CCM na Hatima Ya Bunge La Katiba

CCM na Hatima Ya Bunge La Katiba

Nguruvi3, Rutashubanyuma dudus, Makucha

CCM bado ina amini kwamba bado inaweza kufanya ukarabati mkubwa wa mfumo wa serikali mbili. Ni vigumu kuelewa kama ukarabati huo utafanywa na mchina au nani, lakini kilicho dhahiri ni kwamba given the history, legal and political foundations na maamuzi ya znz kwa mujibu wa katiba yake ya 2010, CCM inapoteza tu muda kudanganya wananchi, pengine for political expediency.
Nguruvi3 alitaka kujua hoja za ccm juu ya faida ya serikali mbili. Ebu tujaribu kulitazama hilo, katika muktadha wa ukarabati wa kichina to sustain serikali mbili:

Maeneo mawili makubwa yatahitaji mabadiliko: kwanza ni kuwa na mambo ya kutosha kwenye orodha ya ya muungano including issues za economy and development. Lakini hili likifanyika, matokeo yake ni kuzidisha malalamiko kwa wazanzibari kwamba hadhi na utambulisho wao kama taifa unapotea. Kwa upande mwingine, ukarabati uki involve kupunguza mambo mengi ya muungano, serikali ya muungano itaishia kushughulika zaidi na mambo ya Tanganyika, na katika hili, zanzibar itaona kwamba Tanganyika ndio muungano wenyewe. Lakini vile vile given mwamko wa watanganyika hivi leo, watanganyika nao wataona si haki nao wasiwe na uhuru wa kuendesha mambo yao kama ilivyo kwa zanzibar.

Eneo la pili linalo hitaji ukarabati wa kichina ili to sustain serikali mbili utahitaji:

Kuondoa mgongano na mgogoro wa kikatiba. Hapa maana yake ni kwamba Zanzibar kubadili katiba yake ili Tanganyika na zanzibar ziwe ni sehemu za nchi moja badala ya kuwa nchi kamili shiriki za muungano. Iwapo Tanganyika na zanzibar zitakuwa ni nchi kamili, haitawezekana kwa nchi moja kuwa na hadhi na uhuru wake na kuacha nchi nyingine isiwe na hadhi and autonomy yake.

Kwa kutazama haya mawili, ukarabati wa kichina wa ccm kwa muungano utakuwa ni mgumu. Ni kwa mantiki hii, solution pekee ni serikali tatu ili kila upande uwe na hadhi sawa ambapo kila upande utashughulikia mambo nje ya muungano huku serikali ya muungano ikibaki na machache ambayo yanaunganisha Taifa. Nje ya hapo, kama alivyopata tamka Nguruvi3, tuvunje jahazi na kila mtu achukue mbao zake, vinginevyo tutaingia kwenye machafuko.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mchambuzi, nadhani hawa CCM wanatuzingua tu na serikali zao mbili ambazo kimsingi sina tatizo nazo kama zitakuwa na support ya majority under free and fair opinions. Niko kinyume na mfumo wa serikali mbili simply kwa sababu CCM wanaung'ang'ania kinyume na MATAKWA YA WANANCHI.

Nikinukuu baadhi ya media, yafuatayo yalitamkwa na MDHAMINI WA CCM, Mzee Peter Kisumo kuhusu issue ya Muungano hapo jana (Jan. 16, 2014):

Kisumo amesema, yeye anaamini muundo wa Serikali mbili kama ulivyo sasa ndiyo mwafaka katika kulinda Muungano, na kwamba kama kuna kasoro zilizoainishwa na tume basi zitazamwe upya.
(Ref. ‘Warioba chanzo cha Serikali tatu’ - Kitaifa - mwananchi.co.tz na https://www.jamiiforums.com/katiba-...i-warioba-ndiye-chanzo-cha-serikali-tatu.html)

Ameniacha hoi hapo kwenye red na ndio aina ya utendaji ambao CCM imekuwa nao kwa miaka 50 ya Muungano; yaani kutoa tu statements za jumla bila suluhisho. Eti "kama kuna kasoro zitamwe upya"! Hivi kasoro za Serikali mbili bado hazijaeleweka kwa baadhi ya wateule wetu kwa miaka yote hiyo? Huu mtindo wa "funika kombe mwanaharamu apite" hauwezi kutufikisha popote bila suluhisho la kudumu hata kama litakuwa chungu namna gani.

Nakubaliana na mdau mmoja aliyesema kwamba CCM walikuwa na kila aina ya fursa kwa zaidi ya miaka 50 kurekebisha kasoro za muungano lakini ama kwa makusudi au kwa bahati mbaya hawakutaka kufanya hivyo. Sidhani kama kwa sasa tunahitaji statements za akina Kisumo zisizotoa japo mwanga wa jawabu.
 
Bila kuongea mengi ni kwamba hakuna nchi yoyote ya "aina moja" na Tanzania ambayo kwa miaka ya karibuni imeweza kutengeneza katiba kwa chini ya miaka mitano. .. kwani sisi Tanzania ni nani. Katiba itapatikana chini ya serikali ijayo
 
Tuko Nyerere alipoona wimbi la mageuzi ya vyama vingi halizuiliki alisoma alama za nyakati akaondoka na kumwachia mwingine aanze alipoishia.

Kikwete hakufanya homework vizuri.Alitaka afanye ambush ya katiba kwasababu kuu mbili
1. Muungano ili watu wasiwe na muda wa kutafakari
2. Kuharakaisha mchakato ili watu wawe na Euphoria na kusahau yale wasiotaka yaguswe
a)Muungano b) Masilahi ya viongozi wastaafu na jinsi ya kujilinda na mahakama

Kwa kufanya hivyo akajikuta anakiuka misingi ya uandikaji wa katiba.
Wakaiga Kenya bila kufikiria mazingira yaliyopo. Waka ignore nguvu ya kizazi cha sasa

Matokeo ni kuwa na tume yenye wajumbe wa SMZ na JMT kuijadili Tanganyika isiyoonekana. Rasimu kwenda bungeni bila Tanganyika kuwepo bali Watanganyika kuwepo.

Watanganyika wanaelewa mambo mengi kuliko walivyodhani. Wanafahamu hawana mamlaka juu ya mambo yao hadi BLW likubali na kiuchumi hawana mafao ya aina yoyote
Wanatambua kuwa wanaweza kusimama wenyewe bila kupoteza lolote znz wakiwa nje.
Msimamo wao huo unawafanya waache ile hali ya 'wenzetu, ahh sisi sote ni Watanzania'

Kama alivyosema Mchambuzi, Tanganyika inahitaji hadhi na autonomy na kwa kujua kuwa haina lolote au chochote cha kupoteza itakuwa na msimamo mgumu sana kuubadilisha.

Tanganyika kutowepo ndilo linawaunganisha pengine kuliko jambo jingine lile.
Kwamba, wamechoka kuendeshwa na SMZ na BLW na wapo tayari kwa namna yoyote

Znz watakuja na msimamo ima wa kutaka kuongezewa mambo yenye manufaa kwao.
Makamu wa rais Seif Idd na Vua wameisema serikali 3 hazina masilahi kwao na msimamo wao ni wa chama wa serikali 2. Tayari wameshaona serikali 3 zilivyo na wanakoelekea.

Tanganyika imechoka kulaumiwa, kutukanwa na kubebeshwa gharama za kiuchumi imefika katika 'point of no return' kwamba hiwezi tena kuwabembeleza kwa pipi kwasababu ya uchovu.

Znz watakuwa na misimamo yao na mingine wasiyotaka ipinde.
Kitakachokoa muungano ni serikali 3 kwasababu 2 zimeshaonekana kuwa hazifai.

Znz wameshaonyesha kuwa wananyonywa na hawataki 2, fine
Tanganyika wameshagundua yale waliokuwa hawajui na sasa hawataki tena.

Ni afadhali yawepo machache ya kuchangia pamoja kila mmoja akiwa na mzigo wake kupitia serikali 3, vinginevyo CCM waanze kutafuta mbao za jeneza la muungano.
Uwezekano wa kupasua jahazi tugawane mbao na misumari ni mkubwa sana.
.
 
Mkuu Nguruvi3,
Nimekuwa natafakari sana bandiko lako #15 kuhusiana na makosa yaliyofanyika na pia scenarios ulizowasilisha; ningependa kusikia mtazamo wako - je unadhani scenario ya kitu similar to G-55 inaweza kujitokeza?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mchambuzi #45
Scenario ya G-55 imerudi tena kwa nguvu zaidi. Safari hii ni G-XXX.
Nguvu ya CCM imebaki kwa akina mama ambao ni loyal tu, kundi dogo kutoka Unguja na kundi la viongozi wenye masilahi mapana katika muungano.

G-XXX inayokuja itaundwa na wabunge wengi wa bunge la JMT kutoka CCM.
Kitakachosababisha uwepo wa G-XXX ni mambo haya

1. Wabunge wamekuwa sensitive na muungano kwa kuangalia sensitization ya uzanzibar.
Wabunge wa bara ukiacha makundi niliyoyataja watasimamia Tanganyika kwasababu tu znz kuukana Utanzania,hiyo itajenga Utanganyika automatically.

2. Kutokana na mwamako wa Watanganyika kuhusu muungano na kuunga mkono serikali 3,
wabunge watalazimika 'to walk a fine line' kati ya loyalty ya chama au matakwa ya constituent

Tofauti na G-55, G-XXX haitweza kuzuiliwa kwasababu zifuatazo
1. Hakuna tena generation ya wazee wenye authority ndani ya CCM kama enzi za mwalimu
2. Wajumbe wanaotetea serikali 2 hawana hoja za mashiko achilia mbali uwezo wa kuzitetea
3. CCM haitapenda kuwa na mgogoro wa makundi kuelekea 2015
4. Chama kimepoteza nguvu ya kudhibiti 'waasi' baada ya vua gamba kushindwa
5. Hakuna kiongozi mwenye uthubutu wa kudhibiti kundi la wabunge zaidi ya 200
6. Mwenyekiti na CC imepoteza nguvu za kichama. Rais/Makamu wanalalamika kama wanachama
7. Uwepo wa vyama vingi unatoa nafasi kwa wenye courage kusimama kidete dhidi ya CCM
8. CCM haipendi kusikia neno uchaguzi kufuatili matoke ya chaguzi zilizopita.
Ingependa iwe na healing process kuliko kutengeneza rift nyingine.

Ni kwa kuelewa ugumu huo, mwenyekiti wa CCM amewaaasa wajumbe waweke masilahi ya nchi mbele. Anatambua kuwa nguvu ya kudhibiti makundi hana na kama atatumia iliyopo kuna uwezekano wa kutokea matatizo mbele ya safari na yeye kubeba mzigo.

Ametambua kuwa mbinu za kuruka hatua za mchakato wa kuandika katiba zimezaa tatizo kubwa ndani ya chama chake. Pia ametambua upinzani utapata popularity.
Hivyo anajikuta njia panda kwa mambo haya
1. Kuwafurahisha wachache wenye masilahi katika muungano na wenye nguvu za kichama
2. Kutenda kilicho sahihi kwa masilahi ya nchi
3. Kutenda tofauti na matakwa ya baadhi ya wanaCCM kupata katiba na kuzua gogoro zito ndani

Kwa mtazamo huu, G-XXX ipo na itaunda 1/3 kutokana na ukiwa 'Tanganyika' kwa vile kuwa wanaojiita Wznz na kwakuzingatia masilahi ya kiuchumi ambayo ni nguzo muhimu ya ushirika wa aina yoyote katika siasa za dunia ya leo.

G-XXX itaungwa mkono na wapinzani na uwezekana wa kupata 2/3 kwa Tanganyika ni mkubwa kuliko Zanzibar

Tatizo lipo Znz ambapo ukweli unafichwa kwa kusema asilimia 60 wametaka mkataba.
Ukweli ni kuwa rift kati ya Unguja na Pemba inakuja katika bunge la katiba.
Mgawanyiko huo utaleta taabu sana katika kupata 2/3 ya znz. Hili tuliachie hapa !
 
Wacha propaganda zako zisizo na mashiko!
Unamsifia yule mnafiki nyerere aliyetuachia uadui mpaka leo!

Ohh wazanzibari hivi ohh vile!
We mdigo inakuhusu nini habari ya visiwani?

Watu wamechoka na huo muungano wa kinafiki alioufanya huyo nyenyere wako na yule mpenda wanawake!

Waacheni wazenji na mipango yao! Na hizo jitihada za kusamabza unafiki wa kuwa wazanzibari ni loyal to others hauto zaa matunda yyt!
Saana utajiabisha tu!. Manake statements zako karibu zote. Wanao kuunga mkono ni wasaliti walewale wa kila siku!

We are watching you young man. !!
 
Tuko Nyerere alipoona wimbi la mageuzi ya vyama vingi halizuiliki alisoma alama za nyakati akaondoka na kumwachia mwingine aanze alipoishia.

Kikwete hakufanya homework vizuri.Alitaka afanye ambush ya katiba kwasababu kuu mbili
1. Muungano ili watu wasiwe na muda wa kutafakari
2. Kuharakaisha mchakato ili watu wawe na Euphoria na kusahau yale wasiotaka yaguswe
a)Muungano b) Masilahi ya viongozi wastaafu na jinsi ya kujilinda na mahakama

Kwa kufanya hivyo akajikuta anakiuka misingi ya uandikaji wa katiba.
Wakaiga Kenya bila kufikiria mazingira yaliyopo. Waka ignore nguvu ya kizazi cha sasa

Matokeo ni kuwa na tume yenye wajumbe wa SMZ na JMT kuijadili Tanganyika isiyoonekana. Rasimu kwenda bungeni bila Tanganyika kuwepo bali Watanganyika kuwepo.

Watanganyika wanaelewa mambo mengi kuliko walivyodhani. Wanafahamu hawana mamlaka juu ya mambo yao hadi BLW likubali na kiuchumi hawana mafao ya aina yoyote
Wanatambua kuwa wanaweza kusimama wenyewe bila kupoteza lolote znz wakiwa nje.
Msimamo wao huo unawafanya waache ile hali ya 'wenzetu, ahh sisi sote ni Watanzania'

Kama alivyosema Mchambuzi, Tanganyika inahitaji hadhi na autonomy na kwa kujua kuwa haina lolote au chochote cha kupoteza itakuwa na msimamo mgumu sana kuubadilisha.

Tanganyika kutowepo ndilo linawaunganisha pengine kuliko jambo jingine lile.
Kwamba, wamechoka kuendeshwa na SMZ na BLW na wapo tayari kwa namna yoyote

Znz watakuja na msimamo ima wa kutaka kuongezewa mambo yenye manufaa kwao.
Makamu wa rais Seif Idd na Vua wameisema serikali 3 hazina masilahi kwao na msimamo wao ni wa chama wa serikali 2. Tayari wameshaona serikali 3 zilivyo na wanakoelekea.

Tanganyika imechoka kulaumiwa, kutukanwa na kubebeshwa gharama za kiuchumi imefika katika 'point of no return' kwamba hiwezi tena kuwabembeleza kwa pipi kwasababu ya uchovu.

Znz watakuwa na misimamo yao na mingine wasiyotaka ipinde.
Kitakachokoa muungano ni serikali 3 kwasababu 2 zimeshaonekana kuwa hazifai.

Znz wameshaonyesha kuwa wananyonywa na hawataki 2, fine
Tanganyika wameshagundua yale waliokuwa hawajui na sasa hawataki tena.

Ni afadhali yawepo machache ya kuchangia pamoja kila mmoja akiwa na mzigo wake kupitia serikali 3, vinginevyo CCM waanze kutafuta mbao za jeneza la muungano.
Uwezekano wa kupasua jahazi tugawane mbao na misumari ni mkubwa sana.
.

Nguruvi3

Unasema Nyerere aliamua kumuachia mwingine tujiulize kamuachia nini kamuachia katiba ya kidikteta ambao athari zake tunaendelea kuziona mpaka hivi sasa.

Rais Kikwete anachofanya ni kuwachia Katiba mpya watanzania pamoja na kuweka sawa kero za muungano.

Watanzania wengi wanamuunga mkono rais wetu kwenye ili swala katiba.
 
Last edited by a moderator:
Wacha propaganda zako zisizo na mashiko!
Unamsifia yule mnafiki nyerere aliyetuachia uadui mpaka leo!

Ohh wazanzibari hivi ohh vile!
We mdigo inakuhusu nini habari ya visiwani?

Watu wamechoka na huo muungano wa kinafiki alioufanya huyo nyenyere wako na yule mpenda wanawake!

Waacheni wazenji na mipango yao! Na hizo jitihada za kusamabza unafiki wa kuwa wazanzibari ni loyal to others hauto zaa matunda yyt!
Saana utajiabisha tu!. Manake statements zako karibu zote. Wanao kuunga mkono ni wasaliti walewale wa kila siku!

We are watching you young man. !!

Mkuu ukisoma post za Nguruvi3 anaonekana anachuki sana na Wazanzibar na hili suala halijaanza leo wala jana.

Mara muungano uvunjike mara Wazanzibar ni mzigo ,uchangiaji wao katika bajet ni mdogo kulingana na gawio wanalopata kutoka katika bajeti.

Nguruvi unataka kuniambia hilo ulioliona wewe huyo baba wenu wa taifa alikuwa halioni au wewe hapa jf ni "great thinker" kuliko members wengine?ushauri wangu kwako punguza/acha chuki Wazanzibar wanahaki kama walivyo watanganyika.

Hivi ulisoma ule uzi wa kadinali Pengo kuhusu serikali tatu mbona sijakuona ukichangia? au kwasababu ni kiongozi wako wakiimani ukaogopa kumkosoa,wasiwasi wake ni kwamba ikiwa kutakuwa na serikali tatu Wazanzibar watakuwa na uhuru wakujiunga na OIC kwa mtazamo wangu hii ni hoja dhaifu sana kwa kiongozi wako/wenu wa kidini na huu mimi naona ni muendelezo wa chuki dhidi ya Wazanzibar na haipendezi hata kidogo ni hayo tu.

ahsanta.
 
Ndugu yangu,mbona waja juu kama moto wa kifuu!! wapi nimemsifia Nyerere katika bandiko hilo?

Tukiongea kwa jazba tutaishia katika tafrani na tashtiti isiyo na faida. Twaweza hitilafiana kwa hili au lile, yajuzu tuzinusru nafsi zetu kwa kurejesha mioyo nyuma tukiziogopa ndimi na kalamu zetu.

Pili,Mi Mbondei na mdigo inanihusu kwasababu ni muungano unaoathiri maisha yangu na kama raia nina haki ya kutoa maoni yangu kama ufanyavyo wewe Alwatan.

Haaa! wewe unasema watu wamechoka na muungano, mbona wengine tulichoka siku nyingi sana sasa hivi tumezinduka tu na kuona kianchoendelea, uchovu imekuwa nao muda mwingi hadi kulewa usingizi. Sio watu ni pamoja na mimi.

Hakuna sababu ya kusambaza unafiki, mimi nipo katika rekodi ya kuwasaidia wznz wafanikiwe mipango yao siku nyingi sana.Wanajamvi wanalifahamu hilo.

Kila mbinu inayoweza kuwasaidia nimewapa, tatizo ni kuwa hawana uthubutu wa kufanya mipango hiyo.

Tatu, unanituhumu kusambaza unafiki, hebu nisikilize kidogo hapa chini.
Tarehe 6 Oktoba Bwawani Hotel, Mansour Himid, Jusa Ismail, Mzee Moyo wote wamesimama waksema kwa maneno yao muungano wanauhitaji.

Majuzi, Vuai Shamsha Nahodha kasema Ulinzi na usalama vinahitajika na znz katika muungano.
Wiki iliyokwisha naibu wa CCM zanzibar kasema wanataka serikali 2
Miezi 4 iliyopita Sheni kasema muungano una faida, wanaolalamika wajiulize elimu ya juu na ulinzi na usalama znz inachangia nini?

Wote hao bila kujali wanasema nini ni wznz.
Wangekuwa na mipango ya pamoja wasingepisha kauli ati, ushanfahamu!

Mwezi wa 11 2013, waunguja wamehoji wapi hati ya muungano wa Unguja na Pemba.
Tena wakasema maneno mazito, Unguja na Dar ni karibu kuliko Unguja na Pemba.
Si mimi ni wao, unafiki wangu unatoka wapi?

Kwasasa kuna makundi 3, la serikali 3, serikali 2 na la Mkataba. Yote hayo yanatoka znz, unafiki anao nani? mimi ninayesema makundi yapo au wanaounda makundi?

Nikamalizia kwa kusema Tanganyika 2/3 inawezekana, je 2/3 kwa znz itawezekana katika mazingira niliyoonyesha hapo juu.

Kumbuka haya ni maoni yangu ambayo hulazimiki kuyasoma achilia mbali kuyafikiria.
Kama ni propaganda basi dharau uendelee na shughuli zako.

Wakati ninapotoa maoni yangu siogopi aibu kwasababu ni maoni yangu.
Aibu itoke wapi kwa kutoa maoni yangu?

Kama nipo wrong sawa nitakuwa nimeelewa kitu, kama nipo sahihi ni vema.
Ujinga nisoweza kuuvumilia ni kuacha kueleza ninachhokifahamu ninachokiona na ninachokiamini.

Unasema 'we're watching you young man' ninafuraha sana una ni watch.
Kumbe kuna mtu ananiona licha ya ukweli kuwa ni propaganda za kidigo na Kibondei.

Kinachokusumbua uni watch ni nini? Kumbe kuna kitu kinachoma kama si kuingia masikioni!
basi hapo ndipo ninapopata faraja.

Usiishie kuni watch, wewe karibu sana nyumbani tule na tuongee na kama ipo haja nitakupa upanga utimize haja zako.

Sijawahi kutishwa nikaogopa , miaka mingi nasubiri kutishwa.
Hiki unachokiandika hujanitisha maana wenzako waliwashwahi kujaribu kabisaa!

Kwani wewe maoni yako kuhusiana na mada hii ni yapi?
kwamba hukuona kitu pamoja na darubini ya ku watch watu.

Please tupe neno ili tupate ilm sheikh, ghadhabu hazifai katika mnakasha, akisema Sheikh Mohamed Said.

Inshaaalah ndugu yangu mjulie hali ahli na vijana hapo nyumbani, mwambie mimi mzeini.

Masalaam
 
Ningekuwa na chuki nisingewapa mbinu za kupata mamlaka kamili.
Hoja ya wznz ni kuvunja muungano, juzi nikawaambia washangilie Tanganyika imerudi na mamlaka kamili yapo njiani.

Tusaidieni kidogo tu, kwmba wasusie bunge . Hapo chuki ipo wapi ?
Ninyi mkisema Tanganyika mkoloni mweusi bukheri kabisa, mimi nikionyesha hakuna Kunyonywa bali Tanganyika inanyonywa naonekana nina chuki.

Kwamba ajisaide kuku, akijisaidi bata kaharisha.
Waungwana niteendeni haki japo kwa bahati mbaya.
 
Nguruvi3

Unasema Nyerere aliamua kumuachia mwingine tujiulize kamuachia nini kamuachia katiba ya kidikteta ambao athari zake tunaendelea kuziona mpaka hivi sasa.

Rais Kikwete anachofanya ni kuwachia Katiba mpya watanzania pamoja na kuweka sawa kero za muungano.

Watanzania wengi wanamuunga mkono rais wetu kwenye ili swala katiba.
Nilichosema ni kuwa Nyerere alipoona wingu la vyama vingi halieupukiki akajitoa kwasababu alijua hailzuiliki na yeye haamini.
Katiba iwe ya kidikteta harama n.k. ni katiba iliyokuwepo, wewe na mimi tumeitumia pamoja na uharamu wake.

Nia ya Kikwete yaweza kuwa njema kabisa, jinsi alivyofanya hakufuata utaratibu ndio maana bunge la katiba linajadili serikali 3, mbili zikiwepo na moja ikiwa njiani.

Haikupaswa kuwa hivyo kilichopaswa kutokea ni kura ya maoni kwanza ili ijulikane kama muungano una haja ya kuwepo aua la.

Nia njema na kutenda kwa njia njema ni vitu viwili tofauti.
 
Hivi ulisoma ule uzi wa kadinali Pengo kuhusu serikali tatu mbona sijakuona ukichangia? au kwasababu ni kiongozi wako wakiimani ukaogopa kumkosoa,wasiwasi wake ni kwamba ikiwa kutakuwa na serikali tatu Wazanzibar watakuwa na uhuru wakujiunga na OIC kwa mtazamo wangu hii ni hoja dhaifu sana kwa kiongozi wako/wenu wa kidini na huu mimi naona ni muendelezo wa chuki dhidi ya Wazanzibar na haipendezi hata kidogo ni hayo tu.ahsanta.
Ritz kwanza, hoja kama hizi zinachusha si kwasababu hakuna ya kujadili bali matusi, kejeli na kashfa tena za kiimani huingia. Wengine eneo hilo hatuliwezi.

Watanzania na wana JF wabadilike na kuangalia mtazamo mpana. Endapo yupo asiye na hoja ni busara kusoma za wengine. Tujenge utamaduni wa kuvumiliana hata kama hatukubaliani.

Kwanza,nichangie hoja kuwa Kadinali Pengo ametoa kauli katika hafla ya kidini.
Ni vigumu kwa hadhi yake kumtenga yeye kama mtu binafsi na yeye kama Kadinali.

Nguruvi nikikaa utupu hakuna atakayejadili.
Kadinali Pengo akijimwagia chai Hotelini ni habari, ndivyo nature inavyo dictate, with great power comes great responsibility. Tunaweza kuitenga kauli yake kijamii lakini kimantiki kauli hiyo ni ya kiongozi wa Kanisa.

Pengo ana haki ya kujadili katiba kama mtu binafsi na kama kiongozi wa kidini.
Hakuna ubaya kwasababu katiba ina govern maisha ya mtu bila itikadi au kuwepo itikadi.

Kazi za viongozi wa kidini ni kusimamia maadili kwa wafuasi au waumini wao, serikali au mashirika.
Ni kueleza upendo, kupinga dhulma na kukemea maovu.
Kitendo cha Pengo kuzungumzia upendo, amani na ushirikiano ni sehemu yake.

Tatizo la hotuba ya Pengo ni kuacha sehemu zinazomhusu na kuzungumzia zingine tena nusu nusu.

1Katiba inazungumzia maadili ya viongozi ambayo yamemomonyoka na kusbabisha ufisadi, wizi na uhalifu.
2.Katiba imezungumzia haki za walemavu ambao katika nchi yetu hawapewi fursa kama raia wengine
3.Katiba inazungumzia haki za akina mama ambao wanateseka kila uchao, watoto kunyimwa haki na hata kuuawawa
4.Katiba inazungumzia ukomo wa madaraka chanzo cha ulafi na kuvimbiwa madaraka.
5.Katiba inazungumzia namna ya kupata viongozi waadilifu kwa ujumla wao watakaowasaidia masikini
6.Katiba inazungumzia haki za watuhumu, wahalifu na wasimamizi wa vyombo vya sheria n.k.
7.Katiba inazungumzia muungano wa nchi mbili.

Kati mambo #1-6 yanagusa maisha ya watu katika eneo la upendo, amani na utulivu kuliko #7 .
Ningemuelewa Pengo kama angeyazungumzia hayo kwa undani na kumpa benefit of doubt kuwa yapo eneo lake.

Kitendo cha kuchukua jambo moja la muungano na kuacha mengine muhimu sana kwa wafuasi wake na taifa kinaleta picha tofauti kabisa.
Tena katika suala la muungano kachukua kipengele cha OIC kama mada kuu. Hapo kuna tatizo tukubaliane.

Pengo akisema muungano wa serikali 3 haufai anakosea sana.
Anakosea kwasababu hoja zake kuwa serikali 3 itaondoa upendo ni mfu.

Serikali 2 kwa miaka 50 zimeondoa upendo licha ya kujadili kero kila siku.
Leo hatuonani kama Watanzania, wznz wanasema mkoloni mweusi, wanadai hata wasichostahili.
Leo wamefikia mahali pakuchoma Watanganyika moto ili waondoke kwao. Wana serikali yao, upendo uko wapi Kadinali?

Pengo alipaswa kwenda mbali na kusema ili tuwe na upendo, amani na mshikamano yeye anapendekeza mfumo gani. Bado bunge la katiba linaweza kuangalia hoja na kuona wapi wanaweza kuboresha au kukataa hoja ya serikali 3 kama ana hoja za msingi. Kadinali hakuonyesha. Hii kwa kiongozi wa kidini haifai kabisa.

Viongozi wa dini wanaongozwa na principles tofauti na wanasiasa.
Wanasiasa wanaongozwa na uongo, uzushi na udanganyifu.
Lazima kauli ya kiongozi wa kidini iwe tofauti na wa kisiasa.
Kwa hilituseme Pengo hana hoja ya maana, the least to say
Nadhani weye unachuki nami ati! wanisingizia kila jambo yakhe. nshaandika huko kwa Pengo, hebu njoo na jingine.
Hili ni kama janguo la nazi kuangikia kichwani, chei chei
 
Nilichosema ni kuwa Nyerere alipoona wingu la vyama vingi halieupukiki akajitoa kwasababu alijua hailzuiliki na yeye haamini.
Katiba iwe ya kidikteta harama n.k. ni katiba iliyokuwepo, wewe na mimi tumeitumia pamoja na uharamu wake.

Nia ya Kikwete yaweza kuwa njema kabisa, jinsi alivyofanya hakufuata utaratibu ndio maana bunge la katiba linajadili serikali 3, mbili zikiwepo na moja ikiwa njiani.

Haikupaswa kuwa hivyo kilichopaswa kutokea ni kura ya maoni kwanza ili ijulikane kama muungano una haja ya kuwepo aua la.

Nia njema na kutenda kwa njia njema ni vitu viwili tofauti.
Hizo ni fikra zako na mtazamo wako ambao siyo sheria wala kanuni, Rais Kikwete, kafuata utaratibu tena kaenda mbali zaidi suala la katiba na muungano kawakabidhi watanganyika na wazanzibar.

Inawezekana wewe ukaona kuwa utaratibu ni kuanza kupiga kura kuhusu muungano lakini Rais pamoja na Tume ya Katiba wameona njia bora ni hii walioitumia.

Rais kasema wazi kama watanzania wataikataa katiba yeye atakuwa hana la kufanya tena atakuwa katimiza wajibu wake kama rais wamepita marais wengi lakini hawakuthubutu kufanya kama aliyofanya JK, naye pia ataondoka atamuachia mwingine.

Suala la muungano wanapingana watu wengi sana hata tanganyika tumeona Kadinal Pengo hataki serikali tatu, baadhi ya wabunge wa CCM wanataka serikali mbili wengine tatu hiyo ndiyo mipaka ya fikra huru kama ilivyo zanzibar.

Bahati mbaya Rais Kikwete uwa hana jema kwako, lakini bahati nzuri Rais Kikwete watanzania wengi wanamunga mkono.
 
Hapa ninachokiona ni kujichanganya. Hatujui hasa tunachokitaka. Mimi nimesoma mabandiko ya baadhi ya wachangiaji katika uzi huu kifupi sielewi ni hasa nini tunakisimamia. Mara zanzibar waamue moja wajitenge na muungano kwa kutumia wawakilishi wao katika bunge la katiba mara zanzibar wakijitenga wataitaji na Pemba na Unguja nao kujitenga na madai mengine yaliojaa vitisho. Kama wazanzibar nikimaanisha wananchi na sio viongozi wanafiki waliopo katika serikali ya zanzibar wanaofanya kazi kwa remote hawautaki Muungano ni kwanini tuwatungie aina ya muungano wasioutaka? By the way mimi nampongeza warioba na tume yake waliokuja na wazo la serikali tatu kwakuwa hili la kuvunja muungano limeonekana gumu basi wazo hili pia si haba ni muelekeo mzuri kwenda kuvunja muungano. Wananchi waliowengi hawataki Muungano huu wa serikali mbili na wanachokitaka hasa Wanzanzibar ni muungano wa mkataba sasa hii ya serikali mbili inatoka wapi? Hapa wote tuwe na sauti moja na tuache unafiki tuseme hatutaki muungano wazanzibar wachukue taifa lao nasi tubakie na taifa letu. Chuki na wazanzibar tupunguze kama wameamua kujitenga ngoja wachukue taifa lao mengine watajua wao.

Kuhusu hoja iliyo mezani nitatoa mchango wangu.
 
Nadhani weye unachuki nami ati! wanisingizia kila jambo yakhe. nshaandika huko kwa Pengo, hebu njoo na jingine.
Hili ni kama janguo la nazi kuangikia kichwani, chei chei

Nguruvi nimesoma hilo bandiko lako hapo juu lakini nimegundua wewe ni Sawa na panya unang'ata na kupuliza na hakuna unafki mkubwa kama huo.

Kipindi cha nyuma kunapost yako nilisoma inasema inakuaje mwananchi wa mtwara anateseka ilhali mapesa kibao yanapelekwa kuwaneemesha Wazanzibar halafu unakuja kusema unawatakia mema Wazanzibar na mimi naamini hizi ni chuki zako nyuma ya pazia la CHADEMA.

Utakumbuka Mwanasheria wa chama chako/chenu Tundu Lissu alisema muungano umesha vunjika lakini utashangaa leo wao ndio watetezi wa serikali tatu,hata yeye ni mmoja katika lile group la wanafki wasio itakia mema Zanzibar.

ahsanta.
 
Ndugu yangu,mbona waja juu kama moto wa kifuu!! wapi nimemsifia Nyerere katika bandiko hilo?

Tukiongea kwa jazba tutaishia katika tafrani na tashtiti isiyo na faida. Twaweza hitilafiana kwa hili au lile, yajuzu tuzinusru nafsi zetu kwa kurejesha mioyo nyuma tukiziogopa ndimi na kalamu zetu.

Pili,Mi Mbondei na mdigo inanihusu kwasababu ni muungano unaoathiri maisha yangu na kama raia nina haki ya kutoa maoni yangu kama ufanyavyo wewe Alwatan.

Haaa! wewe unasema watu wamechoka na muungano, mbona wengine tulichoka siku nyingi sana sasa hivi tumezinduka tu na kuona kianchoendelea, uchovu imekuwa nao muda mwingi hadi kulewa usingizi. Sio watu ni pamoja na mimi.

Hakuna sababu ya kusambaza unafiki, mimi nipo katika rekodi ya kuwasaidia wznz wafanikiwe mipango yao siku nyingi sana.Wanajamvi wanalifahamu hilo.

Kila mbinu inayoweza kuwasaidia nimewapa, tatizo ni kuwa hawana uthubutu wa kufanya mipango hiyo.

Tatu, unanituhumu kusambaza unafiki, hebu nisikilize kidogo hapa chini.
Tarehe 6 Oktoba Bwawani Hotel, Mansour Himid, Jusa Ismail, Mzee Moyo wote wamesimama waksema kwa maneno yao muungano wanauhitaji.

Majuzi, Vuai Shamsha Nahodha kasema Ulinzi na usalama vinahitajika na znz katika muungano.
Wiki iliyokwisha naibu wa CCM zanzibar kasema wanataka serikali 2
Miezi 4 iliyopita Sheni kasema muungano una faida, wanaolalamika wajiulize elimu ya juu na ulinzi na usalama znz inachangia nini?

Wote hao bila kujali wanasema nini ni wznz.
Wangekuwa na mipango ya pamoja wasingepisha kauli ati, ushanfahamu!

Mwezi wa 11 2013, waunguja wamehoji wapi hati ya muungano wa Unguja na Pemba.
Tena wakasema maneno mazito, Unguja na Dar ni karibu kuliko Unguja na Pemba.
Si mimi ni wao, unafiki wangu unatoka wapi?

Kwasasa kuna makundi 3, la serikali 3, serikali 2 na la Mkataba. Yote hayo yanatoka znz, unafiki anao nani? mimi ninayesema makundi yapo au wanaounda makundi?

Nikamalizia kwa kusema Tanganyika 2/3 inawezekana, je 2/3 kwa znz itawezekana katika mazingira niliyoonyesha hapo juu.

Kumbuka haya ni maoni yangu ambayo hulazimiki kuyasoma achilia mbali kuyafikiria.
Kama ni propaganda basi dharau uendelee na shughuli zako.

Wakati ninapotoa maoni yangu siogopi aibu kwasababu ni maoni yangu.
Aibu itoke wapi kwa kutoa maoni yangu?

Kama nipo wrong sawa nitakuwa nimeelewa kitu, kama nipo sahihi ni vema.
Ujinga nisoweza kuuvumilia ni kuacha kueleza ninachhokifahamu ninachokiona na ninachokiamini.

Unasema 'we're watching you young man' ninafuraha sana una ni watch.
Kumbe kuna mtu ananiona licha ya ukweli kuwa ni propaganda za kidigo na Kibondei.

Kinachokusumbua uni watch ni nini? Kumbe kuna kitu kinachoma kama si kuingia masikioni!
basi hapo ndipo ninapopata faraja.

Usiishie kuni watch, wewe karibu sana nyumbani tule na tuongee na kama ipo haja nitakupa upanga utimize haja zako.

Sijawahi kutishwa nikaogopa , miaka mingi nasubiri kutishwa.
Hiki unachokiandika hujanitisha maana wenzako waliwashwahi kujaribu kabisaa!

Kwani wewe maoni yako kuhusiana na mada hii ni yapi?
kwamba hukuona kitu pamoja na darubini ya ku watch watu.

Please tupe neno ili tupate ilm sheikh, ghadhabu hazifai katika mnakasha, akisema Sheikh Mohamed Said.

Inshaaalah ndugu yangu mjulie hali ahli na vijana hapo nyumbani, mwambie mimi mzeini.

Masalaam

Kwanza nataka nikutahadharishe kitu kimoja, Unapo jadili na mimi Tafadhali usiingize mwingine ktk haya malumbano, unless unataka KUCHAFUA HUU UZI,

Unasema wewe umewapa mbinu WAZANZIBARI ZA KILA NAMNA ILI WAFANIKISHE HIO AZMA YAO, NAKUULIZA WEWE @nguruvi3 NANI KAKUOMBA HUO MSAADA?? Na wewe kama NANI wa kuwapa wazanzibari mbinu??
Hichi mi nakiita kiherehere! na upashkuna wa kucheza ngoma si yako!

Pili unasema MUUNGANO UNAKUATHIRI!

Hebu nijuze kidogo, wewe mbondei wa segera, na yule mpemba wa chake ANAE ATHIRIKA NA MUUNGANO HASA NI NANI?? Mbona Unatoa kauli bila kufikiri ndugu! AU ndio namna ya kutafuta sympathy kwa wanajukwaa??

Unantajia hao wajiitao waznz kuwa wametamka kuwa HUO MUUNGANO WANAUHITAJI, Na sababu pekee ulioirudia mara kwa mara ni KUTAKA ULINZI NA USALAMA! Nakuuliza Hao waznzibari Huo ulinzi wanaoutaka ni kwa kumhofu nani hasa??
au UNAMAANISHA wakijitenga Tanganyika Itawavamia??

Zanzibar adui yake ni TANGANYIKA! Na hakuna mwingine! Tena huyo Tanganyika NDANI YA MFUMO KRISTO!

Hao wanafiki wasemao kuwa ZNZBR Inahitaji Tanganyika kuilinda NI VIBARAKA TU AMBAO WAMEWEKWA HAPO KWA MASLAHI! Na hio ndio fikra ya wazanzibari wengi.

Hakuna hapo TZ asiyejua kuwa asilimia 99% ya WAZANZIBARI HAWATAKI MUUNGANO, Hao uliwataja hapo juu, ni ktk wale BLACK SHEEP, ambao ktk kila kundi la waungwana HUTOWAKOSA!

Wazanzibari Hawahitaji mtu kama wewe na Pasco kuwatetea kinafiki, na wakati huo huo Mnapenyeza maneno ya kuwadhalilisha na kuwaona hawanba maana sana!

na istoshe kwa mtu mwenye Upeo wa kawaida tu wa kufikiri akisoma mabango yako na yule mwenzako Pasco, Atagundua 100% kuwa NYINYI SIO WAPENDA HAKI HATTA KIDOGO! Bali ni watu wa kujaribu kupotosha ukweli halisi na kupenyeza propoganda za NYERERE {Mnajifanya kuuma huku mnapuliza.} huo unaitwa UNAFIKI. na ni mbaya kuliko UCHAWI.

WAZANZIBARI HAWAKUHITAJI WEWE WALA MTANGANYIKA YOYOTE KUWASAIDIA KUPIGANIA HAKI ZAKO,TENA HASSA WALE WALIO NDANI YA HUO MFUMO KRISTO!

Wewe kama ni mpenda haki, basi support KILE WANACHODAI WAZANZIBARI, Na SIO kujifanya kuwapa mbinu zako zisizo na mashiko.

Wapi ULIONA FISI AKAMFUNDISHA MBUZI JINSI YA KUTOROKA KWENYE JELA YA FISI WENZAKE??

NA mwisho!Labda lugha inakupa tabu kidogo MI SINA HAJA YA KUKUTISHA WEWE! bali nimekutahadharisha kuwa NAKUTAZAMA UNAVYOMWAGA PUMBA HAPA JUKWAANI UKIZIITA, "MAWAZO YANGU BINAFSI"!

Sasa Kila UTOAPO mawazo MABOVU basi uwe tayari KUKOSOLEWA! Na sio kunikaribisha kwako unipe panga!

Mi nimpige panga mtu mwenyewe yuko njia moja??

ILANI.
Shika heshima yako kuingiza jina la mzee Mohamed said ktk maongezi yangu mi na wewe, au sasa hivi utachukia huu uzi
!
 
Mimi jambo linalozidi kunitia mashaka juu ya hawa wanaotaka serikali mbili yaani muungano huu ubaki ni hoja zao ambazo mimi naziona za kitoto mno. Unapodai serikali tatu itapelekea mzigo kwa tanganyika kuendesha serikali ya muungano na mwisho wa siku unafanya inference yakuwa serikali mbili ndio suluhisho kwanini usifanye inference ya kuwa kila nchi ijitawale yenyewe? Muungano sisi watanganyika tunaoung'ang'ania hasa kwa maslahi gani huku tukifahamu ya kuwa tunanyonywa katika uendeshaji wa muungano huo? Mfano hivi karibu bwana Peter Kisumo alirekodiwa na gazeti la mwananchi
akisema yeye anaamini muundo wa Serikali mbili kama ulivyo sasa ndiyo mwafaka katika kulinda Muungano, na kwamba kama kuna kasoro zilizoainishwa na tume basi zitazamwe upya.
¡°Bila shaka gharama za kuendesha Serikali ya Muungano itabebwa na Tanganyika¡-Tunabebeshwa mzigo bure hao wanaotaka uhuru kamili (Zanzibar) ndiyo wabebeshwe gharama za Serikali ya tatu¡±. Sasa kama umeshajua kuwa zanzibar hawautaki muungano ni nani kasema wanataka serikali tatu? Kwanini kisumo usiseme wavunje muungano?
Kisumo anasema busara ya kawaida ilimtaka Jaji Warioba pia aeleze faida za Serikali mbili ili Watanzania waweze kupima lakini hilo akalikwepa kwa makusudi ili kuhalalisha hoja yake.
¡°Muundo wa Serikali tatu utaleta mgogoro wa kikatiba, aliposema Watanzania wengi wanataka Serikali yao (Tanganyika) mbona idadi ya waliowafikia ni ndogo sana, hakuyasema kabisa?¡± pia
Kisumo anasema kama kweli kuna Watanzania wengi wanataka kuundwa kwa Serikali ya Tanganyika basi hilo litajidhihirisha kwenye kura ya maoni huku akisisitiza kwamba haamini iwapo kuna watu wanaotaka Tanganyika.
Kweli? Mbona watanganyika pia wapo tena wengi tu wasioutaka muungano?
Halafu Nguruvi3 unadai unawasaidia wazanzibar njia za kujitenga huku ukiwa unawatishia kweli unania/kusudia au ndio unafiki uliowajaa wafuasi wengi wa mwalimu Nyerere? Binafsi watanganyika hasa wahafidhina wa muungano ndio tunaochelewesha kuwapa haki waitakayo wazanzibar ya kuwa taifa huru. Swali ni nini hasa tunanufaika watanganyika kwa huu muungano mpaka sisi tuung'ang'anie na huku upande wa pili wao hawautaki?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu ukisoma post za Nguruvi3 anaonekana anachuki sana na Wazanzibar na hili suala halijaanza leo wala jana.

Mara muungano uvunjike mara Wazanzibar ni mzigo ,uchangiaji wao katika bajet ni mdogo kulingana na gawio wanalopata kutoka katika bajeti.

Nguruvi unataka kuniambia hilo ulioliona wewe huyo baba wenu wa taifa alikuwa halioni au wewe hapa jf ni "great thinker" kuliko members wengine?ushauri wangu kwako punguza/acha chuki Wazanzibar wanahaki kama walivyo watanganyika.

Hivi ulisoma ule uzi wa kadinali Pengo kuhusu serikali tatu mbona sijakuona ukichangia? au kwasababu ni kiongozi wako wakiimani ukaogopa kumkosoa,wasiwasi wake ni kwamba ikiwa kutakuwa na serikali tatu Wazanzibar watakuwa na uhuru wakujiunga na OIC kwa mtazamo wangu hii ni hoja dhaifu sana kwa kiongozi wako/wenu wa kidini na huu mimi naona ni muendelezo wa chuki dhidi ya Wazanzibar na haipendezi hata kidogo ni hayo tu.

ahsanta.

Hivi kwa nini watu wengine hawawezi kujadili hoja bila kuweka matakataka kama hayaaa (highlighted)!!!!!!! Du!! mambo ya aibu kabisa!!!!! taratibu mada inataka kugeuzwa.....
 
Najifunza mengi kwenye huu mjadala wenye hadhi ya kuitwa mjadala uliyojika kwenye msatakabali wa nini uwe mwongozo mzuri kwa wajumbe wa bunge la katiba , tuendelee hivyo hivyo kujiuliza je wajumbe waingie kwenye bunge la katiba wakiwa na misimamo yao tayari na kama ni hivyo ni vipi tutakwepe kuelekeza mjadala kwa upande hao wajumbe wenye msimamo wanataka
tutakwepaje ushwishi wa makundi mengine nje ya bge la kaiba kwa mfano vyama vya hiari,makundi ya dini, taasisi za elimu

kwa kupigia debe msimamo wa chama Fulani situnawaelekeza namna kwaba wkwa tofutia matakwa ya chaa chao utata mtafaruku ,kwa jni mundo ulvyotengenezwa kufikia Bunge la Katiba na kujadili rasimu ya pili ni kweli katiba haitapatikana hivi karibuni
 
Back
Top Bottom