CCM Madarakani: Sababu za kuitoa, ugumu wake na mbinu mbadala za kuing'oa

Tusiwe wadhaifu kiivo.....ungekuepo Arusha sidhani kama ungeongea hivo??
Wewe uliekuwepo Arusha unafikiri CCM itaondoka na kipi kikubwa kilichotokea Arusha ambacho kwa utekelezaji wake kunaweza kuiondoa CCM madarakani ?
 
Facts 1: Bila shaka hujaelewa hoja ya Mwiba na kama umeelewa basi umekurupuka kujibu bila hata ya kutumia ubongo. Hoja ya mwiba ni mhimu mno. Kuna umhimu mkubwa sana wa kuwa na tume huru ya uchaguzi, though siungi mkono kwamba tume hiyo itoke nje ya nchi.

Binafsi nafikiri kwamba wajumbe wa tume ya uchaguzi wapendekezwa na vyama vya siasa kwa pamoja. Na wajumbe wa tume hii wasiwe wanachama wa chama chohote. Baada ya wajume kupitishwa na vyama, wao ndo watachaguana ili kumpata mwenyekiti wa tume, makamu n.k.

Mfumo wa utendaji kazi uwe kama ule wa senate ya chuo kikuu, ambapo iwapo chama kimojawapo hakitakuwa na imani na mmoja wa wajumbe wa tume, basi mjumbe huyo anasimamishwa kazi. Hii itasaidia sana kumfanya kila mjumbe na kila mtendaji ndani ya tume kujiona mwenye wajibu kwa vyama vyote bila upendeleo. Kukodi wazungu, haitasaidia kwa kuwa bado chama tawala kinaweza pia kuwanunua hao.
 
Kama vyama hivi vya upinzani vitainyamazia Tume za Uchaguzi bila ya kuzichukulia hatua yeyote ,basi tuelewe kuwa CCM itatawala nchi hii milele na milele.

Kuna idadi ya WaTanzania ,kuna idadi ya waliojiandikisha kama wapiga kura ,kuna waliopiga kura , pia kuna huu msamiati tunaousikia siku hizi wa Uboreshaji wa Daftari la kupigia kura.
Haikubaliki tupo waTz zaidi ya milioni 50 wanaopiga kura hawazidi hata milioni 20.
hayo ya mahesabu weka kando kwani wakiwa wengi au kidogo Tume hazihusiki wala hazipati tabu kuseti nambari hizo ,kwa vile watakalolitamka wao ndio lishapita.

Tumeona katika maandishi Lowasa akimwita Slaa mwongo ,katika barua alimwambia Slaa asihadaike na wingi wa watu wanaohudhuria mikutano, ni lazima akae na kujua siasa za Tanzania zinaendeshwa vipi ,something like that...! Hii ni kukatisha tamaa kisaikolojia iweje yeye Lowasa aliweka kambi huko kwake hivi akizungumza na miti ???

Vyama ni lazima vidai tume hizi za Uchaguzi ziwe huru kabisa zisizohusiana na chama chochote kile hata kama itabidi kukodi wazungu waje watusimamie shughuli za uchaguzi tokea uandikishaji hadi upigaji kura ,tume hizi ni lazima zibadilishwe kikamilifu kama si hivyo basi hakuna siku upinzani utashinda.
Inaweza kuondoka madarakani kama wapinzani wakijipanga vizuri na hasa katika bunge la sasa kutetea mabadiliko ya katiba itakayowapa fursa sawa na chama tawala katika uchaguzi, mfano kuwa na tume huru isiyokingana na upande wowote, pia suala la rais mgombea kuendelea kushikilia madaraka wakati yuko kwenye kampeni hivyo kupewa saport na tume na vyombo vya dola kwa kuwa yeye ndiye bosi wao.
 
wana jf mwakifahamu kifaa cha baiskeli kiitwacho kota pin? Ukitaka kukiondoa kwenye baiskeli unakiondoaje?

nimefanya utafiti kina ktk kipindi hiki nikabaini kweli watanzania hawaitaki ccm katukatu na sio siri wajinga wachache ndio walioipigia kura! Watu wengi wanajiuliza ni wapi hasa ccm inapotoa hizo kura za kuipa ushindi?

kama watanzania wanaikataa ccm kwa njia ya kura lakini bado inang'ang'ania haitaki kupisha ikulu basi muda ukifika tutaitoa kama kota pin inavyotolewa kwenye baiskeli na si vinginevyo. Wasidhani majeshi yanaweza kuzuia nguvu ya umma.
 
Kilichoonekana katika Bunge jipya linaloanza ni kwamba tabia ya uchu wa madaraka ya baadhi ya vyama vya upinzani kunawaondolea watanzania matumaini ya ukombozi kwa kukiondoa Chama dhalimu cha CCM madarakani ifikapo 2015.
Nasema hivi kwa sababu maneno na ahadi zilizotolewa wakati wa kampeni kwamba lengo la kwenda bungeni ni kuwapigania watanzania wawe na maisha bora zinaonekana wazi si kweli. Kinachoonekana sasa ni kwamba TLP, CUF na NCCR- Mageuzi wameingia bungeni kuangalia maslahi yao binafsi na siyo ya wananchi waliowatuma. Hivi vyama ni hatari na ni RECIPE ya CCM kuendelea kuwakandamiza watanzania kwa miaka mingine mingi.

Wangekuwa kweli wanatuwakilisha basi wangetupa kando maslahi yao washirikiane kwa pamoja kama upinzani kummaliza nguvu CCM na hatimaye kuweka nguvu pamoja ili ifikapo 2015 mabadiliko yatokee.

Kwa mtaji huu ulioonyeshwa leo katika kupiga kura za Uspika na TLP, CUF na NCCR- Mageuzi kumpa mwakilishi wa mafisadi ni wazi kuwa hatuna watu mle tuna WASALITI NA WALAGHAI walio walaghai watanzania kura zao. Hawa ni matapeli wanaotowesha matumaini ya watanzania 2015.

Wamepata faida gani wanapokuwa na sera za BORA WOTE TUKOSE, au JINO KWA JINO bila kujali kuwa anayeumia kutokana na maamuzi yao ni wananchi hali wao wakiendelea kupata allowance na mishahara mikubwa.

Inakuwaje wanawasahau waliowafikisha pale haraka namna hiyo wiki mbili tu baada ya sisi kuwapigia kura.

Mimi binafsi imeniuma sana sana, eti kwa sababu hawajapewa nao vyeo na CHADEMA ndo mfanye maamuzi yanyowagharimu watanzania hivi. Hebu tujiulize hapa ni siku mbili tu baada ya bunge kuanza watu wanaonyesha usaliti mkubwa namna hii kwa wananchi, je miaka mitano si itakuwa mnamalizana.

Naomba niwaulize CUF, NCCR-Mageuzi na TLP swali"

1.0 Hivi haya maamuzi mnayofanya ya kujitenga na kupunguza nguvu ya upinzani bungeni yana maslahi gani kwa sisi tuliowatuma?

2.0 Hivi usipopewa hiyo nafasi itakugharimu nini kuwa tu mbunge kama wengine kama unachokifanya si dalili ya kuwa na uchu wa madaraka kwa manufaa binafsi?

3.0 Kama kweli hamna maslahi binafsi kwa nini hamkuonyesha hekima ya kuridhika kuwa mbunge wa kawaida kuonyesha huruma ya kweli kwa wale waliokutuma kuwakomboa?

Mwisho nasema Mwakilishi wa kweli wa wananchi hatafuti mambo binafsi bali anaweka mbele maslahi ya waliomtuma hivyo ninyi mna proof kuwa kwenda bungeni mmefuata mambo yetu .

Sikutegemea katika kipindi hiki ambacho watu wamehamasika kuleta mabadiliko kuna chama kitaenda bungeni kuwa RECIPE ya kukifanya CCM kiendelee kutawala daima
 
Wamejimaliza wenyewe! Bahati nzuri TBC ilikuwa inarusha matangazo live na tumeshtushwa kuona kuwa Mgombea wa CHADEMA hakuungwa mkono na Wapinzani wengine threfore wameturahisishia kazi mwaka 2015 maana tumeshawaweka pamoja na CCM hivyo mwaka 2015 waishangae wakakosa kiti Tanzania Bara, labda CUF wataambulia Unguja na Pemba ambapo wana muungano official na CCM
 
Kilichoonekana katika Bunge jipya linaloanza ni kwamba tabia ya uchu wa madaraka ya baadhi ya vyama vya upinzani kunawaondolea watanzania matumaini ya ukombozi kwa kukiondoa Chama dhalimu cha CCM madarakani ifikapo 2015.
Nasema hivi kwa sababu maneno na ahadi zilizotolewa wakati wa kampeni kwamba lengo la kwenda bungeni ni kuwapigania watanzania wawe na maisha bora zinaonekana wazi si kweli. Kinachoonekana sasa ni kwamba TLP, CUF na NCCR- Mageuzi wameingia bungeni kuangalia maslahi yao binafsi na siyo ya wananchi waliowatuma. Hivi vyama ni hatari na ni RECIPE ya CCM kuendelea kuwakandamiza watanzania kwa miaka mingine mingi.

Wangekuwa kweli wanatuwakilisha basi wangetupa kando maslahi yao washirikiane kwa pamoja kama upinzani kummaliza nguvu CCM na hatimaye kuweka nguvu pamoja ili ifikapo 2015 mabadiliko yatokee.

Kwa mtaji huu ulioonyeshwa leo katika kupiga kura za Uspika na TLP, CUF na NCCR- Mageuzi kumpa mwakilishi wa mafisadi ni wazi kuwa hatuna watu mle tuna WASALITI NA WALAGHAI walio walaghai watanzania kura zao. Hawa ni matapeli wanaotowesha matumaini ya watanzania 2015.

Wamepata faida gani wanapokuwa na sera za BORA WOTE TUKOSE, au JINO KWA JINO bila kujali kuwa anayeumia kutokana na maamuzi yao ni wananchi hali wao wakiendelea kupata allowance na mishahara mikubwa.

Inakuwaje wanawasahau waliowafikisha pale haraka namna hiyo wiki mbili tu baada ya sisi kuwapigia kura.

Mimi binafsi imeniuma sana sana, eti kwa sababu hawajapewa nao vyeo na CHADEMA ndo mfanye maamuzi yanyowagharimu watanzania hivi. Hebu tujiulize hapa ni siku mbili tu baada ya bunge kuanza watu wanaonyesha usaliti mkubwa namna hii kwa wananchi, je miaka mitano si itakuwa mnamalizana.

Naomba niwaulize CUF, NCCR-Mageuzi na TLP swali"

1.0 Hivi haya maamuzi mnayofanya ya kujitenga na kupunguza nguvu ya upinzani bungeni yana maslahi gani kwa sisi tuliowatuma?

2.0 Hivi usipopewa hiyo nafasi itakugharimu nini kuwa tu mbunge kama wengine kama unachokifanya si dalili ya kuwa na uchu wa madaraka kwa manufaa binafsi?

3.0 Kama kweli hamna maslahi binafsi kwa nini hamkuonyesha hekima ya kuridhika kuwa mbunge wa kawaida kuonyesha huruma ya kweli kwa wale waliokutuma kuwakomboa?

Mwisho nasema Mwakilishi wa kweli wa wananchi hatafuti mambo binafsi bali anaweka mbele maslahi ya waliomtuma hivyo ninyi mna proof kuwa kwenda bungeni mmefuata mambo yetu .

Sikutegemea katika kipindi hiki ambacho watu wamehamasika kuleta mabadiliko kuna chama kitaenda bungeni kuwa RECIPE ya kukifanya CCM kiendelee kutawala daima

HAta CHADEMA ina mafisadi kibaoooooo!! Bora hata sisiem wanahesabika!
 
Hivi tukisema wapinzani hapa tuna maana gani? Ni TLP, CUF na NCCR tu? CHADEMA wao ni nani? Kwa mawazo yangu bila ya kuingilia uhuru wa mawazo ya wengine, bado tuna tatizo la ubinafsi. Kwa niliyoyasikia jana, CHADEMA ilikataa kuungana na vyama vyengine kwa sababu tayari wana asilimia 45 inayotosha kuunda kambi, sasa kwa majigambo hayo vyama vyengine vilipaswa kufanya nini?

Kwa kuwa nafasi za Mwenyekiti na Katibu ni mbili na vyama vipo vinne, wasingeliweza kugawana hizo, lakini angalau kauli tu, ari na moyo wa kutaka ashirikiano vingelitosha kuwaweka wapinzani pamoja. Tusubiri kuona WAPINZANI wanafanya nini wakati wa kugawana nafasi za Kamati za Bunge.

Binafsi inaniuma sana kuona wapinzani WOTE wanasambaratika hata kabla ya mchezo kuanza. Kwa ufupi, nakubaliana na kauli kuwa KWA TABIA HII YA WAPINZANI, CCM ITAENDELEA MILELE
 
Mimi naona tunachama cha upinzani serious kimoja tu. Wengine hawa mi siwaelewi elewi. Mare nyingi wanatuchanganya sana katika maamuzi yao. Hivyo, chadema wakijipanga vizuri wanaweza kuchukua nchi. Lakini lazima wawe macho na mamluki pamoja na kufanyia kazi maeneo yote yenye udhaifu ndani ya chama ili kupunguza maeneo ya kukosolewa.
 
Hivi tukisema wapinzani hapa tuna maana gani? Ni TLP, CUF na NCCR tu? CHADEMA wao ni nani? Kwa mawazo yangu bila ya kuingilia uhuru wa mawazo ya wengine, bado tuna tatizo la ubinafsi. Kwa niliyoyasikia jana, CHADEMA ilikataa kuungana na vyama vyengine kwa sababu tayari wana asilimia 45 inayotosha kuunda kambi, sasa kwa majigambo hayo vyama vyengine vilipaswa kufanya nini?

Kwa kuwa nafasi za Mwenyekiti na Katibu ni mbili na vyama vipo vinne, wasingeliweza kugawana hizo, lakini angalau kauli tu, ari na moyo wa kutaka ashirikiano vingelitosha kuwaweka wapinzani pamoja. Tusubiri kuona WAPINZANI wanafanya nini wakati wa kugawana nafasi za Kamati za Bunge.

Binafsi inaniuma sana kuona wapinzani WOTE wanasambaratika hata kabla ya mchezo kuanza. Kwa ufupi, nakubaliana na kauli kuwa KWA TABIA HII YA WAPINZANI, CCM ITAENDELEA MILELE

Sidhani kama ni majigambo kwa CHADEMA bali ni effort yao iliyowafikisha hapo. Walijitahidi kunadi sera zao zikauzika bila support yoyote. Chadema kwa maoni yangu ni wastaarabu sana. Ndiyo chama pekee ambacho akijawahi kuungwa mkono na vyama vingine hivyo na wao wanatakiwa kuonyesha uzalendo kama ambavyo wenzao walifanya huko nyuma.

Pili term iliyopita upinzani ulikuwa CUF na viti vyao vya Zanzibar kama kawa na CHADEMA ilikuwa na 5 Bara na UDP 1. Hivyo CUF hawakufikia asilimia 12 inayotakiwa kuunda kambi ya upinzani ndiyo maana waliungana. Lakini sasa hivi hali ni tofauti CHADEMA wao wataamua kama wataweka baadhi ya wabunge kutoka vyama vingine ni wao kuamua hawalazimiki.
 
huyo mgombea waliyemweka walipatana na hivyo vyama vingine? hivi kama NCCR na Mrema wa TLP wanajisikiaje kuhusu Marando? nafikiri tusilaumu tu. wangeweza kukaa pamoja wakapatana ili wamweke mtu ambaye vyama vya upinzani wangumuunga mkono na si kwa Chadema iweke mtu na wengine walazimishwe kumuunga mkono hata kama hawamtaki. mimi naona vyama vyote vina matatizo makubwa hasa ya UBINAFSI
 
Kuna kitu kimoja watu wengi hawajajua, chama cha siasa ili kiwe imara kinahitaji viongozi makini wanaojua kuchambua mambo, mimi naunga mkono uamuzi wa Chadema wa kujisimamia wenyewe, anaetaka kujiunga nao anakaribishwa, na afuate sera za Chadema, kama watayumbishwa na wachache wenye tamaa ya uongozi na mamluki wa mafisadi watapotea.

Walichofanya CUF, NCCR, TLP, ni sawa ili kuwapa Chadema nafasi ya kuwa chama kikuu cha pinzani kiukweli.

WABUNGE WA CHADEMA KAZENI BUTI, VIJANA TUPO NYUMA YENU.
 
ukweli utabakia kuwa miongoni mwa vyama vyetu tunavyoviita eti ni vya upizani ni kujidanganya, kwani ni mamluki kibao, chama kama cuf tayari wamekipata kile ambacho wakichokitaka kule zenji unategemea wakuunge mkono tayari wanajua wamekata dolla:bowl:
 
Back
Top Bottom