CCM katika hali mbaya Arusha; kigogo mwingine (Bananga) atimkia CHADEMA

Ninamashaka kama hii ndiyo nakala halisi.
But hiyo BLUE paragraph imenivutia sana. Hongera kwa kuiona ile kweli na kuheshimu dhamira yako kwa vitendo

nakala hii ni halisi na kwasasa yupo New Arusha na waandishi wa habari
 
Katika msafara wa mamba kenge hawakosekani.
Ole wako ujulikane kwamba wewe ni kenge utageuzwa SIDE DISH.

Ally Bananga mfuasi mwingine wa EL sina imani na na wewe kabisa CCM we na Millya mlikuwa mnatumikia EL na mtoto wake ""Cadet" Fred Lowassa anyway karibu CDM but tutakaa na nyie kwa tahadhari kubwa
 
akabithiwe katiba na miongozo yote asome kwa makini na kuelewa, kama ana swali aulize kwa wakuu wa chama, pili kama kuna kitu aliiba au alikwapua kifisadi arudishe na atubu toba ya kweli na apewe kipindi cha uangalizi cha miezi 3 ili tujiridhishe kuwa sio mamluki, pia asipewe cheo chochote kwanza hadi kuwe na uthibitisho pasi shaka kuwa ameiva vya kutosha kukabidhiwa dhamana ya uongozi ndani ya chama!!
 
You are warmly welcome to chadema.tuko pamoja hakuna kulala mpaka kieleweke.

People's...........................................

Power...............................................
 
Ally Bananga mfuasi mwingine wa EL sina imani na na wewe kabisa CCM we na Millya mlikuwa mnatumikia EL na mtoto wake ""Cadet" Fred Lowassa anyway karibu CDM but tutakaa na nyie kwa tahadhari kubwa
Makosa aliyoyafanya EL akajiuzulu na fedha iliyoibiwa ni ndogo sana ukilinganisha na hizi walizopiga akina Pinda, Ngeleja na Maige baada ya EL kutoka. Pia tujiulize kwa nini JK hakusema ni UPEPO tu wakati wa Richmond ili Lowassa asijiuzulu lakini sasa anaona ni upepo tu? Hapo kuna siri kubwa! Karibu sana Ally Bananga upande huu wa pili, katika siasa hakuna rafiki wala adui wa kudumu, tusaidiane kumuangamiza adui wa maendeleo ya nchi hii ambaye ni CCM
 
Karibu Ally Bananga,huku hatuna uongozi wa kukupa..utakuwa mwanachama wa kawaida kama sisi.
 
Na bado wataofukuzwa kwa kukemea ouvu ndan ya bunge,kamat ya ccm inakutana na kutafakar kwa nn wabunge wao wanakisalit chama hadharan.Nao huenda wakafukuzwa au wakafungwa midomo.
 
Ni dhahiri kuwa CCM kiliacha dira yake ya kuwa chama cha wakulima na wafanyakazi takriban miaka ishirini iliyopita na sasa kimekuwa ni chama cha matajiri, wezi na viongozi wa miaka nenda rudi ambao wako kwenye harakati za kukirithisha kwa watoto wao. Kimsingi kimepoteza uwezo wake wa kuwaletea maisha bora watanzania ambao wengi wanakabiliwa kwa ukali zaidi na maadui watatu ambao wamekuwa wakiwasumbua tangu uhuru yaani UJINGA, UMASKINI na MARADHI.

Ila kusema ukweli sioni ni kwa vipi CHADEMA kimejiandaa kuziba ombwe la kuwa ni chama cha wanyonge yaani cha wakulima na wafanyakazi ili kibebe matumaini kama CCM kilivyo yabeba kwa miaka mingi kabla ya kutekwa na matajiri. CHADEMA kama ilivyo CCM ni waumini wakubwa wa soko huria ambalo limejengwa kwenye msingi wa mwenye nguvu mpishe.

Ni kweli kuwa chama chochote kitakachoingia madarakani kikiweza kupambana na kudhibiti ufisadi na mianya mingine ya rushwa kinaweza kufanya miradi ya kiserikali kama kujenga barabara, shule na hospitali kuliko inavyofanya CCM hivi sasa. Lakini je hilo ndilo jibu la matatizo ya msingi ya mtanzania (UJINGA, MARADHI na UMASKINI) wa sasa na je jibu hilo yatatupeleka kwenye maisha bora kwa kila mtanzania?

Nayaongea haya nikiwa siyo mwanachama wa chama chochote cha siasa japo ni mfuatiliaji mzuri tu wa harakati za kisiasa.


Just thinking aloud guys.
 
Back
Top Bottom