CCM kumsifia Dkt. Slaa leo hii ni unafiki wa kiwango cha SGR

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,372
Nashangazwa sana na sifa za kinafiki CCM wanazoompa Dr. Slaa leo hii wakati ni CCM hawa hawa walimuita muongo na mzushi wakati alipokuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA.

Isitoshe, ni CCM hawa hawa kupitia serikali ya Kikwete, walimpiga Dr. Slaa virungu wakati wa maandamano ya CHADEMA mkoani Arusha na hata aliekuwa mchumba wa Dr. Slaa nae hakusalimika pamoja na wanachama na viongozi wengine wa CHADEMA.

Kama kuna mwenye ushahidi wa viongozi wa CCM na serikali yake kumsifia Dr. Slaa wakati yuko CHADEMA auweke hapa tuondoe ubishi.

Hata hivyo, muda umetusaidi kugundua kuwa Dr. Slaa naye hakuwa akipinga sera na matendo ya CCM kutoka moyoni, bali alikuwa akifanya vile kutetea kibarua chake kwani mpinzani wa kweli huwezi kurudi CCM wakati CCM ni ile ile kwa sera na matendo yako.

Angekuwa serious, angetafuta chama kingine lakini sio kwenda kutumia serikali ya chama kilekile alichokuwa anakipinga na hivyo hakuwa na tofauti na viongozi wa CHADEMA waliompokea Lowassa kama kweli hiyo ndio ilikuwa hoja yake kuu.

CCM acheni unafiki tena unafiki wa kiwango cha SGR katika swala hili. Msitufanye wajinga na hatuna kumbukumbu.
 
Jamaa kaandaliwa cheo kikubwa Sana , waungwana tusibaniane ugali...hata mbowe alimpokea Lowasa kimaslahi , maisha ni haya haya wakuu...!! Anyway tozo imerudishwa huko, wanangu wa namtumbo tuongezeni bidii kwenye kilimo
 
Katika watu nilioamini uwezo wao ni Dkt Slaa ni nikawa najiuliza sana CHADEMA anafanya nini? Wahenga walisema muda ni hakimu wa haki.

Dkt.Slaa sio mnafiki na wala haujui unafiki, kipindi kile choo kilipopelekwa sebuleni kwa maamuzi ya mtu mmoja hakukaa kimya na akajiweka kando.

Kwa kipindi kirefu Dkt.Slaa alitaka kuiona CCM ya Magufuli na hapo kwa mtu mwenye akili timamu huwezi kuficha hisia zako
 
Mi nadhani kwenye unafiki upande wa hii nchi hakuna upande wote ni wanafiki tu.
JamiiForums-1642026372.jpg
 
Jamaa kaandaliwa cheo kikubwa Sana , waungwana tusibaniane ugali...hata mbowe alimpokea Lowasa kimaslahi , maisha ni haya haya wakuu...!! Anyway tozo imerudishwa huko, wanangu wa namtumbo tuongezeni bidii kwenye kilimo
Lakini ni DKT sla ndo aliratibu, kumleta na kumpokea na kumkaribisha Rais wa mioyo yetu kundini. Na Mwamba kamtendea sana mengi mazuri huyu Dkt uchwara.

Licha ya kumtukana mwamba na kumsema vibaya mwamba hajawahi kumjibu. Mwamba Always turned another cheek.

Linafiki kweli huyu Dkt
 
Mimi namlaumu zaidi huyo mzee kuliko hao CCM, alituaminisha anaongoza mapambano akaaminiwa akawekwa mstari wa mbele halafu wakati ulipofika wa kutoa ushirikiano wake akadanganywa akakimbia.
 
Lakini ni DKT sla ndo aliratibu, kumleta na kumpokea na kumkaribisha Rais wa mioyo yetu kundini. Na Mwamba kamtendea sana mengi mazuri huyu Dkt uchwara.

Licha ya kumtukana mwamba na kumsema vibaya mwamba hajawahi kumjibu. Mwamba Always turned another cheek.

Linafiki kweli huyu Dkt
Ni hatari sn na aibu
 
Hivyo ni viashiria kuwa Dr Mihogo ndio anaaga. Yu karibu kutwaliwa
 
Dr. Slaa ni mwanasiasa wa kweli.

Siyo mchumia tumbo kama akina Mbowe, Lissu na wenzao ambao kutwa kucha wapo pale kuangalia masilahi yao binafsi.

Dr. Slaa ana msimamo kwa kile anachokiamini, alifanya siasa za kisayansi siyo hawa wanasiasa wa leo ambao hawajui hata wanataka nini.

He's amongst true patriots and great politicians we have.
 
Cha ajabu nini mkuu..??.wanasiasa ni wachumia tumbo tuu.. Chadema walimponda sana E.L , lakini hao hao walimpokea na kumpa bendera yao aipeperushe.. Achana nao watakupotezea muda...
 
Jamaa kaandaliwa cheo kikubwa Sana , waungwana tusibaniane ugali...hata mbowe alimpokea Lowasa kimaslahi , maisha ni haya haya wakuu...!! Anyway tozo imerudishwa huko, wanangu wa namtumbo tuongezeni bidii kwenye kilimo
 
Jamaa kaandaliwa cheo kikubwa Sana , waungwana tusibaniane ugali...hata mbowe alimpokea Lowasa kimaslahi , maisha ni haya haya wakuu...!! Anyway tozo imerudishwa huko, wanangu wa namtumbo tuongezeni bidii kwenye kilimo
Kwa umri na historia yake huenda akarudi alikotokea kabla (CCM), na huwezi jua huenda akawa Katibu Mkuu!
 
Back
Top Bottom