CCM Madarakani: Sababu za kuitoa, ugumu wake na mbinu mbadala za kuing'oa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Madarakani: Sababu za kuitoa, ugumu wake na mbinu mbadala za kuing'oa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mag3, Jul 9, 2010.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Jul 9, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,187
  Trophy Points: 280
  Tatizo si Upinzani, CCM haitaondolewa madarakani kwa njia ya kura - huu ndio ukweli!

  Naam, huo ndio ukweli ingawa mchungu, CCM hawako tayari kuachia madaraka kwa njia ya amani, period. CCM inaamini kuwa ina hati miliki katika uongozi wa taifa la Tanzania na iko tayari kutumia kila linalowezekana kuilinda inachodai ni haki hiyo hata kama kwa kufanya hivyo inavunja sheria. Kuna mifano michache inayoonyesha kuwa CCM iko tayari kufanya chochote kile kuwalinda wafadhili wake hata ikibidi kumtoa kafara mwananchi yeyote yule anayekuwa tishio kwake.

  Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa CCM. Horace Kolimba alipojaribu kuikaba CCM kwa uongozi usio na dira na kukataa kusalimu amri mbele ya kikao maalum Dodoma, alipotelea mbali. Baba wa taifa alipoonekana amekuwa mwiba kwani alianza kuukandia wazi wazi uongozi wa CCM, hakuishi kushuhudia uchaguzi wa 2000 ambao nina hakika haungemrudisha Mkapa madarakani. Kwa kuwa hawa wawili walikuwa hawawezi kununulika, CCM haikuwa na njia bali kuhakikisha sauti zao hazisikiki tena.

  Lakini kwa walioweza kununulika ama kutishwa kama Edward Barongo kazi ilikuwa ndogo tu na hii leo idadi ya watu kama hao inaongezeka kila kukicha. Ndani ya CCM wapo wanaopayuka bungeni na kuitwa wapiganaji ndani ya chama lakini wanapowekwa kiti moto kwenye vikao wananywea kama vile hawapo. Ndani ya Upinzani wapo pia wanaochachamaa na kuleta matumaini kwa taifa lakini moto wao huanza kufifia ama kwa kumeza ndoana au kukosa ujasiri kama wa Mbunge wa Kararu (heko Dr. Slaa).

  Wana JF kubaki madarakani kwa CCM kumekuwa jambo la kufa na kupona kwani hatma ya taifa waliokabidhiwa wameiweka rehani kwa wenye fedha kwa tamaa ya mali. Matokeo yake hawafanyi kitu bali kwa maagizo ya waliowaweka madarakani na uchaguzi hauna maana tena. Bunge linafanya kazi kama kamati ya CCM na mahakama imedhihirika inatoa maamuzi kwa maelekezo ya CCM. Juzi tumemshuhudia Tendwa wa ofisi ya msajili naye akitekeleza matakwa ya CCM na hivo hivyo Jaji Makame wa tume ya uchaguzi.

  Kwa kuwa ni wazi CCM haiwezi kuondolewa madarakani kwa njia ya kura, ni njia moja tu tunayo - mapinduzi, kwani tunashuhudia watawala wetu wanaanza kuwapandikiza watoto wao na vijukuu vyao madarakani. Lazima ama tuachane na woga au tukubali kuwa watumwa ndani ya ardhi yetu wenyewe. Bila mapinduzi Marekani, Urusi na Ufaransa zingekuwa wapi ? Nina hakika wananchi wanaochukia ufisadi ni wengi ila woga wao ndio unaowafanya wawe wanyonge na kuwalamba miguu akina Jeetu Patel - vya bure vina gharama.
   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  Jul 9, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Swadakta!
   
 3. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #3
  Jul 9, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Mapinduzi ya namna gani; ya kijeshi au ya kifikra?

  Mimi ninadhani kuwa kama unashauri mapinduzi ya kijeshi, basi husaidii kutatua tatizo na wa hatutaendei popote. Kinachotakiwa ni mapinduzi ya kifikra kwa raia wetu kutoipigia CCM (soma hapa). CCM haiwezi kulazimisha kuendelkea kuwapo madarakani kama wananchi watainyima kura. Ni kweli CCM inaweza kuiba kurakiasi fulani lakini kama kweli wananchi wamemua kutoipigia CCM kura basi hata hizo za wizi hazitatosha kuirudisha madarakani.
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Jul 9, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Utategemea nini kama tume ya uchaguzi, polisi, UWT, TBC1 vyote ni CCM?
   
 5. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #5
  Jul 9, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kicuguu,
  Hata kama raia hawataipigia CCM kura zitapikwa. Unakumbuka yaliyompata Mrema 1995? Mkapa hakushinda uchaguzi ule.
   
 6. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #6
  Jul 9, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Well said mkuu, na It is likely watanzania wengi inaonekana hawaupendi ukweli sembuse huu ambao ni mchungu???????

  Funny enough kuna watu wanadhani mapinduzi ni lelemama iwe ya kijeshi au ya kifikra. The ugly truth is katika mapinduzi yeyote yaliyowahi kutokea siku zote there is an ugly side of it!
   
 7. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #7
  Jul 9, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  I have alwayz believed the same!!!!!
   
 8. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #8
  Jul 9, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,187
  Trophy Points: 280
  Mkuu Kichuguu, labda hukunielewa kwani kwa sasa naamini kabisa kuwa kutoipigia kura CCM hakutaiondoa madarakani kwani hawako tayari kufanya hivyo - kumbuka yaliyotokea Kenya na Malawi ambao kwa vyovyote vile ni wanafunzi kwa mbinu za CCM. Na ninaposema mapinduzi naomba nieleweke sina maana ya mapinduzi ya kijeshi - yawezekana ni kwa kukosa neno linalofaa zaidi ila kwa tafsiri kidogo tu naomba ninukuu kwa kiingereza;
  Neno hapa ni mass mobilization accompanied by civil disobedience. Tatizo ni kuwa si rahisi hii kufanyika kwa amani hapa kwetu kwani waliopo madarakani watatumia nguvu kuzima harakati hizi kama walivyojaribu kufanya watawala wote wadhalimu kabla yao. Kilicho dhahiri ni kwamba hata wafanye nini hawawezi kuzima nguvu ya wananchi kwa ujumla wao. Tulishuhudia mapinduzi kama haya yakitokea Romania, nchi tuliyokuwa na urafiki mkubwa nayo wakati wa utawala wa Nicolae Ceausescu.
   
 9. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #9
  Jul 9, 2010
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  haya ni maneno mazito.
   
 10. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #10
  Jul 9, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,187
  Trophy Points: 280
  CCM wamewekeza sana kwa wafadhili wao na kama hatukuamka hivi sasa na kutambua kuwa hatuwezi kuwatoa madarakani kwa kura basi tujue watatawala kwa miaka mia kama wanavyodai. Hawa watu wanaanza kuwapandikiza hadi watoto wao kwani wanaelewa fika kuwa siku watakapowekwa pembeni itabidi wawajibike kwa kuliuza taifa na kuwaweka rehani watu wake. Kuna watu wana uchungu sana lakini ni kama wamefungwa pingu na wanaishi kama wakimbizi ndani ya taifa lao.

  Hii ni kweli kabisa, mapinduzi yoyote yale yana gharama zake - lazima kuna watakaoumia kwani itakuwa ni ndoto kufikiri hawa mafisadi watasalimu amri kirahisi. Namkumbuka mke wa Ceausescu alivyowakoromea wazalendo na kumtetea mumewe hadi dakika ya mwisho.
   
 11. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #11
  Jul 9, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Kelele za mlango....... Watawala wa kiafrika kila siku ni kama wamelogwa ninakuapia kuwa lau kana CCM itashindwa atakayeingia madarakani atafanya yaleyale ya kung'ang'ania na kutekeleza yale yenye maslahi kwake. Kamwe hata siku moja usitarajie kuwa kupiga kelele na kulalama kutawafanya watawala wa afrika na hasa Tanzania kuwa na utaratibu wa kukubali kushindwa. Ni action pekee itakayoweza kuwaogofya kuwa waking'ang'ania watatolewa kwa nguvu na kupelekwa the hague.

  Ghana wamekuwa na demokrasia ya kukubali kushindwa kwa sababu moja tu uwazi uliopo kwenye uchaguzi na woga wa kushugulikiwa na wananchi kwa riot na kulipizana visasi. Jamaa yangu anatoka Ghana ananiambia huwezi kuiba kura hata moja kwa sababu kuu zifuatazo
  1. Kila mgombea ana kuwa na database yake ya matokeo na kuyajumlisha hata kabla hayajatangazwa

  2. wanatumia vitu kama mobile phones kupata matokeo ya remore areas

  3. Baada ya hapo linafuata zoezi la Reconciliation of results ( yaani wagombea wote wanakuwa pamoja juu ya meza na kujumlisha kituo kwa kituo, na mwisho wanaangalia kama matokeo yao waliyo nayo yanakubaliana na hesabu ya pamoja

  4. Kama kuna mtu namba zake zimekaa vibaya anaangalia kwa nini na kurekebisha. Hata kabla ya kutangazwa mshindi anakuwa amepatikana na wagombea wengine wanakubaliana nayo. Tume ya uchaguzi haina final say kama wagombea wamegomea matokeo

  Hii ndiyo demokrasia

  Njoo Tanzania:
  1. Tume ya uchaguzi ni branch ya makada wa CCM na wamepewa last say katika kusema nani ni mshindi, na kwa matokeo ya Rais ikitangaza hakuna a kuyahoji hata mahakama gani (Huu ni udikteta)
  2. Wasimamizi wa uchaguzi ni wakuruhenzi wa majimbo ambao hawapewi kazi hiyo mpaka wawe na kadi ya CCM
  3. Police wanapandishwa vyeo kwa kuwakandamiza wapinzani (remember mauaji ya Jan 2001 visiwani)
  4. Vituo vya kupigia kura havijulikani hasa ni vingapi hasa vijijini, unakuta kijiji kina watu 200 zintoka kura 2,000

  Ili Tupate mabadiliko kuna haja na sababu ya kuonesha kuwa pasipo na haki hata wewe unayelindwa na FFU 24 hutakaa ufurahie maisha. Tanzania ikiingia kwenye vurugu za kisiasa basi vurugu hizo zitakuwa zimeletwa na CCM na si mwingine. Ninajua ni ngumu kwa watawala kukubali wameshindwa lakini wanaweza kulegitimize ung'ang'anizi huo kwa kuwafanyia watanzania yale wanayojifanyia wao na familia zao nayo ni maisha bora. Kuna madikteta kama Ghaddafi japo wanatawala kiimla ila national share of revenues reaches every family na kuwaanya waone hakuna haja ya kumbadilisha.

  Tusisubiri yaliyotokea Kenya yatokee na kwetu tujifunze kutokana na makosa, ni rahisi sana kuivunja amani kwa kuwafyeka watu wasiokuwa na silaha wanaodai haki yao ila kuwafanya ndugu zao watakaobaki hai wasahau yaliyofanyika haiwezekeni na hii hujenga chuki, chuki hujenga uadui, uadui hujenda visasi, visasi hujenga vifo na vifo hujenga chuki tena yaani inakuwa circle ambayo kuivunja itachukua generations. Tusisubiri yafike huko CCM ikubali kushindwa kwa haki na uhuru. Huo ndiyo uongozi!
   
 12. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #12
  Jul 9, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Are you redeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeyyyyyyyy, raise your hands up!!!
   
 13. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #13
  Jul 9, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Diamond ideas.

  Red alert: Ubaguzi wa tabaka umeanza.
   
 14. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #14
  Jul 9, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Kitu cha kwanza kilichotakiwa kufanywa ni kwa watu wote wanaojiamini kuwa na 'mwamko' ni kuacha kuconform na mfumo dhalili uliopo wa kisiasa ambao sote tunajua hauzai matunda na unalinda maamuzi kwenye kikundi cha wafanyabiashara na wanasiasa wachache ktk mfumo wa mafioso.

  Kuacha ku-conform na mfumo kandamizi kulitakiwa kuanza kwa kuacha kushiriki kwa asilimia 100 uchaguzi wa Oktoba 2010. Kuendelea kushikilia kushiriki uchaguzi ambao unajulikana matokeo yake ni sawa na kujitia pingu sisi wenyewe tayari kuwekwa kwene minyororo ya mfumo huu kandamizi. Hatuezi kutegemea ku-commit gambler's fallacy over and over and over.

  Baada ya hapo, wale wenye mwamko tunapaswa sasa ku-demand new transitional government IMMEDIATELY, serikali ambayo itaweka misingi mipya ya kujitawala ambayo wengi watakubaliana nayo.
   
 15. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #15
  Jul 9, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Subirini Wazee wa Pemba ,wanasubiri mshindo wa Dodoma maana mara hii huenda wakamwaga razi kabisa na kuachana na Uzanzibari na Utanzania
   
 16. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #16
  Jul 9, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Hapana! Mag3 is correct.

  Usiogope mapinduzi, hayo ndo yameiweka Ghana ktk hali bora kuliko yetu. Hata hivyo nchi gani hapa Duniani iliendelea bila nguvu kutumika. Hapa US majimbo yalikusanywa kwa nguvu, UK bado nguvu inatumika, Canada nguvu ilitumika, Japan-udikteta kibao na emporor wao. sasa leo useme CCM ibadilike.

  Baada ya miaka ~50 ya uhuru, hatuhitaji mahubiri ya kubadili fikra. Hawa watu wameshindwa kukubali kubadilika na ktk mtiririko wa maendeleo, hapo sasa tunahitaji Mapinduzi tuuuu!

  Jambo la kukumbuka ni jeshi gani litumike maana wakuu wa majeshi yetu sasa hivi nao wako CCM na inaelekea wameridhika na hali waliyo achiwa maana nasikia hakuna wanachotaka bila kupewa.

  Tukubali kwamba Tanzania hakuna njia ya kuelimisha watu maana hili kundi lenye madaraka linafaidika kwa ujinga uliopo.
   
 17. lukenza

  lukenza Senior Member

  #17
  Jul 9, 2010
  Joined: Apr 11, 2010
  Messages: 120
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mag3

  Mzee una akili sijapata kuona
   
 18. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #18
  Jul 10, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,187
  Trophy Points: 280
  Mkuu Lukenza, sisi Watanzania tuko kama vile tunamsubiri mkombozi fulani aje atufungulie hii minyororo tuliyofungwa na CCM wakati funguo zenyewe tunazo mikononi mwetu tumezishika.

  Kila baada ya miaka mitano tunawasindikiza hawa wezi na walafi kwa nderemo na vifijo hadi kwenye meza kuu iliyosheheni mapocho pocho ya kila aina halafu tunarudi kwenye umasikini wetu, njaa yetu, magonjwa na ujinga usio mfano kusubiri kuwasindikiza tena awamu inayofuata kama tutakuwa hai bado. Pamoja na kukaa madarakani kwa miaka karibu hamsini yeyote anayetaka kuwakomboa wananchi anaambiwa ana uroho wa madaraka na sisi na akili zetu tunapiga vigele gele - kama huu sio uenda wazimu unaotuweka Watanzania kwenye kisiwa chetu cha pekee cha mazezeta, ni nini niambieni.

  Ona wana JF wanaodai kuwa hapa tunamkoma nyani, wanavyoogopa kuchangia hii mada eti kisa, neno mapinduzi limetajwa - kama mbuni wataficha vichwa vyao mchangani kwa kudai eti hiki ni kisiwa cha amani hawataki machafuko wala fujo huku polisi wao wako armed to the teeth kupambana na wananchi, wake kwa waume, ambao hawajabeba hata fimbo.

  Kwamba tunasubiri kumrudisha Kikwete madarakani kwa miaka mingine mitano, nachoka kabisa.
   
 19. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #19
  Jul 10, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Inawezekana mabadiliko kwa njia ya kura tuyangoje kwa miaka 70 -- kama vile kule Mexico mwaka 2001 chama tawala kilipoondolewa madarakani -- au Maldives mwaka 2008. Naamini kwa Tz iko siku tena si mbali sana, kwani urefu wa kamba inayopewa CCM kujinyongea bado haujatimia -la karibu mno!
   
 20. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #20
  Jul 10, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hili kama likifanikiwa, kweli itakua njia mbadala. lakini ni gumu kwa sababu ya Njaa tuliyonayo sisi wapiga kura.
   
Loading...