CCM katika hali mbaya Arusha; kigogo mwingine (Bananga) atimkia CHADEMA

vipi
na yule jambazi alienda kujisalimisha bungeni,anaitwa jumanne mjusi vipi hajabadili muelekeo?? Kwani nilikua namuona mpo wote bega kwa bega kwenye vikao mara nyingi.anyway karibu sana kamanda,lema anakuja atakuvika gwanda usijali.karibu sana
 
Swali dogo:
Nani haswa waliohusika na kusuka project ya M4C ndani ya chadema?

Maana speed yake kwa jamii ni kubwa kama intelligencia ya KGB. Sina imani kama tutafika 2015 na chama kinaitwa ccm madarakani inawezekana tukafanya uchaguzi mpaka tukachoka kabisa kufanya chaguzi ndogo na kuamua kukabidhi nchi mapema kwa chadema.

Hala hala wahamiaji mtusaidie kulinda imani na amani ndani ya chadema yetu mkija kwa shari mtaumbuka huku hakuna nafasi ya ufisadi kabisa
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. TAARIFA KWA VYAHABARI
“Mficha maradhi kifo humfichuwa “

Ni muda mrefu nimeitafakari dhamira yangu na sasa ni wakati muafaka kufikiamaamuzi magumu, Nimeamua kuachia nyadhifa zangu zote ndani ya CCM ambazo ni,MJUMBE WA MKUTANO MKUU CCM TAIFA, MJUMBE WA BARAZA LA MKOA UVCCM, NA M/KITI WAKAMATI YA MAHUSIANO YA UVCCM MKOA ARUSHA AJIVUA GAMBA NA KUTIMKIA CHADEMA.

Yaliyonisukuma ni mwelekeo mbaya wa CCM kwa sasa ambao umejiondoa kuwa Chamacha wanyonge na wakulima na sasa ni chama cha kundi la watu wachache na watotowao ndio sababu yanayoendelea sasa ndani ya CCM yanasikitisha sana.

Usaliti na makundi ndani ya CCM yanatishia kabisa uhai wa chama na tayariyamekwisha angamiza Taifa letu, hata hivyo nafasi ya wa watoto wa wanyongendani ya CCM inazidi kuwa finyu, aidha ujipendekeze kwa wakubwa ili upatenafasi ya kutumikia jamii au Chama, wakati nafsi yangu haiko tiyari kusimamiauovu huu sasa nimeamua kusimamia ninachokiamini bila uoga wala unafiki, namfano Tazameni yanoyoendelea ndani ya UVCCM ARUSHA mikono ya mtoto wa mkubwaunaumaliza umoja huo mkoani hapa. Kamanda Alli kwa niaba ya binadamu wote napenda nikupongeze kwa maamuzi magumu uliyoyafanya na kwamba umesamehewa kwa mapungufu uliyo yatenda aidha ukiwa Ali ama kazini,cha msingi tenda kwa upeo wa akili na moyo wa nafsi yako.NI MATARAJIO YANGU UTAKUWA KAMANDA ULIYETAYARI KULENGA ADUI NA KUMTUNGUA ADUI UNAYEMFAHAMU AMEKAAJE NA ANASIRAHA GANI.NYANI HUYO UMUUE PASIPO KUMWANGALIA USONI.
 
JK endelea kukiboa chama chako naamini na wewe uko karibu kuachia kazi maana upepo huu unaelekea kuwa tsunami
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. TAARIFA KWA VYA HABARI


“Mficha maradhi kifo humfichuwa “

Ni muda mrefu nimeitafakari dhamira yangu na sasa ni wakati muafaka kufikia maamuzi magumu, Nimeamua kuachia nyadhifa zangu zote ndani ya CCM ambazo ni, MJUMBE WA MKUTANO MKUU CCM TAIFA, MJUMBE WA BARAZA LA MKOA UVCCM, NA M/KITI WA KAMATI YA MAHUSIANO YA UVCCM MKOA ARUSHA.

Yaliyonisukuma ni mwelekeo mbaya wa CCM kwa sasa ambao umejiondoa kuwa Chama cha wanyonge na wakulima na sasa ni chama cha kundi la watu wachache na watoto wao ndio sababu yanayoendelea sasa ndani ya CCM yanasikitisha sana.

Usaliti na makundi ndani ya CCM yanatishia kabisa uhai wa chama na tayari yamekwisha angamiza Taifa letu, hata hivyo nafasi ya wa watoto wa wanyonge ndani ya CCM inazidi kuwa finyu, aidha ujipendekeze kwa wakubwa ili upate nafasi ya kutumikia jamii au Chama, wakati nafsi yangu haiko tiyari kusimamia uovu huu sasa nimeamua kusimamia ninachokiamini bila uoga wala unafiki, na mfano Tazameni yanoyoendelea ndani ya UVCCM ARUSHA mikono ya mtoto wa mkubwa unaumaliza umoja huo mkoani hapa.

Lakini pia uzito wa serikali ya CCM kushidwa kuwawajibisha wabadhirifu na wanaotumia vibaya madaraka waliyopewa angalia ubadhirifu mkubwa hivi karibuni uliofanywa na Mawaziri na Watumishi wengine wa Umma, Angalia jinsi Serikali imelichukulia suala la Jairo kwa mzaha, ni hatari kwa Nchi yetu kwamba wakati watoto hawana madawati wako viongozi wakubwa ambao wanashindwa kuchukuliwa hatua kwa wizi wa mabilioni ya fedha.

Sababu ni nyingi sana za kwanini nimeamua kutoka CCM, nikisema niandike zote pengine itanipasa kuandika kitabu hata hivyo ninaamini kuwa nitakuwa na fursa ya kueleza mambo mengi sana kwenye mikutano ya hadhara nitakayofanya na Chama cha kipya CHADEMA.

CHADEMA ,nawashukuru kwa kunipokea na wahaidi utumishi na kazi iliyotukuka, nitajifunza kwenu na pia naamini mtajifunza kwangu ili tuweze kwa pamoja kuleta matumaini kwa wanyonge.

Kwa marafiki zangu na wanachama wa CCM, msihuzunike sana kwani ninatangulia kwenda kuwaandalia makao kwani ninajua nanyi pia mko njiani mnakuja ,hata hivyo sikuwahi kuwa mwema kama malaika tulipokuwa pamoja CCM naamini kuna mahali niliwakosea kama binadamu naomba msamaha kwenu na undugu wetu ubaki , lakini kama maamuzi yangu ya kwenda Chadema yatakuwa yamewauzunisha poleni sana na muendelee kuchukia kwani hatuwezi kuukwaza utu na faraja ya Mwanadamu kwa kufurahisha nafsi za watu wachache.

Asanteni sana karibuni Chadema.


Ally Bananga.
……………………
27/4/2012.


kwafu nao walianza hivi hivi! be careful CDM itakuwa chipolopolo bure!!
 
Karibu katika harakati za Ukombozi.
Asante Baba Ritz kwa kutusaidia kuiua CCM.

Ee Mungu Baba,asante kwa kuwarejesha kundini wanao wapotevu.TUNAKUOMBA UMREJESHE KUNDINI PIA NA FREDRICK MWAKALEBELA(iringa) ILI 2015 AKALICHUKUE JIMBO LINALOONGOZWA NA Lukuvi.
 
kwafu nao walianza hivi hivi! be careful CDM itakuwa chipolopolo bure!!

Tulia unyolewe!!
CDM ikifanya hivi mnaanza kufananisha mara NCCR ilikuwa hivi, mara CUF...

Nyie tulieni tu na bado katika box la kura huko pia hamtaambulia kitu!!
 
Ally Bananga mfuasi mwingine wa EL sina imani na na wewe kabisa CCM we na Millya mlikuwa mnatumikia EL na mtoto wake ""Cadet" Fred Lowassa anyway karibu CDM but tutakaa na nyie kwa tahadhari kubwa
unajua katika siasa hakuna rafiki wala adui wa kudumu!
Cha msingi ni chama kuwa na vision na beliefs katika kile wanachosimamia. Mfano Ujerumani na nimeona pia Ufaransa kuna CDP - Christian Democratic Party na Green Party. Kwa hiyo lengo lao ni kuendeleza nchi kupitia wanachoamini na sio kuwa JK naye katika mkumbo huu akihamia cdm basi ndio aje na zile politics za ccm huko.
 
nimeupenda sana ujumbe wake huyu bwana. Kwa hakika kama trend itakuwa hivi tunaweza kujikuta hadi kufikia 2014 tunatakiwa kurudia uchaguzi wa madiwani na wabunge wengi sana kwa kuwa wengi wao watakuwa wameshahamia chadema. Kwa hili tutapaswa kumshukuru na kumpongeza kikwete kwa kusaidia kuindoa ccm madarakani.
ndio maana uliambiwa ni chaguo la mungu ili aje akomboe tanzania .....kilaini ni nabii sasa si unaona chagua la mungu limeanza kuleta ukombozi
 
Kama hii barua ni ya kweli basi kunakucha, niliyaona zamani sana na nilikuwa na ndoto kama hizi. naona yanatimia. Things fall apart, the center is no longer holding. CCM CCH Aeee, Sayonaraa.
 
karibu sana kaka ila ukae ukijua huku atuvumilii maovu bali ukithibitika ni papo kwa papo hatua za kinidhamu.
jk endelea na msemo wako kuwa upepo tu utapita huu si upepo bali ni kimbuga lazima kikuangushe!
 
Hawa wahanga wa kimbunga cha M4C inabidi tuwaweke kwe hema moja na kuwachunguza kwa jicho la 3 kwani madhara ya kimbunga huwa n makubwa sasa tuipowachunguza kwa ukaibu tunaweza juta baadae, maana ni wengi sana tangu Kamanda Lema na group yake waanze kazi tumevuna wengi sana ambao wamejua kuwa CDM ndio kimbilio lao.

kila msafara wa mamba kenge nao wapo, CDM tuwe makini na hawa wenzetu waliokumbuka shuka saa hizi.
 
Tweeted by Dr. W. Slaa:

Ally Bananga (Mjumbe wa Mkutano Mkuu CCM Taifa, Mjumbe na Mwenyekiti wa Mahusiano UVCCM Arusha), karibu sana CHADEMA na hongera kwa kuamua.
 
Back
Top Bottom