Ntemi Kazwile
JF-Expert Member
- May 14, 2010
- 2,182
- 307
Nina sababu tatu za msingi ambazo zimenifanya niichukie na kutopenda kuiona timu ya CCM na vibaraka wake wakiendelea kunitawala.
- Wameshindwa kulipatia ufumbuzi wa kudumu suala la msongamano wa magari jiji Dsm, licha ya kufanya ziara elfu kidogo nchi za nje zenye mifumo inayoeleweka kwenye majiji yao na wasijifunze lolote.
- Tanzania ni moja ya nchi chache duniani ambayo haina shirika la ndege linalofanya safari za kimataifa, na hakuna jitihada za dhati za kuwawajibisha wale wote walioshiriki kulifilisi shirika letu la ATC.
- Tanzania ni nchi iliyojaliwa kuwa na mpaka na njia kuu ya usafirishaji (bahari) na imeshindwa kuitumia kuwakomboa wananchi wake. Badala ya kuendeleza bandari na miundombinu inayoingia kwenye bandara ya Mtwara kwa ajili ya kuhudumia nchi jirani za Malawi, Zambia, DRC, Mozambique, serikali ya CCM inaelekeza nguvu kuendeleza bandari ya Bagamoyo bila sababu zozote za kuridhisha.
Kwa sababu hizi na nyingine nyingi za msingi, nimeamua kuwanyima kura yangu, naomba uniunge mkono ili tulikomboa taifa hili kwa kuwanyima CCM kura
1. Wameshindwa kushughulikia kikamilifu suala la miundombinu - wote tunajua kuwa miondombinu ni sawa na sensory nerves kwenye mwili wa binadamu, bila kuwa na miundombinu inayofanya kazi na inayokidhi mahitaji ya leo na ya miaka angalau 50 ijayo basi maendeleo itakuwa ndoto.
- Mabarabara yanayojengwa hayakidhi mahitaji yaliyopo, achilia mbali ya miaka 5 ijayo {mfano barabara za jiji la DSM ambazo zimejengwa ktk awamu ya nne - Mandela, Kilwa, etc, sehemu nyingi za nchi hii bado hazifikiki (yakiwemo maeneo yaliyoko mjini kama Kibamba) tangu tupate uhuru miaka 50 sasa.
- Wameshindwa kulipatia ufumbuzi wa kudumu suala la msongamano wa magari jiji Dsm, licha ya kufanya ziara elfu kidogo nchi za nje zenye mifumo inayoeleweka kwenye majiji yao na wasijifunze lolote.
- Tanzania ni moja ya nchi chache duniani ambayo haina shirika la ndege linalofanya safari za kimataifa, na hakuna jitihada za dhati za kuwawajibisha wale wote walioshiriki kulifilisi shirika letu la ATC.
- Tanzania ni nchi iliyojaliwa kuwa na mpaka na njia kuu ya usafirishaji (bahari) na imeshindwa kuitumia kuwakomboa wananchi wake. Badala ya kuendeleza bandari na miundombinu inayoingia kwenye bandara ya Mtwara kwa ajili ya kuhudumia nchi jirani za Malawi, Zambia, DRC, Mozambique, serikali ya CCM inaelekeza nguvu kuendeleza bandari ya Bagamoyo bila sababu zozote za kuridhisha.
2. Imeleta na inaendeleza matabaka katika jamii, ubaguzi wa aina yoyote ile ilikuwa sababu mojawapo iliyowalazimu mababu zetu wadai uhuru kutoka kwa wakoloni. Lakini miaka 50 baadaye serikali imeshindwa kusimamia usawa wa fursa za kujikwamua na changamoto katika maisha yao. Kwa sasa kuna matabaka katika kutoa huduma za jamii kama vile elimu, afya na nyingine nyingi. Viongozi wa serikali yetu hawatumii huduma za elimu, afya zinazotolewa na serikali wanayoiiongoza na badala yake huduma hizi zimebaki kuwa duni zisizokidhi mahitaji na hakuna jitihada zozote za msingi kulirekebisha tatizo hili ambalo baadaye linaweza kusababisha migogoro katika jamii yetu. Leo hii kuna watanzania wachache ambao wanaweza kuvunja sheria yoyote bila kuguswa na chombo chochote cha serikali huku wengine wakiandamwa ili kuwakomesha, haya tumeyaona kwa macho yetu kwenye mchakato wa kura za maoni za ccm ambapo rushwa na vitendo visivyo vya kistaarabu vilitawala lakini ni baadhi tu ndio waliowajibishwa richa ya kuwepo vyombo vyo dola katika kona zote za nchi hii. Ni aibu kwa TAKUKURU kuutangazia ulimwengu kuwa ni Iringa peke yake ndiko kulikuwa na vitendo vya rushwa!
3. Imeshindwa kusimamia rasimali za taifa hili kikamilifu na kushindwa kuwawajibisha wale wote ambao wameliingiza taifa katika mikataba ya kinyonyaji na wageni au watu wengine.
Kwa sababu hizi na nyingine nyingi za msingi, nimeamua kuwanyima kura yangu, naomba uniunge mkono ili tulikomboa taifa hili kwa kuwanyima CCM kura