CCM ivunjike tu

Nafunga na kuomba jina la Lowassa likatwe tuone mikwara yake itaishia wapi. Mtu mmoja fisadi na mwizi hawezi kutishia watu wazima kana kwamba chama ni chake.

Hatuwezi kuongozwa na rais fisadi.


umetawaliwa na wivu na kushindwa kwako maisha kunakutia hasira sna..Lowassa mwizi kaiba nini?miaka yote mmeshindwa hata kumuita kwenye kamati ya maadili kwa huo wizi mnakuja kupanua panua midomo hapa! sasa ni hivi CCM PASUKA
 
Shida sio CCM kufa kabisa
CCM now ni kama 'dead man walking'
shida ipo kwenye replacement tukishaizika CCM
je wananchi wanaiona na kuiamin replacement?
we umeiiona?
Umenena kweli. CCM ikiondoka mbadala ni nini? Vyama vilivyopo hata mgombea wa urais hawana. Sasa nchi itakabidhiwa kwa nani? Naona CCM itaendelea kutawala hata akikatwa mtu.
 

Nakubaliana na Mag3 100%. Haaiwezekani kila mtu anamnyooshea mtu mmoja tu kwamba ndo tatizo CCM, na bado washindwe kumuwajibisha. Ukweli ni kwmba viongozi wote wanayo matatizo, ila mwenzao kawazidi kete tu, tena si wingi wa fedha bali anajua mengi ya wezi wenzake ! Na kwa kuwa wamemnyanyapaa sana kwa zaidi ya miaka saba ndani ya CCM, basi wanao ondoka madarakani ndio waoga, wanajua na yeye akichukua nchi hawatalala usingizi na mihela waliyojichotea kama wehu wakati wa utawala wao italiwa kwa shida saana!. Ndiyo maana Mkuu aliyepo sasa anasafiri kila kukicha ili kutawanya fedha zake angalau apunguze risk ya kupoteza pesa yote kwa kuficha kwenye nchi moja. By any means haya majizi yatapatana tu, na sioni wa kukimbia chama kwa sasa, maana hata huyo katibu Mkuu wanayesema anakijenga chama na kuwanyooshea wenzake vidole kwa ufisadi, ni jangiri namba moja TZ!!
 
Gwalihenzi,
Agree with u 100%
 
Last edited by a moderator:
Mara nyingi mawazo yangu na michango yangu kwenye swala hili, naona kuwa akipitishwa EL kama flag bearer itakuwa shida kubwa kwa ccm na asipopitishwa pia itakuwa shida tu. Ndiyo maana siku zote namuunga mkono El kwenye juhudi zake za kwenda magogoni maana najui ndiye pekee aliyebakia wa kulibomoa hili vampire ccm, na yeye hatafika anakotaka aende. Ndani ya ccm wapo wengi hawampendi El na wamesema waziwazi kumtukana na wapo wengi wanaompenda na wamesema waziwazi. haya makundi mawili umefika wakati wake wakutengana, ambao ndiyo mwisho wa utawala wa mkoloni mweusi
 
Wakati wa Nyerere labda ni historia kwako wewe, mimi nilikuwepo na nnadiriki kusema kuwa hakuna Rais wa Tanzania aliyechukiwa na kutaka kupinduliwa mara nyingi zaidi ya Nyerere.

Mama unaweza kuwa na mawazo huru ktk siasa kuliko kuwa na vihisia na vichuki vya udini. Inawezekana wakati mwingine ukawa na hoja nzuri ila kutokana na mihemko yako na chuki zako kwa viongozi wakristo na hasa kwa sababu ya ukristo wao, basi wengi hupuuza michango yako. I mean hatusomi kabisa.
 
Jamaa hawezi gombea nje ya ccm. Nguvu yake iko kwa baadhi ya viongozi wa ccm. Na nina waswas kama hata hao wanaweza kumpa kura siku ya uchaguz mkuu akigombea urais.
 
Nje ya CCM hana chake. Hauziki. Na hta akigombea kupitia ccm, ccm itahitaj bunduk na mabomu ili jamaa ashinde. Sasa hii itakuwa tunaipelekA wap nchi? Hii nchi ni ya muhimu kuliko mtu mmoja
 
Nafunga na kuomba jina la Lowassa likatwe tuone mikwara yake itaishia wapi. Mtu mmoja fisadi na mwizi hawezi kutishia watu wazima kana kwamba chama ni chake.

Hatuwezi kuongozwa na rais fisadi.
Sijui MMK anamaanisha kile hii picha inaongea!
Kweli maisha yanabadilika, ukiona chama ambacho misingi yake ilijengwa kwenye Uadilifu, ukweli na uchapakazi kinageuka na kuwa chama cha 'macelebrity' na matajiri wanaotumia matrilioni mengi kubakia madarakani badala ya kuyatumia kujenga nchi ni lazima ujiulize.

 
Jamaa hawezi gombea nje ya ccm. Nguvu yake iko kwa baadhi ya viongozi wa ccm. Na nina waswas kama hata hao wanaweza kumpa kura siku ya uchaguz mkuu akigombea urais.
Hili liko wazi kabisamikeimani lakini ni kwa ajili ya wale ccm waliopendekeza sehemu ya 'tunu za taifa' kuwemo katika Katiba Mpya. Tatizo ni kuwa 'king makers' wana mikataba yao ambayo wana 'ccm-imani' wengi hawaijui vizuri na utekelezwaji wake ulishafanyika nusu kwa hiyo hii sehemu iliyobakia isipotekelezwa hata siri za awali zinaweza kuvuja na kusababisha matatizo zaidi kwa 'ccm-maslahi'!

 
Kınachoendelea ndani ya CCM ni uthibıtisho kuwa CCM hakina wasomi ambao wanajiamini.Ni wasomi uchwara,wamejaa hofu na kutojiamini.Kitendo cha watia nia wengi kulalama kuwa rushwa imetamalaki na chama chao kimevamiwa ni upoyoyo.Ilikuwa wawe wamechukua hatua muda mrefu kwa kuwafukuza ama wao kuondoka na kuunda chama kingne ambacho pengne kingeitwa CCM Tanzania.Yamo humo humo, huu ni umburula.Alafu watu haohao wanawalaumu vijana eti ni legelege,mara hawakwenda JKT,mara hawana uthubutu n.k wakati wao ndo mfu kabisa.Mm nasema elimu ya sasa ina ubora kuliko ya wakatı ule!
 
Nafunga na kuomba jina la Lowassa likatwe tuone mikwara yake itaishia wapi. Mtu mmoja fisadi na mwizi hawezi kutishia watu wazima kana kwamba chama ni chake.

Hatuwezi kuongozwa na rais fisadi.

Simtetei lowasa nataka tujiongeze tu kifikra, je akikatwa lowasa chamani ufisadi utakuwa umefikia ukomo!?
 
Simtetei lowasa nataka tujiongeze tu kifikra, je akikatwa lowasa chamani ufisadi utakuwa umefikia ukomo!?

What kind of argument is this you moron? So Mungu alivyoiadhibu sodoma na gomola dhambi na uasherati vilikoma? Lakini kwanini hakuwaacha kama alijua havitakoma?

Kweli Division 5 ni wengi...
 
Mungu ifanye October leo ili tuone mambo makubwa
 
Umenena kweli. CCM ikiondoka mbadala ni nini? Vyama vilivyopo hata mgombea wa urais hawana. Sasa nchi itakabidhiwa kwa nani? Naona CCM itaendelea kutawala hata akikatwa mtu.

That's a misconception. Yaani unaamini kabisa hatuna mbadala wa CCM na ufisadi? Na hivyo tuendelee na hali iliyopo kwa kuwa hatuna cha kufanya? Hatun namna ya kuiadhibu CCM? Kwamba CCM pamoja na madudu yote bado ni bora kuliko mbadala na hivyo wanastahili kuendelea kutawala kwa kuwa "hakuna mbadala"? MaCCM yametumia hoja ya kwamba mbadala ni dhaifu mara nyingi ili kuendelea kung'ang'ania madarakani. Ukiwauliza ni lini mbadala wa CCM ulipimwa na kuonekana ni dhaifu hawana majibu. Ni dhahiri kuwa kuibadili CCM, bila kujali ubora wa mbadala, kutainufaisha jamii kwa kiasi kikubwa.
 
Lowasa ana Achu na madaraka na kweli hatakubali kutengwa na CCM na Wengi ya watia nia hawapo tayari nchi kukaliwa na Lowasa...Muzic bado upo Sylence, ukichanga utajua ucheze vipi
 

Uimara wa kitaasisi, uchama dola,mafisadi> waadilifu na wanafiki> wakweli bila kusahau wasaliti > wazalendo kwa sifa hizi wataendelea kulindana na kujiimarisha kwa maslahi yao na si kukubali kumeguka na ikitokea hivyo Uhuru wa kweli utatimia je wazungu watakubali kutuona tukijiimarisha au wanapenda kutuona tukiendeleea kudhoofishwa na hao vibaraka wao!! Natafakari bado!!
 
What kind of argument is this you moron? So Mungu alivyoiadhibu sodoma na gomola dhambi na uasherati vilikoma? Lakini kwanini hakuwaacha kama alijua havitakoma?

Kweli Division 5 ni wengi...

Jibu swali acha kuidhalilisha hiyo division 1 yako, sababu kubwa inayosemwa juu yake ni ufisadi lakini yeye ndiye fisadi pekee!!? Chama na mfumo mzima chamani ni wa kifisadi ndio msingi wa hoja yangu! ukihitaji cv yangu njoo inbox!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…