CCM: Maazimio ya Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa

Baraka Mina

JF-Expert Member
Sep 3, 2020
581
574
Mazimio ya Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa kilichoketi leo Juni 22, 2021 katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center.

TAARIFA KWA UMMA

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu. Samia Suluhu Hassan, leo Juni 22, 201 ameongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa kilichofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre, Dodoma.

Kamati Kuu ya CCM imempongeza Ndugu Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ndugu Hussein Ali Mwinyi Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kutekeleza ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020/2025 katika nyanja za kijamii, kiuchumi na kisiasa kwa mafanikio makubwa.

Kamati Kuu ya CCM imewapongeza Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka 2021/2022 kwa 94%.

Kamati Kuu ya CCM imefanya uteuzi wa Ndugu Shekha Mpemba Faki kuwa mgombea Ubunge Jimbo la Konde kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi mdogo utakaofanyika Julai 18,2021.

Aidha, Kamati Kuu imefanya uteuzi wa Ndugu Kenan Kihongosi kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) kuanzia Juni 22, 2021.​

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Imetolewa na:
Shaka Hamdu Shaka
Katibu wa NEC - Itikadi na Uenezi.

#ChamaImara
#Kaziinaendelea


IMG-20210622-WA0214.jpg
 
Mbona naona kama Iringa/Njombe ndio CCM haswa, makamu mwenyekiti anatoka Mkoa wa Njombe, Katibu Mkuu wa CCM nasikia nae anatoka Mkoa wa Iringa na hili jina la katibu mkuu wa UVCCM ni kama nalo ni mtu wa Iringa /Njombe, kama ndio hivyo basi shughuli ipo.
 
Mbona naona kama Iringa/Njombe ndio CCM haswa, makamu mwenyekiti anatoka Mkoa wa Njombe, Katibu Mkuu wa CCM nasikia nae anatoka Mkoa wa Iringa na hili jina la katibu mkuu wa UVCCM ni kama nalo ni mtu wa Iringa /Njombe, kama ndio hivyo basi shughuli ipo.
Sijajua kama kuna ukweli katika hilo Ila uongozi unaangalia sifa stahiki na sio sehemu ambayo viongozi wanatokea.
 
Back
Top Bottom