa JF heshima kubwa. Tujaribu kuilinda heshima hiyo kwa manufaa yetu sote.
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Pasco.
 
Ajabu hizi zaonekana ni bora kuliko zile zilizoondolewa,

Kama huezi jibu huja za wanataaluma basi vema upite na kukusanya hayo maandiko/ data zao na uende zifanyia research may be zikakusaidia wewe au wanao na wangineo hata kwa baadaye kulikoni ukhanatha kama tuuonao hapa kwa hoyo Pasco.

Sms sent and delivered wether you like or not.
 
Last edited by a moderator:
Akili ya kuku wa kisasa, atamani kuondoka lakini ashindwa kwa madawa alokula mwenyewe,

Na katika ajabu kumchinja si lazima kutumia nguvu.

Yeye hufa hata kwa kelele tuu.

Alokushinda kwa huja, mahinde kwa ukimya, ya nini kudhihirisha mapungufu ulojikatia tama mwenyewe?@Pasco
 
kuna umuhimu kwetu sote kurudi kwenye mada iliyo mbele yetu kuilinda heshima hiyo kwa manufaa yetu sote.
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Hoja ni iliyo mezani.

Back
Top Bottom