CCM, mna matatizo ya ubongo.? Miaka miwili kaburini, eti bado anaiba kodi za watanzania

Paulsylvester

JF-Expert Member
Oct 15, 2021
1,467
3,381
Kuvaa viatu vya mpambanaji na mtu wa vita, yapaswa na wewe uwe mtu wa vita ikiwezekana Mara mbili yake, kama alikuwa haruhusu sharubu zake ziguswe, kwa wewe iwe marufuku hata kusogelewa tu na kinyamkera chochote, kwani mazoea ni mabaya.

Kwa nini imekuwa ni vigumu sana kuondoa umaarufu wa uchapa kazi wa Mwendazake, ni Kwa sababu moja tu! Mwenye shughuri yake anapoacha kusimamia shughuri yake huku akiuacha mzinga wa asali nje nje huku akijua kuna watu wamejitanabaisha kuwa,wao kazi yao ni kuilamba tu ile asali unadhani kitazaliwa nini?

Hivi nyinyi CCM na wapambe wake, Mnataka kutwambia kwamba, huyu mnayekesha kumsema kuhusu ripoti za fedha za CAG kuwa ameiba, mnamaanisha nini?

2 years kaburini, bado mnasema amekuwa akiiba?

Mnadhani anastahili yote msemayo sasa, pesa muibe nyie halafu mseme asiyekuwepo ndo amekuwa akiiba?

Mnataka kumfunika Mchapakazi wa kweli JPM na asikumbukwe kabisa!

Tendeni mema Kwa wananchi, timezeni ahadi zenu, ondoeni kodi kandamizi Kwa masikini, acheni kujilimbikizia Mali, tumieni vema kodi za watanzania katika kuwaletea maendeleo!

Watu hatuna maji,, utatulazimisha tupende huu utumbo?

Umeme hakuna, Saloon zetu tunalazimika kufunga, tukale wapi na unataka tuupende uongozi wa namna hii

Mnatangaza idadi ya watanzania Kwa chopa, alama za mitaa Kwa chopa, kukitokea ajali ya wananchi, mnaenda mikono mitupu, mnataka tuwapende?

Tunawapenda katika lipi?

Endeleeni kusingizia wasiokuwepo,

Tukutane 2025! Kwenye uwanja wa vita!
 
CCM MBELE KWA MBELE
 
Back
Top Bottom