Lini CCM itatoka madarakani na wapinzani watashika Dola?

A43

JF-Expert Member
Nov 18, 2023
385
757
Hivi ni lini CCM itatoka madarakani, moja ya furaha yangu nikuona Ccm wakipokonywa kiti cha uRais sio kwa ubaya ila tu mabadiriko haya natamani niyaone nikiwa bado hai.

Mimi ni MwanaCCM japo sifungamani na chama kama kimenizaa hapana, napenda maendeleo ni mzalendo, naamini kwenye sera chanya zenye maslah mapana ya Taifa na watu wake hivyo mabadiriko ni mabadiriko tu naombea Taifa langu lipitie nyakati za mabadiriko.
 
CCM sawa itoke tatizo hivi vyama vingine ndio hamna kabisa nachokiona serious japo natamani pia iwe hivyo
 
Uzuri wa Mungu ni wa wote, ni Mungu huyo huyo Chadema mnayemubiria awaingize Ikulu, ndiye yeye aliyewapa CCM kuitawala Tanzania na ndiye anayewafanya waendelee kututawala milele !.
P
CCM haikupewa madaraka na Mungu , imepewa na mawakala wa Shetani Dkt Mahera na Salim Jecha
 
CCM haikupewa madaraka na Mungu , imepewa na mawakala wa Shetani Dkt Mahera na Salim Jecha
This is where Chadema got it wrong always!. Kama ilivyo kwenye uumbaji, ni Mungu huumba kila kitu including shetani, na Mungu ndie huita wote mbele ya haki, vivyo hivyo ni Mungu ndie huweka serikali za mataifa.

Laiti mngeufuata ushauri huu Elections 2015 - Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM Bali ni ... saa hizi zamani Chadema ingekuwa Ikulu!.
P
 
  • Thanks
Reactions: A43
Hivi ni lini CCM itatoka madarakani, moja ya furaha yangu nikuona Ccm wakipokonywa kiti cha uRais sio kwa ubaya ila tu mabadiriko haya natamani niyaone nikiwa bado hai.
Naomba kukuuliza, lets suppose CCM imepokonywa Kiti cha urais, ni nani huyo mwenye uwezo wa kuipokonya CCM kiti cha urais?
P
 
Hivi ni lini CCM itatoka madarakani, moja ya furaha yangu nikuona Ccm wakipokonywa kiti cha uRais sio kwa ubaya ila tu mabadiriko haya natamani niyaone nikiwa bado hai.

Mimi ni MwanaCCM japo sifungamani na chama kama kimenizaa hapana, napenda maendeleo ni mzalendo, naamini kwenye sera chanya zenye maslah mapana ya Taifa na watu wake hivyo mabadiriko ni mabadiriko tu naombea Taifa langu lipitie nyakati za mabadiriko.
= mabadiliko

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
  • Thanks
Reactions: A43
Mimi ni MwanaCCM japo sifungamani na chama kama kimenizaa hapana, napenda maendeleo ni mzalendo, naamini kwenye sera chanya zenye maslah mapana ya Taifa na watu wake hivyo mabadiriko ni mabadiriko tu naombea Taifa langu lipitie nyakati za mabadiriko.
Nakuunga mkono, no matter how good one, akikaa muda mrefu, anachosha, hivyo mabadiliko ni muhimu from time to time, CCM kina utaratibu mzuri wa miaka 10, anakuja mwingine, naomba kukuuliza, ukiondoa CCM, nani mwingine wa kutuletea maendeleo ambaye ni mzalendo, na mwenye sera chanya zenye maslah mapana ya Taifa, ili tumpe Ikulu yetu?.

Sidhani kwamba Kweli Tanzania hatuna watu wakuweza kuliongoza Taifa hili vizuri zaidi ya Wafanyavyo CCM. Naamini hata Nyerere alipostaafu wapo waliodhani sasa tunaelekea kuzimu kama taifa, lakini tizama bado tupo. Vivyo hivyo wewe unadhana hakuna awezaye zaidi ya ccm, mi naamini hilo linawezekana.

Utawala siyo chama ni watu, Imagine ccm wavurugane isambaratike unadhani Tanzania itazama? Taifa litabaki na wapo watu wataliongoza, na unaweza kushangaa labda wataongoza vyema zaidi.
Kuhusu vyama, Ni CHADEMA pekee ndio wanaweza unaweza usiwaone lakini wako wengi sana na wenye uwezo mzuri pia.

Tatizo ni mifumo iliyowekwa na CCM. Tizama sasa hivi wapinzani wanaiomba CCM iondoe sheria na utaratibu unaoifanya iendelee kuwepo madarakani. Yani CCM iruhusu kuondolewa madarakani, kitu ninachamini hakitawezekana. CCM hawatokubali, zitapigwa danadana kutwa kucha lakini haitatokea.

Ukweli ni kwamba CCM ikiruhusu matakwa ya wapinzani juu ya katiba, na CCM wakayaheshimu mabadiriko hayo, nadhnai wataondoka mapema sana. Lakini kwasasa hicho kitu hakipo.

Hivyo Naweza kusema nakubaliana na wewe hakuna wa kuing'oa ccm madarakani kwa mazingira ya sasa.

Solution ya Tatizo unaloliona ni Mifumo ccm iliyojiwekea, na hilo ni tatizo kubwa kwa wanao ota kuoondoa ccm madarakani.

Wanasema "if you don't completely understand the magnitude of the problem, you won't fully appreciate the incedible power of the solution" People need to understand the problem first.
 
it
Uzuri wa Mungu ni wa wote, ni Mungu huyo huyo Chadema mnayemubiria awaingize Ikulu, ndiye yeye aliyewapa CCM kuitawala Tanzania na ndiye anayewafanya waendelee kututawala milele !.
P
Sidhani kama wamekusikia....ngoja niseme tena ""
Uzuri wa Mungu ni wa wote, ni Mungu huyo huyo Chadema mnayemubiria awaingize Ikulu, ndiye yeye aliyewapa CCM kuitawala Tanzania na ndiye anayewafanya waendelee kututawala

najua watabisha, lakini ndiyo hiyo tena.
 
Back
Top Bottom