CCM Madarakani: Sababu za kuitoa, ugumu wake na mbinu mbadala za kuing'oa

CUF, NCCR na TLP in mamluki wa demokrasia hapa tanzania...

Hawana maana kama kweli wamemchagua spika wa mafisadi... ila ni vizuri kujua adui yako ni nani..

Chadema wajipange na wafanye kazi... 2015 nchi ni yetu...
 
Mlitegemea mrema amchague marando? Je cheyo? Je cuf maana cuf ni chama tawala B hao wote si wapinzani bali wachumia tumbo na malengo yao yametimia. Ila NCCR sijui kwa nini wameshindwa kuelewa ukweli maana kwanza wengi ni vijana ambao wamebebwa na zitto kabwe, hapo kuna kitu kimejificha. All in all Chadema ndio chama cha upinzani sasa vingine aidha ni vyama tawala au havieleweki. Ila naamini this time mchezo amba CCM wamezoea kuucheza ndio mwisho wao chadema kazeni bout
 
Maandamano yanahitajika sio kumuondoa Kikwete bali iwe kuiondoa CCM madarakani, natumai wengi mtakubaliana nami, haiwezekani kumuondoa Kikwete kwani tumeambiwa alimaliza miaka mitano, halafu WaTz tukachaguliwa tena kuwa ni chaguo la Mungu...

Tatizo nilionalo sio Kikwete kwani wamepita Vikwete wengi tu, tatizo la nchi hii ni utawala wa CCM ambao unazidi miaka arobaini, Kama bado angekuwepo Nyerere ingelikuwa rahisi sana na pengine tungelishamaliza kazi, ila alisituka na mapema.

Na kama hatuwezi kuipinga CCM kuwepo madarakani kwa muda mwingi hivi sasa, basi wakati mzuri ni 2015 na hakuna kingine, isipokuwa ni kutokubalika uongozi wa CCM baada ya 2015.

Kwa maana hiyo au ikiwa ni hivyo,kipindi hiki kilichobakia CCM wajijue kuwa ni kipindi chao cha mwisho msemo mwingine hata wakishinda hawatakubalika,tutaingia barabarani na kupinga kuendelea kuiongoza nchi hii.

Tumemsikia Warioba akibadili upepo eti ........wanaoihitaji Tanganyika wasikilizwe..... ! Huyu Warioba uzee unamwandama anaweza kuwa sawa na Kingunge wakisaidiwa na Makamba.

Utawala wa CCM ni lazima usitishwe kimaandamano ya kwamba CCM na utawala wake waondoke madarakani haraka iwezekanavyo kwani wananchi walio wengi hali zao ni taabani na hawana wakumlilia kwani utawala wa CCM umeshindwa kuwatimizia au angalau kuwaondolea na kuwapunguzia shida, kila siku ni bora ya jana.

Hali za maisha na usalama wa raia unazidi kudidimia, ni juzi tu wananchi wamevamiwa na kundi la watu zaidi ya 50 na kupigwa vibaya sana, watu ambao siku chache walikuwa katika kizaazaa cha kulipuka kwa mabomu pale Gongolamboto, usalama wa wananchi hakuna,watu wanalala kwa hofu, serikali inafanya uchunguzi, ndio imetoka.

Hali za mipakani ni ujangili kwa kwenda mbele kila kukicha mabasi yanavamiwa ndani ya nchi huru na sio mara moja kwa mwaka bali ni hali iliyoota mizizi, uchunguzi unafanywa, hazina ya nchi inaibwa na wakuu wa CCM kujilimbikizia mihela katika benki za ndani na benki za nje, uchunguzi unafanywa walizipataje, rushwa kubwakubwa zinazoididimiza nchi (radar ndege train) uchenguzi unafanywa sasa tumehama kwenye kamati na tumehamishiwa kwenye uchunguzi huku akizuka mwengine akisema WaTanganyika wanaidai Tanganyika tunaambiwa kunachunguzwa ili madai hayo yasipuuzwe.

CCM ni lazima iondolewe madarakani kwa mikakati ya maandamano ya nchi nzima, tujiandaeni kwa kuwaeleza wananchi kuwa ikiwa CCM itajitangazia ushindi tena, basi ni maandamano katika miji mikuu yote, Tanzania (Tanganyika) na Tanzania (Zanzibar) kwa pamoja, bila ya kujali itikadi za vyama vya siasa dini au kabila.
 
Unanikumbusha song la nitoke vipi?
Naona thorn leo upo ant ccm-its unbelievable
so where were you all that time
 
Mkuu Mwiba, nimekubali kabisa uliyoyaandika hapo juu isipokuwa naona kama ukiwaambia wananchi wengi wakiwemo kada wa CCM ambao wana 'bifu' na Kikwete kuwa unataka kuiondoa CCM basi utapata resistance kubwa. Ila ukianza na the symbol of their hatred or symbol of incompetence (= Kikwete) basi ni wepesi zaidi kupokea wazo la kumng'oa.

Mfano mmoja mzuri nakupa ni mapinduzi ya Misri, walianza na Mubarak has to go lakini sasa hivi wanaendelea kuandamana na kuwatoa mawaziri na wapambe wote wa chama cha Mubarak.

A journey starts with a step, let's go one step at a time na mwishoni tutafika. Ila nakubaliana na wewe 100% katika uliyoyasema hapo juu kwani huwezi kupata maendeleo Tanzania mpaka CCM ing'olewe madarakani!
 
The time has come CCM will die a natural death kama KANU. Naona wamelewa madaraka hawajali wamekuwa kama sikio la kufa....... Hata wale viongozi waadilifu walioko ccm wamemezwa kimejaa fitina, majungu na uzandiki.

Kama Moi alivyoiangusha KANU ndo JK ataingusha CCM na first step ya anguko lao ni uchaguzi wao wa 2012 sababu makundi yanayohasimiana yatafarakana sababu ya urais 2015 so itakuwa vita vya panzi... laiiini kama unanawa
 
Mwiba bandiko lako ni zuri ila kama ni kusubiri 2015 basi utegemee usanii uleule. Nchi hii inahitaji mapinduzi kama yale ya Egypt, mapinduzi ya wananchi ambapo Bunge litavunjwa, katiba ita7imamishwa na wanasiasa hawa WANAFIKI wanaojali matumbo yao wataachwa pembeni tupate wazalendo wa kweli kutuongoza.
 
Susuviri na wengine ambao tunaitazama Tanzania kwa jicho la kuihurumia jinsi inavyoendeshwa, ni lazima tuangalie uwezekano wa sehemu zote, kama ni kumuandama Kikwete au kuandama utawala wake, yote hayo yanaweza kuingia katika matokeo (probabilty), kwa mfano tumeanza na Kikwete tuiangalie sheria inasemaje (Japo sheria zimekuwa zikituandama sisi wananchi tulio chini).

Kikwete hana kosa au sio, amefanywa aonekane ni mshindi wa Uchaguzi mkuu, tume imemtangaza, huu ni muhula wake wa mwisho kesho kutwa anawekwa mwengine, kutokana na ukandamizaji wa haki, tume itamtangaza mwengine hukohuko CCM, hata wananchi wote tukimchagua mpinzani, ndivyo tulivyozoeshwa tukazoea.

Sasa iwapo harakati za kumpinga Kikwete zitagonga ukuta ni lipi linaloweza kufuata? Hapa tulipo kuna mvutano wa vyama vya upinzani kila kimoja kinajiona kiko mbele na kinapendwa zaidi, nionavyo ufa huu unatuweka katika position ambayo tutakuwa ni wenye kutawaliwa milele, sasa ili ufa huu uondoke ni lazima upatikane umoja utakaokuzwa kwa sauti moja, kwa hapa tulipo kuna mvutano wa kivyama, kisheria na umoja umegawika.

Ili kuupata umoja huu ni lazima kugeuzwe mbinu, mbinu ambazo zitaturudisha katika msimamo wa pamoja. Ukiangalia kwa ndani utaona vyama huwa vinatupiana mpira na hata wananchi huwa wanatupiana mpira kwa kusema chama fulani kipo na CCM au kipamoja na mtawala ambae ni CCM hapa huwa tunagawika na hakuna umoja unaopatikana.

Hivyo itatuwia vigumu kujikusanya kwa sasa kumuondoa mtawala asiejali raia, ameshachomekwa na sheria zinamlinda ingawa nguvu za umoja zimeonyesha sheria zinaweza kuwekwa kwenye pose mpaka kijulikane kitakiwacho.

Ingelikuwa rahisi kupinga ushindi wa Kikwete mara tu alipotangazwa na umma ulikuwa tayari kuitikia wito wa pamoja kupinga utangazwaji wa Kikwete, umeona wengine wamesita kisha wakaachia wengine wamekubali wakionekana wakikenua meno na mapengo yote nje, hapa tuna tatizo.

Nilichokiona ni kuandaa maandamano ya kuipinga CCM kuendelea kuitawala nchi hii, miaka waliyoketi madarakani imetosha kama ilivyokuwa imetosha kwa Mubaraka, Ali, Gadafi na wengine wanaofuatilia, basi CCM kama mtawala aliyekaa muda mrefu ni lazima aondoke (Muda mrefu mfululizo) ni lazima aondoke.

Nafasi au Chance kubwa ambayo inaweza kutumika ni hiyo ya kuanza kuikataa CCM kwa maandamano ya hapa na pale ya kwamba imetosha.
 
Last edited by a moderator:
Huu ni Mwiba tunaoufahamu au wamekwiba password yako? Maana siamini ninachokisoma kama kimeandikwa na Mwiba. Kama kweli ni wewe basi hongera kwa kuweza kuzisoma alama za nyakati.
 
mkuu mwiba ni undefined huwa nakuchukia we jamaaa lakini leo thread zako zote unapost vitu by reasoning na sio feelings
 
Ahsante sana kwa kuliona hilo
kwani ni nani asiyeona hali halisi ya maisha?
kwani ni nani asiyeshuhudia kadha wa kadha hapa tz?
hata wale wanafiki siku ya mwisho wataungana tu na wananchi kudai haki zao
Unanikumbusha song la nitoke vipi?
Naona thorn leo upo ant ccm-its unbelievable
so where were you all that time
 
Huu ni Mwiba tunaoufahamu au wamekwiba password yako? Maana siamini ninachokisoma kama kimeandikwa na Mwiba. Kama kweli ni wewe basi hongera kwa kuweza kuzisoma alama za nyakati.
jamani mbona kila mtu baada ya kuchangia mada kwanza mnaanza na kumuuongelea mtoa mada? mmh kazi kweli kweli
 
Hivi akitolewa JK madarakani bado CCM itaendelea kuongoza nini? na nani/
mi nijuavyo Raisi akiachia madaraka automatically na chama chake kinakuwa kimeshajimaliza kabisa.
post za nchi nzima zitakuwa wazi kabisa
Mkuu Mwiba, nimekubali kabisa uliyoyaandika hapo juu isipokuwa naona kama ukiwaambia wananchi wengi wakiwemo kada wa CCM ambao wana 'bifu' na Kikwete kuwa unataka kuiondoa CCM basi utapata resistance kubwa. Ila ukianza na the symbol of their hatred or symbol of incompetence (= Kikwete) basi ni wepesi zaidi kupokea wazo la kumng'oa.

Mfano mmoja mzuri nakupa ni mapinduzi ya Misri, walianza na Mubarak has to go lakini sasa hivi wanaendelea kuandamana na kuwatoa mawaziri na wapambe wote wa chama cha Mubarak.

A journey starts with a step, let's go one step at a time na mwishoni tutafika. Ila nakubaliana na wewe 100% katika uliyoyasema hapo juu kwani huwezi kupata maendeleo Tanzania mpaka CCM ing'olewe madarakani!
 
Back
Top Bottom