CCM isijifiche kwa Putin, bei zilishapanda kitambo sana

voicer

JF-Expert Member
Jul 13, 2020
5,550
11,879
Habari Member's JamiiForums!

Habari Moderators JamiiForums!

Leo tarehe,
08/03/2022.

Watanzania kupitia vyombo vya habari mbalimbali nchini Tumemsikia Mh Samia Suluhu Hassan,
Mwenyekiti wa CCM Taifa, na Rais wa JMT Wakati akihutubia kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani,Sherehe zilizofanyika kitaifa huko Visiwani Zanzibar.

Akituambia Wananchi wa Tanzania Kwamba.....anasikia maneno.. maneno huko mitaani kuhusu Wananchi kulalamikia bei za bidhaa muhimu kupanda na kupelekea ugumu wa maisha mtaani.

Ameendelea kutahadharisha kwamba Tanzania haitakwepa kupanda kwa bei hizo kwa,
Sababu zinasababishwa na janga la vita inayoendelea huko mashariki ya mbali Kati ya Urusi inayoishambulia Ukraine na hivyo kupelekea Urusi kuwekewa vikwazo vikubwa vya kiuchumi na mataifa ya Magharibi pamoja na mshirika wao Marekani.

Jambo ambalo limepelekea kupanda kwa bei ya mafuta Duniani,kutokana na upungufu utakaojitokeza wa bidhaa hiyo muhimu kwa matumizi ya viwanda na usafirishaji. Pia ikumbukwe kwamba Urusi na Ukraine kwa pamoja zinachangia uzalishaji wa chakula Duniani kwa 30%.

My Take

Jambo nililoshangaa na pia kuwashangaza watanzania wengi hapo,ni jinsi ambavyo Mh Rais ameongelea tatizo la malalamiko ya wananchi kuhusu upandaji bei wa bidhaa muhimu za Vyakula na Ujenzi nchini. Kwamba ni kama vile amelisikia leo jambo hili,baada ya kuanza kwa vita hii kati ya Urusi na Ukraine.

Wakati kiuhalisia hii ndiyo imekuwa kero na kilio kikubwa nchini, kwa wananchi wa Tanzania hususan sisi wa kipato cha chini nchini Tena kwa Kwa muda mrefu sana sasa! Wala bei hazijaanza kupanda juzi wala jana baada ya hii vita ya huko Mashariki ya Mbali.

Pamoja na kuipongeza serikali kwa kufanya vizuri kwenye sekta ya Ujenzi wa madarasa na miundombinu inayoedelea kwa sasa nchini,kutokana na mikopo kadhaa toka kwa wahisani.

Umefika wakati sasa wa Serikali ya CCM ilichukulie jambo hili la mfumko wa bei,kwa uzito wa pekee. Kwa kuangalia namna nzuri ya kumsaidia mwananchi ili kumpunguzia makali ya upandaji holela wa bei za bidhaa muhimu madukani.

Sielewi kama Mh Rais hapewi taarifa za hali halisi ya maisha yanayoendelea huku site kwa wapiga kura wake? Yanayotokana na mfumko wa bei holela nchini. Nachelea kusema holela kwa sababu...mfano huu. Tanzania ni moja ya nchi zenye idadi kubwa ya Ng'ombe barani Afrika.
Lakini sasa bei ya nyama kwenye mabucha yetu haishikiki, utadhani tunaagiza ng'ombe kutoka nje ya Tanzania.

Je kwa hili!
Tuamini kwamba hili jambo na Serikali kuonekana kutochukua hatua yoyote. Inawezekana kusababishwa na yeye Mh Rais kuwa Busy kutupambania kupata mikopo huko nje ya nchi.

Na hivyo kutopata fursa ya kuzunguka nchini na kukutana wananchi kisha kuwasikiliza na kuongea live kero zao? Au tuamini kwamba CCM na Wateule wake hawayaishi maisha halisi ya mtanzania aliyeko huko Site mtaani?

Au tuamini kwamba wasaidizi wake wanayaona ila hawayafikishi kwake kwa uhalisia wake? Nasema hivyo kwa sababu kero hii imekuwa kilio kikubwa na imeanza kupigiwa kelele,kila pembe ya nchi kwa muda mrefu sana sasa.

Wala haijaanza juzi wiki iliyopita baada ya vita ya Putin na Zelensky. Iwe kwenye media au kupitia vikao kadhaa vya wadau wa serikali. Watanzania wamesikika wakitoa kilio chao kwa serikali...huku Serikali ikionekana kutochukua hatua stahiki.

Lakini pia bila kupewa jibu wala kauli yoyote kutoka kwa wateule husika wa tatizo hili kubwa.

Hivyo basi! Labda tu tungemuomba Mh,Rais atusikilize na kuangalia ni jinsi gani Serikali yake itasimama bega kwa bega na wananchi kupambana na tatizo hili. Kama alivyosimamia tatizo la Covid19 nchini na kulipa kipaumbele cha ziada.

Basi hili nalo ni janga kubwa pengine madhara yake ni machungu zaidi kwa wananchi kuliko anavyoelezwa na wasaidizi wake na linahitaji kupatiwa ufumbuzi haraka iwezekanavyo.badala ya hivyo inavyoelekea kumgeuza Putin wa Urusi kuwa kichaka cha kujifichia. Serikali ya CCM isiitumie vita ya Urusi kama kisingizio cha upandaji bei nchini.

Pia ielewe kwamba! Kutokana na kukua kwa teknolojia ya mawasiliano Duniani.
Watanzania pia wanapata fursa ya kufuatilia na kupata habari na matukio mbalimbali na muhimu Duniani kwa urahisi na kwa wigo mpana zaidi na hivyo kuwapa uelewa mkubwa wa nini kinaendelea Duniani kwa wakati husika.

Na kama ni hivyo....kwamba CCM wanataka kutumia kichaka cha vita ya Urusi na Ukraine,ili kukwepa jukumu la kudhibiti mfumko wa bei nchini.

Labda basi watuaminishe kama wao waliiota hii vita mapema na kuwaachia wafanyabiashara ruksa ya kupandisha bei kabla ya vita kutangazwa na kuanza rasmi.

Na kama Mh Rais anapotoshwa na baadhi ya wasaidizi wake ndani ya chama na serikali.

Aamke mapema na kuchukua hatua,kabla madhara hayajawa makubwa tunapoelekea hiyo 2025.

Kwa kuwaondoa mapema kwenye nafasi zao maana wameshindwa kutimiza wajibu wao na huenda hawamtakii mema kisiasa.

Naomba kuwakilisha kama commonmwananchi
10101View attachment 2143905
 
Wadau naonba tukumbushane!

Hivi mbolea, mabati, sementi, nondo, petrol n.k vimelalamikiwa kupanda mara dufu baada ya kutokea vita ya Putin?

Inamaana baada ya kauli ya Rais wafanya biashara ndiyo wanapandisha bei tena!

Mi nakumbuka wakati Tz tunalalamika kupanda kwa petrol na dizel Nchi jirani bei ilikuwa chini sana, mfano Zambia, na ndiyo maana baadhi ya watanzania walikuwa wanavuka ili kununua kwa bie nafuu, mfano Tunduma!!!
 
Wadau naonba tukumbushane!

Hivi mbolea, mabati, sementi, nondo, petrol n.k vimelalamikiwa kupanda mara dufu baada ya kutokea vita ya Putin?

Inamaana baada ya kauli ya Rais wafanya biashara ndiyo wanapandisha bei tena!

Mi nakumbuka wakati Tz tunalalamika kupanda kwa petrol na dizel Nchi jirani bei ilikuwa chini sana, mfano Zambia, na ndiyo maana baadhi ya watanzania walikuwa wanavuka ili kununua kwa bie nafuu, mfano Tunduma!!!
Na huo ndio ukweli halisi,kinachoonekana hapa ni kitendo cha kutanguliza kujihami sababu muda si mrefu bei zinaweza kutodhibitika pale impact ya vita hiyo itakapotuingia rasmi.
 
Hakuna chochote cha maana kisichoifurahisha serikali kinajadiliwa kwa kina na hizo media. Sehemu pekee serikali inapokutana na mijadala halisi kuihusu ni huku mitandaoni. Kwenye hizo media Magufuli alishapandikiza hofu, na sasa ni muendelezo tu wa hofu.
Uko sahihi Tindo!

Angalia media za leo zilivyotoka hapo
IMG-20220309-WA0004.jpg
IMG-20220309-WA0008.jpg
IMG-20220309-WA0007.jpg
 
Wadau naonba tukumbushane!

Hivi mbolea, mabati, sementi, nondo, petrol n.k vimelalamikiwa kupanda mara dufu baada ya kutokea vita ya Putin?

Inamaana baada ya kauli ya Rais wafanya biashara ndiyo wanapandisha bei tena!

Mi nakumbuka wakati Tz tunalalamika kupanda kwa petrol na dizel Nchi jirani bei ilikuwa chini sana, mfano Zambia, na ndiyo maana baadhi ya watanzania walikuwa wanavuka ili kununua kwa bie nafuu, mfano Tunduma!!!

Nimecheka sana daa baada ya kumsikia Rais nikajiuliza hivi Rais anaishi nchi gani? Mbona bidhaa karibu zote zimepanda bei kuanzia March 2021

Yani Rais hajui kama mabati ,nondo,mafuta na bidhaa zimepanda bei kabla hata hiyo vita ya Urusi!
 
Back
Top Bottom