Tetesi Kuhusu Visukusuku vya Sokwe-Mtu Wa Beijing
Visukuku vya sokwe-mtu wa Beijing kabla ya kupotea vilihifadhiwa katika sanduku la chuma la usalama la hospitali moja ya mji wa Beijing.
Siku chache kabla ya kuzuka vita ya Pasifiki, profesa Wei Dunrui, ambaye ni mtaalamu mashuhuri wa utafiti wa visukuku hivyo, aliona kuwa hospitali hiyo haikuwa mahali salama tena, hivyo alipendekeza kuvipeleka na kuhifadhiwa visukuku hivyo nchini Marekani. Siku moja ya wiki 2 au 3 kabla ya kuzuka tukio la Pearl Harbor, ofisa wa idara ya huduma ya hospitali hiyo Bo Wen aliarifu kuviweka visukuku 147 yakiwemo mafuvu 5 katika masanduku mawili ya mbao na kuyasafirisha hadi kwenye ubalozi wa Marekani mjini Beijing ili yasafirishwe pamoja na askari wa Marekani hadi Marekani. Lakini tokea hapo visukuku hivyo vilipotea na hakuna habari yoyote kuhusu visukuku hivyo.
Katika miaka ya karibuni, mtaalamu kuhusu elimu ya binadamu Bw. Zhou Guoxing alisikia kuwa siku chache kabla ya kusuka tukio la Pearl Harbor, askari mmoja aliyelinda mlango kati ya makao makuu ya jeshi la baharini la Marekani na ofisi ya ubalozi wa Marekani, aliona watu wawili walikuwa wakibeba sanduku moja na kulifukia katika ua ulioko sehemu ya nyuma ya nyumba ya ofisi ya ubalozi, na alikisia kuwa vitu vilivyokuwemo ndani ya sanduku hilo vilionekea kuwa ni visukuku vya sokwe-mtu wa Beijing. Bw. Zhou Guoxing alifika hapo, lakini hakuweza kuchimba, kwani sehemu hiyo imejengwa nyumba. Visukuku hivyo vilipotea kabla ya miaka miongo kadhaa iliyopita na hakuna habari yoyote kuhusu vitu hivyo. Hayati Zhou Enlai alipokuwa hai aliwahi kusema kuwa ni wachina kadhaa, ambao walikabidhi visukuku vya sokwe-mtu kwa wamarekani na vilipotea mikononi mwa wamarekani, wanasayansi waadilifu wangevirudisha kwa China.
SOKWE MTU WA MAHALE AKIWA KATIKA POZI
SERIKALI kwa kushirikiana na shirika la hifadhi ya taifa (TANAPA) ipo katika mchakato wa mwisho wa kukipandisha hadhi kisiwa tarajiwa cha Saa nane kilichopo katika mkoa wa Mwanza kuwa hifadhi ya taifa
Rai hiyo ilitolwewa na kaimu mkurugenzi mkuu wa kisiwa hicho Donats Kayona wakati akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea kisiwa hicho ili kujionea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo katika visiwa hivyo
Kwa mujibu wa Kayona alisema kuwa tafiti mbalimbali zimeshafanyika ili kuweza kubaini ni wanyama wa aina gani ambao wataaweza kuishi katika kisiwa hicho kwa kuzingatia mahitaji ya kiikolojia
"Wataalamu kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam wameshafika katika kisiwa hiki na kufanya utafiti wa hali ya juu wa wanyama ambao wataweza kuishi katika kisiwa hiki ili kuongeza vivutio vya utalii katika kisiwa hiki na kwamba serikali ipo kati mchakato wa mwisho kabisa wa kukipandisha hadhi kisiwa hiki kuwa hifadhi ya taifa" alisema Kayona
Kayomba alisema kwa sasa kisiwa hicho kina vivutio mbalimbali vya utalii kama vile mapango makubwa ya kuvutia yaliyozingirwa na miamba Swala, Mijusi ya aina mbalimbali,Kobe,Paka Mwitu, Nyoka Mamba aina na aina mbalimbali za ndege
Aliwataja wanyama watakaoongezwa mara baada ya kisiwa hicho kuwa hifadhi ya taifa ni pamoja na pundamilia,mbuzi mawe,Swala granti Dikidiki,Kobe na kwamba itachangia kwa kiasi kikubwa kukidhi mahitaji ya watalii wa ndani na nje
Mbali na mafanikio hayo Kayomba alisema kuwa kisiwa hicho kinakabiliwa na changamaoto kadha wa kadha ikiwemo miundo mbinu ya uendeshaji pamoja na usafiri kwani kisiwa hicho kina boto ndgo na kwamba watalii hupendela boti kubwa
"Tunakabiliwa na changamoto ya usafiri katika kisiwa hiki kwani watalii wengi hawpendi kutumia boti ndogo jambo mablo limekuwa likichangia kwa kiasi kikubwa kutopata wageni wakutosha kwa kuzingatia kuwa hii ni hifadhi pekee hapa nchini kati ya hifadhi 15 iliyopo ndani ya maispaa ya mji wa Mwanza
Kisiwa tarajiwa cha Saa nane kina ukubwa wa kilimita 0.7 za mraba na kwamba miaka 1964 kilikuwa pori la akiba na ilipofika mwaka 2008 kilikabidhiwa rasmi katika shirika la hifadhi ya wanyama pori(TANAPA)