CCM: Majizi Msimchukulie poa Rais Samia

CM 1774858

JF-Expert Member
May 29, 2021
4,984
4,083
Na Romana Mallya

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema mtu ambaye hatakiwi kufanyiwa masihara wala mzaha katika kulinda rasilimali za nchi hii ni Rais Samia Suluhu Hassan,Wale wanaomchukulia ‘poa’ wajaribu waone,

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka alisema
hayo jana alipofanya ziara katika vyombo vya habari vya IPP na kujionea vinavyofanya shughuli zake.

Shaka alifanya ziara hiyo kwa lengo la kujifunza, kuimarisha uhusiano na kufungua milango baina ya chama hicho na vyombo vya habari vya taasisi hiyo.Katika mahojiano maalum yaliyofanywa na vyombo vya habari vya IPP,

Shaka alisema watu wanapomwona Rais Samia wasifirikie kwamba ndivyo alivyo katika undani wake lakini ni mtu makini anayesimamia kwa nguvu zote rasilimali za nchi yetu,

“Tumeshuhudia wote na hatua zimeendelea kuchukuliwa. Wakati mwingine si lazima uchukue hatua ukataka tena dunia nzima ijue.

Ziko hatua nyingi zinazochukuliwa za kinidhamu.Unaweza kusema kwamba kwa nini hatumwoni
anatoka na kusema nimemfukuza huyu na huyu.

Hiyo siyo sifa, kuna ubinadamu na kuna nidhamu ya kimaadili.“Kwa sababu ni maelekezo ya chama na kila jambo liko kwenye maandishi na hakuna jambo limetoka mbinguni, chama tumesema katika kipindi cha miaka mitano tutahakikisha tunasimamia heshima ya matumizi ya fedha za serikali, fedha za walipakodi ili zilete tija na maendeleo endelevu,” alisema.

Shaka alisema hayo baada ya kuulizwa juu ya ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) hususani matumizi ya fedha za Mfuko wa Jimbo kinyume cha malengo yaliyowekwa.

Alisema wajibu wa chama ni kuishauri serikali na kwamba hakuna ambaye atafanya ubadhirifu na kukwepa mkono wa sheria. “Bahati nzuri Watanzania sasa ni waelewa mno. Leo hii nenda kajenge kituo cha afya Kakonko chini ya kiwango uone Watanzania watakavyopiga kelele. inawezekana
CAG akachelewa kufika.

“Watanzania kabla CAG hajafika wao wenyewe wanatosha kuwa Ma-CAG.Kiwango cha uelewa
kimekua hasa kwenye miradi ya maendeleo. Kwenye ziara wanatuambia, ‘Katibu wa Itikadi umekuja
lakini hiki ni kituo cha afya kweli?’” alisema.

KUHUSU MACHINGA KURUDI

Kuhusu wafanyabiashara wadogo, maarufu kama machinga, Shaka alisema CCM imefanya tathmini ya kina kama ilivyofanya kwenye asilimia za mikopo kwa vijana, wanawake na makundi maalum.
“Maeneo hayo mtambuka tumeyafanyia tathmini na wiki kama mbili tumepokea ripoti yake na yapo mambo ya kufanyia kazi. Kama chama tunafuatilia kwa karibu kwa sababu mwisho wa siku Chama Cha Mapinduzi ndiyo matajiri, serikali tumewapa duka watuuzie, wateja wetu ni wananchi lazima tuwe nao karibu, tujue bidhaa tunazowauzia zinauzika na wanaridhika.

“Tumefanya utafiti na tathmini ya kuona namna nzuri ya makundi haya likiwamo la machinga namna
ya kurasimisha biashara zao. Tunashukuru bajeti ya mwaka huu wa fedha 2022/23, Rais Samia ametenga karibia Sh. bilioni 10, hivyo tathmini hii itatupa mwelekeo itumikeje,” alisema.

Hata hivyo, alisema CCM itaishauri serikali namna nzuri inayopaswa kufanyika na maeneo
ambayo watafanyia biashara. Alitoa mfano wa Dodoma ambako ujenzi unaendelea kwa kutumia
fedha za UVIKO-19 na maeneo mengine pamoja na changamoto ikiwamo Dar es Salaam ambako
mambo yanakwenda vizuri.

“Huwezi kukamilisha kwa asilimia 100 ndani ya kipindi kifupi. Utakwenda hatua kwa hatua lakini
mwisho wa siku mtafikia malengo,” alibainisha.


KUHUSU KUTOA AJIRA MPYA

Shaka alisema mradi wa kimkakati wa gesi wa Lindi ndio mkubwa ndani ya mwaka mmoja wa Rais Samia ambao wanaamini utapunguza tatizo la ajira kwa vijana na rika zingine kwa asilimia kubwa.

Alisema waliahidi ajira milioni nane kwa kipindi cha miaka mitano na tathmini ya awali inaonyesha wanakwenda vizuri na wanaamini serikali ikiendelea hivyo kazi yao 2025 itakuwa nyepesi.

KUHUSU KATIBA MPYA

Kuhusu hoja ya Katiba Mpya ambayo hivi sasa kumekuwa na vilio kila kona, Shaka alisema suala hilo
linazungumzika na kwamba waliobeba hoja hiyo tangu mwanzo ni CCM, hivyo hilo si jambo geni.

“Tumeshauri serikali wote mtakuwa mashahidi. Rais Samia alipoingia madarakani alisema ‘Nipeni muda’. Tumempa na tumeona mabadiliko makubwa yamefanyika. Kwanza ameimarisha mfumo wa demokrasia na alivyosema ‘Ninataka kufungua nchi’ wengi wakafikiria atakuja na kufuli na ufunguo aseme ‘sasa nafungua nchi’.

“Amefungua fursa za kiuchumi, amefungua uhusiano wa kikanda na kimataifa. Tulipofikia tukasema
chama hiki ni cha watu na kinachosikiliza na kimebeba ajenda ya taifa, tukasema sasa ni muda muafaka wa kuishauri serikali kuangalia namna bora ya kufufua mchakato wa Katiba, tutakwendaje ndiyo maana tunashauri serikali kaeni mje na kwetu kwa sababu katiba si ya wanasiasa ni ya wananchi.

“Tukisema tulibebe wanasiasa hatutawatendea haki Watanzania. Lazima kuwe na mfumo shirikishi,
wanaweza kuuliza washirikishwe mara ngapi? Hata tukianzia kwenye Katiba Inayopendekezwa lazima washirikishwe lazima turudi kwa wananchi wajue uamuzi utakaochukuliwa kwa mustakabali wa kizazi cha sasa na kijacho,” alibainisha.

“Kwa CCM suala la Katiba Mpya si jambo jipya ni mwendelezo tu wa namna ya kusikia mwelekeo
na kusikiliza ya walio wengi na wataendelea kufanya hivyo. Hata la tume wamepewa nafasi na baadhi
ya vyama wamepewa nafasi kuwasilisha mawazo,” alisema.

KUHUSU UHURU VYOMBO VYA HABARI

Kuhusu uhuru wa vyombo vya habari, kiongozi huyo alisema kuna mafanikio makubwa tofauti na kipindi kilichopita. Alisema kwa sasa watu kupitia tasnia ya habari wanakosoa na kutoa yao ya moyoni na serikali inawasikiliza kama Rais alivyowahi kusema vikosoe kwa staha kwa kutanguliza utaifa, uzalendo na kushauri inapobidi.

“Utakapokosoa kwa jazba au kutengeneza propaganda za kuchochea mambo ambayo hayana mustakabali kwa taifa, tukumbuke hapotezi mtu mmoja bali tutapoteza wengi pengine na kizazi kinachokuja. Tushukuru (wanahabari) mna amani mnafanya kazi zenu vizuri.

Hata vyombo vilivyokuwa vimefungiwa vimefunguliwa na ambaye hajaanza kufanya kazi ni yeye mwenyewe.

“TV mtandaoni zilikuwa changamoto. Ile ni sehemu ya kijana kujiari, sasa unapomwambia kujisajili
tu akalipe Sh. 500,000 mpaka 1,000,000 ilikuwa vigumu. Rais Samia amepunguza tozo kwa sasa
ni Sh. 50,000 mpaka 200,000. Serikali zote (ya Muungano na ya Zanzibar) zinaendeleza azma yake
kulinda na kuimarisha utawala bora, utawala wa sheria na uhuru wa vyombo vya habari,” alisema.

KUHUSU ANDIKO LA RAIS SAMIA

Kiongozi huyo alimshukuru Rais kwa andiko lake aliloliandika kwa vyombo vya habari hivi karibuni
na kueleza kuwa lina nia njema juu ya mustakabali wa nchi.

Alisema walikotoka ni kuzuri, walipo ni kuzuri zaidi na wanakokwenda matarajio ni makubwa zaidi.

“Tukijitathmini namna tulivyokuwa tunafanya siasa miaka mitano iliyopita, siasa zimebadilika ndani ya mwaka mmoja.

Leo tunazungumzia maridhiano ya vyama vya siasa, nani alikuwa anazungumzia miaka mitano iliyopita? Tunazungumzia vyama vya siasa kujifungia kutathmini mwelekeo wao,” alisema.

Shaka alisema andiko la Rais, limewarudisha kwenye uzalendo na utaifa na kuwakumbusha wajibu wao kama Watanzania kwamba vyama vingi vya siasa siyo chuki, uadui wala uhasama, bali vitumike
kama kichocheo cha maendeleo.

“Kama tutaishi kwenye maono ya Rais Samia, nchi hii itapiga hatua kubwa kiuchumi, kijamii na
kisiasa. Nimeona dhamira ya dhati ya Rais Samia kupitia andiko hili. Hata shughuli zetu za siasa huko
mbele, ninaamini kabisa chini ya uongozi wa Rais Samia yawezekana Tanzania tukafanya uchaguzi wa kihistoria 2024 na 2025 kwa sababu ya dhamira na utayari wake.

“Wengine wanasema hahofii chama chake, hawezi kuhofia chama chake ni chama kikubwa, ni chama ambacho kinaaminika, kimebeba matumaini na hatima ya Watanzania. Kimejipambanua ndiyo maana tunasema ni chama kiongozi.

“Andiko la Rais litusukume na liwe funzo kwetu wanasiasa na hata ninyi wana tasnia ya habari na nyingine. Tutumie kama kielelezo na sehemu ya kutukumbusha tulikotoka, tulipo na tunakokwe


IMG-20220709-WA0156.jpg
 
Make hapo kwanza ncheke.

Kiufupi hii nchi tumepigwa na kitu kizeeto kwa hedi..

Anyway rimot ipo msoga.

#MaendeleoHayanaChama
 
Wacha niseme kidogo,

Kama kuna mtu ameachia mifumo ifanye kazi kwa uwazi na kutokumuonea mtu ni huyu Rais Samia,

Kitendo hiki kinawafanya wananchi wenyewe wawajibishane katika levels zao,

Kutumbua mtu sio jambo la kujisifu ila mifumo ikimtumbua atakuwa amepata haki yake,

Hongera sana Mama Samia,
 
wacha niseme kidogo,

Kama kuna mtu ameachia mifumo ifanye kazi kwa uwazi na kutokumuonea mtu ni huyu Rais Samia,

Kitendo hiki kinawafanya wananchi wenyewe wawajibishane katika levels zao,

Kutumbua mtu sio jambo la kujisifu ila mifumo ikimtumbua atakuwa amepata haki yake,

Hongera sana Mama Samia,
Arudishe viwanja na majengo ya umma waliyopora na kuanza kutumia pesa za serikali kukarabati, huu ni wizi.
 
Anayesifiwa asichukuliwe poa wala tu hajali hana habari na hayo mambo ya kulinda resilimali za nchi
 
Mama anaupiga mwingi, tuanze harakati za kumsafishia njia, halafu km inawezekana aongezewe awamu4 mbele....

Nakumbuka magu-fool Kuna wahuni walitakaga kumwongezea muda
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom