CCM must go for the year 2020!

Ccm na Dr. Magufuli watashinda tena sana.

Kwa upinzani wa Tanzania ; kuwapa nchi ni sawa na kuamini kuwa Tai ataacha kula mizigo iliyooza huko nyikani.
 
  • Thanks
Reactions: nao
Hizi lugha siyo zetu, bora ungeandika Kiswahili chetu. Kichwa cha habari kipo tofauti na unachokisema kwenye bandiko lako. CCM must go for year 2020, inamaanisha CCM must stand/contest/contend in the year 2020 which is obvious...
Mkuu error za kiuandishi nimezingindua baada ya post,kwahiyo content iko wazi.
 
Tulia wewe kuna timu inasukwa kwa umakini na wababe wa kisiasa mamafia wa kisiasa huhakikisha 2020 kuna cha kiambulie 14% na 23% ya kura za urais so jiandae kisaikolojia kuna mtu anakwenda kushinda kwa kishindo hao wengine bado sana kukabidhiwa hii nchi inahitajika mikakati na maono siyo matamko yasiyo kuwa na tija kajipangeni
MAHANJU.
 
Nileze ni nchi gani duniani aliibuka mpinzani aliyekulia upinzani akaongoza taifa? Hao marais wote wa Nigeria,Ghana na kwingineko walitokea ruling parts.
Haya ndio madhara ya kujifanya mnajua kuchambua siasa,
Hao walikuwa na heshima tosha! Hawakuwa mafisadi wala kuwa na makandokando mengine!
Mshawishini mtu kama Salim Ahmed Salim, hawa ndo watu wa calibre hii walioshinda nchi zingine wakitokea vyama tawala, sio MAFISADI.
 
ccm ni chama cha makafiri na mafirauni.
Hakina hadhi wala sifa ya kuwa chama tawala kwa ridhaa ya wananchi; isipokuwa kwa hila, ulaghai na mabavu ya dola tu.
Sipendi mawazo kama haya.....mnakaa kudanganya watu kwa faida Zenu binafsi...hamtafanikiwa kamwe
 
Wananchi wameshaichoka CCM na muda wowote wapo tayari kwa mabadiliko lakini wanaotia shaka ni hao wanaohubiri mabadiliko kutoka upande huo.......

I can’t imagine anaondoka CCM anaingia LOWASA na Sumaye........its a big political joke

SIASA ZA NCHI HII ZIMESHAPOTEZA MUELEKEO
This is true my brother.

Upinzani wanapaswa kulaumiwa sana tena sanaa, maana ari ya mabadiliko ipo ila wameshindwa kuvalia njuga masuala ya msingi kama katiba mpya, there is no way wakapata nafasi kwa katiba hii .

Another thing wameamua kuwa chama pinzani tuu ila hawaonyeshi utofauti wa kuaminiwa kupewa madaraka kabisa
 
This is true my brother.

Upinzani wanapaswa kulaumiwa sana tena sanaa, maana ari ya mabadiliko ipo ila wameshindwa kuvalia njuga masuala ya msingi kama katiba mpya, there is no way wakapata nafasi kwa katiba hii .

Another thing wameamua kuwa chama pinzani tuu ila hawaonyeshi utofauti wa kuaminiwa kupewa madaraka kabisa

Ukiacha siasa za majukwaani wapinzani hawana nia ya kuchukua nchi kivitendo.......

Mtaji mkubwa wa wanasiasa wa nchi hii sio weledi wa mambo bali ni UNAFIKI na UZUSHI......

SIKU VIJANA WA NCHI HII WATAKAPOANZA KUTUMIA AKILI ZAO NA KUJITOA KWENYE MIHEMKO NDIO SIKU AMBAYO ZITAKAPOANZA HARAKATI ZA KWELI ZA KUIONDOA CCM MADARAKANI........
 
HATA KAMA CCM IKITOKA CHADEMA MNA NANI WA KUTUFANYA TUMPE KURA MAANA MNAKUWA KAMA WATOTO HAMNA MIPANGO YA KUCHUKUA NCHI MNA MALALAMIKO YA KUCHUKUA NCHI
 
Naona anguko kubwa la ccm


mlogolaje ,
Mkuu ccm ingeweza kuanguka kama Mwenye chair cdm angekuwa na hekima pale mtu anapoondoka kwao.

Angalia ccm wanaimba taarabu na ngojera mtu akiondoka kwenda upinzani.

Wapinzani hasa CDM wanalaani tabia hiyo ya watu wa ccm kuimba taarabu na ngojera.


Ndani ya mwezi uo huo, mwana cdm anaondoka tena hajasema hata chama anachoenda Bali kasema kuwa yeye anasimama mambo ya siasa kwanza ili ajitathimini mwelekeo wake kisiasa.

Sasa, kosa lilelile la kuimba taarabu na ngojera linatoka CDM kwenda kwa mtu aliyehama hicho chama.
Tena mbaya zaidi ni pale mwenye chair wa CDM anapoimba hiyo taarabu na kusoma ngojera kuwa:-
""" kwanza , fulani hata akiondoka huku cdm, ni Sawa maana, tangia ajiunge nasi hatujawahi kuona faida yake "

Kwa tamko hilo, unaona kabisa kuwa kuanzia mwaka 2019 hadi katikati mwa mwaka 2020 watu huwa wanahama vyama ,,,, je, kwa tamko hilo la mwenye chair wa cdm patakuwa na watu wenye shauku ya kujiunga huko CDM!?

Any way, ccm japo inaweza kuwa na madudu mengi ila bado itashinda kwa kishindo hiyo 2020
 
Hiki chama kinalinagamiza sana taifa hili na kuliingiza kwenye matatizo makubwa ya kiuchumi kisiasa na kijamii. Hatuwezi kuwaelewa watu ambao hawana nia njema na watoto wa maskini wanaokosa mikopo vyuoni, hawezi kuwaonea haya watu ambao wanavuruga biashara za watu kwa makusudi, hatuwezi kuwaonea haya watu wanaolea ubaguzi na upendeleo wa wazi wazi.


Nini Cha kufanya?
1.Katiba Mpya, haya ni mahitaji ya wananchi wote na sio wanasiasa flani flani na wala sio maamuzi ya mtu flani.

2.Lazima tuwaambie watawala kwa namna yeyote ile suala la mikutano ya kisiasa ni matakwa ya kikatiba na sio kauli au ruhusa za wanasiasa flani flani.

3.Lipumba na genge lake lazima waondoke CUF, kutumiwa kufifisha nguvu ya upinzani nchini hatutamwelewa na hatumtaki.

4.Mh Zitto na washirika wake lazima wakae pamoja na kuonesha Dhamira ya kweli kuwa wao ni wapinzani ili kuunganisha nguvu ya pamoja.

5. Lazima itumike mifumo na mikakatika yeyote ili kueneza kwa kasi itikadi za upinzani kupenya kila mahali nchini hasa maeneo ya vijijini ili kutahisisha kazi kuelekea 2020.

6.Kama kuna ugumu kwenye nafasi ya urais 2020 basi nguvu uhamie kwenye nafasi za ubunge, upinzani ukubaliane kwa pamoja mapema sana hasa wakati huu kuweka wagombea watakaoungwa mkono na wananchi wa vyama vyote ili kama kuna matatizo yatatuliwe mapema.Tusikubali wagombea wa ubunge wa CCM kupata kura hata kumi kwa namna yeyote ile. Kama wabunge wa upinzani watakua wengi bungeni basi Sipika na Waziri mkuu watatoka bungeni na bunge litadhibitiwa tofauti na sasa, Hoja zote za serikali lazima zipitishwe na bunge kutoka upinzani na hslutakua na mhimili uliojichmbia zaidi tena.

7.Vyamba vya upinzani sasa ni kutengeneza na kuandaa wapiga kura na sio wafuasi,hili ni lakufanyiwa kazi haraka ipasavyo.


CCM MUST GO 2020!
Tukiiondoa ccm tuweke chama gani?
Au tumweke nani?
Chadema wazee wa dili au fisadi Lowasa?
Kijana jitambue
 
Eti wagombea ubunge wasipate hata kura 10 kwa njia yoyote ile!! Kimekuwa kijiwe cha kujazana ujinga..
 
Nileze ni nchi gani duniani aliibuka mpinzani aliyekulia upinzani akaongoza taifa? Hao marais wote wa Nigeria,Ghana na kwingineko walitokea ruling parts.
Haya ndio madhara ya kujifanya mnajua kuchambua siasa,
Siyo kwa makapi haya mnayookoteza Tanzania. That can never happen. Period
 
Back
Top Bottom