CCM inayoongozwa na mwanamke bado ina mfumo dume

Kosinde

Member
Jun 7, 2018
49
60
Wakati napitia pitia orodha ya walioteuliwa kuwania nafasi mbalimbali za Chama Cha Mapinduzi, (CCM), ghafla nikakutana na nafasi mbili ambazo wagiombea wake ngazi ya wenyeviti ni wanaume watupu na nagazi ya Makamu Mwenyekiti ni wanawake watupu. Katika kutafakari endapo jambo hilo limetokea kwa bahati mbaya au ni makusudi nikabaini ni athari ya mfumo dume uliokuwepo tangu awali.

Kinachoshangaza hali hii inatokea wakati ambapo kiongozi mkuu wa chama hicho ni mwanamke tena ambaye amekuwa akijipambanua kuzingatia usawa katika kutoa nafasi mbalimbali, nikajiuliza jambo hili pengine limempitia kwapani na hakuna aliyepata ujasiri wa kumkumbusha.

Katika nafasi ya wagombea mwenyekiti wa UV-CCM wagombea wote ni wanaume na makamu wa nafasi hiyo wote ni wanawake kana kwamba katiba ya chama inaelekeza Mwanaume lazima awe mwenyekiti na makamu lazima awe mwanamke, ni mfumo dume usio kuwa na kifani.

Haijaishia hapo, hata katika nasafi ya mwenyekiti wazazi Taifa wagombea wote ni wanaume na wagombea wa makamu mwenyekiti, wote ni wanawake. Hii haileti taswira nzuri kwa chama ambacho kinaongozwa na mwanamke, tena ambaye amemudu vizuri majuku yake na kuwa mfano mzuri kwa wanawake wengine.

Nafikiri hapa kulikuwa na haja ya nafasi zote kuwa na wagombea mchanganyiko na wote wagombe Uenyekiti na endapo jinsia moja ikishinda mwenyekiti basi makamu awe ni jinsia nyingine aliye na kura nyingi kuliko wenzake wa jinsia hiyo.

Hii ingeleta usawa wa kijinsia katika kuwania nafasi za uongozi ndani ya chama kuliko ilivyo sasa.

ANGALIA ORODHA YA WAGOMBEA

Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa (NEC) imekutana kikao cha kawaida Jumapili 13 Novemba, 2022 chini ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan, Makao Makuu ya Chama, Dodoma.

Pamoja na mambo mengine, Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa imefanya uteuzi wa majina ya wanachama watakaogombea nafasi za uongozi ndani ya CCM na Jumuiya zake katika ngazi ya Mkoa na Taifa kwa mujibu wa katiba ya CCM ya mwaka 1977 Toleo la mwaka 2022 Ibara ya 82(1). Kwa upande wa wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya za CCM ngazi ya Taifa walioteuliwa ni kama ifuatavyo:-

NAFASI: MWENYEKITI UVCCM TAIFA
1. Farid Mohamed HAJI
2. Kassim Haji KASSU
3. Mohamed Ali MOHAMED (KAWAIDA)
4. Abdallah Ibrahim NATEPE

NAFASI: MAKAMU MWENYEKITI UVCCM TAIFA
1. Khadija Khalid ISMAIL
2. Dorice John MGETTA
3. Victoria Charles MWANZIVA
4. Rehema Sombi OMARY

NAFASI: MWENYEKITI UWT TAIFA
1. Gaudencia Mugosi KABAKA
2. Kate Sylvia KAMBA
3. Dkt. Wemael Allen CHAMSHAMA
4. Mariam Mohamed LULIDA
5. Mary Pius CHATANDA

NAFASI: MAKAMU MWENYEKITI UWT TAIFA
1. Latifa Nasser AHMED
2. Thuwaybah Edington KISSASI
3. Hafsa Said KHAMIS
4. Zainab Khamis SHOMARI

NAFASI: MWENYEKITI WAZAZI TAIFA
1. Dkt. CPA. Edmund Bernard MNDOLWA
2. Fadhili Rajabu MAGANYA
3. Bakari Nampenya KALEMBO
4. Said Mohamed MOHAMED (DIMWA)

5. Mwanamanga Juma MWADUGA
6. Ally Maulid OTHMAN
7. Ali Khamis MASUDI
8. Hassan Haji ZAHARA

NAFASI: MAKAMU MWENYEKITI WAZAZI TAIFA
1. Haidar Haji ABDALLA
2. Dkt. Wemael Allen CHAMSHANA
3. Fatma Abeid HAJI
4. Rachel Ntiganyigwa KABUNDA
5. Neema George MTURO
6. Zahoro Salehe MOHAMED
7. Dogo Idd MABROUK

Uchaguzi wa viongozi wa Jumuiya hizo kwa ngazi ya Taifa utafanyika tarehe 24-29 Novemba, 2022. Wagombea wote wanakumbushwa kuheshimu Kanuni za uchaguzi za CCM na misingi ya chama kwa kufanya siasa safi na kuzingatia maadili ya Chama wakati wote.

Aidha Orodha ya majina ya wagombea uongozi Chama na Jumuiya zake ngazi ya Mkoa yatatumwa katika mikoa husika.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Shaka Hamdu Shaka
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa
Itikadi na Uenezi.
13 Novemba, 2022
 
Mfumo dume ndo umeleta Maendeleo duniani na ulithibiti maadili kisawa sawa wenye akili wamenielewa

Wale feminist povu ruksa
 
Back
Top Bottom