CCM katika hali mbaya Arusha; kigogo mwingine (Bananga) atimkia CHADEMA

karibu kamanda.

kazi ya ukombozi imeshavuka mstari wa mwisho sasa inaelekea kwenye ushindi kamili.
 
Kakuja huku kwa makamanda eeehhhh werawera.... 2015 tuwe na choice kubwa ya kuchagua mawaziri..... Lol
 
Ally Bananga mfuasi mwingine wa EL sina imani na na wewe kabisa CCM we na Millya mlikuwa mnatumikia EL na mtoto wake ""Cadet" Fred Lowassa anyway karibu CDM but tutakaa na nyie kwa tahadhari kubwa

Binadamu hubadilika na kuwa mwema, Shetani ndiye tu hana nafasi ya toba, safi sana Banaga..
 
Karibu katika mapambano, huku ni uwanja wa vita si kula raha kama ulikotoka, mapambano yetu yataisha siku Tanganyika ikikombolewa.
 
mh!

nina mashaka sana na hawa wanaojiita vigogo wa ccm kuhamia chadema kwa kasi hii sasa hivi.

inaweza kuwa ni mkakati wa ccm kwa vigogo hawa hawa kuhamia back to ccm at the appropriate time na ku-engineer downfall ya chadema towards october 2015!

chadema... kuweni wakarimu kwa wageni lakini msiwaruhusu kuingia vyumbani mwenu. wapeni chai na juisi hapo hapo sebuleni hadi labda baada ya october 2015.
 
Pole kwa kutabasamu gizani kwa muda mrefu akuna alikuona,njoo utabasamu ukiwa kwenye mwanga utaonekana,karibu utumikie watanzania
 
wajameni hivi hawa si kwamba ni Opportunistics?sitaki kuamini kama wamesoma alama za nyakati kwa uhalisia hasa!kuna uwezekano mkubwa wameona mwisho wa CCM ni 2015 kwa hiyo wanatafuta pa kuegemea.inabidi watizamwe kwa darubni kali hawa!la sivyo CDM itajikuta ni nyumani kw magamba!
 
Ally Bananga mfuasi mwingine wa EL sina imani na na wewe kabisa CCM we na Millya mlikuwa mnatumikia EL na mtoto wake ""Cadet" Fred Lowassa anyway karibu CDM but tutakaa na nyie kwa tahadhari kubwa

ni galasa,sijuhi chadema wataishi vipi kwani ccm walikuwa wanapewa fedha wanaanzisha timbili vinginevyo el aendelee kuwafadhili mpaka hapo yeye atakapotia timu tayari kuwa mgombea wa cdm wa urais 2015
 
Ally Bananga mfuasi mwingine wa EL sina imani na na wewe kabisa CCM we na Millya mlikuwa mnatumikia EL na mtoto wake ""Cadet" Fred Lowassa anyway karibu CDM but tutakaa na nyie kwa tahadhari kubwa

Usiogope mkuu wakifika huku tunawabatiza kwa maji mengi ya M4C then wanakuwa wapambanaji halisi. Karibu Bananga tuendeleze harakati za kuikomboa nchi yetu
 
Karibu sana Bananga nimependa paragraph yako ya mwisho kwa jinsi ulivyowaaga CCM.
Tunamsubiri Abdallah Mpokwa aliyekuwa katibu wa UVCCM Mkoa wa Arusha nasikia amehamishiwa makao makuu Dar.

Vipi mary chatanda naye si aje huku tukamilishe kazi?
 
Natuma shukrani zangu za dhati kabisa kwa rais wetu uliye pale IKULU ya MAGOGONI.Ni kwamba wewe kweli kichwa sababu kwa dhamira yako ya kuitoa CCM kwenye ulingo wa siasa ya Tanzania umeiokoa hii nchi bila wewe kujua.Namwomba mwenyezi MUNGU akujalie maisha marefu ili uje ushuhudie ile kaulimbiu yako ya MAISHA BORA KWA KILA MTZ Ikitekelezwa kwa kasi mpya,Nguvu mpya na Ari mpya.Naomba CDM wakuelewe kuwa wewe ni mtu wao na umewaandalia njia nzuri ya kufika hapo walipo na mpango wako wa kuwakabidhi nchi 2015 bado uko palepale.Bila wewe CDM isingefika hapo ilipo.MPAKA HAPO WEWE NI KAMANDA ULIYEFANYA KAZI YAKO VYEMA.Big up JK!!.
 
Back
Top Bottom