CCM msiongeze chumvi kwenye sifa za Rais Samia

Anna Nkya

Member
Oct 21, 2021
69
341
Ni kweli anafanya kazi nzuri hadi sasa licha ya ukweli kwamba bado hatujafika tunapopataka.

Lakini jamani hizo sifa mnazompa Rais Samia zisitiwe chumvi, msivuke kiasi cha kujifanya kama hii nchi haina tatizo hata moja.

Tumpongeze anapofanya vizuri, tumkumbushe ambapo hapajakamilika, tupinge panapobidi.
 
Sifa haziwezi kukauka toka huko CCM, kwani kila sifa anayopewa ina malengo yake tofauti;

- Wapo wanaosifia ili walipwe ujira wa siku kama hawa wanaopiga kelele kutwa huku jf.

- Wapo wale wanaosifia ili wapate teuzi hata kama wanachosifia hakina maana au kilianzishwa na mtangulizi wake.

- Wapo pia wale wengine wanaosifia kwa kuvimbiwa tu ilimradi wawanyime raha wale wa awamu iliyopita (Sukuma Gang).

- Na mwisho ni wale hiyena hiyena, wenyewe wanakwambia wao ni nambari wani, hawa wanasifia tu bora wapige kelele, makoo yakiwakauka wanarudi zao nyumbani kwenda kunywa maji ya bomba, wengine ya visima, wengine wanakunywa maji ya kuogeshea n'gombe, na wengine wanachimba chimba huko mabondeni bora hata wapate tope wanywe, hawana habari kama t-shirt wameshavalishwa na zimewaenea mtawaambia nini!
 
Back
Top Bottom