CCM must go for the year 2020!

CCM must go for the year 2020!

Watanzania daini katiba mpya ccm itoke vinginevyo mtapata tabu sana
 
naona mawaziri na manaibu wao na wakuu wa vitengo wanapita tu kwenye hii thread kwa tahadhari😀😀😀
 
safari hii atapata 10m.....

usisahau lowassa alipata kura kutokana na chuki kwa ccm sio kwa sababu ya usafi wake

Lowassa ni mchafu kiasi ambacho kwa akili za kawaida kutojua au kutambua ni mchafu unajidhalilisha wewe, anaweza hata akakuvua nguo ukabaki kimya kwa mahaba hayo

ccm ni wachafu, lowassa ni walewale mkuu...kuwa mkweli

Slaa angepata kura 4m mwaka 2015, mwaka 2020 angeongeza..2025 nchi ingeenda upinzani
Ni kweli kuwa kuna kura za chuki, na uchaguzi wowote hizo lazima ziwepo tuu. Wapo ambao 2015 hawakuipa Chadema kura kwa chuki za kuondoka kwa Slaa pia.
Kuhusu uchafu wa Lowassa mie sikatai, lakini ndio udhaifu wa CCM huo, mtu ni mchafu na wanashindwa kumshughulikia mpaka anasema hadharani kuwa kama unaushahidi twende mahakamani na bado wanapiga kelele kuwa huyo ni fisadi kama wapinzani wasio na serikali wanavyopiga kelele!
CCM imeshaondoka mioyoni mwa watu, na kama sio kutumia hila na nguvu hakiwezi kushinda hata kidogo, kweli ccm imefikia mahali kukodi watu wa kumshangilia Rais anapohutubia? Hata JK tuliyesema ana udhaifu mkubwa hakupata kufanya ujinga kama huo
 
Back
Top Bottom