CCM kukomba wapinzani, tafsiri yangu

JEKI

JF-Expert Member
Aug 16, 2013
4,845
2,938
Kumekuwepo na wimbi kubwa la CCM kuchukua wapinzani kwa gia kuwa wamemuelewa Rais, kwa upande wangu hoja hii ni dhaifu sana, kwani ukimuelewa mke/mme wa mtu ndo unahamia kwake? Pia ukimuelewa leo haimaanishi basi ataendelea kueleweka siku zote, kwa mtu makini kama umemuelewa Rais basi unatakiwa ubaki kumfatilia kama kweli ataendelea kueleweka ili huko mbele asije akabadilika.

Kwa maoni yangu kitendo hiki cha CCM kukomba wapinzani inaonesha CCM imeishiwa, haina tena watu ndani ya chama chake wenye uwezo, hata nature tu inasema, upepo huvuma kutoka kwenye mgandamizo mkubwa kwenda mgandamizo mdogo.

Ni maoni yangu na si lazima yafanane na yako.
 
Huna lolote mzandiki wewe. Mmeishiwa hoja za msingi mnabaki kukengeuka kwenye mitandao ya Kijamii. Fanya kazi,usije ukaja na Uzi kesho ukilalamika mkeo/mumeo anatafunwa na dada/kaka wa kazi.
 
Hoja hiyo ni dhaifu mno kwa mtu mwenye kujitambua na kutafakari mambo kwa mapana yake, unamuelewa mtu kwa jambo moja unaacha kumuelewa kwa mengi ni uendawazimu wa hali ya juu sana. Na hoja yao kubwa imejikita kumuelewa kwenye ufisadi na kuacha kutafakari mengi yahusuyo uchumi, usalama wa raia na mali zao, mahusiano kimataifa, uminywaji wa uhuru wa mawazo, tatizo kubwa la ajira kwa vijana n.k. Sasa mtu anapoona watu kila siku wanaokotwa watu kwenye masandurusi wakiwa wamekufa na haoni kama ni tatizo huyo mtu ana tatizo mahali, mtu anaona uchumi unavyodorora lakini haoni kama ni tatizo huyo mtu anapaswa kujitafakari sana, anaona kabisa serikali haina mipango mahususi ya kupambana na tatizo kubwa la ukosefu wa ajira halafu haoni kama ni tatizo mtu huyo anapaswa kuchakata akili yake kama yuko sawa sawa.

Kwa ufupi wote wanaotimkia ccm hawana hoja zozote shawishi kwa umma uhalali wao wa kwenda huko zaidi ya blah blah tu.
 
Wakati mwingine hata Rais hahusiki ila kuwa wapambe wanajua kinachompendeza ...
 
sure.
 
Kumekuwepo na wimbi kubwa la CCM kuchukua wapinzani kwa gia kuwa wamemuelewa Rais, kwa upande wangu hoja hii ni dhaifu sana, kwani ukimuelewa mke/mme wa mtu ndo unahamia kwake? Pia ukimuelewa leo haimaanishi basi ataendelea kueleweka siku zote, kwa mtu makini kama umemuelewa Rais basi unatakiwa ubaki kumfatilia kama kweli ataendelea kueleweka ili huko mbele asije akabadilika.

Kwa maoni yangu kitendo hiki cha CCM kukomba wapinzani inaonesha CCM imeishiwa, haina tena watu ndani ya chama chake wenye uwezo, hata nature tu inasema, upepo huvuma kutoka kwenye mgandamizo mkubwa kwenda mgandamizo mdogo.

Ni maoni yangu na si lazima yafanane na yako.
Tafsiri yake CCM wanahela na watoa rushwa wakubwa
 
Kwenye siasa wanachama huwa hawatoshi ni kama pesa kila siku unazisaka
ni kweli, lakini sidhani kama ni busara kutafuta pesa kwa kujidhalilisha na hata kuuza utu wako ili tu upate pesa kwa kuwa hazitoshi.
 
Huna lolote mzandiki wewe. Mmeishiwa hoja za msingi mnabaki kukengeuka kwenye mitandao ya Kijamii. Fanya kazi,usije ukaja na Uzi kesho ukilalamika mkeo/mumeo anatafunwa na dada/kaka wa kazi.

Vumilia tu hiyo ndio tabia ya ukweli kuuma.
 
Back
Top Bottom